Thursday, 10 July 2025
SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA UONGOZI NA USIMAMIZI WA ELIMU KUPITIA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA SHULE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (katikati) akiwa naMwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Leonard Akwilapo (wa tatu kulia),Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid pamoja viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Elimu Kata wakati wa ufunguziwa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
***********
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu nchini kwa kutoa mafunzo ya uongozi, usimamizi na utawala bora kwa walimu wakuu wa shule za awali na msingi pamoja na maafisa elimu kata kutoka Tanzania Bara.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika ADEM, Julai 9, 2025 Bagamoyo mkoani Pwani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha viongozi wa elimu kusimamia kwa ufanisi shughuli mbalimbali za shule ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu, uimarishaji wa mazingira salama ya kujifunzia na kuongeza uandikishaji wa wanafunzi.
“Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba viongozi wa elimu wanakuwa na uwezo wa kiutendaji na kiuongozi katika kuhakikisha elimu bora inatolewa nchini,” amesema Prof. Nombo.
Aidha, amebainisha kuwa Wizara kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), itaendelea kutoa mafunzo endelevu kwa viongozi wa elimu wa ngazi mbalimbali pamoja na wadau wa elimu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule kwa ufanisi.
"Matumaini yetu ni kwamba ADEM itaendelea kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa lengo la kuimarisha uongozi wa elimu kwa njia endelevu na yenye tija," ameongeza .
Katika hatua nyingine, Prof. Nombo amesema Serikali kupitia Mradi wa BOOST, unaotekelezwa kwa utaratibu wa malipo kulingana na matokeo, inalenga kushughulikia changamoto za usimamizi na ujenzi wa miundombinu ya shule, zikiwemo changamoto za utekelezaji hafifu wa miradi, vitendo vya ubadhirifu na migongano ya kimaslahi miongoni mwa watendaji.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid amesema awamu ya kwanza ambayo imezinduliwa leo (Julai 9, 2025) kitaifa, imejumuisha mikoa 12 yenye washiriki kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Lindi, Mbeya, Arusha, Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mtwara na Singida.
Amesema walishafanya mafunzo kwa wakuu wa shule 17,817, na sasa mafunzo hayo yatafanyika kwa maafisa elimu kata 3956.
"Awamu ya kwanza imejumuisha jumla ya maafisa elimu kata 1978 na awamu ya pili itaitimisha maafisa elimu kata waliobakia kwenye mikoa 14, ambayo itakayojumuisha pia maafisa elimu wa halmashauri, manispaa na majiji 186 na afisa elimu mikoa 26". Ameeleza Dkt. Maulid.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
Baadhi ya maafisa elimu kata wakiwa katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla ya ufunguzi imefanyika leo Julai 9, 2025.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Wednesday, 9 July 2025
MSAADA WA TAASISI YA NVeP NA BARRICK WAENDELEA KUNUFAISHA TAASISI ZA KIJAMII NCHINI
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa (wa pili kutoka kulia) akikabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa kikundi cha Busindi Asali zilizotolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kushoto ni Mwanzilishi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow,hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini,Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa taasisi ya St. Justin Foundation katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa kiongozi wa taasisi ya Sustainable Planet Foundation katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow akishirikiana na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa kukabidhi hundi ya msaada wa shilingi milioni 20 kwa viongozi wa kikundi cha Nazareth katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
***
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa shilingi milioni 80 kwa mashirika manne yasiyo ya kiserikali kutoka mikoa ya Shinyanga, Mara, Pwani na Dodoma kwa ajili ya kukabilianana changamoto mbalimbali za kijamii.
Mashirika yaliyonufaika na msaada huo kila moja likiwa limepata shilingi milioni 20 ni Busindi Asali, St.Justin Foundation,Nazareti Group-Nkulabi na Sustainable Planet Foundation.
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP, imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii mbalimbali zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 35 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto , utunzaji wa Mazingira na kuendeleza miradi midogo midogo ya kujikwamua kimaisha.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wakati wa ziara yake ya kikazi nchini iliyofanyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Mining Corporation, Mark Bristow, amesema kuwa taasisi ya ya NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii kuendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuwataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake, Meneja wa taasisi ya St. Justin Foundation lenye makao mkoani Mara, Juma Songo, ameshukuru NveP kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kukabiliana na changamoto za kijamii kupitia taasisi hizo.
Naye katibu wa kikundi cha Busindi Asali,Tatu Lukuba, amesema kuwa msaada huo kwao ni mkubwa na utawawezesha kupanua mradi wao wa ufugaji wa nyuki na kuwezesha wanakikundi kujikwamua kimaisha na kuboresha maisha yao na familia zao.
"Waswahili walisema akufaaye kwa dhiki ni rafiki,tunashukuru msada huu mkubwa tulioupata kutoka Nvep na Barrick" amesema.
MUME WANGU ALIANZA KUKATAA KURUDI NYUMBANI TIBA YA PETE YA MAPENZI ILIREJESHA FURAHA YETU

Nilianza kuona mabadiliko kwa mume wangu baada ya miaka minne ya ndoa. Kwanza alikuwa mtu wa furaha, mwenye bidii ya kutunza familia, na kila siku alihakikisha anarudi nyumbani mapema. Tulikuwa marafiki wakubwa, tulicheka pamoja, tulisali pamoja, na tuliota maisha ya baadaye kama watu wawili waliounganishwa na upendo wa kweli.
Lakini ghafla, alianza kubadilika.Soma zaidi






















