Friday, 30 October 2020

Dr Mwinyi Ashinda Urais Zanzibar kwa Asilimia 76

 


Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imemtangaza mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa ZEC, Jaji Hamid Mahamoud Hamid amesema  wagombea urais walikuwa 17 waliopigiwa kura  498,786 sawa na asilimia 88.07 ya wapiga kura 566,352 waliojiandikisha.

Amesema kura zilizoharibika zilikuwa 10,944 sawa na asilimia 2.19.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 96 (2 na 3) ya Sheria ya Uchaguzi namba 4 ya 2018, namtangaza rasmi Dk Hussein Ally Mwinyi wa CCM kuwa amechaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, 2020,” amesema.

Jaji Hamid amesema ZEC imehakiki matokeo ya wagombea wote wa Zanzibar na kujiridhisha kuwa yako sahihi.

Amesema mgombea anayefuatia ni Maalim Seif Sharif Hamad wa chama cha ACT Wazalendo aliyepata kura 99,103 sawa na asilimia 19.87.

.


Share:

Thursday, 29 October 2020

AHMED SALUM ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI JIMBO LA SOLWA


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza na wakazi wa Kata ya Didia Halmashauri ya Shinyanga wakati akifunga kampeni za uchaguzi Oktoba 27,2020.

Na Marco Maduhu - Shinyanga 
Mgombea wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Ahmed Salum (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020 baada ya kupata kura 68,066 akifuatiwa na Washington Kasonzo (CHADEMA) aliyepata kura 11,785, Aloyce Shija (CUF) kura 1,111 na Leonard Kitile (NCCR – Mageuzi) kura 526. 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Solwa Hoja Mahiba amesema waliondikishwa kupira kura katika jimbo la Solwa ni 190,962,waliopiga kura ni 83,040,kura halali ni 81,488 na kura zilizoharibika ni 1552.
Share:

Angalia Picha : MAELFU WAJITOKEZA KATAMBI AKIWASHUKURU WANANCHI KUMCHAGUA KUWA MBUNGE SHINYANGA MJINI

Share:

Ester Bulaya apoteza ubunge Bunda Mjini

Ester Bulaya amepoteza jimbo la Bunda Mjini baada ya kushindwa na Robert  Maboto wa CCM  aliyepata kura 31,129 huku Bulaya akipata kura 13,258

Share:

Zitto Kabwe Apoteza Ubunge Kigoma Mjini.....CCM washinda


Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Kigoma Mjini amemtangaza Kirumbe Ng'enda wa CCM kuwa Mshindi wa Ubunge wa Jimbo hilo kwa kupata kura 27,638 akifuatiwa na Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo  aliyepata kura 20,600.


Share:

Lazaro nyalandu Aangushwa Ubunge Singida....CCM Washinda

Mgombea ubunge kupitia Chadema Lazaro Nyalandu ameshindwa ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini baada ya kushindwa na mgombea wa CCM, Rashid Mandoa aliyepata kura 43,847.



Share:

Profesa Jay apoteza Jimbo la Mikumi, CCM washinda

 

Aliyekuwa Mbunge anayeongoza watu na wanyama Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Prof Jay wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kutetea nafasi ya Ubunge baada ya kupitwa na Denis Lazaro wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mikumi amemtangaza Denis Lazaro wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya kiti cha Ubunge kwa kupata kura 31,411 sawa na asilimia 62.7 dhidi ya mpinzani wake Joseph Haule Prof Jay wa CHADEMA aliyepata kura 17,375 sawa na asilimia 34.7


Share:

Mchungaji Peter Msigwa Aangushwa Iringa Mjini.....Aliyeshinda Ubunge ni Jesca Msambatavangu


 Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini amemtangaza Jesca Msambatavangu wa CCM kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 36,034 dhidi ya mpinzani wake Peter Msigwa Chadema aliyepata kura 19,331 .

Mchungaji Peter Msigwa alikuwa akilitetea Jimbo hilo la Iringa aliloliongoza kwa miaka 10
.

Share:

KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI....CCM YANYAKUA KATA ZOTE ...SALOME MAKAMBA AKAMATWA

Patrobas Katambi

Na Damian Masyenene, Shinyanga
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ametangazwa mshindi wa ubunge baada ya kupata kura 31,831.

Katambi ametangazwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho leo Oktoba 29, 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi, huku mpinzani wa karibu wa Katambi, Salome Makamba wa Chadema akiambulia nafasi ya pili kwa kupata kura 16,608.

Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hicho walikuwa ni Godwin Makomba (ACT Wazalendo) aliyepata kura 883, Charles Shigino wa NCCR Mageuzi (133), Abdallah Issa Sube (Demokrasia Makini) kura 99, Yahya Khamis wa UDP kura 69 na Malengo Elias wa TLP kura 65.

Msimamizi huyo wa uchaguzi ameeleza kuwa katika zoezi la upigaji kura Jimbo la Shinyanga Mjini, wapiga kura walioandikishwa ni 120,944, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni 50,453, idadi ya kura halali ni 49,688 na zilizo haribika ni 765.

Katika hatua nyingine, Mwangulumbi amebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vyote vya udiwani katika kata 17 za jimbo hilo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba 

Wakati huo Jeshi Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shi nyanga Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Salome Makamba kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana usiku na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba  tukio hilo limetokea Oktoba 28, mwaka huu saa mbili usiku , ambapo Makamba aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.

ACP Magiligimba amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo, jeshi la polisi lilimsaka mtuhumiwa na kumkamata na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG


Share:

Ester Matiko Aangushwa....Michael Kembaki wa CCM Ashinda Ubunge Tarime Mjini

 Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kushindwa na mshindani wake, Michael Kembaki wa Chama cha Mapinduzi.

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Elias Ntiruhungwa amesema kuwa Kembaki ameshinda kwa kupata kura 18,235 huku Matiko akipata kura 10,873 na mgombea wa NCCR Mageuzi, Ester Nyagabona akipata kura 143.


Share:

🔴LIVE: Tume ya Uchaguzi ikitangaza matokeo ya awali ya urais Nchini Tanzania


🔴LIVE: Tume ya Uchaguzi ikitangaza matokeo ya awali ya urais Nchini Tanzania


Share:

CCM Yashinda Ubunge Mtwara Mjini


 Hassan Seleman  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameshinda ubunge Mtwara Mjini kwa kupata kura 22,411 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Nachuma aliyepata kura 13,586. Hassani Abdallah wa Chama cha ACT-Wazalendo amepata kura 1,113.


Share:

CCM Yashinda Ubunge Jimbo la Handeni

 


Reuben Kwagilwa CCM ametangazwa kushinda ubunge jimbo la Handeni kwa kura 15,241 sawa na asilimia 67 dhidi ya wapinzani wake Sonia Magogo CUF amepata kura 6,713 ADC Twaha Said amepata kura 310, James Stima Chadema amepata kura 296 na Makame Semndili TLP amepata kura 31


Share:

John Heche Aangushwa....Mwita Waitara Ashinda Ubunge Tarime Vijijini


Mwita Waitara CCM ameshinda ubunge Jimbo la Tarime Vijijini kwa kupata kura 35,758 dhidi ya mpinzani wake Heche John aliyepata kura 18,757

Msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Waitara kushinda kwa asilimia 95 dhidi ya mpinzani wake Heche aliyepata asilimia 10



Share:

Hawa Ghasia (CCM) Ashindwa Ubunge.....CUF Yaibuka Kidedea


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini amemtangaza Hassan Mtenga wa CCM kuwa Mshindi wa Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kwa kupata kura 22,411 akifuatiwa na Mgombea wa CUF, Maftaha Abdallah Nachuma aliyepata kura 13,586.


Share:

Sebastian Kapufi (CCM) Ashinda Ubunge Mpanda mjini


Mpanda Mjini:  Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sebastian Kapufi ameshinda nafasi ya Ubunge kwa kupata kura 24,020, akifuatiwa na Rhoda Kunchela wa Chadema aliyepata kura 13,611.





Share:

George Mkuchika Atangazwa Mshindi Kiti cha Ubunge Newala Mjini


 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Newala Mjini Mkoani Mtwara amemtangaza George Huruma Mkuchika wa CCM kuwa Mshindi wa kiti cha Ubunge Newala Mjini kwa kupata kura 18,705 akifuatiwa na Issa Juma Chilindima (CHADEMA) mwenye kura 12,546.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger