Tuesday, 3 June 2025

CHAMA CHA USHIRIKA UDURU WASHINDA KESI,SHAMBA LARUDISHWA RASMI


Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Hassan Bomboko, amesema kuwa, shamba la Chama cha Ushirika Uduru Makoa lenye ukubwa wa ekari 358 limepokelewa rasmi na chama hicho baada ya kushinda kesi dhidi ya mwekezaji, Elisabeth Stegmeir.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Uduru Makaa, Wilayani Hai, Mhe. Bomboko ameeleza kuwa, hukumu ya kesi hiyo ilitolewa tarehe 28 Mei 2025, baada ya mchakato wa muda mrefu uliodumu tangu mwaka 2022.

Mhe. Bomboko amesema kuwa mwanzo, chama hicho cha ushirika kilimkodisha mwekezaji huyo kwa makubaliano maalum, lakini baadaye mwekezaji huyo alikiuka masharti na kuacha kulipa kodi kwa kipindi cha miaka minne.

“Huwezi kuamua kukaa kwenye eneo la watu kwa miaka minne bila kulipa kodi, ilhali mali hiyo siyo yako. Najua mlikuwa mnasubiri sana hukumu hii, na niwaambie tu: hukumu imetoka, mmeshinda kesi, na sasa huyu mwekezaji anatakiwa kuondoka katika eneo lenu,” amesema Mhe. Bomboko.

Hata hivyo, Mhe. Bomboko amewasihi wananchi kuepuka kuvamia eneo hilo au kufanya fujo, akisisitiza kuwa, shamba ni mali ya chama, lakini taratibu za kisheria lazima zifuatwe ili mwekezaji huyo aondoke kwa amani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe, amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea ili mwekezaji huyo aondoke rasmi na shamba lirudishwe kwa chama.

“Ni ukweli usiopingika kwamba shamba hili ni letu na ni haki yetu – hilo halina mjadala. Tunakamilisha taratibu nyingine ili makabidhiano yafanyike na haki yetu ipatikane. Tumefanya kazi mchana na usiku kuhakikisha shamba hili linarejea mikononi mwa chama,” amesema Mhe. Mafuwe.
Share:

Monday, 2 June 2025

MILA POTOFU ZINAVYO CHOCHEA MIMBA ZA UTOTONI NA KUATHIRI NDOTO ZA VIJANA WILAYANI CHEMBA


Mwezeshaji wa mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Vena Assenga (kulia) akizungumza na makundi mbalimbali wakiwemo wazee wa mila,viongozi wa dini,na watendaji wa serikali kwenye mdahalo uliowakutanisha kwa ajili ya kujadili usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo kwa wanawake na vijana  wilaya ya Chemba . 

Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Katika kijiji cha Kidoka, wilayani Chemba, mkoa wa Dodoma, mdahalo wa wazi umeibua mjadala mzito kuhusu athari za mila na desturi potofu zinazofanyika katika jamii kwa kisingizio cha kuenzi utamaduni wa Mtanzania.

Mdahalo huo ulioandaliwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland kupitia mradi wa Tuinuke kwa Pamoja, umebaini kuwa mila zinazohusishwa na ngoma za unyago na jando zimegeuka chanzo kikuu cha mimba za utotoni, utoro mashuleni, na kuvunjika kwa ndoto za vijana wengi.

Wazee wa kimila, viongozi wa dini, akina mama, wawakilishi wa serikali za vijiji na mashirika ya kiraia walishiriki mdahalo huo uliolenga kutafuta njia za kufanikisha usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vinavyowakwamisha wanawake na vijana.

Sheikh Salamu Hando, mmoja wa washiriki kutoka Kidoka, ameeleza kwa uchungu jinsi baadhi ya ngoma za unyago zinavyohusisha mafundisho yenye mwelekeo wa ngono kwa watoto wa kike ambao bado hawajafikia umri wa utu uzima.

“Tunawaambia watoto kuwa sasa wamekuwa watu wazima, huku tukiwafundisha stadi za ndoa na tendo la ndoa, jambo ambalo linawapotosha na kuwasukuma kwenye majaribu ya mapenzi kabla ya wakati,” amesema Sheikh Hando.

Naye Arafa Hukomo, mjumbe wa kituo cha taarifa na maarifa katika kijiji hicho, ameongeza kuwa kutokana na kukosekana kwa sheria kali za kudhibiti desturi hizo, baadhi ya wasichana huishia kupata ujauzito wakiwa bado wadogo.

"Matokeo yake ni watoto wa kike kuacha shule na kukosa fursa ya kujitegemea baadaye kimaisha," ameeleza Hukomo.

Mbali na wasichana, vijana wa kiume nao wameathirika,Wengi wao hutoroka shule na kukimbilia mijini wakisaka ajira zisizo rasmi ili kujitafutia kipato, hatua ambayo huwapeleka mbali na ndoto zao za kielimu.

Amesema, “Jamii inawafanya vijana waamini kuwa mtu mzima ni yule anayeweza kujitegemea kiuchumi, hata kwa njia isiyo rasmi,” alisema mmoja wa washiriki wa mdahalo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa kijiji hicho, Samalu Lupande, ameangazia kiini kingine cha tatizo kuwa ni umaskini wa kaya.

Amesema kuwa wazazi wengi, hasa katika familia masikini, huwalazimisha au kuwasihi watoto wao wasome kwa kiwango cha kawaida tu, au hata kuacha shule, ili wawasaidie katika shughuli za kiuchumi.

Amesena wazazi wengine huwashawishi watoto wasifanye vizuri kwenye mitihani ili wasiendelee na masomo,hii hutokea kwa sababu hawana uwezo wa kugharamia elimu ya juu,” amesema.

Mbali na hayo,ameeleza kuwa umasikini umekuwa kichocheo cha wasichana kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono kwa ajili ya kujikimu.

“Mtoto anakwenda shuleni bila chakula, hana vitabu, hana sare za shule anapotokea mtu kumsaidia, hata kama kwa masharti ya rushwa ya ngono, anakubali,hii ni hatari kwa maendeleo ya jamii,” anafafanua Lupande.

Kutokana na hayo Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Vera Assenga amesisitiza kuwa lengo kuu la mdahalo huo ni kuchochea mabadiliko ya kijamii kupitia utungaji wa sheria rafiki kwa mtoto wa kike.

Ameeleza kuwa si mila zote ni mbaya, lakini ni muhimu kuchuja yale maudhui ambayo yanapingana na ustawi wa watoto na vijana.

“Tunapaswa kutofautisha kati ya ngoma kama sanaa ya utamaduni na mafundisho yake.

Tukiweka sheria madhubuti, tutaweza kubaki na utamaduni wetu bila kuharibu maisha ya watoto wetu,” amesema Assenga.

Naye Deogratius Temba, mwezeshaji wa mradi wa Tuinuke kwa Pamoja unaotekelezwa Chemba na Kondoa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland, ameeleza kuwa mradi huo umejikita katika kuondoa vikwazo vya kijinsia vinavyomkandamiza mwanamke na kijana.

Ameeleza kuwa kupitia mijadala na midahalo ya kijamii kama hii, jamii huamshwa kiakili na kijamii, na hivyo kuwa tayari kubadilika.

Mjadala huu unaashiria mwamko mpya katika wilaya ya Chemba,mwamko wa kuhoji na kuchuja maudhui ya mila na desturi zetu.

Amesema ni dhahiri kuwa jamii inahitaji mabadiliko ya haraka kwa mila zisizofaa ili kuwaepusha watoto wa kike na wa kiume dhidi ya athari zinazotokana na desturi potofu.

"Tunafahamu tunawajibu wa kuzitii mila na tamaduni zetu, lakini jamii yetu inafaa kufahamu kuwa kuna mila hazifai kuzingatiwa kwa kuwa zimepitwa na wakati, ni wajibu wa kila mdau kushiriki katika mapambano haya kwa kuweka mbele maslahi ya watoto na kizazi kijacho, amesisitiza.

Pamoja na mambo mengine Mdahalo huo ulioandaliwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland kupitia mradi wa Tuinuke kwa Pamoja, ulibaini kuwa mila zinazohusishwa na ngoma za unyago na jando zimegeuka chanzo kikuu cha mimba za utotoni, utoro mashuleni, na kuvunjika kwa ndoto za vijana wengi.


Share:

MOROCCAN SAHARA: UK CONSIDERS MOROCCO’S AUTONOMY PROPOSAL AS MOST CREDIBLE TO SETTLE THE DISPUTE


The United Kingdom “considers Morocco’s autonomy proposal, submitted in 2007 as the most credible, viable and pragmatic basis for a lasting resolution of the dispute” over the Moroccan Sahara, and “will continue to act bilaterally, including economically, regionally and internationally in line with this position to support resolution of the conflict”.

This position was expressed in a Joint Communiqué signed, Sunday in Rabat, by the Secretary of State for Foreign, Commonwealth and Development Affairs of the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland, David Lammy, and the Minister of Foreign Affairs, African Cooperation and Moroccan Expatriates, Nasser Bourita.

This document underlines that the UK “follows closely the current positive dynamic on this issue under the leadership of His Majesty King Mohammed VI.” It adds that London “recognises the importance of the question of Western Sahara for the Kingdom of Morocco,” noting that this settling this regional dispute “would strengthen the stability of North Africa and the relaunch of the bilateral dynamic and regional integration.”

The UK affirms, in the Joint Communiqué signed at the Foreign Ministry headquarters, that UK “can consider supporting projects” in the Sahara, notably as part of “the UK Export Finance’s £5bn commitment to support new business across the country.”

It also underlines that the UK “recognises Morocco as a key gateway to Africa’s socio-economic development and reaffirms its commitment to deepening engagement with Morocco as a partner for growth across the continent”.

In this document, “both countries support, and consider vital, the central role of the UN-led process,” reaffirming “their full support for the efforts of the UN Secretary-General’s Personal Envoy, Mr. Staffan de Mistura.” To this end, the UK underlines that it is “ready, willing and committed to lend its active support and engagement to the Personal Envoy and the parties.”


“As a Permanent Member of the UN Security Council, the United Kingdom agrees with Morocco on the urgent need to find a resolution to this long-held dispute, which would be in the interest of the parties”, the document notes, adding that “the time for a resolution and to move this issue forwards is long-overdue, and would strengthen the stability of North Africa and the relaunch of the bilateral dynamic and regional integration,”.

This new position of the United Kingdom, a permanent member of the UN Security Council, aligns with the strong stances expressed by many major powers, notably the United States, France, and Spain.

This new position of the United Kingdom, a permanent member of the UN Security Council, reinforces the growing international momentum driven by His Majesty King Mohammed VI in support of the Autonomy Plan under Moroccan sovereignty.

It also confirms the credibility of this initiative and the broad consensus backing it to reach a final resolution to the regional dispute over the Moroccan Sahara
Share:

Sunday, 1 June 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 2,2025

Magazeti
















Share:

MAHAKAMA 'KESHO' KUSIKILIZA KESI YA TUNDU LISSU 'Live' MOJA KWA MOJA MITANDAONI

Mahakama ya Tanzania imetangaza kuwa mashauri ya jinai namba 8606/2025 na 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu yatasikilizwa Jumatatu, 2 Juni 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Mashauri hayo yatarushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya Mahakama (www.judiciary.go.tz) ili kuruhusu wananchi kuyafuatilia bila kuhudhuria mahakamani.

Ukumbi wa Mahakama utachukua watu wachache tu: Mawakili wa Serikali (10), wa Utetezi (60), na Waandishi wa Habari (10). Wananchi wengine wanahimizwa kufuatilia kesi kupitia mitandao kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya kuimarisha uwazi na matumizi ya TEHAMA.

Matangazo ya moja kwa moja yataanza kabla ya saa 2:30 asubuhi. 


Share:

NILIVYOOKOA TITI LANGU LISIKATWE KISA SARATANI


Jina langu ni Lily kutokea Mombasa, nakumbuka takribani miezi minane iliyopita, nilianza kupata maumivu yasiyo ya kawaida kwenye titi langu la upande wa kulia.

Maumivu yalikuwa makali sana hadi kupelekea mara nyingi kulazimika kuomba likizo kazini kwangu ili nipumzike nyumbani. Hapo nilikuwa na umri wa miaka 27 tu na bado sijaolewa. Hivyo, nilihangaikia sana afya yangu katika umri mdogo.

Hali hiyo ilianza wakati naoga siku moja, niliona kifua changu kumelegea kuliko kawaida na nilihisi uzito usio wa kawaida kama kulikuwa na mawe makubwa ndani.

Nikiwa na wasiwasi, nilitafuta matibabu mara moja. Baada ya kufanya vipimo kadhaa, Daktari alitoa habari zenye kuhuzunisha, nazo ni kwamba nilibainika kuwa na saratani ya matiti. Ugunduzi huu ulikuja kwa kuchelewa sana, hivyo tiba pekee iliyopendezwa ilikuwa ni chemotherapy.

Nikiwa nimehuzunishwa, sikutaka kukubali tiba hiyo hasa katika umri wangu na hali yangu ya kutoolewa, nilimsihi Daktari achunguze matibabu mbadala. Hata hivyo, alisisitiza kuwa tiba hiyo ndio sahihi kwangu.

Nikiwa nimefadhaika, nilirudi nyumbani, nikiwa sina tumaini na msongo wa mawazo. Baada ya muda, Daktari alionya kwamba saratani ilikuwa ikienea haraka na kwamba upasuaji ungehitajika ndani ya mwezi huo.

Nikiwa nimekata tamaa kabisa, nilikutana na ushuhuda kwenye mtandao wa Facebook kutoka kwa mwanamke aliyedai kuponywa saratani na Kiwanga Doctors ambao ni wataalamu wa tiba asilia.

Ingawa nilikuwa na mashaka kuhusu ushuhuda huo, niliamua kujaribu tiba kutoka kwa Kiwanga Doctors. Kwa mshangao wangu, walinihakikishia kwamba wanaweza kuponya saratani yangu bila upasuaji, kwa kutumia mchanganyiko wa mitishamba na uchawi.

Basi nilipewa mchanganyiko maalum wa mitishamba ili ninywe na nikafanyiwa tambiko la uponyaji. Kwa mshangao, ndani ya siku chache tu, niliona mabadiliko makubwa katika kifua changu. Uchunguzi uliofuata ulipobaini kuwa hakuna dalili zozote za saratani, hata wataalamu wa matibabu walishangaa.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

BARRICK YAWEZESHA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA IRINGA KUPATA MAARIFA YA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA KONGAMANO LA AIESEC


Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick nchini, Elly Shimbi akiongea katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa AIESEC Tanzania, Vicent Manira akiongea wakati wa kongamano hilo.
Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick nchini, Elly Shimbi (kushoto) akimpongeza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa,Mussa Constantine baada ya kumkabidhi cheti cha ushiriki wa kongamano hilo,wengine pichani ni Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Iringa,Fanleck John, wa pili kutoka kulia ni Rais wa AIESEC Vicent Manira na Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mkwawa,Doto Busagara.
Mmoja wa washiriki akipokea cheti cha ushiriki
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi ya washiriki wakifurahi wakicheza kwa furaha wakiwa na vipeperushi vya Barrick ambayo imedhamini kongamano hilo
Baadhi ya Washiriki katika picha ya pamoja na watoa mada na wadhamini waliokuwa wamekaa meza kuu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick katika kongamano hilo.
**

Vijana wasomi nchini waliopo vyuoni wametakiwa kuongeza bidii, maarifa katika masomo yao na kuwa wabunifu ili kuweza kupenya kwenye soko la ajira kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo migodini sambamba na kuweza kujiajiri kwa kutumia taaluma zao pindi wamalizapo masomo sambamba na kuchangamkia fursa muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma.

Ushauri huo umetolewa na , Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick, Elly Shimbi, wakati akieleza shughuli za kampuni na program zake wezeshi kwa jamii kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji kwa vijana ya AIESEC Tanzania ambalo limedhaminiwa na Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ambalo limefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

Alisema Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, itaendelea kutafuta rasilimali watu kwa ajili ya kufanya kazi kwenye migodi yake ikiwemo vijana wanaohitimu kutoka kwenye vyuo vikuu mbalimbali na vya ufundi vya kati hapa nchini na lengo kubwa kuhakikisha inaendelea kuibua vipaji na kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Ni muhimu kwa vijana wasomi kukuza utamaduni kwa kushirikiana na kuwasiliana kwa karibu (networking) katika juhudi za kusaka ajira na kutafuta fursa mbalimbali za kuwakwamua kimaisha ili kuleta matokeo Chanya kwenye jamii,” aliongeza Shimbi.

Bw. Shimbi, aliwaeleza washiriki kuwa migodi inayomilikiwa na Barrick nchini ya North Mara na Bulyanhulu imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu kuomba ajira mara tu wanapomaliza masomo na wakiwa kazini wanapata nafasi ya kujengewa uwezo na kampuni pia kampuni inayo programu ya kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi wanapokuwa bado wako vyuoni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa AIESEC Tanzania, Vicent Manira, alisema kuwa mapinduzi ya teknolojia yamesukuma mabadiliko makubwa kwenye sekta ya ajira ambapo ubunifu na ujuzi kuhusu sayansi na teknolojia ni muhimu kwa vijana ili kuweza kuingia soko la ushindani wa ajira hapa nchini sambamba na kuibua fursa za kujiajiri.

''Hivi sasa tupo kwenye kipindi ambacho kunatokea mabadiliko ya sayansi na teknolojia siku hadi siku,ili kutobaki nyuma ni muhimu kusoma kwa bidii sambamba na kufuatilia mabadiliko yanayojitokeza na kuathiri kila fani vilevile kuwa wabunifu",alisema Manira.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameipongeza kampuni ya Barrick nchini kwa kufanikisha wanafunzi kujengewa uwezo kupitia udhamini wa semina za kuwajenga kitaaluma wanafunzi zinazoandaliwa na AIESEC Tanzania kila mwaka.

 "Tunaipongeza Barrick kwa kuwezesha Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa kwani tumeweza kujifunza mengi kuhusu fursa mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzichangamkia", alisema Mussa Constantine kutoka Chuo Kikuu cha Mkwawa kwa niaba ya wenzake.

Semina za kuwanoa vijana wasomi vyuoni kupitia taasisi ya AIESEC kwa udhamini wa Barrick nchini mwaka huu tayari zimefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Zanzibar.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 1,2025



Magazeti




Share:

Saturday, 31 May 2025

Video Mpya : LUTEMA - SHIKOME

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger