Wednesday, 30 September 2026

DKT. YONAZI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UTURUKI


Na, Mwandishi Wetu – Ankara Uturuki

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameupongeza Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki kwa kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kidiplomasia, biashara, uwekezaji, na maendeleo ya kijamii.

Dkt. Yonazi ametoa pongezi hizo alipotembelea Ofisi za Ubalozi huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mjini Ankara, Uturuki iliyolenga kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kuongeza maarifa ya kiufundi na kukuza ushirikiano katika kupunguza vihatarishi vya maafa, kukabiliana na dharura na mifumo ya kurejesha hali kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kiteknolojia.

Dkt. Yonazi amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki unazidi kuimarika kwa kasi kubwa, ukiongozwa na diplomasia ya kiuchumi, miongozo ya kimkakati kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ya Tanzania, pamoja na ziara za kitaifa za viongozi wakuu wa nchi hizo mbili.

Naye Kaimu Balozi Bi. Levina Maleo ambaye ni Mkuu wa Utawala wa ubalozi amempongeza na kumshukuru katibu Mkuu huyo kwa kutembelea ofisi za Ubalozi na kueleza kuwa wataendeleza mashirikiano yaliyopo kati ya nchi hizo mbili na kuendelea kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa za elimu, afya na kijamii.
Share:

WRRB YAKUTANA NA WAENDESHA GHALA KUWEKA MAMBO SAWA KABLA YA MSIMU WA KOROSHO



Na.Mwandishi Wetu.

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imefanya mazungumzo na Umoja wa Waendesha Ghala kujadili mazingira ya kiutendaji ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika kuelekea Msimu wa Korosho 2026/27 unaotarajiwa kuzinduliwa Oktoba 12, 2026.

Kikao hicho kimefanyika leo Septemba 29, 2026 jijini Dodoma kimeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu na kuhudhuriwa na viongozi wa Umoja huo pamoja na Watalaamu wa Bodi hiyo, ili kutafuta ufumbuzi wa hoja mbalimbali walizoziibua hivi karibuni.

Miongoni mwa mambo waliyokubaliana katika kikao hicho ni kuzingatia matakwa ya mwongozo wa msimu wa korosho 2026/27 na kwamba masuala yaliyoibuka kinyume na matakwa hayo hayatumika.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw.Bangu amesisitiza ghala zitakazokidhi vigezo stahiki ndio zitapewa leseni katika msimu huo ili kuhakikisha korosho ghafi inahifadhiwa kwenye ghala bora hasa ikizingatiwa kuwapo na tahadhari ya mvua za El nino.

"Maghala yasiyo na viwango yatakataliwa hii ni kutokana tahadhari za mvua za El nino tunataka korosho yetu isiathiriwe na ubora, tunawahimiza wakulima wahakikishe korosho inakaushwa vizuri kulingana na vigezo vya unyevu vilivyowekwa,"amesema.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Abdulkarim Masoud ameishukuru WRRB kwa kukutana nao na kujadili malalamiko yao ambayo yatawezesha kupata ufumbuzi na kuendelea na msimu huo.

"Hatujafanya hivi kuharibia mtu bali ni njia ya kutafuta ufumbuzi wa malalamiko yetu ili msimu wa korosho ufanyike kwa ufanisi,"amesema.





Share:

NEMC YATOA MAAGIZO MATATU KWA WAISHIO MABONDENI MKOA WA MOROGORO


-Ni kufuatia tahadhari za mvua za El niño zinazotarajiwa kunyesha nchini

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa maagizo matatu kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuhama maeneo ya mabondeni, kusafisha mitaro, kuepuka ukataji miti kiholele sambamba na Utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa ni tahadhari za mvua za El niño zinazotarajiwa kunyesha nchini.

Wito huo umetokewa na Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bw. Elibariki Bajuta wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyofanyika tarehe 28 na 29 Septemba 2026 iliyoongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe mhandisi Hamad Yusuf Masauni iliyolenga kukagua maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Mvua za El niño Mkoani humo.

Akizungumza na wananchi mara baada ya ziara hiyo, Mhe. Waziri Masauni Hamad Masauni

amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha wananchi wanaishi katika Mazingira salama dhidi ya maafa huku akizitaka Taasisi ushirikishwaji wa Jamii wakati wa ujenzi wa miundombinu kama vile mifereji na makaravati ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Aidha, Mkurugenzi Bajuta amesisitiza wananchi kudhibiti matumizi ya Mifuko ya plastiki ambayo inachangia Kwa kiasi kikubwa kuziba Kwa mitaro ya kupitisha maji.

Maeneo yaliyokaguliwa katika ziara hiyo ni pamoja na eneo la ujenzi wa tuta la Reli ya SGR katika eneo la Mkundi hadi Lukobe, Mto Diwale (Kata ya Kichangani - Turiani), Eneo la Dumila (Mto Kikundi), Mto Mkondoa- Kidete Kata ya Kasiki pamoja na mto Mto Lumemo- Halmashauri ya mji wa Ifakara huku ikishirikisha TRC,Bodi ya Maji ya Bonde, TARURA, TANROAD, pamoja na Halmashauri za Morogoro mjini, Kilosa, Mvomero na Ifakara.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 30, 2026




Magazetini Leo





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger