Wednesday 30 November 2016

Tanzia: RPC Singida afariki dunia

x
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Peter Kakamba, amefariki dunia  usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua maradhi ya tumbo, Jeshi la Polisi limethibitisha.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo amesema Kamanda Kakamba amefia hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital iliwasiliana na Kaimu Kamanda Towo kupata uthibitisho wa taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii mapema leo kuwa SACP Kakamba ameaga dunia, baada ya kukosa ushirikiano kutoka kitengo cha mawasiliano cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyokuwa inasambazwa kupitia mtandao wa WhatsApp mapema asubuhi, ilimnukuu Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu akisema: “IGP anasikitika kutangaza kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Peter Kakamba kilichotokea usiku wa saa nne katika Hospitali ya Muhimbili DSM.

Kamanda Kakamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa maradhi ya tumbo alikuwa amefanyiwa operesheni hivi karibuni.”

Kwa mujibu wa Towo, mwili wa marehemu Kakamba utawasili Singida kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Rukwa kwa ajili ya maziko.
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2017

 Image result for TANZANIA GO.TZ

 Kwa majina;

MKOA WA ARUSHA  >>BONYEZA HAPA<<

TUNAENDELEA KUONGEZA MIKOA,TEMBELEA BAADA YA MDA MFUPI

MASWAYETU BLOG TEAM! 
Share:

Ajali ya Gari Yaua Watu 6 rukwa

Watu  sita wakiwamo mfungwa na wanafunzi wamekufa huku wengine wanane
Share:

Magazeti ya Leo Jumatano NOV 30 2016



Share:

FAHAMU JINSI FEDHA ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA ZILIVYOTUMIKA




Ndugu zangu kama ambavyo tunakumbuka Tarehe 10/09/2016 majira ya saa 9 na dakika 27 Alasiri maeneo ya Kanda ya ziwa hasa Mkoani Kagera kulitokea tetemeko la ardhi linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter ambapo Kitovu cha
Share:

HIZI HAPA KURASA ZA NDANI ZA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER TAREHE 30.11.2016

Share:

Tuesday 29 November 2016

Ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya Brazil imeanguka

Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 76 wamefariki dunia huku watano wakipona.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.

Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
Share:

Batch 9 Allocations for the 2016-2017 SUA Continuing Freshers Students Receiving Loan from HESLB

Share:

ASILIMIA 95 YA DARASA LA SABA WAENDA SEKONDARI, 28,638 WAKOSA SHULE 2017


WANAFUNZI 526,653 sawa na asilimia 94.8 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza huku 28,638 wakishindwa kupangiwa shule katika awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 268,052 sawa na asilimia 94.5 ya wasichana waliofaulu na wavulana ni 258,601 sawa na asilimia 95.2 ya wavulana waliofaulu. Wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2016 walikuwa 795,739, huku 244 wakifutiwa matokeo ya mtihani kutokana na udanganyifu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana mjini hapa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema wanafunzi waliochaguliwa wamegawanyika katika makundi manne likiwemo la shule za bweni kwa wenye ufaulu mzuri ambao waliochaguliwa ni 900 wavulana 480 na wasichana 420.
Alisema kwa shule za bweni za ufundi waliochaguliwa ni 1,005, shule za bweni kawaida ni 780, shule za bweni kwa wenye ulemavu ni 723 na shule za kutwa wanafunzi waliochaguliwa ni 523,245. Alisema jumla ya wanafunzi 3,408 sawa na asilimia 0.6 wamechaguliwa kwenda sekondari za bweni.
Jumla ya watahiniwa 555,291 walifaulu sawa na asilimia 70.36 ya wanafunzi waliofanya mtihani, kati yao wasichana ni 238,753 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 271,538 sawa na asilimia 48.9.
Ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 ukilinganisha na asilimia 67.84 kwa mwaka 2015. Simbachawene alisema katika uchaguzi huo, wanafunzi 28,638 hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza, na kuitaja mikoa ambayo wanafunzi wamebaki ni Dar es Salaam (18,820), Arusha (4,752), Songwe (1,465), Kigoma (1,208), Manyara (1,141), Lindi (608), Mbeya (406) na Katavi (238).
Aidha, waziri huyo alisema kati ya wanafunzi 1,060,588 walioanza darasa la kwanza 2010, wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2016 ni 795,739 sawa na asilimia 75 ya wanafunzi walioandikishwa wakiwemo wasichana 422,562 sawa na asilimia 53.1 na wavulana 373,177 sawa na asilimia 46.9 ya waliosajiliwa.
Akizungumzia udanganyifu, alisema watawavua madaraka kwa waliokuwa waratibu elimu kata na walimu wakuu, kuwashitaki mahakamani na kupeleka mashauri yao Tume ya Utumishi ya Walimu, baada ya udanganyifu kuongezeka ambako watahiniwa 244 wamefutiwa matokeo mwaka 2016 ikilinganishwa na wanane wa mwaka jana.
Alizitaja shule zilizohusika kwenye udanganyifu huo ni Shule ya Tumaini na Little Flower za Sengerema mkoani Mwanza, Mikahamakumi iliyopo Sikonge, Tabora ambazo ni za binafsi, wakati za serikali ni Kondi Kasandalala iliyopo Sikonge, Tabora, Qash iliyopo Babati na St Getrude iliyopo Madaba mkoani Ruvuma.
Aidha, alisema 10 bora za serikali ni Kazunzu iliyopo Halmashauri ya Buchosa (Mwanza), Mwanahegele ya Maswa (Simiyu), Huruma ya Mbinga (Ruvuma), Kabanga ya Ngara (Kagera), Butumba B (Jiji Mwanza), Masoko ya Kilwa (Lindi), Lyambamgongo ya Bukombe (Geita), Kilimani ya Geita Vijijini, Magufuli ya Chato na Nkome ya Geita Vijijini, Geita.
Alisema shule 10 zilizofanya vibaya ni Chohelo ya Mvomero (Morogoro), ambayo ni ya mwisho kitaifa ikifuatiwa na shule za Iloliento, Longido (Arusha), Mwalebi na Nchilila Meatu (Simiyu), Magingi ya Mvomero, Kilole ya Lushoto, Tanga, Zege ya Korogwe, Tanga na shule tatu za Lubchi, Kitengo na Mgata za Morogoro vijijini.
Share:

Breaking News:HAYA HAPA MAJINA ZAIDI YA 25000 YA WANAFUNZI FORM 6 WALIOCHAGULIWA KWA MUJIBU WA SHERIA KUJIUNGA VIKOSI MBALIMBALI VYA JKT AWAMU YA PILI 2016







Kama utahitaji kuangaliziwa jina lako/AU la ndugu yako kwa "usahihi" na "kasi ya ajabu" (ambapo utajibiwa ndani ya mda mfupi) kama umechaguliwa kujiunga na jkt na kambi uliyopangwa. tafadhali fanya yafuatayo;
Share:

HIZI HAPA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOV 29 2016

KURASA ZA MICHEZO LEO

Share:

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU WANAFUNZI WA DIPLOMA KUTOKWENDA DIGRII CHUO KIKUU

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetoa ufafanuzi kwamba haijapiga marufuku watu wenye Stashahada wenye sifa kujiunga na vyuo vikuu badala yake
Share:

Wizara ya Elimu imekanusha kuhusu kuzuia wenye Diploma kwenda chuo kikuu

Image result for TANZANIA.GO.TZ
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBER TAREHE 29.11.2016

Share:

Monday 28 November 2016

Rais Magufuli Apokea Marais Wawili Ikulu Jijini Dar es Salaam

Share:

Picha: Makonda Atinga 'Uwanja wa Fisi' Wanapojiuza Madada poa,Atangaza kuvunja nyumba zote


Share:

SERIKALI Yapiga Marufuku Kusoma Degree Bila Kupita Form Six



Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katikals mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger