Friday 26 February 2016

TANZIA:MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU SUA Bsc.IRRIGATION AND WATER RESOURCE ENGINEERING AMEKUTWA KAFARIKI KATIKA PORI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ipatapo jana mida ya saa 9 jioni nilipata meseja ikisema  kwamba kuna mwanafunzi kakapotea ni mwaka wa kwanza kozi ya irrigation engineering-sua,wenzako wanaekaa nae room walisema kwamba mwenzao alikuwa ni mgonjwa hivyo siku hiyo aliondoka tangu asubuhi na laiacha simu yake ndani na wakidhani ameenda sehemu ya karibu,hadi kufikia mida ya jioni alikuwa hajarudi.
Leo mida ya mchana huu nimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa hostel zao Mr.hatibu Kilenga ambae amesema kwamba;

"Kwa masikitiko makubwa  napenda kuwajulisha ndugu wana SUA wanafunzi wote ,waafanyakazi na watu wote kwamba leo asubuhimajira ya saa tano asubuhi baada ya heka heka za kumtafuta ndugu yetu YEREMIA MBENDULE,hatimae tumemkuta katika pori la uwanja wa suaakiwa tayari amefariki dunia,tukiwa na polisi tunampeleka marehemu hospitali ya mkoa wa morogoro kwa taratibu nyingine.
Namshukuru Rais wa chuo Mr.Ndunguru,makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mr.Salim na wanafunzi wote kwa ujumla kwa jitihada za kumtafuta mpendwa wetu"
Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!AMEN

Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza kozi ya Bsc.irrigation and resource engineering na jumatatu alikuwa anajiandaa kuanza mtihani wake wa mwiho wa muhula.

Uongozi wa MASWAYETUBLOG unapenda kutoa pole kwa familia ya marehemu.
Share:

Vigogo Watatu Wa Mradi wa Mabasi ya (DART) Wafikishwa Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo, wamepandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5.

Mbali na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na kusomewa mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Walisomewa mashitaka na wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jackline Nyantori akisaidiwa na Estazia Wilson na Stellah Mafuru.

Nyantori alidai kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi 2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5.

Katika mashitaka yanayomkabili Mwakatobe, inadaiwa Juni 29, 2005 katika ofisi za kodi Ilala, Dar es Salaam, alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), wakati akiwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2004 na ya 2005 ya kampuni yake ya Yukan Business, jambo lililosababisha alipe kodi ndogo.

Awali, Wakili Nyantole alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amewasilisha hati ya kuruhusu mahakama hiyo, kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi hivyo washitakiwa wataruhusiwa kujibu mashitaka yao.

Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Takukuru ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hawana pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa.

Hakimu Mwijage alisema Asteria, Katale na Kugesha watapata dhamana endapo kila mmoja atakuwa na mdhamini mmoja anayefanyakazi serikalini au kwenye taasisi inayofahamika, atakayesaini hati ya Sh milioni 15. Pia kila mshitakiwa awasilishe Sh milioni 15 au hati isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 15.

Kwa upande wa Mwakatobe, dhamana yake ipo wazi endapo atapata mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi inayofahamika, asaini hati ya Sh milioni tano.

Wote waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti. Asteria na Katale wametakiwa kuwasilisha hati hizo Machi 3 mwaka huu. Kesi itatajwa tena Machi 9 mwaka huu.
Share:

Basi La Mashimba Express La Kahama- Mwanza Lapata ajali Kuua Watu Wanne

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watu wanne wamefariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo  katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu  Mkoani Shinyanga

Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ilisababishwa  na  gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu  wawili  waliokuwa  katika  gari  hilo  akiwemo  dereva  walifariki  dunia  papo hapo

Mganga mfawidhi wa hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo  walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.

Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi .
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 26 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday 25 February 2016

Download | Millian Ft. Diamond Platnumz - Nyota Ya Mashariki [Audio]

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://my.notjustok.com/track/download/id/71508/by/zWVUMsRAZa

Download | Millian Ft. Diamond Platnumz - Nyota Ya Mashariki [Audio]

https://my.notjustok.com/track/download/id/71508/by/zWVUMsRAZa
- See more at: http://www.johventuretz.com/2016/02/millian-ft-diamond-platnumz-nyota-ya-mashariki.html#sthash.2mlWkRF1.dpuf

Download | Millian Ft. Diamond Platnumz - Nyota Ya Mashariki [Audio]

https://my.notjustok.com/track/download/id/71508/by/zWVUMsRAZa
- See more at: http://www.johventuretz.com/2016/02/millian-ft-diamond-platnumz-nyota-ya-mashariki.html#sthash.2mlWkRF1.dpuf
Share:

Tangazo la nafasi za masomo kwa awamu ya pili ya mwaka wa masomo 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO AWAMU YA PILI – MWAKA WA MASOMO 2015/2016
MKUU WA CHUO – TAASISI YA UHASIBU TANZANIA [TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA)] ANAWAKARIBISHA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2015 NA WALE WALIOMALIZA MIAKA YA NYUMA, KUJIUNGA NA KOZI YA CHETI CHA AWALI YAANI BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE (NTA LEVEL 4) KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 AWAMU YA PILI (SECOND INTAKE) KATIKA KAMPASI ZAKE ZA DAR ES SALAAM, MBEYA, SINGIDA, MTWARA, MWANZA NA KIGOMA KWENYE FANI ZIFUATAZO:-
  • UHASIBU (ACCOUNTANCY)
  • UNUNUZI NA UGAVI (PROCUREMENT & LOGISTICS MANAGEMENT)
SIFA ZA KUJIUNGA NA KOZI ZA CHETI CHA AWALI:
  • Mwombaji awe amefaulu angalau masomo 3 kwa kiwango cha alama “D” au zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne; Au

  • Awe na cheti cha mafunzo ya ufundi daraja la pili (NVA 2) kutoka chuo cha VETA, ambaye pia ana ufaulu wa masomo angalau mawili kwenye matokeo ya kidato cha nne.
FOMU ZA KUJIUNGA NA CHUO ZINAPATIKANA OFISINI NA KWENYE TOVUTI YA TAASISI www.tia.ac.tz. FOMU ZIRUDISHWE KATIKA KAMPASI ZETU.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI IJUMAA TAREHE 04/03/2016.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA:
SIMU Na. 0714 914 805, 0754 376 371; AU
Baruapepe: tia@tia.ac.tz
Share:

HUYU NDIO BABA MZAZI WA MOROMBOSO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Maromboso kutoka Yamoto Band ameamua kumuonyesha baba yake Mzazi baada ya Jamaa mmoja wa Bodaboda Kujitangaza kuwa yeye ndiye Baba Maromboso, Maromboso aliposti Picha na Kuandika “Huyu Ndo Baba yangu …..Mzee Yusuph Kilungi … Sasa huyo jamaa Wa Tegua mtego ” Boda boda anayejita Baba Maromboso ajipange“
Share:

HII NDI NYUMBA MPYA YA MENEJA WA DIAMOND PLATNUZM "BABU TALE"-VIDEO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Meneja wa  Msanii mkali Tanzaia Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa Tiptop Conection, Babu Tale leo amepost video kwenye Instagram yake ikionyesha Mjengo ambao anaumiliki.
Share:

Jibu la Diamond Kwa Wanaosema Ame Copy Video ya ‘Make Me Sing’ Kwa Lil Wayne.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Msanii Diamond ameamua kuwatolea uvivu watu wanaosema kuwa video yake mpya ya wimbo wa make me sing
alioshirikiana na rapper A.K.A kutoka Afrika kusini ameiga video ya Got money ya Lil wayne.

Aidha Diamond amethibitisha ule usemi wa hakuna jipya chini ya jua kwa kusema kuwa hakuna mtu yeyote atayefanya kitu kwenye muziki ambacho hakijafanyika.

“Watu wanashindwa kuelewa,kila kitu ambacho kinafanyika sasa hivi kwenye muziki kuanzia video,mashairi vyote vilishafanyika,vyote vilishaimbwa ,ni kama vinafanyika kwa marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye,kwa sababu ukisema nakupenda watu washaimba,sikupendi washaimba vyote yaani” alifunguka Diamond.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger