Sunday, 28 January 2024

TPA YAIKABIDHI KAMPUNI YA ANOVA CONSULTING ENEO ITAKAPOJENGA BANDARI MBAMBA BAY


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA ) tarehe 27 Januari,2024 imeikabidhi rasmi kampuni ya Anova Consulting Company ltd eneo itakapojengwa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bw.Manga Gassaya amesema kampuni hiyo itasimamia ujenzi wa Bandari hii ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika viwango na kukamilika kwa muda uliokubaliwa katika mkataba.

Aidha amesema kuwa kinachofanyika ni kumuonyesha msimamizi wa mradi (Anova Consult) mipaka ya eneo la ujenzi.

Makabidhiano hayo ni kufuatia mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba Bay uliosainiwa disemba 4,mwaka jana ambapo kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co ltd ndio itaendeleza ujenzi wa Bandari hiyo.
Share:

TGNP YAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI WA KIJINSIA


MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) wanaendesha mafunzo ya masuala ya uongozi wa kijinsia ili wanajamii waweza kuenzi nguvu za pamoja, na kuhusisha wanawake katika ngazi za maamuzi ikiwa ni sehemu ya kuleta mabadiliko kwenye jamii na kuwainua kiuchumi.

Mafunzo hayo ya siku kumi kwa ajili ya masuala uongozi wa kijinsia wamewajumuisha wanawake kutoka nchi mbalimbali za afrika ikiwemo kenya, uganda, zimbabwe, rwanda, Ghana, burundi, afrika kusini na Nigeria.

Ameyasema hayo Januari 27, 2024 Jijini Dar es Salaam, Afisa wa program Mafunzo wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai kuwa washiriki hao wamejifunza wanajamii wanaweza kuenzi nguvu za pamoja na kuhusisha wanawake katika ngazi za maamuzi.

Pia washiriki hao walitembelea kituo cha taarifa na maarifa kipunguni lengo ni kujifunza wanawake walivyowezesha kubadilisha jamii juu ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa maswala ukeketaji, mimba za utotoni, ukatili wa vipigo na kutunza mazingira ili kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Sangai amesema wanawake wamefundishwa jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala ambao wanatumia kwenye matumizi yao, nakuuza ili kujipatia fedha katika kukuza uchumi wao, pia wametumia mbolea kuzalisha wadudu kupitia takataka ambao wanakuwa chakula cha kuku n.k

"Katika hayo majumuiko ya kujifunza wametumia kama fursa ya kupata taarifa ya ukeketaji, watoto kuozeshwa kwenye umri mdogo, wanaotembea na wanafunzi, vipigo ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa baadhi ya ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia" amesema Anna Sangai

Hivyo, amebainisha kuwa kituo cha taarifa na maarifa kinaendeshwa na wanawake Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na katibu wote ni wanawake hii inaonesha ni jinsi gani wanawake wakipewa fursa wanaweza kuongoza vizuri na kuleta mabadiliko kwenye jamii.
Share:

MANYARA WASHEREKEA KUMBUKIZI YA KUZALIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga ameongoza zoezi la upandaji wa miti lililoendana na ukataji wa keki kwa ajili kusherekea miaka 64 ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Akiongoza zoezi hilo la upandaji na kukata keki lililofanyika Januari 27, 2024 katika Shule ya Sekondari ya Katesh - Hanang, Mhe. Sendiga amesema Miti zaidi ya 3,000 imepandwa katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya tope, mawe na magogo ikiwa ni njia mojawapo ya kurejesha uoto wa asili uliopotea kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea mwishoni mwaka mwaka jana.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Manyara, wananchi pamoja na watoto walioadhirika katika maporomoko hayo.

Mkoa wa Manyara umejipanga kupanda miti milioni 10 kwa mwaka 2024.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 28,2024


















Share:

Saturday, 27 January 2024

NILIJUA MWANAMKE MWEMA KUMBE TAPELI MKUBWA!

Jina langu ni Musa kutokea Moshi, Tanzania, kazi yangu mimi ni dereva wa Lori, kuna dada nilikutana nae club nikabadilishana nae namba, siku hadi siku tukawa wapenzi.

Siku moja nikamtoa dinner, tukapiga story nyingi sana, baada ya hapo akaja magetoni, akanielezea shida zake kuwa anasoma chuo uhasibu na hana pa kukaa, Hostel ni michosho akawa anaishi na mashoga zake mtaa.

Basi hata msosi kwake ilikuwa shida, hivyo akaniomba tuishi wote, mwanaume sikuwa na shida, nikasema kwa kuwa ameridhia maisha ya ghetto, nikawa naishi nae.

Mimi muda mwingi nasafiri, tulikuwa tumepanga room moja, basi kwakuwa nimeongeza mtu ndani, tukahamia chumba mbili yaani chumba na sebule.

Tutabadili furniture za ndani na mwanaume nikaongeza vitu ile mamaa asipate shida akiwa nyumbani. Kwa bahati mbaya au nzuri, huku akisoma, nikampa ujauzito, ndio misukosuko ikaanzia hapo.

Akawa analazimisha kuitoa, yaani hataki kuzaa, kwangu mimi ilikiwa baraka hivyo ilibidi nimbembeleze ili mambo yawe sawa.

Baadae akaja kukubali hadi mama yake akaja Moshu, akaonana na ndugu zangu wakapanga mengi tu. Sasa siku moja, nipo kwenye mishe, napigiwa simu na majirani vyombo vyangu vimechukuliwa demu kasepa. Kuja kufatilia namkuta kwa msela yaani mwanaume mwingine amehamia kwake.

Nikaenda polisi, demu kuitwa kanikana hanijui na pale tulipopanga ni kwake kisa tu nilikuwa namtumia hela ya kodi na mkataba umejazwa jina lake maana mimi muda mwingi nipo safirini sikai home.

Kwa kifupi akawa amenitapeli mali zangu, yaani vitu vyote vya ndani na ule ujauzito alikuwa ameutoa, ni jambo ambalo liliumiza sana moyo wangu kwa sababu nilimpenda na kumuamini sana.

Ndugu zangu wakanishauri niende kwa Kiwanga Doctors nikamfanyie dawa, nilikubali ushauri wao, nami nikafanya hivyo mara moja bila kujali chochote kile. 

Baada ya kufanyiwa dawa ile na Kiwanga Doctors, yeye mwenyewe alinipigia simu na kuniambia nikachukue vitu vyangu, mwili wake ulikuwa umeharibika sana kwa vipele na makovu kwa sababu ya dhuluma aliyonifanyia.

Alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa sana, huku akiomba msamaha, ndipo tulipiga tena simu kwa Kiwanga Doctors ili aweze kumuondolewa kadhia hiyo, aliiondoa ila kwa sharti moja, kulipa faini ambayo aliilipa mara moja.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.


Share:

Friday, 26 January 2024

FEZA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA WA ELIMU

 

........................

Shule ya Feza nchini imesema hivi karibuni imekuwa ikikumbana na changamoto kutoka shule za Serikali kutoka na mindombinu kuboreshwa hivyo kutumia kama chachu ya wao kufanya vizuri zaidi katika kuleta ufaulu.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Mwalimu Mkuu msaidizi wa Feza Shabani Mdoe, amesema hatua ya serikali kuboresha mazingira yake kumeifanya shule hiyo nayo kuendelea kuboresha mazingira yake hivyo kwa mwaka 2023 kuweza kufaulisha wanafunzi wao wote wa kidato Cha nne kwa daraja la kwanza.

Amesema kwa mwaka 2023  wanafunzi 76  wamefaulu kwa daraja la kwanza ambapo  zaidi ya wanafunzi 47 wamepata 1.7 ambapo ufaulu huo unatokana na jitihada za shule hiyo katika kufundisha kwa weledi.

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne kwa mwaka 2023 wa shule hiyo tulipata wasaa wa kuzungumza nao ambao wamepata daraja la kwanza 1.7 wamesema kuwa ufaulu walioupata unatokana na jitihada za kusoma kwa bidii,kusali na mazingira yaliyo salama kujifunzia.

Shule za Feza nchini ni moja kati ya shule zinazofanya vizuri zaidi katika kufundisha  na mara zote zimekuwa ziliingia 10 bora hapa nchini Hali inayochangia sekta ya elimu nchini kukua zaidi.


Share:

SIRI KOM SECONDARY KUNG'ARA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2023... "TUNAWAPOKEA NA KUWAONGEZEA THAMANI WALIOKATALIWA KWINGINE"


Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ni shule inayosifika vizuri kitaaluma kutokana na kuendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.


Kufuatia Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Januari 25,2024, Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi amesema matokeo hayo yamewaacha vizuri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 26,2024, Koyi amesema kati ya wanafunzi 142 zaidi ya wanafunzi 135 wanatarajiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

“Matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 sisi KOM yametuacha vizuri kutokana na tulivyokuwa tunawaandaa watoto na aina ya watoto tuliokuwa nao, tumefaulu kwa kiwango kikubwa kwa mfano tunategemea kupeleka Kidato cha Tano watoto zaidi ya 135 ambayo ni sawa na asilimia 96 ya wanafunzi wote 142 waliofanya mtihani, hili ni jambo la kujivunia kwani zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaenda High Level kutoka kwenye shule moja”,ameeleza.

Koyi amesema mafanikio makubwa yanayoonekana KOM yanatokana jitihada zinazofanywa na walimu na wanafunzi lakini pia kutokana na kwamba KOM inachukua wanafunzi wa kawaida kabisa na wanafanya vizuri kwenye mitihani baada ya kuwaongezea thamani.

Ameeleza kuwa KOM Secondary imekuwa ikipokea wanafunzi wa kawaida kabisa ambao wamepunguzwa kwenye baadhi shule hivyo wanajivunia kuona wanafunzi waliokataliwa mahali pengine wakienda hapo KOM wanawaongezewa thamani na wanafaulu vizuri kwenye mitihani na kuendelea na elimu ya kidato cha tano.


“Matokeo tumeyapokea vizuri na tumejaribu kufanya uchambuzi watoto wetu wameendelea kufanya vizuri zaidi na wengine wame Improve (wamekuwa na mabadiliko) zaidi. Kwa kweli sisi tunajivunia ufaulu wa vijana wetu ukizingatia KOM tupo tofauti na shule zingine, kulikuwa na suala la kupunguza watoto. Sisi hatupunguzi watoto kwa mfano kwa hili darasa la kidato cha nne lililomaliza mwaka 2023 tulianza tukiwa na wanafunzi 78 na tumemaliza tukiwa na wanafunzi 142, hii inaonesha kuwa badala ya watoto kupungua, sisi watoto wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka”,amesema Koyi.
“Katika sera za baadhi ya shule wanasema mtoto asipofika wastani flani anapunguzwa. Kwa sisi KOM wanafunzi ambao hawajafika wastani tunaamini kwamba tukiwachukua tunawaongezea thamani na hawa wanafunzi ambao wamekuwa wakiongezeka katika shule yetu, wengi wao wamepunguzwa kwenye shule zingine zenye sera ya kupunguza wanafunzi ambao hawajafikia wastani flani lakini sisi tunawachukua na kuwaongezea thamani na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani”,ameongeza Mkurugenzi huyo wa KOM Secondary School na Kom Pre & Primary School.


Katika hatua nyingine amewaomba wazazi kuwa na mwamko wa kupeleka wanafunzi shule huku akiahidi kuwa KOM itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwapa mafunzo walimu hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mtaala mpya wa masomo kwa kidato cha kwanza.

Mawasiliano zaidi KOM Secondary School

+255 767 618 213
+255 768 105 820
+255 767 483 046


Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi akizungumza kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023
Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi akizungumza kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga

Picha na Kadama Malunde 1 blog



Bofya Hapa Kutazama  Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne(CSEE) 2023 na Mtihani wa Maarifa (QT)

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger