Wakazi wa jiji la Mwanza wamekumbwa na sintofahamu baada ya kijana mmoja asiyefahamika kusadikiwa kujirusha kwenye jengo la ghorofa ya tatu katika hoteli ya Gold Crest iliyopo jijini humo.
Taarifa za awali za kifo cha kijana huyo zinaeleza kuwa baada ya kudondoka kutoka ghorofani, alipoteza maisha papo hapo.
Wakizungumza mapema asubuhi, wakazi wa mji wa Mwanza wameonyesha kusikitishwa na kifo cha kijana huyo anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 ambae chanzo cha kifo chake hakijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amelizungumzia tukio la kifo cha kijana huyo akisema kuwa taarifa za awali walizozipata kuhusu tukio hilo hazikuwa za kweli kwa kuwa eneo ambalo inadhaniwa amejirusha na eneo ambalo umekutwa mwili wake ni tofauti.
"Haiingii akilini kuwa umbali ule ambao inadhaniwa mtu amejirusha na eneo la barabara ambalo amekutwa, haiwezekani pia mtu amejirusha akafika chini akawa mgongo wake mzima, kichwa kizima na hakuna hata tone la damu, kwahiyo kwa taarifa za awali, mimi nakanusha kuwa mtu huyu hajajirusha".
0 comments:
Post a Comment