Friday, 31 May 2019
NAMNA WAKULIMA WANAVYOPOTEZA FURSA KWA KUTOKUCHANGAMKIA FURSA
Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga akionyesha maziwa yanayotegenezwa kwa kutumia korosho.
Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga akionyesha maziwa yanayotegenezwa kwa kutumia korosho.
Mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Tari- Naliendele, Regina Msoka akinyesha bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia mabibo ya korosho, juisi kusho na kulia ni mvinyo.
Mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Tari- Naliendele, Regina Msoka akinyesha bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia mabibo ya korosho, juisi kusho na kulia ni mvinyo.
Chupa zenye mvinyo ulio tayari kwa ajili ya kwenda sokoni.
Chupa zenye maziwa yanayotengenezwa kwa kutumia korosho.
****
Mara nyingi wakulima wa korosho hulima zao hilo kwa lengo la kuuza korosho ghafi ambazo kwa kiasi kikubwa husafirishwa kwenda nje nchi na baadhi yao wachache huzibangua ili kuziongezea thamani.
Lakini bado wamekuwa wakipoteza mapato kwa kiasi kikubwa kutokana na kutotumia vyema fursa inayopatikana kwenye korosho.
Kutokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele katika zao hilo mkulima anaweza kuzalisha bidhaa nyingine kwa mbali na ile korosho anayoiuza ikiwa ghafi.
Katika zao hilo kuna tunda la bibo ambalo wakati wa mavuno mkulima hulazimika kutenganisha bibo na korosho ndipo apeleke korosho ghalani. Wakulima wengi huyateketeza kwa moto licha ya kuwa yanafaa kuzalisha bidhaa kama mvinyo, jam na juise’
Mtaalamu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Tari- Naliendele, Regina Msoka anasema mkulima anapopata kilo moja ya korosho ghafi shambani anaacha mabibo kilo tisa huku akiambulia kati ya Sh 2,400 hadi 4,000 kulingana na bei ya mnada.
“Mkulima akipata kilo moja ya korosho ghafi maana yake ameacha kilo tisa za mabibo shambani unaweza kuona ni jinsi gani anaacha bidhaa ambayo ni muhimu shambani,”anasema Msoka
Anabainisha katika katika kilo tisa ya mabibo yakisindikwa na kutengenezea mvinyo na kuuthaminisha ana uwezo wa kupata Sh 100,000 huku kilo moja pekee ya korosho hazidi Sh 4,000.
“Ukipiga hesabu za haraka katika kilo kumi za korosho ana mabibo kilo 90 maana yake ana Sh 40,000 ya korosho na ambaye anatumia mabibo kutengeneza mvinyo ana Sh 1milioni kwa hiyo hapo unaona ni faida gani iliyopo kwenye mabibo,”anasema Msoka na kuongeza;
“Tumefanya utafiti teknolojia zipo tuna uwezo wa kutengeneza juisi ya mabibo ambayo haina ukakasi, ambapo katika mabibo kilo moja unapata nusu lita ya juisi,wengi wanakimbia bibo sababu ya ule ukakasi wake,sisi tumefanikiwa kuutoa na pia tunapata juisi nzuri, tunapata jam na pia mashine zinapatikana Sido na tunaendelea kutoa mafunzo kwa badhi ya wakulima,”anasema
Kutokana na bibo kutohifadhika kirahisi anasema baadhi ya wakulima huyakausha na kutenegenezea pombe za kienyeji maarufu kama ulaka ambazo hazijathibitishwa kwani kiutaalamu.Anasema kitaalamu yanapaswa kutunzwa sehemu yenye ubaridi (cold room).
Muda wa kupata mvinyo, jam na juisi
Ili kupata mvinyo uliokamilika inahitajika miezi mitatu ili kuyasindika mabibo ili ukomae ambapo kilo moja ya mabibo una uwezo wa kuzalisha lita moja ya mvinyo.
Ili kupata juisi zinahitajika siku mbili ambapo mtengenezaji anahitaji mabibo kilo moja ili kupata nusu lita ya juisi na kwa jam ni siku moja.
Utengenezaji siagi ya korosho na maziwa
Mtafiti Msoka anasema kwa kutumia kilo moja ya daraja la mwisho ambalo ni vipande vidogo vya korosho (small pieces WW450) baada ya kubanguliwa na kupangwa katika madaraja unaweza kutengeneza siagi kilo moja ambayo huuzwa Sh 20,000 na korosho hizo thamani yake ni Sh 10,000 kwa kilo.
“Badala ya kuuza korosho Sh 10,000 natengeneza siagi kilo moja na kuuza Sh 20,000,nikitoa gharama za uzalishaji bado nitakuwa na faida, na nikitumia kilo moja hiyo hiyo ya korosho nina uwezo wa kupata maziwa takribani lita tatu ambazo nitaziuza Sh 25,000,”anasema
Kuhusu madaraja ya korosho,Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga anasema kwenye saizi ya mbegu kiutafiti wamefanikiwa kuwa na mbegu ambazo zina ukubwa unaostahili kwenye soko kwa maana zinazokidhi daraja kubwa na kuvutia wanunuzi kutoka nje.
Anafafanua daraja la mbegu 500 nchini hazipo na badala yake zipo zinazokidhi daraja kubwa la mbegu 180 huku zile za daraja la 450 zikiwa ni chache sana na ndizo hutengenezea maziwa na siag.
“Korosho za Tanzania zina ubora wa kimataifa unaokubalika kwa sababu tuna mbegu ambazo tumezizalisha na tumezigundua zina sifa za soko la kimataifa na ndio maana tunahimiza wakulima wetu wapande mbegu bora kutoka Naliendele il tunapoenda kwenye ushindani soko lolote la kimataifa hakuna anayetushinda,”anasisitiza Dk Kapinga
Anafafanua kutokana na baadhi ya watu kama watoto kushindwa kutafuna korosho au kuwa na mzio (allergy) ya maziwa ya ng’ombe ndio sababu za wao kuwa na utafit wa maziwa ya korosho.
Upatikanaji wa malighafi
Msoka anasema malighafi wanazotumia kutengeneza mvinyo,jam na juisi hupatkana katika mashamba yao ya utafiti huku korosho zinazotengenea ,maziwa na pinetbutter hutokana na korosho zinazobanguliwa katika kiwanda kilichopo kwenye taasisi hiyo kwa ajili ya utafiti.
Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk Bakari Msangi anasema kwa kuwa Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele imeshafanya utafiti na kuthibitisha teknolojia inayoweza kutumika watu wachangamkie fursa.
Anasema wafanyabiashara wakubwa wanatakiwa kuona fursa na kuweka viwanda katika mikoa inayozalisha korosho kwa kuanzisha viwanda vitakavyozalisha bidhaa zitakazotokana na mabibo.
“Wanachotakiwa ni kuona tayari katika level ya research tumeprove teknolojia kwamba inaweza na tumeshatoa product zinazoingia sokoni, kwa hiyo tunawavutia wawekezaji wa ndani na nje waone umuhimu wa kuweka viwanda,”anasema Dk Msangi
Hata hivyo, anasema kwa kuwa sasa ni uchumi wa viwanda hawawalengi tu wajasiriamali wadogo, bali wafanyabiashara wakubwa na watunga sera wote.
“Watu wote wanaoongelea sera za nchi wajitahidi kuitangaza teknolojia hii ambayo imeshahakikiwa na Naliendele kuhamasisha watu kuwekeza katika maeneo yanayozalisha korosho ili kutumia hii product (bidhaa) ambayo inapotea,ni potential area,”amesema Dk Msangi
Wakulima
Mkulima Elisha Millanzi anasema katika msimu mmoja ana uwezo wa kupata korosho tani mbili hadi tatu na mabibo yatokanayo na korosho hizo hutengeneza juisi ya kunywa wawapo shmbani na yanayosalia ambayo ni mengi huyateketeza kwa moto pindi yanapokauka.
Pia, anasema wapo baadhi ya watu huyatumia kutengenezea pombe maarufu kama ulaka pindi yanapokuwa mabichi na hutumika katika familia na hutumika kama burudani ya familia na wengine huyakaush na kutengenezea pombe ya gongo ambayo hairuhusiwi.
“Unapokula bibo linakuwa na asili ya sukari, mara nyingi tunakamua na kuchuja na kunywa bila hata kuweka sukari wala kuongeza maji, hata kama uko shambani umekosa maji ya kunywa unayakamua na kunywa,”anasema Millanzi
“Kama serikali ikituletea viwanda vya kutengeneza bidhaa nyingine itakuwa imetusaidia kwa sababu tunatupa rasilimali nyingi, mtu akivuna tani kumi ina maana kila korosho moja ilikuwa na bibo lake moja hapo mabibo na yenyewe ni tani kumi au zaidi,”
Mikakati iliyopo
Mbunge wa Tandahimba, Katani Katani anasema baadhi ya wakulima hutengeneza pombe asili ya gongo ambayo haina viango na hairuhisiwi nchini na hivyo kupelekea mabibo mengi kuteketezwa.
Anasema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele unahitaji mashine zitakazotakiwa kufanya uzalishaji.
“Bahati nzuri waziri wa kilimo tulifika naye Naliendele anajua mabibo yanaweza kutengeneza mvinyo, kwa hiyo tunajaribu kuangalia namna iliyo sahihi tuweke kwenye sera ya kuona hilo jambo linaweza kuwanufaisha wakulima kwa namna nyingine,”anasema Katani
WAZIRI BITEKO ASHUHUDIA MAKABIDHIANO YA DHAHABU ILIYOKAMATWA MWANZA
Na GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameshuhudia makabidhiano ya mali ikiwemo dhahabu iliyokamatwa katika Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, ikisafirishwa kinyume na sheria baada ya kutaifishwa na mahakama kuwa mali ya Serikali.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni dhahamu kilo 319 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.018, fedha taslimu shilingi 305, mzani wa kupimia ubora wa
madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi januari mwaka huu wilayani Sengerema.
Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa serikalini baada ya kutaifishwa pia.
Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Madini, Khatibu Kazungu (wa kwanza kulia) wakishuhudia vipimo vya madini yaliyokamatwa wilayani Sengerema kabla ya kufanya makabidhiano.
Makabidhiano ya mali hizo yamefanyika leo jijini Mwanza na kushuhudiwa pia na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Madini yaliyokamatwa yakipimwa kabla ya makabidhiano kufanyika, hatua hii inajiri maada ya mahakama kutaifisha madini hayo.
Watuhumiwa 12 wakiwemo wenye mali wanne na askari polisi wanane walikamatwa wakihusishwa kuhusika na utoroshaji wa madini hayo wilayani Sengerema ambapo wenye mali walipatikana na hatia na kuhukumiwa huku askari polisi wakikana mashtaka dhidi yao ambapo bado kesi yao inaendelea mahakamani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakishuhudiano vipimo vya madini hayo kabla ya kufanyika makabidhiano.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia makabidhiano ya madini hayo.
Tazama video hapa chini
MJAMZITO AJIPASUA TUMBO KUTOA MTOTO TUMBONI RUKWA
Mwanamke mmoja anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa Kusini Magharibi mwa Tanzania.
Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na bi Joyce Kalinda.
Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua umbo, Mganga mkuu wa wiaya ya Nkasi Dokta Hashi Mvogogo alizungumza na gazeti la Habari Leo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo.
Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaj mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.
Daktari huyo amesema saa tisa alfajiri ya kuamkia siku ya Alhamisi, mwanamke huyo alifika katika kituo cha afya cha Kirando na kuanza kupiga kelele, akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua.
Alisema kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo mja mzito kusubiri kidogo kisha alikwenda kumhudumia mgonjaw mwingine, lakini aliporejea mahali apokuwepo hakumkuta.
Kwa mujibu wa Dokta Mvogogo,ilipotimu alfajiri saa 11 mja mzito huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamembeba mtoto mchanga.
Watu hao walisema mwanamke huyo alikuwa amejipasua tumbo na kumtoa mtoto tumboni.
''Tumbo lilionekana limepasuliwa na kitu chenye ncha kali.Alipofika aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yakekwani alikua amepoteza damu nyingi, lakini pia mtoto alipewa matibabu kutokana na kutolewa tumboni bila kufuata utaalamu unaotakiwa na sasa wote wanaendelea vizuri na matibabu,'' Dokta Mvogogo aliiambia Habari Leo.
Dokta Mvogogo amesema tukio hilo limeripotiwa polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ni nini kilichotokea kwa mama huyo.
''Uchunguzi unaofanywa pia unahusisha mtaalamu wa magonjwa wa akili ambaye tunataka achunguze ili kubaini kama mama huyo ambaye huo ni uzao wake wa nane ana ugonjwa wa akili au la,'' alieleza Daktari huyo.
Chanzo - BBC
MTOTO ACHOMWA MOTO,AKATWA VIWEMBE KISA KAKOMBA MBOGA YA KISAMVU
Mkazi wa Kata ya Buhalahala mjini Geita, Magreth Digugulo, anadaiwa kumchoma moto na kisha kumkatakata na wembe mjukuu wake kwenye mkono wa kulia kwa madai ya kukomba mboga.
Mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alizungumza na Nipashe jana nyumbani kwao alitaja sababu za kufanyiwa kitendo hicho kuwa ni kujipakulia mboga aina ya kisamvu.
Alisema siku ya tukio, hakuwa amekwenda shuleni ila hakuwapo nyumbani na baada ya kurudi alipakua mboga kidogo akala na baada ya bibi yake kurudi, alimwita na kumkaripia ndipo akamchoma moto na kumkatakata vidole na wembe.
"Sikuwa nimeenda shuleni siku hiyo. Baada ya kutoka kucheza nilikuja nyumbani kula, sikumkuta bibi hivyo nikajipakulia mboga kidogo nikala. Bibi aliporudi akasema nimekomba mboga ndiyo akanifanyia hiki kitendo," alisema.
Baadhi ya majirani ambao walishuhudia tukio hilo, akiwamo Ayoub Bwanamadi, ambaye ni Mratibu wa Mtandao wa Marafiki wa Elimu, alisema walipata taarifa za tukio hilo na baada ya kusogea eneo la tukio, walitafuta namna yakumsaidia mtoto huyo.
Kwanza, alisema walitaka kujua nini chanzo cha tatizo na walimuuliza bibi yake akawajibu mtoto amekomba mboga ndiyo maana amemchoma moto.
Alisema tabia hiyo inaonekana imezoeleka kwa bibi huyo kutokana na mtoto kuonekana na majeraha mengine makubwa kwenye mwili wake ambayo yamekwisha pona.
"Hali ilivyo kwa huyu mtoto ni kama matukio haya ni ya kujirudia. Ukitazama kwenye kiganja cha mkono wake kuna kovu moja na mtoto anavyodai bibi alishawahi kumchoma kwenye majivu kabla ya tukio hili," alisema Bwanamadi.
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Kata hiyo, Neema Emmanuel, alisema alipokea taarifa ya tukio hilo na kumpeleka mtuhumiwa polisi kisha kumpeleka mtoto hosptalini kwa ajili ya matibabu.
"Mwezi huu wa tano (Mei) matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara. Hili ni tukio la nne kutokea kwenye kata yangu, mengine tumeshayafikisha kwenye ngazi husika. Hata hivyo tunawashukuru wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za matukio haya," alisema.
Babu mzazi wa mtoto huyo, Stephano Matata, alisema tukio hilo limemsikitisha kutokana na mtoto huyo kutokuwa na msaada wowote wa malezi ya wazazi wake kwa kuwa anaishi na bibi yake kwa sababu mama yake mzazi ameshatokomea kwenye machimbo huku baba akiwa hajulikani ni nani.
"Mimi huwa sikai hapa nyumbani, lakini nilivyopata taarifa hizi zilinisikitisha kwani huyu mtoto ni kama hana wazazi. Mimi nitamchukua nikae naye kwa sababu hana msaada mwingine," alisema Matata.
Kutokana na kitendo hicho, bibi huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili kuhojiwa kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
NEC YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA ZA MUDA ZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura.
Kwa mujibu wa tangazo la maombi ya ajira hizo lililosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Mabamba Rajabu Moses, Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45 wametakiwa kuomba.
Sifa zingine za waombaji ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
“Awe na uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software an kuyatatua” ilisema sehemu ya tangazo hilo.
“Awe na uwezo wa ku-istall programu za kompyuta an kutoa msaada wa kuifundi wa TEHAMA kwa watumiaji. Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai an awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo”,ameongeza.
Sifa nyingine za ziada za kazi hiyo zimetajwa kwenye tangazo hilo linalopatikana kwenye Tovuti ya NEC ya www.nec.go.tz na mitandao ya kijamii ya NEC.
ARIF TANZANIA ATAKA WENYE KIPATO KUSAIDIA WASIO NA KIPATO
Na Shushu Joel,Chalinze.
Taasisi ya Miraj Islamic Centre yenye makao yake mkuu jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa watu wote walio na nafasi ya kipato kuwasaidia wasio na kipato kama ilivyoagizwa katika vitabu vya Mungu.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Arif Yusuf Abdulrehman maarufu Arif Tanzania alipokuwa akizungumza na baadhi ya waislamu wakati wa zoezi la kuwagawia futari wakazi wa Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Arif Tanzania alisema taasisi yake imekuwa miongoni mwa taasisi za kuigwa nchini na nje kwa jinsi inavyojitolea kuwasaidia Watanzania wote pasipo kujali dini zao wala kabila huku lengo likiwa ni kuwaonyesha wale wasio na uwezo kuona ni sawa na wenye uwezo.
"Unaposaidia wenzako Mwenyekiti Mungu anakuongezea kutokana na jinsi wale unaowasaidia wanakuombea uweze kupata ili uendelee kuwasaidia zaidi",alisema Arif Tanzania.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki cha mwezi huu wa Ramadhan taasisi ya Miraj Islamic imewezesha sehemu mbalimbali kwa ajili wananchi vyakula na tende kwa baadhi ya mikoa kama vile Arusha,Pwani,Mwanza,Kigoma,Zanzibar na mikoa mingine kwa kusudi la kuwasaidia wasio na uwezo wa kipato ila wamefunga katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Aidha alisema Taasisi yake imekuwa msaada mkubwa kwa serikali kutokana na jinsi inavyojitoa katika masuala ya kusaidia watu mbalimbali ili waweze kujikwamua katika maisha yao,watu hao ni pamoja na kuwasaidia usafiri walemavu,vijana kuwapatia mashine za kukamulia juisi na wengine kuwapatia pikipiki kwa ajili ya kufanya shughuli za boda boda, akinamama kuwawezesha kwa vyerehani ya ushonaji.
Alisema kama kila mwenye nafasi ya kipato akijitolea kwa moyo mmoja basi Watanzania wengi watafikiwa na kuwawezesha ili nao waondokane na umaskini walionao.
Arif Tanzania pia aliipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi inavyofanya kazi zake na viongozi wa dini zote na kuwakomboa watanzania wa hali za chini kwenye imani zao pasipo kubagua.
Kwa upande wake Ashura Juma (81) mkazi wa Vikindu katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani aliipongeza taasisi ya Miraj Islamic Centre kwa jinsi inavyojitolea katika kutoa misaada mbalimbali kwa wanyonge.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupitia taasisi hiyo familia yake imekuwa moja ya wanufaikaji wakubwa kwa kupata misaada mingi ikiwemo chakula kwa ajili ya futari,fedha na mahitaji mengine mengi ya kibinadamu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa halmashauri ya Chalinze katika wilaya ya Bagamoyo, Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amesema kuwa misaada hiyo inayotolewa na taasisi hiyo imekuwa na tija kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu kutokana na uhitaji wa futari kwenye kipindi hiki.
Mbali na hilo Kikwete alisema pongezi hizo si kwa wananchi bali hata serikali imekuwa ikinufaika na Arif Tanzania kupitia taasisi zake zinazojitolea kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya wanyonge.
"Kutokana na jinsi taasisi hii inavyojitolea katika ufanikishaji wa wa misaada ni lazima sisi kama wawakilishi tuisemee vizuri ili wengine wajitokeze "alisema .
MHUBIRI ATUKANA MAASKOFU WASIOMHESHIMU...WAUMINI WANAOMVIZIA MKEWE
Mhubiri mwenye utata James Ng'ang'a wa Kanisa la Neno Evangelism Center nchini Kenya ametishia kuchukua hatua mikononi mwake na kuyafunga matawi mengine ya kanisa lake kwa kile alichokitaja kama kukosewa heshima.
Wakati wa ibada, Ng'ang'a amewaonya waumini, maaskofu dhidi ya kummezea mate mkewe.
Ng'ang'a aliyekuwa mwingi wa hasira aliyataja majina ya baadhi ya waumini wa kanisa hilo la Neno Evangelism Center.
"Mengi yamekuwa yakisemwa. Iwapo mtashindwa kumheshimu mke wangu nitawafukuza katika kanisa hili. Wakati huu sasa nitawaonesha uwezo wangu,You will know my true colour" Ng'ang'a alitishia.
Haijabainika wazi kile mtumishi huyo alimaanisha kwa kutamka kukosewa heshima lakini aliwakemea baadhi ya waumini kwa madai ya kumvizia mkewe.
Hakukomea hapo tu bali alizidi kuwaonya baadhi yao kwamba iwapo hawatabadili mienendo atawachukulia hatua.
"Vile vile, mwanamke yeyote ambaye atamkosea heshima mke wangu nitamfurusha humu kanisani. Utaondoka katika kanisa langu na kuanzisha lako,"aliongeza.
Matamshi yake yaliwashtua waumini kanisani humo, ambao hawakuwa na la kufanya ila kuketi kitako na kumsikiza kwa makini huku wakisalia kumkodolea tu macho.
Machi, 2019 alijipata pabaya baada ya kushtakiwa kwa kumtishia mwanahabari Linus Kaikai wa Citizen TV, baada ya Linus kupendekeza wachungaji wote ni sharti wawe na shahada ndipo wahudumu kama mapasta.
Mhubiri huyo ambaye amezongwa na utata si haba alifunga ndoa na mkewe Mercy Murugi kwenye sherehe ya kifahari ilyoandaliwa Windsor Golf Club na kuhudhuriwa na wanasiasa mashuhuri.
MSIKILIZE HAPA
MSIKILIZE HAPA
VAZI LA WAZIRI MKUU LAZUA GUMZO...ATINGA NA SUTI YA SKETI NA SANDOZI IKULU
Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi amepata fursa ya kumtembelea rais wa Kenya Uhuru kenyatta
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi.
Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.
Vazi alilovalia ni maarufu nchini kwa wanaume wa Fiji likifahamika kama na jina Suti ya Sulu.
Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra.Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.
Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino.
Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kukutumia pini.
Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji Tangu enzi za ukoloni katika katika karne ya kumi na tisa. Mwanzo zililetwa na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizi zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na ukristo.
Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.
Sulu za wanaume wanazovaa rasmi huitwa -sulu vakataga.
Vazi la sulu pia huvaliwa kama sare rasmi ya polisi na jeji nchini Fiji
Sulu zilizoshonwa na mifuko huvaliwa kawaida kama vazi la ofisi na rasmi pamoja na shati na viatu vya wazi (sandozi) na upande wa juu huvaa koti na tai.
Katika hali fulani, mtu anapoingia na Sulu kanisani huonekana kama mtu mwenye heshima nchini Fiji.
Sulu zilizoshonwa pia huvaliwa kama sare za polisi na jeshi.
Vazi rasmi la sulu huwana na urefu wa hadi chini ya magoti na hukatwa kwa mathalani umbo la pembe tatu.
Huku uvaaji wa Sulu mara nyingi huwa ni wa lazima kwa Wafiji wakati fulani, baadhi ya jamii wakati mwingine hukatazwa kuzivaa.
Makubwa Haya : WASHIRIKI WA MISS INDIA 2019 WOTE WANAFANANA AISEE!! WOTE WEUPE PEEEE!!
Ni shindano ambalo lilianzisha safari ya nyota wa sinema za Bollywood Priyanka Chopra, ndio maana shndano la mwaka huu la Miss India limewavutia washiriki wengi ambao walitabasamu wakati walipopiga picha za kujitangaza.
Lakini badala ya wao kujivunia ufanisi wao kwa hatua waliyopiga, wamejipata katikati ya mzozo kufuatia picha ambayo wakosoaji wanasema zinaashiria kuwa waandaaji wa shindano hilo wanavutiwa na watu waliyo na ngozi nyeupe.
Picha hiyo iliyochapishwa katika gazeti la Times la India -haikuwa na neno kwasababu ilionesha kundi la wanawake warembo 30 wanaoshiriki shindano la mwaka huu la Miss India.
Lakini wakati watumiaji wa mtandao wa Twitter walipoanza kuisambaza picha hiyo wakiuliza: "Picha hii ina makosa gani?" ndipo ilianza kuwavutia watu.
Baadhi ya watu waliidhihaki picha hiyo wakisema huenda wote ni mtu mmoja
Kadri picha hiyo ilivyosambazwa mitandao ndivyo ilivyoendelea kupata umaarufu hata hivyo wakosoaji walisisitiza kuwa washiriki hawakuwa na makosa lakini walihoji kuwa shindano hilo liliwavutia watu weupe hatua ambayo iliibua gumzo la jinsi wahindi wanavyoshabikia ngozi nyeupe.
Waaandalizi wa shindano hilo hawajatoa tamko lolote kufikia sasa.
Mashindano ya urembo yamekuwa yakiangaziwa sana nchini India tangu miaka ya katikati ya -1990.
Taifa hilo linajivunia warembo kadhaa maarufu walioshinda mataji ya Miss Indias, kama vile Aishwarya Rai, Sushmita Sen na Bi Chopra, ambao walishinda mataji ya kimataifa.Aishwarya Rai muda mfupi baada ya kuvikwa taji la Miss World 1994
Baadhi ya washindi wa shindano hilo pia walijiunga na tasnia ya uigizaji wa filamu za Bollywood ambayo inasadikiwa kuwalipa vizuri zaidi waigizaji wake.
Kwa miaka kadhaa taasisi zinazowapa mafunzo wasichana wanaotaka kujiunga na masuala ya ulimbwende zimebuniwa kote nchini humo.
Lakini waliyonufaika zaidi na mafunzo hayo ni wanawake waliyo na ngozi nyeupe.
Si jambo la kushangaza
Dhana ya uweupe kuhusishwa na urembo nchini India imekuwepo kwa muda mrefu na kumekuwa na madai kuwa mwanamke mweupe ni mzuri kuliko mweuyeusi.
Krimu ya Fair and Lovely -ambayo inaongeza weupe ilipovumbuliwa miaka ya 1970, ilitokea kuwa bidhaa ya urembo iliyonunuliwa kwa wingi nchini India.
Kwa miaka mingi waigizaji maarufu wa sinema za Bollywood wamekuwa wakifanya matangazo ya biashara ya kuidhinisha krimu hiyo.Waandalizi wa mashindano ya urembo wamekosolewa kwa kuwapendelea zaidi washiriki weupe.
Matangazo ya biashara ya krimu kama hizo ziliwaahidi watumiajiwake sio tu ngozi nyeupe, laini na ya kupendeza bali pia ziliangaziwa kama tiketi ya kumfanya mtu kupata kazi nzuri, mpenzi na kuolewa.
Shindano kama hili linawapendelea washiriki weupe mara nyingi hutumiwa kuendeleza dhana hiyo potovu kuhusu maana halisi ya urembo
Miaka ya hivu karibuni kumezinduliwa kampeini zinazopinga dhana kwamba kuwa ni ngozi nyeupe ndio kigezo pekee cha urembo.
Kupitia Hashtag ya #unfairandlovely, katika mtandao wa Twitter, waandalizi wa kampeini hizo waliwahimiza watu kusherehekea ngozi nyeusi.
Lakini juhudi hizo hazijakomesha kuongezeka kwa bidhaa za urembo zinazodaiwa kuwa na uwezo wa kuwafanya watu kuwa weupe.
Wale wanaounga mkono utumiaji wa bidhaa hizo za urembo wanasema kuwa ni uamuzi wa mtu binafsi lakini kimekuwa na ripoti za mamodo weusi kutengwa wanapotoa maombi ya kutaka kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu za Bollywood.
Chanzo -BBC
STAND UNITED WAISHANGAA TFF...SASA WAPIGA DEBE KUSAKA WACHAWI WA SHERIA ZA SOKA
Uongozi wa klabu ya wapiga Debe wa Stand united maarufu Chama la wana ya mjini Shinyanga, umesema haujaridhishwa na maamuzi ya shirikisho la soka nchini, TFF, la kuishusha daraja klabu hiyo inayolingana alama na timu ya Kagera Sugar ambayo imebakizwa ligi kuu soka ya Tanzania bara, licha ya Stand United kuongoza kwa magori mengi ya kufunga.
Mwenyekiti wa Stand United Chama la wana Dk. Ellyson Maeja, amesema wameshangazwa na maamuzi ya TFF ya kuishusha daraja Stand United mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu soka ya Tanzania bara, kwa vigezo vya magoli ya kufungwa licha ya kuongoza kwa magoli ya kufunga dhidi ya timu ya Kagera Sugar ambayo inalingana alama 44 katika msimamo wa ligi hiyo.
Stand United hadi ligi kuu inamalizika imeshinda mechi 12 na kufungwa mechi 18 magoli ya kufunga magoli 38 na kufungwa 50 huku Kagera Sugar ikishinda mechi 10 na kufungwa mechi 14 imefunga magori 33 na kufungwa magori 43.
Kufuatia hali hiyo ambayo imeleta mijadala mbalimbali kwa mashabiki wa soka na klabu ya Stand United uongozi umepanga kutafuta washauri na wabobezi wa sheria za soka ambapo klabu hiyo itatoa tamko rasmi la kukubali kushuka daraja au kukata rufaa.
Thursday, 30 May 2019
Picha : DC MBONEKO AFUNGA MASHINDANO YA UMISSETA MKOANI SHINYANGA... ASISITIZA VIJANA KUBEBA MAKOMBE KITAIFA
Na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amefunga rasmi mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA 2019) Mkoani Shinyanga, na kuwataka washindi watakaoungana na kuwa timu moja ya mkoa, wakashiri kikamilifu katika mashindano hayo ngazi ya kitaifa huko Mtwara, na kupata ushindi wa makombe mengi.
Mashindano hayo ya (UMISSETA) yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack Mei 27, 2019 ambapo yamefungwa leo Mei 30 na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwenye viwanja vya CCM Kambarage mjini humo, ambapo washindi wamepewa zawadi za makombe.
Mashindano yalishirikisha timu mbalimbali kutoka halmashauri ya Kahama Mji, Msalala, Ushetu, Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kwa kuchezwa mpira wa miguu, kikapu, pete,tenesi, wavu, riadha, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya.
Akizungumza wakati akifunga mashindano hayo,Mboneko amewataka washiriki ambao watachaguliwa kuwa timu moja za kwenda kushiriki (UMISSETA) ngazi ya kitaifa, wawe kitu kimoja na kutobaguana kuwa huyo anatoka halmashauri nyingine, bali washindane kama timu moja ambayo inatoka mkoani Shinyanga na hatimaye kuibuka na ushindi.
“Nawapongeza wanafunzi wote mlioshiriki kwenye mashindano haya ya (UMISSETA) ambapo mmeonyesha vipaji vyenu na wote ni washindi, lakini hamtaweza wote wanafunzi 704 kwenda kushiriki ngazi ya kitaifa, bali tutachagua wanafunzi 120 ili wakatuwakilishe na tunataka mrudi na makombe mengi,” amesema Mboneko.
“Na mtakapokuwa kambini muwe timu moja na kutobaguana kuwa huyu anatoka halmashauri hii, sitaki kitu kama hicho bali nataka muwe ndugu kwani nyie wote mnatoka Shinyanga, na mkashindane kweli kweli kwa kuonyesha vipaji vyenu na kuupatia sifa mkoa wetu,”ameongeza.
Pia amewataka washindi ambao watachaguliwa kwenda kushiriki mashindano hayo ngazi ya kitaifa, wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu na siyo kwenda kuchafua sifa ya mkoa.
Naye Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi, amewataka wanafunzi hao pindi watakapokuwa huko Mtwara, waonyeshe vipaji vyao ikiwa michezo ni ajira kwa sasa.
Aidha washindi waliopatikana kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) Mwaka 2019 mkoani Shinyanga, mpira wa miguu wavulana ni halmashauri ya Msalala, wasichana halmashauri ya Shinyanga, mpira wa mikono (Handball) wavulana Manispaa ya Shinyanga, wasichana Kishapu, Volleyball Manispaa ya Shinyanga, wasichana halmashauri ya Shinyanga.
Kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana na wasichana washindi ni kutoka halmashuri hya Shinyanga, mpira wa pete Kahama Mji, Tenesi mshindi wavulana na wasichana ni Halmashauri ya Shinyanga , riadha wavulana Shinyanga, wasichana Kishapu, ngoma kutoka Ushetu, kwaya Kahama Mji, usafi na nidhamu wavulana Kahama Mji, wasichana Shinyanga.
Hata hivyo katika mashindano hayo ya UMISSETA (2019) Mshindi wa jumla alitoka halmashauri ya Shinyanga , huku kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘MICHEZO NA SANAA KWA ELIMU BORA NA AJIRA.’
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifunga rasmi mashindano ya michezo ya UMISSETA 2019 na kuwataka washindi ambao wamechaguliwa kushiriki ngazi ya kitaifa wakawe kitu kimoja na kupata ushindi wa makombe mengi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akiwataka wanafunzi ambao wamechaguliwa kwenda Mtwara kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua fainali ya mashindano ya (UMISSETA 2019) kati ya timu ya mpira wa miguu Kahama Mji na Msalala huku kwa upande wa wasichana ni Kahama Mji na Shinyanga , na kuwataka wacheze kwa nidhamu kwa kuonyesha vipaji vyao.
Fainali ikiendelea kuchezwa kati ya timu ya Kahama Mji wenye jezi ya njano pamoja na Msalala wenye jezi nyekundu, ambapo hadi dakika 90 zinakamilika walitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na hatimaye kwenda kwenye matuta ili mshindi aweze kupatikana.
Penati/Matuta yakipigwa ambapo Msalala waliibuka na ushindi wa magoli 4 kwa matatu dhidi ya Kahama Mji na hatimaye kuwa mabingwa rasmi kwa mpira wa miguu katika UMISSETA Mwaka (2019) Mkoani Shinyanga.
Mchezo wa Fainali wa mpira wa miguu ukichezwa kati timu ya wasichana ya Shinyanga wenye Jezi ya Lightblue, na Kahama Mjini wenye Orange, ambapo Shinyanga waliibuka na ushindi wa goli moja na kuwa mabingwa.
Wanafunzi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiangalia fainali ya michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya (UMISSETA) 2019 Mkoani Shinyanga.
Wanafunzi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiangalia fainali ya michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya (UMISSETA) 2019 Mkoani Shinyanga.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga na kusubiri washindi kupewa makombe yao.
Wadau wakishuhudia fainali ya mashindano ya UMISSETA.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA).
Hamasa zikitolewa uwanjani.
Wanafunzi kutoka Ushetu wakitoa burudani ya ngoma.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji wa timu ya Msalala kabla ya kuanza kucheza fainali na timu ya Kahama Mji, kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kahama Mji, kabla ya kuanza kucheza fainali na timu ya Msalala kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa mpira wa miguu kutoka halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi kombe kwa washindi wa mpira wa miguu kwa upande wa wasichana kutoka halmashauri ya Shinyanga.
Ukabidhiwaji wa makombe kwa washindi ukiendelea kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga mwaka 2019.
Ukabidhiwaji wa makombe kwa washindi ukiendelea kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa jumla kwenye hitimisho la mashindano hayo ya michezo ya UMISSETA Kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Awali makombe yakiandaliwa tayari kwa kukabidhiwa washindi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga mwaka 2019.
Waamuzi nao wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufunga Rasmi mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga Mwaka 2019.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog