Tuesday 17 October 2017

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU IFM BATCH 2 2017/2018

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA BUGANDO UNIVERSITY-SECOND BATCH 2017/2018


  • UN GLOBAL GOALS AWARDEE Read More...
    Mr. Felix Manyogote, an MD 5 Students at CUHAS-BUGANDO will be honored a UN Global goal "Leave No One Behind" Award for demonstrating leadership and exceptional results in improving the maternal and child health in Tanzania
Share:

Moshi Co-operative University (MoCU): Approved Degree Applicants by TCU 2017/2018- ROUND 2

MoCU logo
Share:

Stella Maris Mtwara University College-STEMMUCO: Selected Degree Applicants 2017/2018. (ROUND 2)

Image result for STEMmuco
Share:

ARUSHA TECHNICAL COLLEGE-ATC: Applicants selected to Join Bachelor Degree Programmes in Academic Year 2017/2018-2nd Round

Width170 logo 1489733649
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJINGA CHUO KIKUU MUM-SECOND BATCH 2017/2018

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOFANIKIWA KUPITA USAILI ULIOFANYIKA CHUO KIKUU DUCE

 
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA MAGOGONI NA TANGA 2017/2018

Tokeo la picha la TANZANIA.GO.TZ
Share:

SABABU KUBWA ZILIZOFANYA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA ZAIDI YA 44000 KUKOSA VYUO VIKUU AWAMU YA KWANZA NA PILI 2017/2018

Habari zenu,

Kwa mara nyingine tena baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika,tumerudi kwa kasi isiyopimika.

Leo tunapenda kuzungumzia kuhusu sababu zilizofanya wanafunzi wengi wakose nafasi za kuchaguliwa vyuo vikuu katika awamu ya kwanza na ya pili 2017/2018.

Awali kabla ya yote mfumo wa udahili ulikuwa chini ya TCU kwa miaka kadhaa hapo nyuma ambapo wanafunzi walikuwa wakiomba kupitia TCU,kwa mwaka huu ahali imekua tofauti baada ya wanafunzi ana wazazi wengi kulalamika kuwa TCU imekuwa ikiwapangia vyuo ambavyo hajachagua na kuifanya serikali kuelekeza kuwa sasa wanafunzi wataomba vyuo moja kwa moja chuoni.

Nikianza na hili,TCU imekuwa ikipangia watu vyuo vikuu ambao walikua na sifa ndogo ,Kwa mfano mtu una E E ambazo ni minimu qualification za kujiunga chuo na umeomba vyuo vya 5 lakini kutokana na ushindani unakosa chuo hivyo TCU wanaamua ili usikose chuo wanakupangia kozi yoyote ambayo itakufaa chuoni.

Watu wengi walilalamikia hili bila kujua dhumuni la TCU kufanya vile wakati ule,sasa wanafunzi wameomba moja kwa moja chuoni kozi mbalimbali na imekua ni kilio kikubwa sana kwa sababu vyuo vimekua (hasa vyenye majina makubwa) vikidahili wanafunzi wenye maksi za juu tu. na kuwafanya wanafunzi wengi hasa wenye sifa za kwenda chuo kikuu namaanisha D D AU C E kukosa nafasi katika kozi walizoomba.

SABABU KUBWA iliyowafanya wanafunzi wengi wakose vyuo ni ushindani mkubwa uliopo katika kozi husika na vyuo husika walivyoomba wanafunzi.

Kwa takwimu za haraka ni kwamba asilimia zaidi ya 80 ya wanafunzi walioomba vyuo mwaka huu walioomba vyuo kama SUA,UDSM,DUCE,MUCE,SAUT,UDOM na MUHAS  na kuvifanya vyuo hivi vichukue wanafunzi wenye ufaulu wa juu na wengi wao kukosa.

Hivyo ninazidi kuwashauri wanafunzi ambao bado hawajapata vyuo vikuu waombe vyuo ambavyo ambavyo wanadhani havina ushindani kuliko kukosa chuo na kukaa nyumbani,kwa sababu maisha ya mtaani ni magumu sana na huwezi jua  mwakani vigezo vikawaje.

Na kwa wale waliopata kuchaguliwa nawapongeza na kuwasihi wakasome kwa moyo wote na wakelewe darasani ili elimu watakayoipata waje waitumie mtaani kujiajiri.

Taarifa hii imendaliwa na 
MMILIKI WA MASWAYETU BLOG
(Blooger boy)

Share:

UDSM Kusomesha Wanaopatwa Majanga

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeanzisha utaratibu wa kuwasomesha wanafunzi wasiojiweza kifedha, wakiwamo wanaoshindwa kulipia ada na malazi baada ya wazazi au wategemezi wao kufariki dunia.
Hayo yalielezwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Rwekeza Mukandala alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum na Nipashe ofisini kwake chuoni hapo jana.
Prof. Mukandala (64), alisema kuna wakati mwanafunzi hujiunga na chuo hicho na kujitegemea kwa ada na malazi, lakini katikati ya masomo wazazi au walezi wake wakafariki dunia, hivyo kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu.
Kutokana na changamoto hiyo, alisema UDSM kupitia baraza lake la chuo imekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi hao wachache wanaopatwa na majanga hayo.
"Kunakuwa na wanafunzi wanakuwa na shida sana, labda alikuja anajitegemea, wazazi wake ghafla wanakufa, Chuo kupitia baraza lake kimekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi hao wachache wenye shida kubwa ya kujikimu juu ya maisha," alisema Prof. Mukandala.
Alisema baraza hilo liliamua kwa mwanafunzi halali ambaye ameshadahiliwa kila kitu na baadaye baadhi ya majanga yakamtokea katika maisha yake na kumuathiri kimasomo, ili asiathirike zaidi kwa kushindwa kupata chakula na huduma nyingine, chuo kitampa msaada.
"Haswa pale mwanafunzi anakuja analia, sijala, baba mama wamekufa, wengine wanakuja hapa wazazi wao wamekufa kwenye ajali, wengine wamepata matatizo mbalimbali," alisema na kufafanua zaidi:
"Huko nyuma tulikuwa na uwezo wa kuwasaidia kwa kutoa fedha zangu mfukoni, lakini kwa sasa chuo kina utaratibu uliopitishwa na baraza kwa kuwasaidia wanafunzi waliopata shida ambazo haziwezi kutafutiwa ufumbuzi kwa haraka na kwa muda mfupi."
Alisema fedha wanazopewa wanafunzi hao na chuo kikuu hicho kikongwe zaidi nchini ni msaada na hivyo hazirejeshwi na wahusika hawawekwi kwenye orodha ya watu wanaopaswa kurejesha mikopo ya Bodi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ya Nipashe na mtaalamu huyo wa sayansi ya siasa:
SWALI: Usumbufu katika kupata mikopo ndiyo tatizo namba moja la wanafunzi wa elimu ya juu kwa sasa. Kwa uzoefu wako kama mkufunzi lakini pia kama mtawala, ni vigezo gani vinaweza kuwa mwarobaini na mkanganyiko uliopo?
Prof. Mukandala: Nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania zinatambua haja ya kutoa elimu kwa wananchi wake.
Serikali ya Tanzania kwa awamu mbalimbali imeliona hilo, kwamba baada ya matatizo mbalimbali yaliyokuwa yanajitokeza ikaleta sera ya mikopo, msingi wake ukiwa ni wanafunzi wapewe mkopo kisha watarejesha baadaye wakishahitimu.
Baada ya kuanzisha sera hiyo, kulikuwa na changamoto nyingi mojawapo ni wanafunzi waliokuwa wanahitaji mkopo kuwa wengi, huku fedha kuwagawia wanafunzi ziakiwa ni kidogo
Hapo mwanzo wa sera hiyo kulikuwa na tatizo kubwa la mchakato wa namna ya kuwapata wanafunzi halisi wenye shida ya mkopo.
Walengwa ambao ni watoto wa maskini na wasio na wazazi ndiyo walihitajika wapate mikopo. Hapo ndipo matatizo yakaanza, hapo ndipo kulikuwa na mtafaruku na kutoelewana na uzembe.
Kwa serikali ya awamu ya tano hatua zimeshachuliwa za kuongeza pesa. Pia serikali imeshapitia vigezo kuhakikisha wale walengwa ambao ni watoto wa maskini na yatima wanapata mikopo.
Kitu ambacho wananchi wanapaswa kufahamu ni kwamba, serikali haisaidii elimu kupitia utoaji wa mikopo tu. Kwa vyuo vya umma serikali inagharamia pia kulipa mishahara yote ya watumishi, majengo makubwa yote ya vyuo vikuu yanajengwa na serikali, aidha kupitia mikopo au pesa ya moja kwa moja.
Kwa mwaka uliopita vijana wengi walipata mikopo kwa kozi zilizopewa kipaumbele, hata zile ambazo hazikuwa katika kipaumbele wanafunzi wake walipewa mikopo kwa asilimia mbalimbali.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) nayo imefanya makusanyo kwa wadaiwa, hali itakayosaidia serikali kutoa zaidi mikopo kwa wanafunzi wengine.
SWALI: UDSM ndiyo chuo kikuu namba moja kwa ubora wa elimu ya juu nchini. Matatizo yanayozunguka elimu hiyo kwa sasa, ikiwamo usumbufu katika upatikanaji wa mikopo, yanatishia nafasi hiyo kwa kiasi gani?
Prof. Mukandala: Masuala ya uwezo wa kulipia gharama za masomo kwa wanafunzi ni changamoto iliyopo dunia nzima.
Hata kampeni za urais Marekani zilizofanyika hivi karibuni walikuwa wanazungumzia masuala ya namna ya kutoa elimu kwa watu binafsi na taasisi za serikali.
Chuo ni lazima kiwe na mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo kwa kushirikiana na wadau wote serikali na vyama vya wanafunzi. Serikali wanatoa miongozo na vigezo, bodi ya mikopo wanatekeleza hilo.
Sisi kama uongozi wa chuo tunajaribu kufuatilia na kuhakikisha kwamba huo utekelezaji unakwenda vizuri na hakuna mtu anayeonewa na kila mtu anayestahili anapatiwa mkopo.
Kwa wanafunzi ambao wanajilipia wenyewe chuo kina utaratibu wa kuwawezesha kulipa kidogo kidogo, lengo likiwa ni kuwawezesha kumaliza masomo yao.
Imeandikwa na Gwamaka Alipipi na Sanula Athanas >>NIPASHE
Share:

Monday 16 October 2017

Centre for Foreign Relations-CFR: Candidates Selected for Bachelor Degree 2017/2018

Image result for cfr ac tz
Share:

Tumaini University Makumira: Majina ya Walio-CONFIRM pamoja na "ADMISSION LETTER" Zao 2017/2018

Share:

Ardhi University: Applicants selected to undertake various Postgraduate Programmes for 2017/2018 Academic year

Share:

BREAKING NEWS:TCU IMETANGAZA AWAMU YA 3 YA KUTUMA MAOMBI 2017/18

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa Awamu ya Pili ya
Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali
ulimalizika tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa
sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu
kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba 2017. Tume inapenda kusisitiza yafuatayo:
a) Awamu hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na
ya Pili kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
 
b) Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara moja
kwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika;
c) Awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma
maombi katika awamu mbili zilizopita);
d) Waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo
kimoja hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18
e) Waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa
masuala yote yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU.
f) Waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao.
Aidha, Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha
ni ule ule uliotumika katika awamu mbili zilizopita za Udahili.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania


Share:

NACTE:HAYA HAPA AJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VYA AFYA NA UALIMU NGAZI YA DIPLOMA NA CHETI AWAMU YA PILI 2017/18

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 16.10.2017

Share:

Sunday 15 October 2017

TANGAZO KUTOKA TAMISEMI KWA WALIMU WOTE WA ARTS WANAOTAKA KUHAMA 2017

Image result for NEMBO YA TAIFA
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger