Wednesday, 1 October 2025

WAANDISHI WA HABARI TABORA WAPEWA MAFUNZO KUKABILIANA NA TAARIFA NA HABARI POTOFU KIPINDI CHA UCHAGUZI

Mwezeshaji wa mafunzo ya kupambana na habari potofu (fake news), Kadama Malunde akitoa mada kuhusu mbinu za kubaini taarifa/habari potofu/uzushi kwa waandishi wa habari mkoa wa Tabora

Mwezeshaji wa mafunzo ya kupambana na taarifa potofu (fake news), Kadama Malunde, akiwasilisha mada kuhusu mbinu za kubaini na kukabiliana na taarifa/uzushi kwa waandishi wa habari mkoa wa Tabora.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kupambana na habari potofu (fake news), misinformation na disinformation kwa waandishi wa habari mkoa wa Tabora

 ***

Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), umetoa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari mkoani Tabora yenye lengo la kupambana na changamoto za habari na taarifa potofu (fake news) hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili Oktoba 1 - 2,2025) yanayofanyika Mkoani Tabora Afisa Programu wa UTPC, Andrew Marawiti, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Ukweli Kwanza wenye lengo kuu la kuimarisha weledi wa waandishi wa habari na uimara wa wananchi dhidi ya upotoshaji wa habari hasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

“Tunataka kuwajengea uwezo angalau waandishi wa habari 100 juu ya mbinu za kukabiliana na habari habari potofu (misinformation), upotoshaji (disinformation) uhakiki wa taarifa na mbinu za kisasa za kutumia Akili unde (Artificial Intelligence) katika kuthibitisha ukweli wa habari. 

Pia tunalenga kuwawezesha waandishi chipukizi, hususani wanawake, ili wawe mstari wa mbele katika mapambano haya,” amesema Marawiti.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog, ametoa mada kuhusu namna ya kutambua na kupambana na taarifa na habari potofu 'Fake News'.

Katika wasilisho lake, Malunde ameeleza kuwa mitandao ya kijamii imekuwa chanzo kikubwa cha kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi, hususani katika nyakati nyeti kama uchaguzi, majanga au masuala ya afya.

Ametaja aina za taarifa potofu kuwa ni pamoja: Misinformation – taarifa zisizo sahihi lakini hazikusudiwi kudanganya (mfano: kusambaza picha ya tukio la zamani ukidhani ni la sasa), Disinformation – taarifa za uongo zinazotengenezwa kwa makusudi ili kupotosha (mfano: propaganda za kisiasa), Malinformation – taarifa sahihi zinazotolewa kwa nia ovu au nje ya muktadha (mfano: kutumia taarifa ya kweli kumdhalilisha mtu) na Fake News – habari za kughushi ambazo huwasilishwa kama taarifa halali (mfano: uongo kuhusu viongozi wa kitaifa).

Malunde amesisitiza kwamba jukumu la waandishi wa habari ni kuhakikisha hawasambazi taarifa bila uhakiki, bali wawe mabalozi wa ukweli na weledi katika jamii.

“Watu wengi hushindwa kutofautisha ukweli na uongo. Hali hii inachangia kusambaa kwa habari potofu ambazo huiga muundo wa habari halali kutoka magazeti au vituo vya habari, lakini hubeba maudhui ya uongo au yaliyopotoshwa. Fake News ni aina ya misinformation au disinformation ambayo huwasilishwa kama ‘habari ya kweli’, lakini kimsingi ni ya uongo, imeundwa kupotosha, kuchochea hisia au kuendeleza ajenda fulani,” ameeleza Malunde.

Amezitaja mbinu muhimu za kukabiliana na changamoto hiyo kuwa ni pamoja na kuepuka kusambaza taarifa mara tu unapoiona mtandaoni.

“Usikubali taarifa kwa urahisi; fikiria kabla ya kusambaza. Soma zaidi ya kichwa cha habari kwani mara nyingi hupotosha maana halisi ya taarifa. Kagua picha, video na maandishi kwa makini kabla ya kuamini au kusambaza”.

“Chanzo cha taarifa kina maana kubwa. Kabla hujaamini, hakikisha kwanza uhalali wa yule anayekuletea taarifa hiyo. Usisambaze taarifa kabla ya kuthibitisha ukweli wake ili kuepuka kusambaza upotoshaji. Tafuta taarifa hiyo kutoka kwa vyombo vya habari vinavyoaminika au wataalamu wa uhakiki wa ukweli (fact-checkers)”,ameongeza Malunde.

 Washiriki wamefundishwa mbinu mbalimbali za uthibitishaji wa habari, ikiwemo kutumia reverse image search kupitia Google na njia nyingine kugundua asili ya picha na video, kulinganisha taarifa na vyanzo vinavyoaminika, pamoja na kusoma zaidi ya vichwa vya habari ili kuhoji uhalisia wake.

Mafunzo haya yanafanyika ikiwa Tanzania inajiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wakati changamoto ya upotoshaji wa taarifa mitandaoni imekuwa kubwa duniani kote.

UTPC inatarajia kuwa kupitia mafunzo haya yanayotekelezwa kwa kushirikiana Taasisi ya Jamii Africa, kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uholanzi - Tanzania, waandishi wa habari wataimarika katika kulinda maadili ya taaluma na kusaidia wananchi kupata taarifa sahihi, hatua itakayoongeza imani kwa vyombo vya habari na kuimarisha mchakato wa uchaguzi.
Share:

DKT.ABDALLAH AZINDUA KIWANDA DARASA CHA KUBANGUA KOROSHA CHA CAMARTEC MANYONI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiangalia jinsi korosho zinavyobanguliwa mara baada ya kuzindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika  Septemba 30,2025.

Na.Alex Sonna-MANYONI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, amesema uanzishwaji wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni ni hatua muhimu katika kuongeza thamani ya zao la korosho na kukuza ajira kwa wananchi hususan wanawake na vijana.

Akizungumza Septemba 30,2025 wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho, Dkt. Abdallah amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuliwezesha zao la korosho kupitia utafiti, pembejeo zenye punguzo na mafunzo kwa wakulima, hivyo kuhitajika uwekezaji sambamba wa kuongeza thamani.

“Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 494 kufanikisha uanzishwaji wa kiwanda hiki. Lengo letu ni kuhakikisha wakulima na wajasiriamali hawabaki wauzaji wa malighafi pekee, bali wanapata nafasi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye thamani kubwa zaidi,” amesema Dkt. Abdallah.

Aidha ametaja bidhaa zinazoweza kupatikana kutokana na ubanguaji na uchakataji wa Korosho kuwa ni pamoja na siagi ya korosho, juisi ya mabibo, mvinyo wa mabibo, mafuta ya ganda la korosho, kuni mbadala na mabibo makavu ambapo bidhaa hizo zina soko kubwa ndani na nje ya nchi, na zitasaidia kuongeza mapato kwa wananchi na Taifa kupitia fedha za kigeni.

Dkt. Abdallah amesema kuwa Kiwanda hicho pia kitaleta suluhu ya changamoto za ukosefu wa teknolojia na elimu ya amali ya kuchakata korosho na mabibo, jambo ambalo limekuwa likiwakwamisha wakulima na wajasiriamali wadogo.

“Kukosekana kwa viwanda vya kuchakata kumetufanya tubaki wauzaji wa korosho ghafi pekee, hali iliyodumaza bei ya zao hili. Bidhaa zilizoongezwa thamani zina soko pana na ndizo zenye faida kubwa,” Amesisitiza.

Amesema kuwa mbanguaji wa korosho kwa kutumia teknolojia za kawaida ana uwezo wa kubangua kati ya kilo 40 hadi 80 kwa masaa nane, na kutoa kilo 10 hadi 20 za korosho zilizokamilika, hali ambayo inaonyesha nafasi kubwa ya kiwanda hicho kuwa kichocheo cha ujasiriamali na ajira.

Hata hivyo , amewataka wananchi wa Manyoni na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za mafunzo na ujasiriamali zitakazotolewa kupitia kiwanda hicho,zitasaidia kuongeza kipato, kukuza ajira na kuimarisha ushindani wa soko la korosho nchini.

“Ni imani yangu kuwa wananchi wataendelea kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuendeleza sekta ya viwanda kwa manufaa ya Taifa,” amesema Dkt. Abdallah

Pia Dkt. Abdallah amehitimisha kwa kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha viwanda vya aina hiyo vinaanzishwa katika maeneo mengine ya uzalishaji wa korosho ili Tanzania isinufaishe tu kwa kuuza ghafi, bali pia bidhaa kamili zinazotokana na korosho na mabibo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt Vincent Mashinji amesema Wilaya yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara Pamoja na Wizara nyingine za kisekta katika kuendeleza na kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara hususani katika kuendeleza Viwanda vidogo vya Kati na vikubwa ili kuongeza Ajira, Pato la Taifa na kukuza uchumi kwa ujumla.

Awali akitoa taarifa ya kiwanda hicho Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama ameeleza chimbuko la kiwanda hicho ni utafiti wa uhitaji wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini ambnao umekuwa ukifanyika mara kwa mara na Serikali kupitia utafiti huo ulibaini kuwa ubanguaji wa korosho nchini,hususani kwa wakulima na wabanguaji wadogo ni changamoto.

"Lengo kuu la kiwanda hicho ni kutoa mafunzo,hivyo kiwanda kina kazi kubwa ya kuhakikisha watanzania wenye nia ya kuwekeza,kujiari au kuajiriwa kwenye ubanguaji wa korosho wanapata elimu sahihi ya amali katika eneo hilo"amesema

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Camartec, Prof. Valerian Silayo,amesema kuwa kiwanda hicho cha kubangua korosho ni miongoni mwa hatua zinachukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto kwenye kuchakata mazao ya kilimo,Mifugo,Uvuvi na Misitu.

"Serikali kupitia CAMARTEC inaendelea kufanya utafiti utakaopelekea kutatua changamoto za upotevu wa mazao mbalimbali kwa kubuni teknolojia sahihi zenye ufanisi na uhimili wa korosho"Amesema Prof.Silayo


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, akipokelewa mara baada ya kuwasili katika Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa ajili ya kukizindua kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, akipokelewa mara baada ya kuwasili katika Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa ajili ya kukizindua kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akizindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiangalia jinsi korosho zinavyobanguliwa mara baada ya kuzindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiangalia jinsi korosho zinavyobanguliwa mara baada ya kuzindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiangalia jinsi korosho zinavyobanguliwa mara baada ya kuzindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiangalia jinsi korosho zinavyobanguliwa mara baada ya kuzindua Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida,hafla iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt Vincent Mashinji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi.Anastazia Tutuba Ruhamvya ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Camartec, Prof. Valerian Silayo,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama,akitoa taarifa ya kiwanda hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo katika Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho cha Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Masigati wilayani Manyoni Mkoani Singida, iliyofanyika leo Septemba 30,2025.
Share:

WATOTO WAPEWE ULINZI, WASIINGIZWE KWENYE SIASA – NSSC


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Umoja wa Kitaifa wa Asasi za Kiraia wa Shule Salama (NSSC) umetoa rai kwa vyama vya siasa na wagombea nchini kuepuka kuwatumia wanafunzi na watoto katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ukisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za watoto na kinyume cha sheria.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, wanachama wa umoja huo wamesema kumekuwepo na matukio ya wanafunzi kutolewa darasani kushiriki mikutano ya kampeni, hali ambayo ni hatari kwa usalama, ustawi na haki ya mtoto ya kupata elimu.

Mkuu wa Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Bw. Makumba Mwemezi, aliyemuwakilisha Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, amesema ni wajibu wa asasi za kiraia kulinda watoto hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

“Malezi na makuzi ya mtoto ni suala la kitaifa linalovuka mipaka ya kisiasa. Tunataka kuona asasi za kiraia zikisikia na kuzungumza kwa niaba ya watoto, badala ya kunyamaza wakati haki zao zinavunjwa,” amesema Mwemezi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Programu kutoka shirika la My Legacy, Amina Ali, amesema kuna viashiria vya ongezeko la matumizi ya watoto kwenye shughuli za kisiasa, jambo linalokiuka Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 (Tanzania Bara) na Sheria ya Mtoto Zanzibar Na. 6 ya mwaka 2011.

“Tunahimiza vyama vyote vya siasa na wagombea kujitenga kabisa na matumizi ya watoto kwenye kampeni. Ni hatari kwa makuzi yao na ni kinyume cha sheria,” amesema.

Naye Meneja Mradi kutoka Tanzania Child Rights Forum (TCRF), Rogasian Masawe , ameongeza kuwa mazingira ya kampeni si rafiki kwa watoto kutokana na msongamano, kelele, lugha kali na vurugu zinazoweza kutokea.

“Watoto hawapaswi kuwepo katika mazingira hayo, hata kama ni kama watazamaji tu,” amesema 

Kwa upande wake, Bi. Cleopatra Ngesi kutoka TAMWA, ametoa wito kwa vyombo vya habari kuhakikisha havitumii picha au kauli zinazodhalilisha watoto katika taarifa za uchaguzi.

“Ni wajibu wa wanahabari kuwalinda watoto badala ya kuwafanya nyenzo za kisiasa,” amesema.

Aidha, Mratibu wa Mradi wa Jukwaa la Utu wa Toto (CDF), Irene Ernest, amewasihi wazazi na jamii kuhakikisha watoto hawaingii maeneo ya kampeni, vituo vya kupigia kura au mikusanyiko ya kisiasa.

“Wazazi wanapaswa kuwa walinzi wa mstari wa mbele wa watoto wao. Huu si wakati wa kuwaacha mitaani au kuwapeleka kwenye mikutano ya kisiasa. Haki ya mtoto ya kulindwa ni ya kikatiba,” amesema Bi. Irene.

Kwa pamoja, wanachama wa NSSC wamesema wanatarajia kuona Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa amani huku haki na usalama wa watoto vikitangulizwa mbele kama kipaumbele cha taifa.

p>
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger