Thursday, 31 July 2025

✨ VICTORIOUS BEAUTY GALLERY – KITUO CHA MITINDO NA UREMBO MJINI SHINYANGA!

@malundeblog

✨ VICTORIOUS BEAUTY GALLERY – KITUO CHA MITINDO NA UREMBO SHINYANGA! Karibu Victorious Beauty Gallery, kituo cha kipekee kinachokuletea bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zinazokamilisha urembo na mtindo wako. Hapa, tunakuletea kila kitu kinachokufanya uonekane wa kipekee na ujiamini kila siku! πŸ’Ό Mabegi ya Kifahari Tunayo mabegi, mikoba ya sherehe yanayong’aa, ya ofisini yenye mvuto hadi ya kila siku yenye ubora wa kipekee – tunayo yote! πŸ’ Vifaa vya Urembo Mikufu, pete na hereni, cheni, bracelets, zinazoongeza haiba na mvuto wako kwa kila tukio. πŸ‘™ Nguo za Ndani Kwa faraja na urembo wa kweli – tunakupa nguo za ndani kwa ajili ya wanaume na wanawake zenye ubora wa kimataifa zinazokupa kujiamini. ⌚ Saa za Kisasa Onyesha hadhi yako kwa saa zenye mvuto wa kifahari na mitindo ya kipekee. 🏺Marashi Yenye Ubora Nukia kitajiri na marashi bora kabisa na yakipekee yatakayo kupa kujiamini siku yako nzima. 🎁 Kwa Nini Utuchague? ✅ Bidhaa za ubora wa juu ✅ Bei nafuu zinazokubaliana na kila bajeti ✅ Huduma ya heshima na ya kirafiki ✅ Bidhaa mpya kila siku πŸ“Œ Tembelea Duka Letu Leo! Ngokolo Mtumbani – Jengo la Shija Lodge, Mkabala na Kanisa la FPCT πŸ“² Wasiliana nasi: 0756 955 516 🌟 Victorious Beauty Gallery Urembo Wako, Fahari Yetu!

♬ Mali safi - Guddy the G


VICTORIOUS BEAUTY GALLERY – KITUO CHA MITINDO NA UREMBO MJINI SHINYANGA!

Karibu Victorious Beauty Gallery – Duka lako la kisasa linalokuletea bidhaa bora zinazokuongezea mvuto, haiba, na kujiamini kila siku!

πŸ’Ό Mabegi ya Kifahari

Tunatoa mabegi ya aina mbalimbali – ya ofisini, ya sherehe, na ya kila siku – yote yakiwa ya kisasa, yenye uimara na mvuto wa kipekee.

πŸ’ Vifaa vya Urembo

Pete, mikufu, hereni, cheni, na vikuku vinavyoongeza mng’ao wa urembo wako kwa kila tukio na mavazi.

πŸ‘™ Nguo za Ndani zenye Ubora wa Kimataifa

Kwa wanawake na wanaume – laini, maridadi na za kuvutia. Unapendeza ndani na nje!

Saa za Kisasa

Saa zinazoonyesha hadhi yako – kutoka mitindo rasmi hadi casual, zote zikiwa bora na zenye kuvutia.

🏺 Marashi ya Kipekee

Nukia tofauti! Tunayo manukato ya kisasa yenye harufu ya kuvutia, ya kudumu na ya kipekee.

🎁 Kwa Nini Uchague Victorious Beauty Gallery?

✅ Bidhaa zenye ubora wa juu
✅ Bei nafuu na rafiki kwa bajeti yako
✅ Huduma ya kitaalamu, ya heshima na ya kirafiki
✅ Bidhaa mpya kila siku – uwe wa kwanza kung’ara!

πŸ“Œ Tembelea Duka Letu:
Ngokolo Mtumbani, Jengo la Shija Lodge, Mkabala na Kanisa la FPCT, Shinyanga.

πŸ“ž Wasiliana Nasi Sasa: 0756 955 516

🌟 Victorious Beauty Gallery – Urembo Wako, Fahari Yetu! 🌟













Share:

MWENGE WA UHURU KUPOKELEWA 'Kagongwa' SHINYANGA AGOSTI 3! RC MBONI MHITA ASEMA UTAPITIA MIRADI YA BILIONI 17.3

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni M. Mhita, anatarajiwa kuongoza mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaowasili rasmi mkoani Shinyanga tarehe 3 Agosti 2025, ukitokea mkoani Tabora. Mwenge huo utapokelewa katika Kituo cha Mabasi cha Kagongwa, kilichopo Wilaya ya Kahama.

Katika ziara hiyo ya Mwenge, unatarajiwa kukimbizwa kwa umbali wa kilometa 819.2 ndani ya halmashauri zote sita za mkoa huo, ukipitia miradi 44 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi bilioni 17.3.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, Mwenge huo utakagua, kufungua na kuzindua miradi ya afya, elimu, maji, miundombinu na shughuli za vijana na wanawake zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mhita, amewaomba wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki mapokezi ya Mwenge huo wa kitaifa kama ishara ya mshikamano, uzalendo na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha huduma kwa jamii.

“Mapokezi haya ni ya kihistoria, hivyo ni fursa kwa wananchi kuonyesha mshikamano wao na kufuatilia kwa ukaribu ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unaohamasisha amani, maendeleo, mapambano dhidi ya rushwa na matumizi ya dawa za kulevya,” amesema Mhita.

 Mwenge wa Uhuru 2025 unatarajiwa kuwa chachu ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Share:

MARIAM IBRAHIM, HAWA MCHAFU WAIBUKA KIDEDEA UBUNGE VITI MAALUM PWANI


Kibaha, Julai 30, 2025: Katika uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika leo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kwamfipa – Kibaha Mjini, wagombea Hawa Mchafu Chakoma na Mariam Ibrahim awameibuka vinara katika nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani.

Jumla ya wagombea wanane (8) waliingia kwenye kinyang'anyiro hicho, ambapo kura 2,108 zilipigwa huku kura halali zikiwa ni 2,103 na kura 5 zikiwa zimeharibika. Wapiga kura waliojitokeza ni 2,095.


Katika matokeo hayo:


● Hawa Mchafu alipata kura 802


● Mariam Ibrahim alipata kura 645


● Nancy Mutalemwa kura 449


Fatuma Uwesu (71), Irene Makongoro (52), Sifa Mwaruka (44), Rehema Issa (26), na Rehema Mssemo (7).


Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi, zoezi hilo lilifanyika kwa amani na utulivu mkubwa, huku wajumbe wa CCM wakionyesha hamasa ya hali ya juu kuchagua wanawake watakaowakilisha mkoa huo bungeni.


Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Hawa Mchafu aliwashukuru wajumbe wa CCM kwa kuendelea kumuamini na kuahidi kuwa sauti ya wanawake na vijana wa Pwani haitazimika ndani ya Bunge.


“Nitashirikiana na kila mmoja wenu kuimarisha mshikamano, maendeleo ya kijinsia na ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kitaifa,” alisema Hawa Mchafu.


Kwa upande wake, Mariam Ibrahim – ambaye ni miongoni mwa nyuso mpya zilizowika kwenye kinyang’anyiro hicho – alielezea furaha yake kwa kupewa fursa ya kuwakilisha kundi la wanawake na vijana wapya katika siasa za mkoa huo.


Zoezi hilo linaonesha msukumo wa CCM wa kuendeleza usawa wa kijinsia na kutoa nafasi kwa viongozi vijana, hasa wanawake, kushiriki katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia Bunge.




Share:

JUMBE AAHIDI USHIRIKIANO KWA WAGOMBEA WALIOPENYA MCHUJO UBUNGE SHINYANGA MJINI "UONGOZI NI HITAJI LA WAKATI"


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe, aliyekuwa akiwania kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ameishukuru CCM kwa kumpa nafasi ya kushiriki katika mchakato wa awali wa kura za maoni ndani ya chama.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Jumbe amesema kuwa ingawa jina lake halijarudi katika orodha ya waliopitishwa, mchakato huo umempa uzoefu mkubwa kisiasa na umemjenga zaidi katika uelewa wa chama.

Nashukuru chama changu kwa kunipa nafasi ya kushiriki mchakato huu bila vikwazo vyovyote. Nimejifunza mengi na nimepata fursa ya kuimarika zaidi kisiasa. Nipo tayari kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu na kupigania ushindi wa chama chetu katika uchaguzi mkuu,” amesema Jumbe.

Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na wagombea waliopitishwa na kutoa ushirikiano wote unaohitajika kuhakikisha CCM inabaki imara.

Uongozi ni wa wakati, na naamini chama chetu kimetoa nafasi kwa watu sahihi,” amesisitiza.
Kwa sasa, Jumbe amewataka wanachama na wafuasi wake kuungana na chama katika kuhakikisha ushindi wa CCM unaendelea kushamiri Shinyanga Mjini na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempitisha Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, kugombea tena ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini. Katambi sasa atachuana na wagombea wengine waliopitishwa, akiwemo mwanasiasa mkongwe Stephen Masele, aliyewahi kulitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 (2010–2020) na kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Naibu Waziri wa Nishati na Madini.

Wengine waliopitishwa ni Abubakar Gulamhafiz Mukadam, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, pamoja na Eustard Athanace Ngatale, Hassan Athuman Fatiu, Hosea Muza Karume na Paul Joseph Blandy, ambao kwa pamoja wanatajwa kuongeza mvuto na msisimko wa kisiasa katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha, mchakato huu unaelezwa kuwa unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu, kwani Katambi na Masele wanatajwa kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa.

Imeelezwa kwamba iwapo jina la Jumbe, ambaye pia alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na nguvu alizojijengea kwa wananchi, lingerejea, Shinyanga Mjini ingeshuhudia mapambano makali ya kisiasa kati ya vigogo hao watatu.
"Licha ya jina lake kutorudi, wachambuzi wa siasa wanasema ushawishi wa Mhandisi James Jumbe umeacha alama kubwa ndani ya CCM na jamii. Iwapo jina lake lingerejea, Shinyanga Mjini ingeshuhudia kinyang’anyiro cha kihistoria dhidi ya vigogo watatu akiwemo yeye (Jumbe)  na Patrobas Katambi pamoja na Stephen Masele.

Kama jina la Jumbe lingerejea, mapambano yangekuwa makali zaidi, Jumbe ana mtaji wa moja kwa moja wa wananchi na chama, hali hiyo ingeibua kinyang’anyiro cha kweli cha ‘nguvu tatu’ - Jumbe-Masele-Katambi ambacho kingetikisa siasa za Shinyanga Mjini”, wanasema Wachambuzi wa siasa.

Mchakato wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 unaendelea.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger