Monday, 15 August 2016

BASATA wamtoa Nay wa Mitego ‘Kifungoni’, licha ya kurekebishwa mara mbili bado wasisitiza wimbo wake ‘Pale kati’ hauna maadili.

...

Baraza la sanaa nchini BASATA, limemfungulia msanii wa Bongo Flava Nay Wa mitego kuendelea kufanya shughuli za muziki kama kawaida.
Hatua hiyo inakuja baada ya Baraza hilo kumfungia Nay kujihusisha na muziki tarehe 27 july kutokana na wimbo wake wa ‘Pale Kati’ kutokuwa na maadili.
Pamoja na kumtoa kifungoni rapa huyo, BASATA bado inaendelea kuufungia wimbo wake wa ‘Pale kati Patamu’ ambao licha ya kuirudia na kuirekebisha mara mbili baraza hilo haujaridhika nao.
Katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza, amedai bado wanamtazama Nay katika uangalizi maalum ili kujiridhisha kama amejirekebisha.
“Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/7/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego  kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:
1.Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa
2.Kulipa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000/-)
3.Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari na kwenye akaunti  zake za mitandao ya kijamii
4.Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’ ili ubebe maudhui yenye maadili
Msanii huyo ametekeleza adhabu zote zilizotajwa hapo juu, hata hivyo pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekesho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huo hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger