Wednesday, 26 November 2025

NI MPANGO MCHAFU; NIA NI KUHUJUMU UCHUMI NA MAISHA YA WATANZANIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefichua kwamba vurugu za Oktoba 29 hazikuwa tu uharibifu wa mali, bali zilikuwa ni jaribio lililopangwa la kuhujumu na kuua uchumi wa nchi na kudhoofisha maisha ya Watanzania mmojammoja.

Akizungumza kwa hisia, na wahariri na waandishi wa habari waandamizi jijini Dar es salaam,Dkt. Mwigulu alieleza jinsi wahuni hao walivyolenga miundombinu muhimu.

"Mpango uliwekwa pasiwe na miundombinu ya hawa watu kusafiri. Walipanga kuchoma stendi ya mabasi ya Magufuli, kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi na reli ya SGR. Hizi siyo mali za Serikali, ni mali za umma," alisema.

Alisisitiza kuwa uharibifu huo uliathiri maisha ya kila siku ya Mtanzania: "Maisha ya Mtanzania mmojammoja yanahusisha mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kujipatia riziki zao. Hawa watu wasipotoka unataka wale nini?"

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kusisitiza kwamba fedha zinazotekeleza miradi mikubwa—kama vituo vya DAWASCO, barabara, na zahanati—si za Serikali, bali ni za Watanzania.

"Ukinunua shati kuna sehemu unapeleka kujenga barabara, unakuwa umetenga sehemu ya kutumia na sehemu umejinyima ili kuchangia maendeleo ya nchi. Hivyo unapochoma kituo cha DAWASCO kinachowapa maji safi na salama, unataka hawa watu waishije?" alihoji Waziri Mkuu, akionyesha jinsi hujuma inavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja.

Aliwataka watanzania kuelewa njama za makusudi zinavyopangwa ili kuvuruga mfumo wa maisha na kudidimiza maendeleo yaliyopatikana nchini.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 26, 2025

Share:

Tuesday, 25 November 2025

SIMBA SC YAKUBALI KIPIGO NYUMBANI DHIDI YA PETRO ATLETICO DE LUANDA



Klabu ya Simba SC imepoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo, Novemba 23, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 78 na kiungo Benardo Oliveira Dias, maarufu kama “Benny”, akiipatia Petro Atletico ushindi muhimu ugenini.

Simba ilijitahidi kusaka bao la kusawazisha katika dakika za mwisho, lakini ukuta wa Petro ulibaki imara huku kipa wao akifanya kazi ya ziada kuzuia jaribio la mwisho la Moses Phiri.

Kwa matokeo haya, Wekundu wa Msimbazi wanalazimika kusaka ushindi katika michezo yao ijayo ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 25, 2025


 














Share:

Monday, 24 November 2025

DKT. TUTINDAGA GEORGE WA KISIWA CHA SAANANE ATWAA TUZO YA UBUNIFU WA MAZAO YA UTALII



Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, akionesha Tuzo yake ya Ubunifu wa Mazao ya Utalii.


Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, Kamishna Msadizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, akipokea Tuzo ya Ubunifu wa Mazao ya Utalii, jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, ametunukiwa Tuzo Maalum ya Ubunifu wa Mazao ya Utalii, ikiwa ni sehemu ya Top 100 Executives List Awards 2025.

Hafla ya utoaji tuzo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 20, 2025, ambapo Dkt. Tutindaga alitangazwa kuwa “Chief Innovation/Head of Product Design and Innovation of the Year.”
 
MAZAO YA UTALII ALIYOYABUNI

Baadhi ya mazao mapya na maboresho aliyoyaendeleza katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane ni pamoja na:
Boat Safari katika Ziwa Victoria, Rock Hiking, uimarishaji wa maeneo ya mapumziko (picnic sites), michezo ya majini, kutazama machweo ya jua, na uboreshaji wa huduma za malazi ya kitalii.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo, Dkt. Tutindaga aliwashukuru wageni waliohudhuria na kuendelea kuwakaribisha wananchi kutembelea Hifadhi ya Saanane.

“Nashukuru sana kupata nafasi hii. Kama Mhifadhi, naendelea kuwakaribisha kutembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane,” alisema.

Aidha, alimshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Musa Kuji, kwa kuwawezesha viongozi wanawake kufanya ubunifu katika majukumu yao.

“Tuzo hii ni heshima kwa uongozi mzima wa TANAPA. Tumepata fursa ya kufanya ubunifu katika maeneo mbalimbali, na leo imeleta matokeo haya,” aliongeza.

Hifadhi zetu ni urithi wa thamani kwa Taifa. Kutembelea vivutio vya TANAPA kunachangia uhifadhi, uchumi na maendeleo ya jamii.

Tanzania ni mahali pa kuvutia karibu tutembelee hifadhi zetu!
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger