Friday 23 September 2016

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU UDOM 2016/2017

Share:

MPYA:TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU USHIRIKA 2016/2017

MoCU logo
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI-TEKU 2016/2017

Share:

UDOM:HII HAPA RATIBA YA SUPPLIMENTARY EXAMS 2015/2016

 Logo
CHSS & CBSL SUPPLEMENTARY_SPECIAL EXAMINATION TIMETABLE FOR 2015_2016 FINAL
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO CHA ST.FRANCIS-IFAKARA 2016/2017

Share:

Mhadhiri chuo kikuu mbaroni kwa kumkashfu Rais Magufuli


Idadi ya watu wanaokamatwa kwa tuhuma za kumkashfu Rais John Magufuli kupitia mitandao ya kijamii imezidi kuongezeka baada ya polisi kumkamata Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa (Muce), Dk Oscar Magava (48).

Dk Magava amekuwa mtu wa kumi kukamatwa na polisi katika kampeni za jeshi hilo kudhibiti uhalifu chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema Dk Magava alikamatwa akiwa Sumbawanga na alirudishwa mkoani Iringa.

Mjengi alisema Septemba 15, mwaka huu walipata taarifa kuwa mhadhiri huyo anatumia mitandao ya kijamii kumkashfu Rais. Alisema waliamua kumsaka na walipopata taarifa kuwa Dk Magava amekwenda Sumbawanga waliwasiliana na polisi wa huko wakamkamata na kumrudisha Iringa.

Hata hivyo, Kamanda Mjengi hakuyataja maneno aliyotumia Dk Magava kumkashfu Rais kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kamanda Mjengi aliwatahadharisha wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuitumia kwa ajili ya maendeleo na si kutukana wala kukashfu viongozi au watu wengine.

Watu mbalimbali wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumkashifu Rais au jeshi la polisi.
Share:

BAADA YA TCU KUSHUSHA VIWANGO,BODI YA MIKOPO IMEGOMA KUONGEZA MDA WA KUTUMA MAOMBI 2016/2017


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema haiwezi kutoa mikopo kwa waombaji wapya walioomba baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kushusha viwango vya udahili.

Wiki iliyopita, TCU ilitangaza kushusha viwango vya udahili bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, amesema tume  hiyo haiwezi kuongeza muda kwa wanafunzi wapya kwa ajili ya kuomba mkopo kutokana na mchakato huo kufungwa.

Amesema tofauti na tume ya vyuo vikuu ambayo inaweza kufungua udahili na kutoa majina ya wale waliopata nafasi ndani ya siku tatu, HESLB huhitaji muda mrefu kupitia taarifa za waombaji hadi kutoa matokeo.

Kuhusu marejesho ya mikopo kwa wahitimu wa elimu ya juu waliokopeshwa na bodi hiyo, Mwaisobwa amesema idadi kubwa ya wadaiwa na waajiri wamejitokeza kulipa madeni yao na kuhakiki taarifa za madeni yao.

“Idadi kubwa ya wadaiwa wamejitokeza kulipa na kuhakiki taarifa zao, pia hata waajiri wengi wamejitokeza na kuthibitisha hili ni kwamba mapato tuliyokusanya yameongezeka kwa kiasi kikubwa” amesema Mwaisobwa.

Amesema wanaokaidi kulipa, watambue kuna sheria zitakazowabana, ikiwa ni pamoja na vifungo na penati, lakini hilo halitangulizwi bali mpaka mkopaji aonekane kukaidi.
Share:

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa TTC,Amteua Bw. Waziri Waziri Kindamba Kuchukua Nafasi Hiyo


Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Bw. Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo tarehe 23 Septemba, 2016.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Septemba, 2016
Share:

Scholarships for Masters and Doctorate programmes tenable in the Republic of Korea

Share:

Serikali yaonya dhidi ya kampuni za ajira Zinazotapeli Watu


WIZARA ya Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu imetaka wananchi kuepuka kampuni za uwakala wa ajira nchini ambazo hutangaza nafasi za ajira huku zikiwataka waombaji kulipia ili kusailiwa.
Msemaji wa Wizara hiyo, Ridhiwan Wema jana alisema kampuni za namna hiyo hawazitambui na hivyo hazina usajili wa kufanya shughuli hiyo nchini.
“Hizi kampuni sisi hatuzitambui, mtafuta kazi hatakiwi kutozwa fedha isipokuwa kampuni inaingia makubaliano na mwajiri ambaye amempa kazi ya kumtafutia wafanyakazi,” alisema Wema.
Alitaka wananchi wawe makini na wasikurupuke kutuma maombi kabla ya kujiridhisha kama kampuni zimesajiliwa na ili kupata taarifa sahihi, mwombaji anaweza kufika Wizara ya Kazi na kuuliza, kwa kuwa wao ndio wasajili pia wakibaini uwepo wa kampuni hizo watoe taarifa wizarani na Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Aidha, aliwasihi wananchi hususan vijana, wasiwe wepesi kulipia gharama, kwa sababu huduma ya ajira haipaswi kutozwa fedha kwa kuwa si haki kutoa kazi kwa masharti ya kulipwa, hali ambayo inaashiria vitendo vya rushwa.
Wema alibainisha kuwa kampuni zinazofanya shughuli za uwakala wa ajira nchini zimesajiliwa na Wizara ambapo moja ya masharti yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kutowatoza waombaji wa nafasi za ajira zinazotangazwa.
Alisema kuna vigezo vingine pia vinavyozingatiwa, ili kukidhi usajili ambapo huainishwa kwa majina na taarifa za mahali pa kudumu zilipo ofisi za kampuni na kufahamu kama zimesajiliwa kwenye mamlaka husika, mfano Brela, hayo yote ni kwa ajili ya kufanya urahisi wa kizifuatilia pindi kunapozuka utata.
Aliongeza kwamba vigezo vingine ni kujiridhisha kama ina wataalamu wa kutosha kwenye masuala ya ajira, ambapo baada ya kujiridhisha husajiliwa na kuzitangaza kwenye vyombo vya habari.
Wema alitaka wananchi watambue kuwa kampuni zinazotangaza nafasi za ajira huku zikitaka waombaji walipie fedha kwa ajili ya usaili si salama kwao, hivyo wanatakiwa kuepukana nazo na kutoa taarifa.
Nuh Yusuf ambaye ni Ofisa wa kampuni ya Zoom ambayo ni wakala wa ajira nchini, alisema sababu kubwa ya kuendelea kwa utapeli wa mtandao ni kukosekana kwa ushikiano wa karibu na vyombo vya sheria hususan Jeshi la Polisi katika kudhibiti suala hilo.
“Tumejaribu kufuatilia suala hilo TCRA kitengo cha TZ-CERT, tukashauriwa twende Polisi na mmoja ambaye alipatwa na hilo tatizo, tulipofika kituo cha Polisi cha Oysterbay hawakuonesha ushirikiano wowote,” alisema Yusuf
.
Share:

Rais Magufuli ateua viongozi wa juu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)

Share:

HIZI HAPA KURASA ZA NDANI ZA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBER 23 2016

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBER TAREHE 23.9.2016




Share:

Thursday 22 September 2016

Bodi ya vyombo vya habari vya CCM - gazeti la Uhuru publishers yajiuzulu

upload_2016-9-22_15-22-53.png
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 337 WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU ARUSHA UNIVERSITY 2016/2017

Share:

UDOM:APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES

 Logo

APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES

The University of Dodoma (UDOM) wishes to announce the names of candidates selected for admission into various PhD programmes for the academic year 2016/17.
Admission letters for successful candidates are available in UDOM Graduate studies offices at the main administration building, Office No. 124, Third Floor.
For enquiries please visit UDOM Graduate studies offices at the main administration building, Office No. 131,Third Floor or send email through udomgsce@yahoo.com

List of Successful PhD Applicants 2016-2017 BATCH II
Share:

MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017



Image result for TCU.GO
Habari yako,

Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger