Ni kwa
neema ya Mungu tu mpenzi msomaji tumefanikiwa kukutana tena katika safu
hii ya Mahanjumati ambapo leo tutajifunza kupika tambi za zabibu kama
maombi ya wengi yalivyohitaji.
MAHITAJI
– Tambi – Maji
– Hiliki – Mdalasini
– Zabibu kavu – Sukari
– Mafuta ya kupikia
JINSI YA KUPIKA
Bandika maji jikoni yaache yachemke, baada ya hapo yaepue na uyaweke pembeni.
Weka sufuria la kupikia tambi jikoni na
umimine mafuta kiasi unachoona kinatosha yaache yachemke kisha weka
tambi na uanze kuzikaanga mpaka zikauke na zibadilike na kuwa rangi ya
udhurungi ‘brown’.
Ziepue na uchuje mafuta halafu zirudishe tena jikoni.
Chukua maji ya moto kidogo weka sukari,
hiliki na mdalasini koroga kisha weka kwenye tambi, hakikisha unaendelea
kuweka maji mpaka ziive huku ukiwa unapunguza moto.
Weka zabibu kisha zifunike ili maji yakauke.
Zikishakauka maji, epua na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
0 comments:
Post a Comment