TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda
kuwajulisha wananchi juu Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na
Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa
wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24 Agosti, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa
kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi.
Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye
tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na
Kidato cha Tano, inabidi ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi awamu ya pili mwaka mwaka
2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions)
inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
23 Agosti, 2017
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Tafadhali bofya chini Kujua Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment