INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hivi
karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za kazi
kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti Makao
Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.
Habari
hizo si za kweli,JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali lina
mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba wananchi
wazipuuzie taarifa hizo.
Aidha
JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za jeshi
bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi kinyume na utaratibu
huu,unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ.