Saturday, 4 October 2025

STAND UNITED YATAMBULISHA WACHEZAJI WAPYA


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KOCHA wa Timu ya Pamba Jiji ambayo inashiriki kucheza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026, Francis Baraza, amesema Stand United wana timu nzuri, na wakipata "Support": watafanya vizuri katika Ligi ya Championship na kurejea Ligi kuu.

Amebainisha hayo leo Oktoba 4,2025 mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Stand United katika Tamasha la Siku ya Wana lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage pamoja na kutambulishwa wachezaji wapya wa Stand United.
Amesema mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na kila Timu imeonyesha ubabe wake,na kwamba ameiona Timu ya Stand United namna ilivyocheza kuwa ni Timu nzuri na wanawachezaji ambao wanauzoefu na wamewahi kucheza katika Timu kubwa.

“Timu ya Stand United ni nzuri,inachohitaji ni Support tu kutoka kwa mashabiki wao na wadau wa mpira ili iweze kufanya vizuri zaidi na kurejea ligi kuu,”amesema Baraza.
Kocha wa Timu ya Stand United Idd Cheche,amesema Timu yao ni nzuri ila bado kuna changamoto ndogo ambazo ameziona dhidi ya mchezo wao na Pamba Jiji, na kwamba watarudi katika uwanja wa mazoezi kuzifanyia kazi,na kwamba kabla ya kuanza ligi ya championship watakuwa imara zaidi.

“Mapugufu ambayo nimeyaona siyo mengi,kuna makosa madogo madogo ambayo tunakwenda kuyarekebisha na tutafanya vizuri,”amesema Cheche.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa Timu ya Stand United,anasema kikosi walichonacho ni kizuri zaidi kulika msimu uliopita na kwamba msimu huu wa Champioship lazima warejee ligi kuu.

Amesema,wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo ili kuinga mkono timu hiyo na iweze kusonga mbele na kwamba msimu huu watapita moja kwa moja kushiriki ligi kuu na hakuna tena kucheza playoff.


Aidha,katika Mchezo huo Stand United na Pamba Jiji hadi dakika 90 zinamalizika walitoka bila ya kufungana.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa Timu ya Stand United akizungumza.
Kocha wa Pamba Jiji Francis Baraza akizungumza.
Kocha wa Timu ya Stand United Idd Cheche akizungumza.
Wachezaji wapya wa Timu ya Stand United Chama la Wana.
Share:

DKT. NINDI: SERIKALI ITAENDELEA KUWA KARIBU NA WAKULIMA ILI KUHAKIKISHA CHANGAMOTO ZINATATULIWA KWA WAKATI

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Stephen Nindi, ameongoza kikao maalum katika Bonde la Uyole, Mbeya, tarehe 03 Septemba 2025 kilicholenga uhamasishaji wa matumizi ya Mbolea. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi wa Serikali, wataalamu wa kilimo na wakulima, jambo lililoonesha mshikamano mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza mwanzoni mwa kikao, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Rodrick Mpogolo, alieleza umuhimu wa Mkoa wa Mbeya kama kitovu cha kilimo kwa Nyanda za Juu Kusini na kubainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia upimaji wa udongo na kuongeza tija kwa wakulima. Alisisitiza kuwa fursa zilizopo, hususan kwenye kilimo cha Mpunga, Chai, Parachichi na Kokoa, zinaweza kuongeza uchumi wa wakulima endapo changamoto ndogo zilizopo zitatatuliwa kwa ushirikiano.


Wakulima wa Scheme ya Iganjo walioshiriki kikao hicho wameipongeza Serikali kwa juhudi zake, huku wakibainisha maeneo yanayohitaji kuimarishwa. Wameeleza kuwa upatikanaji wa pembejeo bora na za gharama nafuu, pamoja na huduma za ugani zinazowafikia moja kwa moja shambani, ni mambo muhimu yatakayoongeza uzalishaji na ubora wa mazao yao.

Aidha, wakulima wameonesha imani kubwa kwa Serikali kutokana na hatua za kivitendo zinazochukuliwa, ikiwemo ushirikiano wa karibu na taasisi kama TFRA na TARI katika kupima udongo na kushauri matumizi sahihi ya mbolea. Wamesema matarajio yao ni kuona elimu hiyo ikiwafikia wakulima wengi zaidi ili kuboresha mavuno na kipato cha kaya.

Wataalamu kutoka taasisi mbalimbali wamewatoa hofu wakulima kwa kueleza kwamba tayari kuna mpango wa kusambaza vifungashio vya mbolea vinavyokidhi mahitaji ya wakulima wadogo, kuhakikisha mawakala wanabandika bei za mbolea za ruzuku kwa uwazi, na kuongeza kasi ya upimaji wa udongo katika maeneo yote ya Mkoa wa Mbeya.

Dkt. Nindi, katika hotuba yake, amewashukuru wakulima kwa mwitikio wao mkubwa na kusisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la mkulima ili kunufaika na ruzuku za Serikali. Pia alielekeza kuanzishwa kwa mashamba darasa kwa kushirikiana na wadau, pamoja na kuhakikisha kuwa huduma za ugani zinawafikia wakulima mara kwa mara.

Mkutano huo ulimalizika kwa matumaini mapya, huku wakulima wakiondoka wakiwa na ari ya kuongeza uzalishaji na kushirikiana na Serikali katika safari ya kukuza sekta ya kilimo. Hatua zilizopendekezwa na maagizo yaliyotolewa yametafsiriwa na wakulima kama suluhisho la changamoto nyingi, na uthibitisho kuwa kilimo kinaendelea kuwa injini ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

 

Share:

KARIBU SPECIALISED EYE CLINIC KAHAMA - UPIMAJI MACHO BURE OKTOBA 9

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger