Sunday, 15 June 2025

KAMISHNA WA UMEME NA NISHATI JADIDIFU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM

▪️Aridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi

▪️Awataka wakandarasi kuzingatia viwango na TANESCO kuongeza usimamizi ili kuepuka ongezeko la gharama

▪️Aisisitiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika

Na. Agnes Njaala, Dar es Salaam

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, tarehe 12 Juni 2025, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme ya Gridi Imara inayoendelea katika Jiji la Dar es Salaam, na kutoa maelekezo muhimu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.

Miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha huduma bora na ya uhakika kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Kamishna amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo, licha ya changamoto mbalimbali za kimazingira, na kusisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

“Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa, lakini nimeagiza wakandarasi waharakishe kazi, vifaa vipatikane kwa wakati, na viwango vya kazi vizingatiwe ili miradi hii itoe matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi,” amesisitiza Mhandisi Luoga.

Akifafanua amebainisha kuwa miradi hiyo ya kimkakati, inayotekelezwa na TANESCO kwa ufadhili wa Serikali, inalenga kuboresha huduma ya umeme kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini. Aidha, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo muhimu.

Katika maagizo yake, ameitaka TANESCO kuongeza usimamizi kwa wakandarasi katika kuhakikisha upatikanaji wa vifaa kwa wakati, na kusimamia ubora wa kazi ili kuepuka ongezeko la gharama zitokanazo na ucheleweshaji.

Kwa upande wake, Mhandisi Abdallah Chikoyo, Meneja wa Miradi ya Kuzalisha Umeme TANESCO aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji , ameahidi kuongeza juhudi katika usimamizi wa miradi na kuweka mipango kazi inayotekelezeka kwa wakati.

“Tumejipanga kuongeza nguvu katika usimamizi wa miradi hii, na kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ufanisi, tukitimiza wajibu wetu katika kuboresha huduma ya umeme nchini,” amesema Mhandisi Chikoyo.

Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Serikali katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo Kamishna Luoga alitembelea vituo vya umeme vya Ubungo I, Mabibo, Kinyerezi na Gongo la Mboto. Katika vituo hivyo, kazi ya ufungaji wa mashine umba zenye uwezo mkubwa  (transformers) inaendelea kwa kasi ya kuridhisha, ikiwa ni hatua ya kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme jijini Dar es Salaam.


Share:

JINSI MAMA MJANE ALIVYOWEZA KULIPA SH70 MILIONI YA MKOPO KWA URAHISI


Je, umewahi kuwa katika hali kuandamwa na madeni na hukujua jinsi ya kujiondoa hapo?. Je, umewahi kukumbana na tishio la kupoteza nyumba yako na mali zako kutokana na mkopo ulionao kwa wakopeshaji wasio na huruma ambao hawajali hali yako?.

Ikiwa umejibu ndiyo kwa mojawapo ya maswali haya, basi hauko peke yako, watu wengi nchini na duniani kote wanapambana na matatizo ya kifedha ambayo yanaonekana kuwa magumu kutatuliwa.

Wanaishi kwa hofu na dhiki, hawawezi kufurahia maisha yao na familia zao, lakini vipi nikikuambia kuna suluhisho la matatizo yako tena kwa njia rahisi tu?.

Itakuwaje nikikuambia kwamba kuna mganga wa jadi mwenye nguvu ambaye anaweza kuroga na kuzidisha kiasi chochote cha pesa ulichonacho?. Je, nikikuambia kwamba unaweza kukupata pochi ambayo huongeza maradufu pesa yoyote inayowekwa ndani yake?.

Inaonekana nzuri sana kwa kweli, sivyo? Naam, ni kweli na tuna hadithi ya kuthibitisha hayo. Kutana na Eneka, mama mjane kutoka Kitale ambaye alirithi deni kubwa kutoka kwa marehemu mumewe, Joe Nabulindo.

Joe alikuwa mfanyabiashara wa sukari katika eneo kubwa zaidi la magharibi mwa Kenya, lakini utajiri wake ulianza kufifia huku sekta ya sukari ikizidi kuimarika na uagizaji wa sukari kutoka nchi jirani za Sudan, Tanzania na Uganda.

Hii ilimsukuma Joe kwenye deni lake, aliwasiliana na benki mbili ambazo zilimpa mkopo wa Ksh42 milioni, akiwa na matumaini kwamba pesa hizo akiziwekeza katika biashara hiyo, zitafufua sifa yake iliyopotea.

Kama ilivyotabiriwa, biashara ilianza kuimarika na nyota yake ikaanza kung’aa tena. Hata hivyo, jina lake lilipozidi kukua, Joe akawa anapigwa vita na washindani wake ambao walimuona kuwa tishio katika biashara ya sukari.

Walipanga genge la uhalifu na kumuua Jumatatu asubuhi akiwa kwenye geti la kampuni moja ya sukari akisubiria mlango ufunguliwe ili aingie na kufanya oda ya takriban mifuko 700 ya sukari. Majambazi hao waliondoka na takribani Ksh3 milioni alizokuwa amebeba kwenye kiti cha nyuma cha gari lake.

Mkewe, Eneka alijaribu kusimamia biashara hiyo vizuri lakini ilishikana baada katika takriban miaka minne, huku madeni yakitakiwa kulipwa na hakuwa na fedha za kulipa na mwisho siku benki ikaja kukamata mali zake ili kufidia deni lao.

“Nilikuwa na huzuni, sikujua la kufanya, hawakutaka kunisikiliza. Niliuza nilichoweza lakini haikutosha, lakini nilikuwa nimejiambia siwezi kupoteza nyumba yangu ya bei ghali kwa mkopo wa chini ya Sh70 milioni,” alisema Eneka.

Eneka baadaye alikuja kusikia habari kuhusu Kiwanga Doctors kupitia kwa rafiki yake ambaye alikuwa amefiwa na mtoto wake wa pekee na wakamsaidia kubeba ujauzito tena.

Kufuatia kuwaomba msaada wao, Kiwanga Doctors walichukua hatua na kutangaza utaratibu wa kurejesha mkopo, kupitia matambiko yao walimsaidia mjane huyo kulipa deni hilo.

Pia walimpa pochi ya fedha na hii ilileta mafanikio makubwa kwake, fedha zozote alizoweka kwenye pochi hiyo na kuzitumia katika biashara ziliongeongezeka haraka, na hivyo kumwezesha kulipa mikopo hiyo haraka zaidi na sasa amemaliza deni hilo na anaendelea na biashara yake.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

BARRICK YAWEZESHA NA KUSHIRIKI KONGAMANO LA AIESEC LA KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI VYUO VIKUU ARUSHA


Wanafunzi wakigawiwa vipeperushi vyenye miongozo ya kuchangamkia fursa za ajira
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Mmoja wa washiriki akiuliza swali
Wageni katika meza kuu wakifuatilia matukio
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo
**

Kampuni ya Barrick nchini kwa mara nyingine imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha, lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA).

Kupitia kongamano hilo, Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha wamepatiwa mbinu mbalimbali kutoka kwa wataalamu, za kuchangamkia fursa zinazojitokeza ikiwemo za ajira, kujiajiri pia jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea kutokea siku hadi siku yanayoathiri upatikanaji wa ajira.

Pia Wanafunzi wamewezeshwa kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Wanafunzi pia wamepata nafasi ya kujua shughuli zinazofanywa na kampuni ya Barrick na programu mbalimbali za kijamii zinazotekelezwa na migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa.

Wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo wamepata fursa ya kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira,ubunifu na jinsi ya kuendeleza vipaji vyao pia mchango wa kampuni katika kukuza uchumi wa kijamii nchini sambamba na kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Milenia.

Barrick imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kupata mafunzo ya vitendo katika katika migodi yake‘Field attachments’, sambamba na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania wenye weredi wa taaluma mbalimbali katika migodi yake nchini pia imekuwa ikitekeleza programu za kuwainua vijana kiuchumi ili wasibaki nyuma.

Kongamano la AIESEC mwaka huu tayari limefanyika katika vyuo vikuu vilivyopo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma,Iringa na Zanzibar kwa udhamini wa Barrick kwa kushirikiana na wadau wengine.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 15,2025


l


Magazeti
Share:

Saturday, 14 June 2025

AJALI YA BASI, LORI YAUA WATU 9 KUJERUHI 44 MOROGORO


Na Farida Mangube, Morogoro

WATU tisa wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hai lenye namba za usajili T523 EKM kugongana na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari lenye namba za usajili T406 CZS – T804 BUB katika eneo la Lugono Melala, barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema kuwa ilitokea majira ya alasiri ya Juni 12, 2025 katika kijiji cha Lugono Melala.

Kwa mujibu wa Afisa uhisiano Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scolastica Ndunga hospitali hiyo imepokea miili ya marehemu tisa, ambapo kati ya miili hiyo, mitano ni ya wanaume na minne ni ya wanawake.

Amesema hospitali imepokea majeruhi 44, wakiwemo watu wazima 37 na watoto saba. Amesema majeruhi wengi wamepata mivunjiko na wanaendelea kupatiwa matibabu ya haraka chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya.

Ndunga ameongeza kuwa miili minne kati ya tisa tayari imetambuliwa na ndugu wa marehemu kupitia vitambulisho walivyokuwa navyo. Miili mingine bado haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, ikisubiri utambuzi na taratibu zaidi kutoka kwa familia husika.


CHANZO- MICHUZI BLOG
Share:

Friday, 13 June 2025

GCLA YAWATUNUKU VYETI WANAFUNZI NA WALIMU BORA ZAIDI WA MASOMO YA SAYANSI


Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetoa zawadi kwa kuwatunuku vyeti wanafunzi wahitimu 48 na walimu 8 waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024 kwa kutambua bidii na kujituma kwao katika kusoma masomo hayo.

Zawadi hizo zimehusisha mshindi wa kwanza hadi wa tatu kwa wasichana na wavulana kwa kila somo kwa kidato cha sita na kidato cha nne.

Akizungumza leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama, amesema kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeendelea na utaratibu wa kila mwaka wa kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika masomo hayo kitaifa katika mitihani yao ya kidato cha sita na nne.

"Kwa kuwa wingi wa ufaulu katika masomo hayo, ni ufanisi mkubwa katika maendeleo ya watoto wenyewe, shule wanazotoka, wazazi pamoja na taifa katika kuhimili matokeo ya ukuaji wa sayansi na teknolojia". Amesema

Amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali zenye kuwezesha na kutoa msukumo kwa wanafunzi kupenda kusoma masomo sayansi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya baadaye kwa vijana kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, na mchango wake kwa maendeleo endelevu.

Aidha amesema kuwa Serikali imewapa nafasi sawa watoto wa kitanzania kupata elimu kwa kuondoa ada kwa elimu ya msingi na sekondari, kuajiri walimu wa sayansi, kuboresha maabara na maktaba za kujifunzia, kuweka miundombinu mbalimbali kama vile vifaa na mifumo ya TEHAMA pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa na madawati.

"Mheshimiwa Rais hakuwasahau wanafunzi wenye changamoto mbalimbali kwa kuwawekea miundombinu rafiki katika shule wanazosoma ili kuhakikisha hawabaki nyuma katika kujipatia elimu". Amesema.

Kwa upande wa sekta ya Afya, amesema kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu hasa katika ujenzi wa majengo yenye kukidhi mahitaji na ununuzi wa mitambo na vifaa mbalimbali vya kisasa ili kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya.

Amesema kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali, ni mnufaika mkubwa pia wa masomo ya sayansi ikihitaji watalaam wa kemia, vinasaba vya binadamu, sayansi ya chakula, mazingira, tiba asili na watalaam wa mitambo ya uchunguzi wa kimaabara ambao wote kwa pamoja wanahitaji kujengwa kupitia masomo ya Kemia, Biolojia, Hisabati na Fizikia.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu wa kutoa zawadi mwaka 2007 hadi kufikia leo, Mamlaka itakuwa imetoa tuzo na zawadi kwa jumla ya wahitimu/wanafunzi 432 na walimu 56.

"Tangu kuanzishwa kwake utaratibu huu umepata mafanikio mengi ikiwemo kuongeza hamasa kwa wanafunzi na kuongeza nguvu kazi ya wataalam katika sekta ya afya na sekta nyinginezo zinazohitaji taaluma ya sayansi". Amesema Dkt. Mafumiko.

Amesema takwimu zinaonesha tangu kuanza kwa utaratibu huo zaidi ya asilimia sabini na tano (75%) ya wanafunzi wanaozawadiwa hususani kwa kidato cha sita wanajiunga vyuo vinavyotoa taaluma ya afya ikiwemo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Afya Bugando, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Herburt Kairuki.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa walimu waliwawezesha wanafunzi wahitimu kufanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa walimu waliwawezesha wanafunzi wahitimu kufanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Dkt. Nyambea alimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Dkt. Nyambea alimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi wakiwa kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi wakiwa kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

MAAFISA HABARI WA MIKOA WATAKIWA KUITANGAZA PROGRAMU YA KIZAZI CHENYE USAWA


Na WMJJWM- Dodoma

Maafisa Habari wa Mikoa wametakiwa kuitangaza kwa nguvu Programu ya Kizazi Chenye Usawa ili kusaidia utekelezaji wa haki na usawa wa kiuchumi nchini.

Wito huo umetolewa, Juni 12, 2025, jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,  Merkion Ndofi, wakati akizungumza katika kikao cha kuwajengea uelewa Maafisa Habari kuhusu utekelezaji wa programu hiyo.

Ndofi amesema Maafisa Habari ni wadau muhimu katika maeneo yao kwa kuwa ni wasemaji wa miradi mbalimbali ya Serikali na anaamini kupitia wao taarifa kuhusu Programu ya Kizazi Chenye Usawa zitasambaa na kufahamika zaidi kwa jamii.

“Programu hii imekuwepo kwa muda mrefu na sasa inatimiza miaka mitano. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alishiriki Mkutano wa Kizazi cha Usawa uliofanyika Paris na akaahidi kuwa kinara katika kutekeleza haki na usawa wa kiuchumi,” amesema  Ndofi.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo manne ya kipaumbele ambayo ni, Uwezeshaji wa kijinsia kwenye sekta binafsi, Kazi zenye staha kwa wanawake katika sekta rasmi na isiyo rasmi,Upatikanaji wa rasilimali za uzalishaji kwa wanawake, na Ubunifu na utekelezaji wa miradi ya kiuchumi kwa wanawake.

“Niwapongeze kwa kujitokeza kushiriki kikao hiki na niwashukuru waajiri wenu kwa kutambua umuhimu wa programu hii. Hii inaonesha wazi kuwa wanathamini nafasi ya habari katika maendeleo,” ameongeza Ndofi 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia katika Badru Abdnoor, amewataka Maafisa Habari kupaza sauti kuhusu Programu ya Kizazi Chenye Usawa ili jamii ifahamu fursa zilizopo na kuweza kushiriki kikamilifu.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Juliana Kibonde amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Maafisa Habari, na ndiyo sababu imeamua kuwakutanisha ili kujadiliana kwa pamoja kuhusu namna bora ya kuitangaza programu hiyo kwa ufanisi.

Nao Maafisa Habari hao wamesema baada ya kupata uelewa huo watahakikidja wananchi katika mikoa yao wanaielewa Programu hiyo ili waweze kunufaika na utekelezaji wake hasa katika kuwa na jamii yenye Usawa wa Kijinsia katika nyanja mbalimbali.

Share:

Thursday, 12 June 2025

APATA KAZI YA MSHAHARA MNONO HUKU AKIACHA POMBE BAADA YA MIAKA 10


Kijana mmoja aitwaye Musa alianza kunywa pombe mapema mwaka 2014 akiwa katika shule ya upili, hii ni kutokana na shinikizo la rika lake, hivyo akajikuta kila wikiendi anakunywa pombe kwa siri katika baa za mtaani kwao.

Baada ya miaka nane pombe ikawa imekolea kwenye damu yake, kichwa chake na moyo wake, huku mkewe Salome akizoea kula Sukumawiki wiki nzima maana mumewe fedha zote anazimalizia kwenye pombe.

Mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano bado hajaanza shuleni kwa sababu ya kukosa fedha, mkewe anachoweza kufanya ni kununua chakula cha mtoto pekee ila suala la shule hawezi kumudu gharama zake.

Kusema kweli maisha ya Musa yamekumbwa na urahibu wa pombe, unajua urahibu ni aina ya utumwa, unajikuta unatoa ahadi kwamba utaacha lakini baada ya muda unajikuta tena katika ulevi huo.

Ndivyo yalivyo maisha ya Musa yeye si mteja tena katika Baa ya Hashtag huko Rombo, yeye ni mbia, mtu mashuhuri na mteja mwaminifu wa Baa hiyo kwa miaka mingi.

Hata hivyo, ilikuwa mshtuko mkubwa kote Rombo wakati Musa alipata kazi yenye malipo mazuri, huku akiachana kabisa na pombe ambayo imeharibu maisha yake kwa miaka mingi. Lakini ilikuwaje akapata ushindi huo?.

Musa alikutana na mwanafunzi mwenzake wa zamani ambaye naye kama yeye alikuwa amekunywa pombe bila kukoma tangu mwaka 2018 ila aliacha kutokana na matibabu bora ya mitishamba kutoka kwa Kiwanga Doctors.

Basi alimpa Musa mawasiliano ya Kiwanga Doctors na maelekezo ya muhimu, alifka kwa wataalamu hao na mara moja walishughulikia tatizo lake.

Ndani ya mwezi mmoja tu, Musa alisema siku za giza katika maisha yake zimekwisha. Mkewe alisherehekea hatua hiyo kubwa kama vile ameshinda bahati nasibu ya mamilioni ya fedha.

“Mimi na pombe tumeachana rasmi na sitaki kurudi nyuma, ninataka kuijenga familia yangu, wameteseka vya kutosha. Asante sana kwa Kiwanga Doctors kwa kunisaidia kushinda ulevi na kuniwezesha kupata kazi nzuri,” alisema Musa.

Vilevile Kiwanga Doctors wana uzoefu wa miongo kadhaa ya kutibu kwa kutumia dawa kali za mitishamba kuponya magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, kisonono, kaswende, TB, miguu kuvimba au kuwaka moto n.k.

Hushughulikia matatizo ya jumla kuanzia kushinda kesi za mahakama, kushinda bahati nasibu, ulinzi wa familia na mali na hutabiri kwa usahihi nyota.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger