Christian Bella ‘Obama’
Wiki iliyopita ndipo tulianza na
Christian Bella ‘Obama’ kwenye kolamu hii akisimulia juu ya maisha yake,
aliishia kusimulia pale ambapo hali ya kiuchumi kwenye familia yao
ilipobadilika kutoka ya ‘kishua’ na kuwa ya kifukara, akalazimika
kuingia mitaani kujitafutia kipato, akajifunza pia kutengeneza mikate
kwenye kiwanda-bubu kilichokuwa nyumbani kwao na rafiki yake Junion
Kumbukumbu.
Tambaa nayo…
Tambaa nayo…
“Enhee, baada ya kuanza kujifunza
kutengeneza mikate nini kiliendelea?” nilimuuliza Bella huku nikikaa
sawa kwenye kiti, aliendelea kusimulia baada ya kupiga mafunda mawili
matatu ya kinywaji chake fulani hivi bariiidi.
Anasema kuwa baada ya kufahamu vizuri
kutengeneza mikate na kuanza kuingiza mkwanja wa kueleweka kwa ‘level’
yake kiasi kwamba akawa hategemei tena kupata pesa ndogondogo kutoka
nyumbani kwao, alijikuta akipiga chini kwenda shule na kujikita zaidi
kwenye masuala ya kutafuta pesa na kuhudhuria kwenye vikundi vya uimbaji
pamoja na rafiki zake.
“Nilipoachana na shule baba aliumia sana
maana alichoamini urithi wa mtoto ulikuwa ni kwenye elimu tu, aliniita
mara kadhaa na kunionya juu ya uamuzi wangu lakini wakati huo sikuhitaji
kumsikiliza mtu yeyote zaidi ya sauti niliyokuwa naisikia ndani yangu,”
alisema Bella.
“Ni sauti gani hiyo uliyokuwa unaisikia?” nilimuuliza huku nikimtazama kwa makini.
“Niache shule, nitafute pesa na kufanya muziki,” alijibu.
“Niache shule, nitafute pesa na kufanya muziki,” alijibu.
“Mama vipi, yeye aliupokeaje uamuzi wako huo wa kuacha shule?”
“Ulionekana kumshangaza, hakuamini kama ningeweza kufanya hivyo, pia kama mzazi alijaribu kunisihi lakini sikuhitaji kurudi nyuma.”
“Enhee, nini kikaendelea?”
“Ulionekana kumshangaza, hakuamini kama ningeweza kufanya hivyo, pia kama mzazi alijaribu kunisihi lakini sikuhitaji kurudi nyuma.”
“Enhee, nini kikaendelea?”
“Basi bwana; baada ya kukacha skuli
sikupenda kuishi tena nyumbani maana tayari mimi na wazazi wangu
zilikuwa haziungi tena freshi, kwa hiyo nilichoamua kufanya ilikuwa ni
kuondoka nyumbani na kwenda kuishi magetoni kwa washkaji zangu.”
“Nikiwa huko mishemishe za muziki ndiyo
zikaanza rasmi maana nao walikuwa katika harakati hizohizo, sasa kule
kwetu Kongo kipindi cha nyuma kwa vijana wadogo ambao wanafanya ishu za
muziki walikuwa wanatunga nyimbo wakishazikariri wanatengeneza bendi na
kuanza kufanyia mazoezi kwenye majumba mabovu huku ala za muziki zikiwa
madebe.”
“Kwa hiyo na nyie mlifanya hivyo?”
“Ndiyo, tulifanya hivyo na kila jioni tulikuwa kwenye jumba bovu f’lani hivi karibu na nyumbani kwao na mshkaji wangu Bosei Junioh tukifanya yetu, huwezi amini watu walikuwa wanajaa kinoma kila waliposikia tunaimba, baada ya muda tukaanza kuwa vizuri na kuwa kivutio mtaani.”
“Ndiyo, tulifanya hivyo na kila jioni tulikuwa kwenye jumba bovu f’lani hivi karibu na nyumbani kwao na mshkaji wangu Bosei Junioh tukifanya yetu, huwezi amini watu walikuwa wanajaa kinoma kila waliposikia tunaimba, baada ya muda tukaanza kuwa vizuri na kuwa kivutio mtaani.”
Bella anaendelea kuwa matumaini na
mwanga juu ya kufanikiwa kimuziki alianza kuvipata kutokana na
kukubalika huko kwenye mitaa ya kwao, anasema kilichomfurahisha zaidi
kwa wakati huo ilikuwa ni wasichana wengi wa mtaani kwao kuanza kuhitaji
kuwa naye kimapenzi.
“Kutokana na umri ilikuwa ni vigumu
kujizuia kuruka na baadhi yao waliokuwa wananivutia na kunihitaji, hata
hivyo nilikuwa na msichana f’lani ambaye nilikuwa nina mpenda sana, huyo
alikuwa kila kitu kwangu, lakini tofauti na wengine yeye hakuwa anataka
kabisa tufanye mapenzi.”
“Alikuwa ana umri gani?” nilimuuliza.
“Alikuwa ana umri gani?” nilimuuliza.
“Miaka kumi na sita.”
“Wewe?”
“Wakati huo kumi na nane na ndiyo umri nilioanza kufanya mapenzi.”
“Mkh…”
“Wewe?”
“Wakati huo kumi na nane na ndiyo umri nilioanza kufanya mapenzi.”
“Mkh…”
“Siku zikasonga mbele, kila kitu kuhusu
masuala yangu na wasichana wengine yalikuwa ni siri kubwa kwa huyo
niliyempenda, nikazidi kustrago kwenye ishu zangu za muziki
nilipofikisha miaka kumi na tisa ikabidi niende kuomba kujiunga kwenye
Bendi ya Chateau du Soleil.”
“Baada ya kupeleka maombi yangu kwenye
bendi hiyo ambayo ilikuwa inamilikiwa na tajiri mmoja aitwaye Frank
Isekya rafikiye mkubwa na Papa Wemba nikapangiwa siku ya kufanyiwa
usaili kabla ya kunikubali au kunibwaga kwenye bendi yao.”
Baada ya maneno hayo Bella anachukua
glasi yenye kinywaji akipendacho mezani na kubugia mafunda matatu, kisha
anairudisha mezani na kunitazama huku akitabasamu, macho yake
yalinifanya nipate swali la haraka la kumuuliza.
“Bila shaka kumbukumbu za usaili ndizo zinakufurahisha?”
“Asikwambie mtu, siku hiyo nakumbuka usiku wake sikupata usingizi kabisa, akili yangu yote ilikuwa kwenye usaili ambao ningeufanya kesho yake, lakini kikubwa nilikuwa nimepania kujikamua sawasawa nipate nafasi na nilimuomba Mungu hilo liwezekane.”
“Asikwambie mtu, siku hiyo nakumbuka usiku wake sikupata usingizi kabisa, akili yangu yote ilikuwa kwenye usaili ambao ningeufanya kesho yake, lakini kikubwa nilikuwa nimepania kujikamua sawasawa nipate nafasi na nilimuomba Mungu hilo liwezekane.”
Je, nini kitaendelea? Bella atafanikiwa
kupita kwenye usaili huo? Vipi kuhusu mpenzi wake anayempenda sana,
wataishia wapi? Usikose wiki
0 comments:
Post a Comment