Sunday 24 September 2017

MATUKIO KATIKA PICHA:MKUU WA WILAYA YA BUSEGA, DC TANO S. MWERA AZINDUA ALBUM AICT MKULA

...
Mkuu wa wilaya Busega akiwa amesimama katika picha,akiongea jambo wakati wa uzinduzi wa album AICT Mkula.
Mkuu wa wilaya ya Busega DC. Tano S mwera amehudhuria uzinduzi wa album kwaya ya AICT mkula mjini Besega.

Wakati wa uzinduzi huo wa album hiyo ambayo itakua ikipatikana kwa gharama ya tshs 10000 tu kwa CD ,Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo adhimu kuwaasa wananchi waliohudhuria uzinduzi huo  kuwa wanapaswa kuheshimu na kusikiliza mahubiri wanayoyapata sehemu za ibada ambayo yatawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii zao.

Mh.Dc alizitaja changamoto ambazo wanapaswa kuzitatua ikiwa ni pamoja na mimba za utotoni,madawa ya kulevya,uvuvi haramu,mauaji ya Albino na mauaji ya vikongwe. 

Pamoja na hayo Mheshimiwa Dc alikamilisha kwa kuwashukuru wananchi waliohudhuria uzinduzi huo na kuwasihi kuendelea kuishi kwa amani na kufata taratibu na sheria za nchi.


Baadhi ya watoto waliohudhuria uzinduzi wa album ya AICT Mkula.













Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger