Thursday, 14 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 14,2025

 


 

   

                

    


Share:

Wednesday, 13 August 2025

WAWILI WAKWAMA WAKATI WA TENDO, MAMIA WAJITOKEZA KUSHUHUDIA


Kizazaa kilizuka baada ya mwanaume mmoja na mwanamke waliodaiwa kuwa katika uhusiano wa siri kukwama wakati wa tendo la ndoa. Tukio hilo lilijiri majira ya alfajiri kwenye nyumba ya kulala wageni iliyo karibu na soko kuu, na liliwavutia mamia ya wakazi waliokusanyika kushuhudia kisa hicho kisicho cha kawaida.

Mashuhuda wanasema kwamba kelele za maumivu kutoka chumbani ziliwashtua wahudumu wa hoteli, ambao walipojaribu kuingia ndani walikuta mlango umefungwa kwa ndani. Ilibidi wavunje mlango, ndipo wakawakuta wawili hao wakiwa wamelala uchi na wakilia kwa uchungu, wakiwa wamekamatana na kushindwa kutengana hata walipojaribu kujitoa kwa nguvu.
Share:

Tuesday, 12 August 2025

HANDENI MJI YAALIKA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MRADI WA KUCHAKATA MAWE



Na Mwandishi Wetu, Handeni

HALMASHAURI ya Mji Handeni, mkoani Tanga, imetoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika mradi wa kuchakata mawe na kokoto ili kuongeza mapato ya ndani na kuchochea maendeleo ya halmashauri hiyo.

Akizungumza Agosti 12, 2025 katika ziara ya kukagua mradi huo uliopo milima ya madini ya mawe ya Kwedihegwa na Kwaluhizo Kata ya Kideleko mjini humo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Maryam Ukwaju, amesema mradi huo unatarajiwa kuwa chanzo kipya cha mapato ambacho kitatoa ajira kwa wananchi wa maeneo jirani, sambamba na kuchangia utekelezaji wa miradi ya kijamii.

“Niagize Idara ya viwanda, biashara na uwekezaji harakisheni kukamilisha taratibu zote muhimu na kuweka mazingira wezeshi na taratibu za kupata mbia zitafanyika kwa kutumia mifumo ya ununuzi wa umma kwa kushirikiana Kituo cha uwekezaji kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP Center),”amesema.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara, Danson Mongi, amesema mchakato wa kuwekeza katika milima hiyo uliidhinishwa katika vikao vya kamati ya fedha na utawala na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani Mei 8, 2025.

Amesema hadi sasa Halmashauri ya Mji imelipia leseni za uchimbaji mdogo ambazo zimetolewa na Tume ya Madini Julai 18, 2025 kwa kipindi cha miaka saba ambazo ni PML Na.02977 katika mlima Kwaluhizo lenye ukubwa wa Hekta 4.96 na PML Na.02978 kwenye mlima Kwedihegwa lenye ukubwa wa Hekta 4.97.


Na Mwandishi Wetu, Handeni

HALMASHAURI ya Mji Handeni, mkoani Tanga, imetoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika mradi wa kuchakata mawe na kokoto ili kuongeza mapato ya ndani na kuchochea maendeleo ya halmashauri hiyo.

Akizungumza Agosti 12, 2025 katika ziara ya kukagua mradi huo uliopo milima ya madini ya mawe ya Kwedihegwa na Kwaluhizo Kata ya Kideleko mjini humo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Maryam Ukwaju, amesema mradi huo unatarajiwa kuwa chanzo kipya cha mapato ambacho kitatoa ajira kwa wananchi wa maeneo jirani, sambamba na kuchangia utekelezaji wa miradi ya kijamii.

“Niagize Idara ya viwanda, biashara na uwekezaji harakisheni kukamilisha taratibu zote muhimu na kuweka mazingira wezeshi na taratibu za kupata mbia zitafanyika kwa kutumia mifumo ya ununuzi wa umma kwa kushirikiana Kituo cha uwekezaji kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP Center),”amesema.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara, Danson Mongi, amesema mchakato wa kuwekeza katika milima hiyo uliidhinishwa katika vikao vya kamati ya fedha na utawala na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani Mei 8, 2025.

Amesema hadi sasa Halmashauri ya Mji imelipia leseni za uchimbaji mdogo ambazo zimetolewa na Tume ya Madini Julai 18, 2025 kwa kipindi cha miaka saba ambazo ni PML Na.02977 katika mlima Kwaluhizo lenye ukubwa wa Hekta 4.96 na PML Na.02978 kwenye mlima Kwedihegwa lenye ukubwa wa Hekta 4.97.
Share:

MGAOMBEA URAIS WA CCK ACHUKUA FOMU INEC, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE




Na Dotto Kwilasa, Dodoma

David Daud Mwaijojele, amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Kijamii (CCK)katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, baada ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza dirisha la uchukuaji wa fomu kwa wagombea urais.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha taratibu zote katika makao makuu ya NEC jijini Dodoma leo Agosti 12,2025, Mwaijojele amemshukuru Mwenyekiti wa Tume na watendaji wake kwa kuendesha mchakato huo kwa utaratibu mzuri, uwazi na ufanisi.

“Nawashukuru INEC kwa maandalizi bora na usimamizi wa kitaalamu wa zoezi hili,hii ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba,” amesema.

Mwaijojele ameeleza kuwa CCK imejipanga kuendesha kampeni zinazolenga masuala yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja, akitaja vipaumbele vikuu kuwa ni kuendeleza kilimo cha kisasa, kuongeza ajira hasa kwa vijana, kuboresha elimu, pamoja na kuimarisha ustawi wa wastaafu.

Amesisitiza kuwa sera za chama chake zitaweka mazingira rafiki yatakayo wezesha wastaafu kustaafu kwa kujiamini na kuishi kwa amani, akisema wastaafu wengi huingiwa na hofu kutokana na changamoto za kiuchumi baada ya kustaafu.

Katika sekta ya kilimo, Mwajojele amesema CCK itahakikisha upatikanaji wa pembejeo bora, masoko ya uhakika na teknolojia ya kisasa ili kuongeza tija na kipato cha wakulima huku akiahidi elimu walimu na ubora wa mitaala.

Mwajojele atakuwa akiwania nafasi ya urais akiwa na mgombea mwenza, Masoud Ali Abdalla, ambaye ameahidi kushirikiana naye kikamilifu kutekeleza sera na mikakati ya chama.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umepangwa kufanyika Oktoba 2025, na zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea litaendelea kwa muda uliopangwa na NEC.

Share:

Monday, 11 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 12,2025



Magazeti

Share:

Sunday, 10 August 2025

NILIACHWA NA KILA RAFIKI BAADA YA KUWA TAJIRI GHAFLA, SIRI YA MAFANIKIO YANGU ILIPOJULIKANA WOTE WALITUBU



Nilikuwa nimezoea maisha ya kawaida ya umaskini. Siku zote nilipambana kuendesha maisha yangu, nikitafuta vibarua vya hapa na pale mjini Mbeya ili nipate pesa ya chakula na kodi. 

Nilikuwa na marafiki wengi wa karibu hasa wanawake tuliokuwa tukisaidiana kila mara mambo yalipoenda kombo. Tulikuwa kama dada; nilifikiri urafiki wetu ungekuwa wa milele.
Share:

WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA EWURA NANENANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI



Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina, akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maonesho ya Wakulima ya Nane Nane, Kanda ya Ziwa Magharibi, yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Na.Mwandishi Wetu.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupitia maonesho ya Wakulima ya Nane Nane, Kanda ya Ziwa Magharibi, imefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 300, wakiwemo waliowasilisha malalamiko mbalimbali yanayohusu huduma za umeme na maji.

Hayo yameelezwa Agosti 8, 2025 na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Mhina amesema katika kipindi cha maonesho hayo , banda la EWURA lilitembelewa na wastani wa watu 40 hadi 50 kwa siku, waliopata huduma za elimu pamoja na fursa ya kuwasilisha changamoto zao.

“Tumepokea malalamiko mbalimbali, hasa kuhusu ucheleweshwaji wa kuunganishiwa umeme pamoja na matatizo kwenye ankara za maji. Baadhi ya changamoto tumeweza kuzitatua papo kwa papo,” amesema Mhina.

Ameongeza kuwa kupitia ushiriki huo, EWURA imeweza kuwafikia wananchi wa aina zote kutoka wale wenye kipato kikubwa hadi wa kipato cha chini ambao mara nyingi hawapati fursa ya kufika katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo mijini.

Mhina alibainisha kuwa EWURA imebaini baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi zingeweza kutatuliwa na watoa huduma kama TANESCO na mamlaka za maji iwapo zingetatuliwa kwa uwajibikaji wa karibu zaidi.

“Tuna mpango wa kufanya kikao cha pamoja na TANESCO na mamlaka zote za maji katika Kanda ya Ziwa kabla ya mwisho wa Septemba. Lengo ni kutoa semina elekezi kwa watoa huduma na wanasheria wao ili kukumbushana wajibu wao kwa wananchi,” alisema Mhina.

Aidha, alisema baadhi ya malalamiko yataanza kufanyiwa kazi kuanzia wiki inayofuata, na kusisitiza kuwa EWURA itaendelea kuhakikisha watoa huduma wanazingatia viwango vya ubora na utoaji wa huduma kwa mujibu wa sheria.

Mhina pia alisema ushiriki wa EWURA katika maonesho hayo umetimiza moja ya majukumu yake ya msingi ya utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika kupata huduma bora za nishati na maji.

“Kupitia majukwaa kama haya, tunatoa elimu ya moja kwa moja kwa wananchi kuhusu namna ya kushughulikia changamoto zao, taratibu za kupata huduma, pamoja na kuelewa wajibu wa mtoa huduma,” aliongeza.
Share:

KIBONDE WA CHAMA CHA MAKINI ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS INEC



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde. Mgombea huyo wa MAKINI aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Aziza Haji Suleiman (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde. Mgombea huyo wa MAKINI aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Aziza Haji Suleiman (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. Kusho ni Mhe. Jaji Asina Omar akiwa na Mhe. Balozi Ramadhani Omar Mapuri.
Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. Kulia ni Mhe. Dkr. Zakia Mohamed Abubakar akiwa na Mhe. Magadalena Rwebangira



Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Mahakam aya Rufaa Jacobs Mwambegele






Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza


Mgombea akisaini kitabu


Mgombea Mwenza akisaini kitabu
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger