Monday, 31 May 2021

Africa Indigenous Landscape Program Officer at Nature Conservancy

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

A LITTLE ABOUT US Founded in 1951, the Nature Conservancy is a global conservation organization dedicated to conserving the lands and waters on which all life depends. Guided by science, we create innovative, on-the-ground solutions to our world’s toughest challenges so that nature and people can thrive together. We are tackling climate change, conserving lands, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

NTRI Livestock Marketing Officer at Nature Conservancy

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

A LITTLE ABOUT US Founded in 1951, the Nature Conservancy is a global conservation organization dedicated to conserving the lands and waters on which all life depends. Guided by science, we create innovative, on-the-ground solutions to our world’s toughest challenges so that nature and people can thrive together. We are tackling climate change, conserving lands, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA AZZA HILAL HAMAD, PRISCA KAYOMBO RAS MPYA SIMIYU, CAMILIUS WAMBURA DCI

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
**
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Azza Hilal Hamad kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na nafasi yake kuchukuliwa na Prisca Joseph Kayombo ambaye alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Bi. Azza aliteuliwa jana Mei 29, 2021 kushika wadhifa wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, ambapo sasa kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu iliyotolewa usiku huu, Azza atapangiwa majukumu mengine.



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 31,2021











Share:

Sunday, 30 May 2021

MKE WA PASTA ACHAPANA MAKONDE NA MWANAMKE MWENZAKE LIVE KANISANI


Video moja inasambaa kwenye mtandao wa kijamii ikiwaonyesha wanawake wawili wakipigana kanisani katika eneo la Umuahia, jimbo la Abia nchini Nigeria.

Kulingana na Sunday Ogirima, ambaye alichapisha video hiyo kwenye mtandao wa Facebook, kati ya wanawake hao mmoja ni mke wa pasta na muumini wa kanisa hilo. 

Ogirima ambaye anaonekana kuwa mwandishi wa habari, alisema hawezi kunyamazia kitendo hicho kwa sababu ni cha aibu na ndio maana alianika video hiyo mtandaoni.

Katika video hiyo, mwanamke aliyevalia rinda la blu ndiye mke wa pasta Akaa na anayepokezwa kichapo ni binti ya shemasi wa Kanisa la AG Worship Center.

 Ogirima alifichua kuwa sababu za wawili hao kupigana kanisani ni kwamba Bi Akaa alikuwa amepanga njama na kundi la TAG kunyakuwa kanisa hilo kimabavu lakini mume wake alikataa kushirikiana naye.

Kutokana na kuhofia, shemasi na binti yake walikwenda kufunga kanisa hilo ili kumzuia Bi Akaa kuuza kanisa hilo kwa TAG.

 Bi Akaa aliwakaripia shemasi na bintiye kwa kumzuia kuuza kanisa hilo kwa TAG na kutaka kusalia katika kundi la TST.

 Kisha baada ya kurushiana maneno, mke wa pasta alianza vita na kumtupa chini binti ya shemasi.

Via Tuko news
Share:

WAZALISHAJI WA MAZIWA TANGA WAJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) KWA KUWEZESHWA NA BENKI YA CRDB

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa ilifanyika Jijini Tanga
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa ilifanyika Jijini Tanga
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa hiyo ilifanyika Jijini Tanga
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline Senzighe
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa ilifanyika Jijini Tanga
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa iliyofanyika Jijini Tanga

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline Senzighe

 

 

WAZALISHAJI wa Maziwa Tanga mjini wataanza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU).

Hatua hiyo inatokana na kuingia makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF waliingia siku chache zilizopita za kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa utaratibu wa Ushirika Afya. 

Katika makubaliano hayo, Benki ya CRDB itamlipia mwana ushirika michango ya bima ya afya kwa wakati na mwana ushirika huyu atairejesha bila riba wakati wa msimu wa mauzo. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda amesema kuwa ushirikiano huo na Benki ya CRDB ulianza tangu Mei 5, 2021 kwa pande zote mbili kusaini Makubaliano ambayo yatawawezesha wanachama walio kwenye Vyama vya Ushirika kunufaika na huduma za matibabu kupitia bima ya afya bila kuwa na changamoto ya kifedha.

 

“Mfuko umeazimia kuwafikia watanzania wote na huduma za Bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi ndio maana tumekubaliana na Benki ya CRDB ambao ni wadau wakubwa wa wana ushirika nchini kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya bila changamoto ya kifedha”alisema Mapunda.

 

Akizungumzia huduma, Mapunda alisema kuwa mwana ushirika na familia yake atapata huduma zote za matibabu katika mtandao mpana wa vituo zaidi ya 8,000 Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.

 

Akizingumza katika tukio hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB iko mstari wa mbele katika kuhudumia wana ushirika kwa namna mbalimbali na sasa inamwezesha mwana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa kulipia michango yake kwa mwaka ili wakati wa mauzo ndipo airejeshe bila riba yoyote juu yake.

 

“Tunaungana na Serikali yetu katika kuhakikisha wana ushirika nchini wanafanikiwa kwa kuwa na uhakika wa matibabu na katika hili Benki ya CRDB tutamchangia mwana ushirika mchango wa bima ya afya wa mwaka wa Shilingi 76,800 na mwenza wake kiwango hicho hicho na kwa kila mtoto Shilingi 50,400 kwa mwaka.

 

Alisema nia yao ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na bima ya afya kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza na tumeanza na kundi la wana ushirika kwa sababu ndio sekta inayoajiri watu wengi zaidi nchini” alisema Dkt. Witts.

 

Akizungumzia huduma za Benki ya CRDB alisema Wana ushirika hawata pata shida ya huduma za kibenki kwa kuwa ina mtandao mpana wa matawi 246, wakala zaidi ya 19,000 na ATM 550 nchi nzima hivyo ni rahisi kwao na wananchi wengine kupata huduma kwa karibu zaidi.

 

Mpango huu unazinduliwa kwa Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini ukiwa ni mwendelezo wa kuwafikia wana ushirika wote nchini hivyo wanachama kupitia Vyama vyao vya Ushirika wanahimizwa kujiunga kwa kuwa ni wa manufaa, hauna riba yeyote kwa mkulima na wanarejesha michango ya bima ya afya baada ya mauzo ya bidhaa husika.

 

Tangu kuanza kwa ushirikiano huu baina ya NHIF na Benki ya CRDB Mei 5, 2021, vyama vya Chunya Tobacco-growers Cooperative Union (CHUTCU), Maziwa Cooperative Union (MCU), Muungano wa Wauza Maziwa wa Rungwe (MWAMARU) na Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) vimeshaanza kunufaika na tunategemea vyama vingi zaidi kujiunga na kunufaika na mpango huu.

 

Awali akizungumza wakati tukio la kutiliana saina kwa ajili ya kutekeleza makubaliano Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema hilo ni jambo nzuri na lenye tija kubwa kwa kwa manufaa zaidi ya wazalishaji wa maziwa mkoani humo

 

DC Mwilapwa Benki ya CRDB na NHIF kwa jinsi walivyokuja na mpamgo huo utasaidia kuleta  manufaa makubwa kwa wananchi kutokana na kwamba dira ya Taifa ya maendeleo 2020/2025 inaeleza kwamba itakapofika 2025 watanzania wote wawe wameingia kwenye mpango utakaowahakikishia wanaweza kupata huduma ya afya wakati wowote bila kujali vipato vyao.

 

“Wakati huo utakapofika kwenye lengo hilo namna peke yake kuhakikisha watanzania wanapata tiba bila kupitia vipato vyao ni kupitia huduma ya afya hivyo ni wazo jema kutekeleza azma ya serikali lakini kutekeleza mambo makubwa lazima uwe na uwez,i rasiliamali fedha”Alisema

 

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza kwa mpango huo ambao alisema unaitoa kimasomaso Serikali watanzania ni jambo jema watokee watu ambao wanakubaliana nalo nao ni Benki ya CRDB ambao wamesaidia kuwezesha kwenye uwezeshaji wa kifedha.

 

 “Mmewezsha mkopo usio na riba mnapofanya hilo hamtekelezi lile la 2020/2025 ambalo ni la Tanzania lakini mnatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ambavyo yanafikia mwaka 2030 wenzetu umoja wa mataifa wanafikiria dunia watu wote wawe wameingia kwenye mpango wa bima ya afya lakini sisi tunasema kabla ya wengine wote duniani hawajafikia tutakuwa tumefika 2025”Alisema DC Mwilapwa.

 

Alisisitiza kwamba Mfuko wa Bima ya Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamefanya kazi yao kutekeleza agizo la serikali na CRDB wanafanya kazi kusaidia jitihada za mfuko huo lakini jambo jingine mliloliangalia ili unufaike lazima uwe mwana ushiriki hivyo watakwenda kuona maendeleo makubwa kwenye ushiriki kwa kupatiwa bima ya afya,

 

Naye kwa upande wake Mrajis wa vyama vya Ushiriki mkoa wa Tanga Jacquiline Senzighe  alitoa shukruani kwa mwelekeo uliopo mbele yao wa kuwa na bima ya afya kwa wafugaji lakini mpango huo unategemewa kwenye ushiriki wote na hizo ni habari njema zenye manufaa makubwa kwao.

 

Alisema kwa sababu wanaushirika lazima watoke ili waweze kutoka wanapaswa kuwa na afya njema huku akieleza kwa sasa mkoa wa Tanga inafanyika kwa kuanzia vyama vya ushirika vya wafugaji ambao vikifanya vizuri zaidi vitasaidia vyama vyengine kufikika kwa urahisi zaidi.

 

“Lakini nitoe wito kwa vyama vya ushirika na viongozi mliopata mkopo lakini lazima mtambue kwamba marejesho yake ni kupitia zile shughuli ambazo wanaushirika wanazifanya kila siku ”Alisisitiza .

 

Mrajisi huyo alisema iwapo mkopo huo ukiendelea vizuri na wakiendelea kufanya ushirikiano mzuri wataendelea kufungua wigo mpana kwa vyama vyengine vya ushirika vya mchepuo mwengine kuweza kunufaika nao.

 

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) Athumani Mahadhi alisema chama hicho kilianzishwa mwaka 1993 wakiwa na lengo la kutafuta soko la wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa mkoa wa Tanga.

 

Alisema kwea sasa wana vyama wanachama 28 na wafugaji mmoja mmoja wamefikia kwa mkoa mzima wamefikia 6285 huku akieleza katika mpango huo wa bima ya afya wao kama TDCU na vyama vya  wanaona kama itakuwa itachochea baadhi ya watu ambao sio wanachma  kuona ipo haja ya kujiunga kwenye vyama vya ushirika kutokana na kwamba huduma ya afya pia inapatikana huko.

 

 

Share:

Waziri Wa Maliasili Na Utalii Dkt.ndumbaro Kuwashawishi Mawaziri Kujifunza Mchezo Wa Gofu


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro aahidi kutumia ushawishi wake kuwahamasisha Mawaziri wenzake pamoja wa watu kawaida  kujifunza mchezo wa gofu kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier kufanya hivyo

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa Mabalozi na Wataalamu wa nchi mbalimbali ambao ni Wachezaji na Wanachama wa Chama wa gofu nchini kufuatia kumalizika kwa mashindano ya Gofu  yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania yaliyofanyika Mwezi April mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

 Hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu imefanyika nyumbani kwa Balozi huyo, Mhe.Frederic Clavier  na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania  ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.

Amesema kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier mbali ya kuwahasisha Mawaziri pia atawahamasisha Wabunge kujifunza mchezo huo ili kuwa timu bora ya Bunge ya mchezo wa gofu  hali itakayopelekea Wabunge hao kuendeleza mchezo huo katika majimbo waliyotoka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro amewapongeza Washiriki hao na kuwaaahidi kuendeleza mchezo huo kwa kuunganisha na utalii wa michezo ili kuhamasisha Mabalozi hao kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

‘” Nawaahidi  kuandaa mashindano mengi zaidi ya Gofu ambayo nitawashirikisha karibu  vivutio vya Utalii ili mkishacheza gofu mbajipumzisha kwa kuwa tembo na simba” alisema Ndumbaro

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier ametoa wito kwa Watanzania kujifunza mchezo wa gofu huo kwani ni mchezo kama michezo mingine

Amewatoa hofu Watanzania kuwa mchezo huo haubagui ni wa watu wote wenye kipato cha chini na cha juu na sio mchezo wa Watu wa Matajiri na Wasomi  pekee

Amesema gofu ni mchezo rahisi sana kujifunza na sio mchezo mgumu, ” Jitokezeni kujifunza mchezo wa Gofu ni ajira na pia ni burudani kama ulivyo mchezo wa mpira wa miguu” alisema Mhe.Balozi Frederic Clavier

Katika hatua nyingine amempongeza Waziri Dkt. Ndumbaro kwa kuwa Mwanachama pekee wa Mchezo wa Gofu kati ya Mawaziri wote nchini Tanzania na hivyo kutoa wito kwa Mawaziri wengine kucheza mchezo huo.


Share:

ASKARI WA UHAMIAJI WALIOMTESA ALEX WAKIDAI NI TAPELI WASIMAMISHWA KAZI


Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dkt.  Anna Makakala
***
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji imewasimamisha kazi wafanyakazi wake watatu kutokana na tukio la askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi ilivyoonekana katika mitandao ya kijamii.
Video hiyo inayosambaa mtandaoni inamuonesha Alex akipewa mateso mbalimbali ikiwemo kulowanishwa maji kwa kutumia bomba la maji huku akiwa amelala kwenye maji, kuruka kichura pamoja na kugaragara kwenye mchanga.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amesema Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli anayefahamika kwa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini, Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dkt. Makakala amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

" Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" ,Dkt.Makakala.

Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weled, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka) Na Idara hiyo ya Uhamiaji inaomba kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria.

 Chanzo - Michuzi Blog

Share:

KATIBU WA CHAMA CHA WASIOAMINI UWEPO WA MUNGU AJIUZULU

Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Nchini Kenya (AKS) kimepata pigo kubwa kufuatia kujiuzulu kwa katibu wao Seth Mahiga baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja unusu.

Mahiga amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wake akisema amekutana na Yesu na hataki tena kuendelea kupiga kampeni za kumkana Mungu nchini.

Katika taarifa Jumamosi, Mei 29, 2021 rais wa chama hicho Harrison Mumia, alimtaja kama kiongozi aliyekuwa amejitolea mhanga na kumtakia kila la heri katika uhusiano wake mpya na Yesu Kristu.

"Tunamtakia Seth kila la heri katika uhusiano wake mpya na Yesu Kristu, tunamshukuru kwa kutumika chama hiki na bidii kwa zaidi ya mwaka mmoja unusu," ilisoma taarifa hiyo.

Chama hicho pia kilitangaza kuwa kiti hicho ki wazi na kuwaalika Wakenya kutuma maombi.

Chama hicho kilitangaza kuwa kiti hicho ki wazi na kuwaalika Wakenya kutuma maombi.

Kujiuzulu kwa Mahiga kulizua hisia mseto mtandaoni huku wanamtandao wengi wakimupa kongole kwa hatua hiyo.

Baadhi walimuhimiza Mumia kufuata mkondo huo wa mwangaza. Hii hapa baadhi ya maoni ambayo TUKO.co.ke imekuchagulia. Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga alisema: "Rais.Endapo unategemea tu kipengee cha 32(1) cha katiba ambacho kinasema kila mtu ana haki ya kuabudu, dini, mawazo, imani na maono. Haki hii si ya kuchezea."

Share:

JINSI NILIVYOSAIDIA MWANANGU KUACHA KUTUMIA POMBE NA MADAWA YA KULEVYA


Wazazi tunakutana na changamoto sana kutoka kwa watoto wetu haswa unapomlea mtoto wako kwa maadili mazuri ila tunapokuwa unakuta anaanza kuwa na tabia tofauti sana.

Unakuta mtoto wako anatumia madawa ya kulevya,sigara,bangi na Pombe. Akiwa anatumia hivyo vitu mtoto hawezi kukusikiliza kama mzazi wake na wengine kutoa matusi na maneno ya kashfa kwa wazazi wao pale anapokuwa tiyari katumia hivyo vitu bila kujua kesho yake itakuwaje.

Mimi ni mzazi wa watoto 2( Kiume,kike), Mtoto wangu wa kwanza ana umri wa miaka 35 wa kiume na wa kike ana umri wa miaka 30.Nimepata shida sana katika kuwalea watoto wangu haswa baada ya Baba yao kufariki wakiwa bado wadogo sana.

Niipitia changamoto kubwa sana haswa katika upande wa kifedha ila nilijituma kadri ya uwezo wangu wote watoto wangu wapate elimu na malezi bora.

Mwanangu wa kiume aliweza kusoma hadi kufikia hatua ya kujiunga masomo ya chuo kikuu na baada ya kujinga chuo kikuu alianza tabia ya kutumia pombe na madawa ya kulevya. Nilivyoweza kugundua hiyo tabia nilihisi ni ujana unamsumbua zaidi nilimkarisha chini na kumuonya juu ya hiyo tabia aliyoanza. Aliweza kudilika kwa siku kadhaa na kisha akaanza tena hadi ikafikia hatua ya kushindwa kuendelea na masomo yake.

Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kumshauri na kumtafutia watu wa kumshauri ila hakuweza kubadilika.

Kila kukicha mtoto wangu alizidi kubadilika zaidi anakunywa pombe na kulala katika mabaa na wakati mwingine harudi nyumbani kwa siku kama 3 yupo huko na walevi wenzake.

Niliweza pokea malalamiko mengi kutoka kazini kwake kuwa hafiki kazini hivyo ingepelekea yeye kufukuzwa kazi muda wowote.

Alipofikisha miaka 30 bila kuwa na mke ikabidi nijitahidi kumtafutia mwenza wake nikihisi kuwa ataweza badilika na kupata maendeleo maana kila pesa ambayo alikuwa anapewa kazini yote ilikuwa inaishia kwenye pombe na madawa ya kulevya.

Mimi kama mzazi nilikuwa naumia kila siku ya Mungu kwa sababu ni kijana ambaye nilitegemea atanisaidia pamoja na mdogo wake ila miaka 30 hana chochote zaidi nilitamani kuona kijana wangu anakuwa na familia ili nipate wajukuu lakini yote hayo hayakuweza kutokea hata hivyo hakuna mwanamke ambaye angeweza vumilia tabia yake.

Ikanibidi nianze kutafuta usaidizi maana kijana wangu umri unaenda ndipo rafiki yangu mzazi kama mimi aliweza nipatia namba ya Dr. Kiwanga+254 769404965,website www.kiwangadoctors.com ili niweze tambua shida ni nini kwa sababu kijana wangu hakuwa na tabia chafu ,alikuwa mtoto msikivu,niliweza kushauriana nae kwa jambo lolote ila baada ya kujiunga masomo ya chuo kikuu kila kitu kilikuwa tofauti sana.

Niliweza eleza shida yangu vizuri kwa Dr. Kiwanga akaniambia kuwa nimtumie baadhi ya taarifa kuhusu kijana wangu nikatuma, kisha akaniambia nisubiri kwa muda wa saa 1 niwasiliane nae.

Baada ya muda kutumia nilipiga simu tena ndipo Dr. Kiwanga akaniambia kinachomkuta mtoto wangu ni nini,Mtoto wangu anatumia hivyo vitu kwa sababu kuna kitu kinamsukuma kufanya hivyo wala si kwa matakwa yake.

Dr. Kiwanga alizidi kuniambia hata shida zinazonikuta kazini kwangu bila kumwambia mwisho kabisa akanionesha mbaya wangu ni nani.

Baada ya kutambua shida nilimuomba anisaidie mtoto wangu aache kutumia pombe na madawa ya kulevya ndipo
Dr. Kiwanga akanipatia dawa ya kutumia kwa siku 7.Baada ya kuanza kutumia dawa kama nilivyokuwa nimeelekezwa kijana wangu alianza kubadilika pole pole na baada ya week 2 kupita alikuwa hawezi kusogelea watu ambao alikuwa anatumia nao pombe na madawa ya kulevya.

Miezi 3 kupita kijana aliweza kupata mwenza wake na kwa sasa nina wajukuu 2 kutoka kwake. Asante Dr. Kiwanga, katika mazungumzo na Dr aliweza kuniambia kuwa anatibu magonjwa sugu kama Miguu kuwaka moto chini,Sukari,Nguvu za kiume,Gonorrhea,Syphilis,TB na Pressure.Pia anasaidia kumrudisha mpenzi, Kusafisha nyota, Kupata kazi,kupata promotion kazini,Kufunga Mme/mke asiende nje ya ndoa.

Unaweza kumpata Dr. Kiwanga kwa namba+254 769404965 au tembelea website yaowww.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.


Share:

CHAVITA KOROGWE YAENDESHA WARSHA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA


CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) wilayani Korogwe mkoani Tanga kimeendelea kutoa elimu kwa watoa huduma za Afya wilayani  ili itumike kwa watu wenye ulemavu viziwi kuweza kupata huduma bora  za Afya  pindi wanapofuatilia upatikanaji wa huduma katika  vituo vya afya.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society (Fcs), yanalenga kuwahakikisha watu wenye ulemavu wanatambuliwa wanapata takwimu au taarifa ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya huduma za afya ipasavyo ili kuodokana na dhana ya unyanyapaa

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CHAVITA wilaya ya Korogwe Happyness Kuboja alisema kuna wakati wanfuatilia huduma hizo wanapata vikwazo kutoka kwa wahudumu wa Afya kwa kutozingatia miongozo inayotolewa na serikali juu ya kuwapatia kipaumbele Watu wenye ulemavu. matokeo yake tunakosa huduma ama kupata huduma tofauti na ugonjwa wenyewe wanapofika katika vituo vya kutolea huduma za afya kiasi cha kushindwa kupata matibabu.

“Tumekuwa tukipata kero nyingi sana tunapokwenda kupata huduma za afya kutokana na wahudumu kutokuelewa miongozo mbali mbali inayowahusu linalotupelekea wakati mwingine kukosa huduma na kuishia kurudi nyumbani huku tatizo likiwa linabaki bila kupatiwa ufumbuzi alisema Kuboja.

“Lengo kubwa lamafunzo haya ni kuwaelimisha wahudumu wa afya jinsi ya kupanganga mikakati ya uboreshaji wa huduma kuwapokea na kuwahudumia wenye ulemavu wa kusikia na wengineo  wakati wanapofika kupata huduma” aliongeza.

Kuboja aliiomba serikali kutenga bajeti ambayo ni endelevu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wahudumu katika taasisi zote ili kuweza kuwajenga kimawasiliano na kuondoa dhana potofu inayopelekea wenye ulemavu kuonekana ni watu wasiofaa kwenye jamii.

Naye Katibu wa chama hicho ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa mafunzo hayo Mr Ally Nassoro alisema mafunzo hayo ya siku tatu ni maalun kwa wahudumu wa afya pekee lakini pia wataendelea kuyatoa kwa wahudumu wengine ili kuweza kujenga wigo mpana wa upatikanaji wa huduma  kati ya watu wenye ulemavu 

Nassoro alifafanua kwamba kwa kufanya mafunzo hayo wataweza kuondoa hali ya unyanyapaa kwa wenye ulemavu wanapokwenda kutibiwa hospitali na vituo vya Afya.

“Tunajaribu kuwaelimisha wahudumu kufuata miongizo na Sera ya Taifa ya huduma za afya alisema.

Pia aliwataka wale wote wanaopata mafunzo hayo kutumia vyema katika hospitali na vituoni kuwapatia huduma bora watu wenye ulemavu.

Aidha washiriki wa mafunzo hayo walipendekeza Kupatiwa mafunzo ya mawasiliano ya Lugha ya Alama ili kuweza kuwasilisha na viziwi pindi wanapofika maeneo ya huduma hii itakuwa rahisi kwao kuwahudumia ipasavyo.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 30,2021

 

Share:

RAIS SAMIA AMTEUA AZZA HILAL HAMAD KUWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA SIMIYU


Azza Hilal Hamad
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala Mikoa. Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Lakini pia aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , Albert Msovela amehamishiwa mkoa wa Mara huku  Balozi Batilda Salha Buriani akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Balozi Batilda amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan


Share:

CHELSEA YATWAA TAJI LA MABINGWA ULAYA, YAICHAPA MAN CITY 1-0 URENO


TIMU ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City usiku huu Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto, Ureno.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 42 akimalizia pasi ya kiungo mwingine wa kimataifa wa England, Mason Mount.

Hilo linakuwa taji la pili tu la Ligi ya Mabingwa kwa The Blues baada ya lile walilolitwaa msimu wa 2011–2012 wakiwafunga wenyeji, Bayern Munich katika fainali Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 chini ya kocha wa muda, Mtaliano Roberto Di Matteo.

Ushindi huu ni mwendelezo wa ubabe wa kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kwa kocha Mspaniola wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Pep Guardiola baada ya kuifunga pia Man City 1-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili 17 na 2-1 kwenye ligi Mei 8.

 Via Binzubeiry blog
Share:

Saturday, 29 May 2021

Breaking News: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA, WATENDAJI WA TAASISI USIKU HUU... TAZAMA MAJINA YOTE HAPA

 Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa baadhi ya makatibu tawala wa mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakiza kwenye vituo vyao vya kazi. Lakini pia amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger