Thursday 19 January 2017

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARY TAREHE 19.1.2017

Share:

JESHI LA SENEGAL KUIVAMIA GAMBIA USIKU WA KUAMKIA LEO ILI KUMNG'OA RAIS YAHYA JAMMEH ALIEOGOMA KUACHIA MADARAKA

Jeshi la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha Jammeh ambayo ni leo  ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi uliopita.

Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz yuko nchini Gambia kwa kile kilichotajwa kuwa ni juhudi za mwisho za kumshauri bwana Jammeh kuachia madaraka kwa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal.

Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
Chanzo: BBC
Share:

Wednesday 18 January 2017

AUDIO | Bill Nass Ft. Mwana FA - Mazoea | Download

Share:

Tuesday 17 January 2017

Nogesha Upendo Ya Vodacom Yaja Na Tsh Bilioni 32 Za M-pesa

Wakati wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.

Awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio hilo kampuni hiyo  imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja wetu.

“Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.

Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200 washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.
Share:

Magazeti Ya Leo Jumanne ya January 17 2017


Share:

Monday 16 January 2017

HII HAPA TAARIFA KAMILI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016


Share:

Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya January 16 2017




Share:

Sunday 15 January 2017

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger