Friday, 3 January 2025

Video Mpya : BHUSHEMELI - MWAKA WA MAFANIKIO

Share:

Video Mpya : SUMBI MDOGO vs NGELELA - NGOMA LIVE

Share:

Thursday, 2 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 3, 2025

Magazeti


         
Share:

KAYA 16,275 KUNUFAIKA NA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU MKOANI MTWARA


-Wananchi wahamasishwa kuchangamkia fursa

-Wamshukuru Rais Samia kwa programu hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka mradi wa majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% kwa wananchi wa maeneo ya vijijini mkoani humo.

Ametoa shukrani hizo Januari 2, 2025 Ofisini qkwake Mkoani Mtwara wakati wa utambulisho wa mradi na mtoa huduma atakayesambaza majiko hayo mkoani humo ambaye ni Kampuni ya Taifa Gas uliofanywa na Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emanuel Yesaya.

"Tumepokea mradi huu ambao unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya na pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi," alisema Kanali Sawala.

Mhe. Kanali Sawala alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua majiko hayo ya ruzuku.

"Mhe. Rais anawapenda wananchi wake, ametuletea mradi nasi tuupokee na tumuunge mkono kwa kununua majiko haya ya ruzuku ili kulinda afya zetu sambamba na kuimarisha mazingira kama alivyoazimia," alisisitiza Kanali Sawala.

Aidha, alitoa wito kwa REA na Taifa Gas kuhakikisha wanashirikiana na viongozi katika maeneo yote ili waweze kuufahamu mradi na hivyo kurahisisha utekelezaji wake.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi, Mhandisi Yesaya alisema REA inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia 2024-2024 kupitia programu mbalimbali ili kufanikisha azma ya Serikali ambayo muasisi wake ni Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na lengo la kulinda afya za wananchi wake pamoja na kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Tunaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unaelekeza ifikapo mwaka 2034; asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi kupikia," alifafanua Mhandisi Yesaya.

Alisema jumla ya majiko ya gesi 16,275 ya kilo sita pamoja na vifaa vyake yatasambazwa katika wilaya tano za Mkoa wa Mtwara ambazo ni Mtwara, Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba ambapo kila wilaya itapata majiko 3,255 na mwananchi atalipia shilingi 19,500 tu na kwamba gharama nyingine imebebwa na Serikali.

Alisisitiza kuwa mtoa huduma atawajibika kusajili na kuandaa orodha ya wananchi watakaopatiwa majiko hayo. "Majiko haya yatauzwa kwa wananchi wenye vitambulisho vya NIDA au namba inayoweza kuhakikiwa; hakuna mwananchi atakayeruhusiwa kununua mtungi wa ruzuku zaidi ya mmoja," alisisitiza.

Kwa nyakati tofauti wananchi mkoani humo walimshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi huo na waliahidi kumuunga mkono kwa kuendelea kuhamasishana na kuelimishana ili kufikia azma.
Share:

Ngoma Mpya : NYANDA MALIGANYA - NOMA


Hii hapa kazi mpya ya Nyanda Maliganya inaitwa Noma!!
Share:

Wednesday, 1 January 2025

WATENDAJI NGAZI YA MKOA WA RUVUMA WAPATIWA MAFUNZO YA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Na Regina Ndumbaro, Ruvuma

Watendaji wa ngazi ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Wilaya za Mbinga, Nyasa, na Songea wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kusimamia zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Jeshi la Wananchi, Chandamali, na kuhudhuriwa na Hakimu Japhet Bwire Manyama, ambaye alitoa viapo kwa maafisa watendaji hao.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na  Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura na TEHAMA Taifa, Stanslaus Mwita, kwa niaba ya Mheshimiwa Jaji Mstaafu Jacob Mwambegele, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. 

Akizungumzia mafunzo hayo,yaliyoanza rasmi leo, Tarehe 1 Januari 2025M kurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura na TEHAMA Taifa, Stanslaus Mwita, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha watendaji jinsi ya kujaza fomu za uandikishaji na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voter Registration System - VRS) kwa ufanisi. 

"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora. Mafanikio ya zoezi hili yanategemea ushirikiano wa karibu kati ya watendaji wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa, na wadau wengine wa uchaguzi",amesema.

Pia, maafisa wa TEHAMA watapata mafunzo maalumu ya kushughulikia changamoto za kiufundi (troubleshooting) zitakazojitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika vituo vya kujiandikisha.

Mwita ameongeza kuwa mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji wapiga kura, hatua itakayosaidia kuhakikisha uwazi na kupunguza vurugu zisizohitajika. 

Aidha, maafisa wa uandikishaji wamehimizwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa watendaji wa maeneo yao na kubainisha kuwa vitambulisho walivyopewa na Tume ni utambulisho wa kutosha katika maeneo waliopangiwa.


Share:

WAZIRI KOMBO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MAGHARIBI B


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesema kuimarika kwa miundombinu ya Mahakama ni hatua muhimu itakayowawezesha wananchi kupata huduma katika mazingira mazuri, salama na rafiki.

Ameyasema hayo leo Januari 1, 2025 wakati akiweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Magharibi B huko Kisakasaka, Zanzibar.

Balozi Kombo amesema, kwa miaka mingi mahakama zimekuwa na changamoto ya miundombinu ya majengo na Serikali inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi imedhamiria kumaliza changamoto hizo kwa kujenga majengo mapya na ya kisasa.

"Kwa mfano jengo lililokuwa likitumiwa na Mahakama ya Magharibi B pale Mwanakwerekwe lilikuwa finyu mno kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa na kuwapa usumbufu waliofuata huduma mahali pale," alisema Mhe. Kombo.

Waziri huyo ameongeza kuwa, pamoja na ufinyu huo, pia halikuwa rafiki kutokana na kukosekana nafasi kwa ajili ya maofisa wa Mahakama.

Vilevile, kukosekana kwa huduma za watu wenye mahitaji maalumu na maegesho kulisababisha muda mwingi wananchi walikuwa wanazagaa kwa kukosa sehemu tulivu ya kusubiri huduma.

Amesema, hali hiyo ndiyo iliyosababisha Serikali kuchukua hatua za makusudi kuja na mradi wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya mikoa na wilaya Unguja na Pemba.

Pia, amesema ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo saba ambao ulipangwa kufanyika katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Kwa upande wa Unguja, Balozi Kombo amesema, mradi huo wa Loti Nambari 2 unajumuisha majengo manne ambayo ni: Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini, Mahakama ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Mahakama ya Mkoa wa Kusini na Mahakama ya Wilaya ya Magharibi B.

Serikali inaendelea kuwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya majengo ya ofisi, hivyo ni wajibu wa watumiaji wa miundombinu hii na wananchi kwa ujumla kuitunza ili iweze kudumu kwa miaka mingi ijayo.
Share:

BENKI YA CRDB YAFUNGUA MATAWI MAPYA MUGANGO, SIRARI MKOANI MARA

 

Katika kuufunga mwaka 2024 kwa huduma bora, Benki ya CRDB imefungua matawi mapya mawili mkoani Mara yaliyopo Mugango katika Wilaya ya Musoma Vijijini na Sirari wilayani Tarime.


Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa amesema uzinduzi wa matawi hayo ni sehemu ya jitihada za Benki kuiishi kaulimbiu yake ya ‘ulipo, tupo’ kwa kuwafuata wananchi katika kila pembe ya nchi na kuwapa huduma bora za fedha kwa maendeleo yao binafsi na kuchangia uchumi wa taifa pia.
“Mkoa wa Mara una shughuli nyingi za kiuchumi kuanzia migodi mikubwa na machimbo ya madini, uvuvi, kilimo na biashara ya mpakani hivyo ni muhimu kuwa na huduma za uhakika za fedha ili kuwajumuisha wananchi kwengi katika uchumi. Ulikuwa ni mpango wa Benki yetu ya CRDB kuhakikisha tunafungua matawi haya mawili kabla mwaka 2024 haujaisha,” anasema Raballa.


Kabla ya ufunguzi wa matawi hayo mapya, Raballa amesema wananchi wa maeneo hayo walikuwa wanapata huduma za benki kupitia kwa mawakala waliotapakaa maeneo tofauti. Kwa mkoa mzima wa Mara, amesema Benki ya CRDB inao zaidi ya mawakala 600 wakiwamo 195 wanaohudumia katika Wilaya Ya Tarime na 35 Musoma Vijijini.
“Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya wateja wilayani Tarime na Musoma, Benki yetu iliona kuna umuhimu wa kuboresha huduma ili kuendana na mahitaji yaliyopo sasa na yatakayojitokeza baadaye. Tulifanya utafiti wa kina kabla ya kujenga matawi haya yatakayowahudumia wananchi wa Mugango na Sirari pamoja na maeneo jirani,” amesema Raballa.


Kutokana na uzinduzi wa matawi hayo mawili, Benki ya CRDB sasa imefikisha jumla ya matawi 10 mkoani Mara ambayo ni Musoma, Tarime, Bunda, Serengeti, Nyamongo, Rorya, Shirati, Mugango na Sirari hivyo kuifanya kuwa na mtandao mpana zaidi wa matawi nchini kuliko benki nyingine yoyote nchini.
Akifungua tawi la Sirari, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mheshimiwa Meja Edward Flowin Gowele amesema huduma za fedha ndio msingi wa maendeleo ya mwananchi binafsi, kaya na taifa kwa ujumla hivyo kilichobaki ni umakini wa wananchi kubuni miradi itakayowainua kiuchumi kwa kuzikabili changamoto zilizopo kwenye maeneo yao ili kunufaika na fursa zinazojitokeza.

“Tawi hili ni sehemu salama kwa wananchi kuhifadhi akiba zenu za fedha. Ni mahali ambapo wafanyabiashara mtapata mikopo ya kuimarisha miradi yenu na wafanyakazi nao wataweza kutimiza malengo yao. Benki ni rafiki wa kila mwananchi anayewa na kupanga maendeleo yake, tulitumie tawi hili kujinufaisha kwa kujenga uchumi imara wa kila mmoja wetu,” amesema Mheshimiwa Gowele.

Licha ya kunufaika na mikopo inayotolewa, Mheshimiwa Gowele amewahimiza wananchi wa Sirari, Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara na Tanzania nzima kwa ujumla kuwekeza kwenye Hatifungani ya Samia Infrastructure Bond inayoendelea kuuzwa na Benki ya CRDB ili kupata fedha zitakazowezesha ujenzi wa barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
“Ukiwekeza katika hatifungani hii una uhakika wa kupata faida ya asilimia 12 inayotolewa kila mwaka kwa muda wote wa miaka mitano wa uhai wake. Lakini, kumiliki hatifungani hii ni sawa na kuwa na nyumba, unaweza kuitumia kama dhamana kuchukua mkopo kutoka taasisi yoyote ya fedha. Nawasihi kila mmoja wenu na Watanzania wote kwa ujumla, kuitumia fursa hii kuwekeza kwenye hatifungani hii,” amesisitiza Mheshimiwa Gowele.

Kwenye uzinduzi wa tawi la Mugango, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Musabila Kusaya amesema ni fursa kwa wananchi wa Musoma kunufaika na huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB zikiwamo zilizo chini ya Programu ya Imbeju inayolenga kuwawezesha vijana na wanawake.
“Ufunguzi wa tawi hili umesogeza kwa karibu fursa za Programu ya Imbeju. Nawaomba wajasiriamali mlitumie tawi hili kupata mitaji wezeshi itakayosaidia kuinua biashara zenu. Hapa, mtapata ushauri wa kitaalamu ia wa namna bora ya kukuza shughuli zenu kwa maendeleo binafsi na taifa pia,” amesema Kusaya.

Sambamba na ufunguzi wa tawi la Benki ya CRDB Sirari, Benki ya CRDB imekabidhi madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzi kwa wanafunzi wa Wilaya ya Tarime. Madawati hayo yamepokelewa na Mheshimiwa Gowele aliyesema yatasaidia kupunguza uhaba uliopo katika shule za msingi na sekondai wilayani Tarime.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger