Friday, 26 July 2024

SHIRIKA LA IUCN LAUNGANA NA SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA 'BAHARI MALI'

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani amesema serikali ina mpango wa kupanda miti aina ya mikoko 250 kila mwezi.

Dkt. Buriani ameyasema hayo leo Julai 26, 2024 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mikoko Duniani, ambapo mkoani Tanga imeadhimishwa kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi, eneo la Sahare, jijini Tanga.


Amesema mpango huo utatekelezwa kupitia mradi wa Bahari Mali unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na shirika lisilokuwa la kiserikali la International Union for Conservation Nature (IUCN).


Aidha Dkt. Burian, amesema uboreshaji wa mazingira ya bahari ni muhimu kutokana na mchango wake katika kuzifanya fukwe kuwa nzuri zenye kuvutia. Pia amesema uwepo wa mikoko unatoa uhakika wa mazingira bora ya matumbawe na mazalia kwa viumbe wa baharini hususani samaki.


"Pamoja na kuboresha mazingira ya bahari, mikoko inachangia uzalishaji wa hewa ya ukaa yenye manufaa makubwa kiuchumi na uhifadhi wa mazingira yetu" amesema Dkt. Buriani.


Naye Meneja Mradi wa Uhifadhi wa Bahari wa IUCN, Joseph Olila, amesema mradi huo unatekelezwa katika Wilaya mbili za Pangani na Mjinga, lakini pia unatekelezwa Micheweni katika kisiwa cha Pemba.


"Miongoni mwa manufaa ya mradi huo ni ongezeko la mapato kwa jamii na ukuaji wa uchumi wa bluu, urejeshwaji wa mikoko iliyotoweka, utawala katika sekta ya bahari na kutengeneza mipango ya uvuvi endelevu" amesema.


Akisoma risala kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini, James Nshale, Mhifadhi Misitu Mkoa wa Tanga , Lawrence Bryson amesema, uwezo wa mikoko katika udhibiti wa hewa chafu ni mara tano zaidi ya misitu iliyopo nchi kavu.


"Lakini pia manufaa ya mikoko yapo kwenye utengenezaji wa asali bora na kupelekea kuibuliwa kwa utalii wa mikoko baharini" amebainisha Mhifadhi huyo.
Share:

Ngoma Mpya : LUNG'WECHA NG'WANAITULI - MAKANISA

Hii hapa ngoma ya Manju Lung'wecha Ng'wanaituli inaitwa Makanisa 
 
Share:

SSI ENERGY TANZANIA LTD YASAINI MKATABA WA UJENZI WA MRADI WA UMEME JUA WA MEGAWATI 100MW KAHAMA

Kampuni ya uzalishaji wa umeme jua ambayo inamilikiwa na Mhe. Stephen Masele ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais Mstaafu wa Bunge la Afrika imesaini mkataba wa ujenzi wa megawati 100 za umeme wa Solar ambao utaingizwa katika gridi ya taifa.

Hafla ya utiaji saini kati ya SSI ENERGY TANZANIA na Mhandisi Alex Wu ambaye ni mkurugenzi mkazi wa kampuni ya kimataifa ya Sinohydro Corporation kutoka nchini China ambao ndiyo wakandarasi watakaojenga mradi huo imefanyika leo Julai 26,2024 katika ofisi za SSI ENERGY TANZANIA jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo,  Mhe. Masele Stephen amesema Mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa  na hususani Kanda ya Ziwa ambayo imekuwa na matatizo ya upungufu wa umeme.

"Hakika leo historia imeandikwa kwa kampuni ya kizalendo kufanya uwekezaji mkubwa wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 300 za Kitanzania. 

Kampuni yangu imekuwa katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa megawati 10mw ambao unagharimu zaidi ya bilioni 30 za kitanzania hapo Kahama katika vijiji vya Chapulwa na Mondo ambapo mradi wetu utakamilika mwezi Machi 2025, hivyo tunayofuraha kubwa leo kusaini kandarasi ya ujenzi wa hatua ya pili ya mradi mkubwa katika historia ya nchi ya ujenzi wa megawati 100mw", amesema Mhe. Masele.

"Eneo la Kahama ni moja ya maeneo ya Kimkakati kwa kuwa baada ya kufungwa kwa Mgodi wa Buzwagi eneo hilo limegeuzwa kuwa eneo la uwekezaji na kuvutia miradi mbali mbali ya kimkakati, mfano Mgodi wa Tembo(Kabanga Nickel) unatarajia kujenga rifainali ya kuchakata nickel ambapo watajitaji matumizi makubwa ya umeme ikikadiriwa kufika megawati 75mw, vile vile Kahama ni sehemu muhimu ya kibiashara katika ukanda wa ziwa victoria.
SSI ENERGY inakuwa kampuni ya kwanza ya kizalendo kufanya uwekezaji mkubwa hapa nchini katika sekta ya umeme jadidifu (renewable energy)", ameongeza Masele.

Share:

Thursday, 25 July 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 26,2024

Share:

ALIA KAMA MTOTO BAADA YA KUIBA MTOTO WA JIRANI

Nakumbuka mwaka jana mtoto wa jirani yangu alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa anacheza na wenzake karibu na eneo la nyumbani, mzazi wake alipita kila nyumba kumuulizia lakini hakuweza kumpata.

Tulimsaidia kumtafuta hadi vijiji vya jirani lakini hatukuweza kufanikwa kumpata, tuliamuaa kuripoti kisa hicho kituo cha Polisi ambao nao walitueleza kuwa wataanza uchunguzi siku inayofuata.

Hata hivyo, kwa umri wa mtoto yule, miaka mitatu tulijua tu kuna mtu kambeba maana asingeweza kutembea kwenda mbali, mama yake aliamua kuacha na kazi akaanza kumtafuta maeneo mbalimbali lakini hakufanikiwa.

Kutokana na kuacha kazi na kuanza kumtafuta mtoto wake, mama yule alianza kuishi maisha duni kutokana na ukosefu wa kipato pamoja na kuwa na msongo wa mawazo. Nikiwa kama mwanamke mwenzake, kila mara nilienda kumtembelea kwa lengo la kumfariji na kumpelekea chochote kitu.

Katika mazungumzo yetu aliniambia kuwa amesikia kwa mtu kuwa kuna Daktari wa kiasili ambaye anaweza kumsaidia, nilimuuliza jina lake akaniambia halifahamu.

Basi ikabidi niwashe data ya simu yangu na kuanza kutafuta katika mtandao wa google, tulitafuta kwa muda hadi pale tulikutana na tovuti ya Kiwanga Doctors ambayo ni www.kiwangadoctors.com, tulisoma orodha ya huduma mbalimbali ambazo anatoa kwa wateja wake na kubaini anaweza kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo.

Tulichukua namba zake ambazo ni +255763926750 au +254769404965 na kufanya naye mawasiliano mara moja, baada ya ganga ganga zake alisema mtoto atapatikana ndani ya siku tatu.

Cha kushangaza zaidi na kilichovutia umati wa watu wengi siku iliyofuata, ni kitendo cha jirani yetu mmoja mtu mzima kuanza kulia kama mtoto mchanga, alilia kwa sauti kubwa kuanzia asubuhi hadi usiku, ilifika hatua hadi sauti ikawa inamuishia, hakuweza kuzungumza chochote zaidi ya kulia.

Nilifahamu huyu ndiye aliyekuwa amemficha yule mtoto, nilienda kwa mama yake na kumuomba tuende hapo licha kuwa kuna umati mkubwa wa watu.

Tulifika na mara tu alipomuona mama mtoto alinyamaza na ndipo watu nao walizidi kusogea kujua nini kinaendelea, alimshika mama mtoto mkono na kuingia naye ndani na kumuonyesha chumba alichokuwa amemficha.

Tulimchukua mtoto, wakati tunataka kuondoka alianza tena kulia kama mtoto mchanga, na hapo ndipo tulipompigia tena simu Kiwanga Doctors kuomba muongozo wake kuhusu jambo hilo. Alimpigisha faini aliyeiba mtoto, kisha kutoa maelekezo anayopaswa kufanya ili hali hiyo kukoma.

Mwisho.


Share:

WADAU WA JINSIA NA MAENDELEO WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA NGUVU KUDHIBITI VITENDO VYA UTEKAJI WATOTO


IMEELEZWA kuwa vitendo vya kishirikina, visasi, hali ngumu ya maisha, biashara haramu, ukosefu wa elimu, kuporomoka kwa maadili na tamaa ni miongoni mwa vyanzo vya watu wanaodaiwa kupotea au kutekwa .

Hata hivyo, ili kuondokana na hali hiyo, watu wanatakiwa kuwa na moyo wa imani, kuwepo kwa ushirikiano, kukamata waganga wasio na vibali, elimu iongezwe kwenye jamii, makanisa na misikiti yasiyo na mafundisho mazuri yadhibitiwe , malezi bora na kuwakumbusha watoto wajibu wao, vyombo vya dola kutimiza majukumu yake na kuwalinda wanaotoa taarifa za vitendo hivyo.

Hayo wameyaeleza Wadau wa Jinsia na Maendeleo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam katika Semina za Jinsia na Maendeleo zinazofanyika kila Jumatano katika Viwanja Vya TGNP- Mtandao huku ikihusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Akizungumza katika Semina hiyo, Hamisi Masanja Mkazi wa Manzese amesema kwa sasa ushirikiano kutoka kwenye vyombo vya ulinzi wa raia na mali zao ni mdogo kwani ushirikiano huo ungekuwepo masuala haya ya utekaji wa watoto usingekuepo.

Ameongeza kuwa ni vyema kikosi cha polisi kifanye kazi yake na wananchi kutoa ushirikiano pale utekaji unapitokea.

“Kitu kikitendeka kwanza kitilie hamu kukifahamua kama unaona kinahitaji msaada toa msaada hatakama wa kupiga kelele ili kuokoa maisha yale muhusika” amesema Masanja

Naye Mpegwa Noa kutoka Makulumla amesema masuala ya utekaji wa watoto wazazi wengi wanalalamika hivyo ameiomba serikali kufatilia watekaji hao na kuwachukulia sheria stahiki ili kukomesha mauaji na utekaji ambao umeenea katika baadhi ya maeneo nchini.

Aidha ameiomba serikali kuongeza ulinzi mashuleni na kuwataka wazazi na walimu kushirikiana kuhakikisha mtoto anafika shuleni anakabidhiwa mwalimu na mtoto atakapotoka shuleni akabidhiwe mzazi ili kukomesha vitendo vya utekaji.

Kwa upande wake Afisa Programu Sera kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania, Rogathe Loakaki alisema kama mtandao wa kijinsia Tanzania wanaamini katika hizo sauti za wengi kwani zitawasaidia kudai hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na uwajibikaji kwa wale ambao wanasababisha vitendo hivyo lakini pia kuweza kupata sapoti kutoka kwa wadau wengine hasa serikali ambao ndiyo wanasimamia vyombo vya maamuzi kwa nchi na vyombo vya ulinzi.

“Mambo makubwa yaliyoibuka ni hatua mbalimbali ambazo tumekubaliana kuchukua ikiwemo kuweza kufanya tafiti shirikishi, tumeweza kutoa madodoso ili waweze kutoa mawazo yao na pia kuwashirikisha wanajamii wenzao na tuweze kupata tawimu za uhalisia kama kweli tatizo hili lipo kwenye jamii na kwa kiasi gani”

“Katika miaka 25 ijayo vitendo kama hivi hativitaki kwahiyo tumetumia fursa hii tunakoelekea kwenye maandalizi ya dira hii kupaza sauti kwamba dira inapotengenezwa izingatie usalama kwa jamii nzima asiwepo yoyote ambaye atakatiliwa hasa makundi ya wanawake na watoto” ameeleza Rogathe.

Pamoja na hayo amesema TGNP kwa pamoja watashirikiana na serikali pamoja na vyombo vya ulinzi ili waelewe kwamba jamii ni jicho gani wanalo juu ya suala hilo la utekaji wa watoto nchini.

Share:

TAFORI YAANIKA FURSA KUPITIA MISITU NA NYUKI


Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imewasisitiza Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya Misitu na Nyuki, kwa kuwekeza katika misitu na kushiriki katika ufugaji nyuki kwa kuzingatia njia sahihi zilizofanyiwa utafiti ili wapate tija katika rasilimali za misitu zilizopo nchini.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Matumizi ya Misitu Dkt. Chelestino Balama wakati akiongea na baadhi ya timu ya wataalamu wa misitu na nyuki na waandishi wa  habari wa  waliofika ofisi za TAFORI Mkoani Morogoro na kutembelea baadhi ya tafiti zinazofanywa.

"Sisi kama taasisi ya TAFORI tunafanya tafiti ambazo ni kwa ajili ya kuboresha vipato kwa jamii lakini pia kwa ajili ya kuboresha uchumi wa nchi yetu .Mojawapo ni tafiti ya kuzalisha miti katika maeneo mbalimbali ili kuwa na taarifa sahihi za miti anbayo  inafaa kupandwa katika eneo fulani ambapo Vijana wengi wamejikita huko na imekuwa ni sehemu ya ajira"-Alifafanua Bw. Balama

"Lakini pia taasisi yetu imefanya utafiti ambao unahusika na kuangalia rasilimali za misitu ikiwemo kuona ni namna gani zinachangia kwenye kuokoa malighafi katika viwanda vya Misitu hapa nchini na utafiti huu umekuwa na mchango mkubwa kwenye kuleta ajira kwa vijana, maana wamejikita kuanzia kwenye mnyororo mzima. wa Mazao ya misitu"-Bw. Balama

Afisa Mtafiti Mkuu kutoka TAFORI ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi tafiti ya uzalishaji Misitu Dkt. Stephen Maduka ambaye amebainisha uwepo wa bustani ya miti ya  Utafiti ya TAFORI iliyopo Ofisini kwao kwa lengo mahususi ya kufanya utafiti katika kunusuru miti ya asili isitoweke ikiwemo mti wa Mkurungu, Msandali na Msekeseke inayovunwa kwa wingi kwa ajili ya biashara ya utengenezaji samani, kuongeza thamani ya miti ya asili ya matunda.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi ya Utafiti wa Ufugaji Nyuki TAFORI Bw. Allen Kazimoto amewataka Vijana na Wanawake kushiriki kikamilifu katika Ufugaji Nyuki kwa kuzingatia ubora wa Mazao ya Nyuki yanayokudhi soko la ndani na pia la Kimataifa ili waweze kupata tija katika Ufugaji.

Aidha Bw. Kazimoto ametoa rai kwa Watanzania kuacha kufanya shughuli za Kibinadamu pamoja na Matumizi ya viuatilifu vya mazao ya Kilimo yanayosababisha makundi ya Nyuki kupungua kila mara.






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger