Wednesday, 21 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 21, 2025



Magazetini leo

Magazeti
Share:

Monday, 19 May 2025

DUNIA IMEISHA: MAMA APAGAWA NA KIJANA!



Kuna siku kulijitokeza kisa cha kushangaza mtandaoni baada ya kijana mmoja, Moses, 19, kudai kuwa mama yake bado anamchukulia kama mtoto mdogo, anasema kutokana na kuwa mtoto pekee na wa kiume analizimika kukubaliana na jambo hilo.

Moses anadai kuwa mama yake bado anataka kumnyonyesha angali tayari ni mtu mzima, mama yake hukasirika anapomkataa kila anapomvuta karibu ili kumpa titi zake laini.

Anafichua kwamba mama yake, mwanamke wa makamo katikati ya miaka 49 hivi anaendelea kuvuka mipaka yake, mara nyingi humuomba kulala naye kitandani.
Share:

WATU WOTE WAMEOKOLEWA KWENYE AJALI YA MGODI MWAKITOLYO ...WAPUUZENI WANAOZUA TAHARUKI– DC MTATIRO


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius S. Mtatiro
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius S. Mtatiro, ametoa taarifa rasmi kuhusu ajali ya mgodi iliyotokea katika Mgodi wa Dhahabu wa Mwakitolyo, unaomilikiwa na Kikundi cha Wachimbaji cha "HAPA KAZI TU!", Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, akithibitisha kuwa watu wote waliokuwa kifusini wamepatikana.

Katika taarifa hiyo, Mtatiro amesema kuwa baada ya tukio hilo, alifika eneo la ajali mara moja akiwa na timu za uokozi, na kwa kushirikiana na wananchi, waliendesha zoezi la uokoaji kwa kutumia mashine za kisasa za migodini. 

Mashine zaidi ya 10 zilikuwepo, lakini ni mashine 4 pekee zilizohitajika kukamilisha kazi hiyo.

"Tumefanikiwa kuwaokoa watu 11 wakiwa hai, na watu 6 tumewatoa wakiwa wamefariki. Ukiwa pale eneo la ajali utaona tulihamisha kifusi chote kilichowaangukia watu na kukichambua kwa mashine na mikono, hakukuwa na mtu mwingine yeyote aliyebakia ndani ya kifusi," amesema Mtatiro.

Ameeleza kuwa eneo la ajali ni wazi na pana kiasi kwamba hata mashine 20 za kuchimba zinaweza kuingia kwa wakati mmoja, hivyo wananchi walishuhudia moja kwa moja hatua zote za uokoaji.

Aidha, Mtatiro amesema hakuna mtu yeyote anayekosekana katika eneo la Mwakitolyo na Shinyanga, na familia zote zimethibitisha kuwa watu waliokosekana ghafla ni wale waliopatikana—yaani, 6 waliofariki na 11 wanaoendelea na matibabu.

"Ukiwa pale eneo la ajali utaona tulihamisha kifusi chote kilichowaangukia watu na kukichambua kwa mashine na mikono, hakukuwa na mtu mwingine yeyote aliyebakia ndani ya kifusi, na zoezi la uokoaji lilifanyika wananchi wote wakiwa wanaangalia kwa sababu lile ni eneo la wazi na ni eneo pana ambalo zinaweza kuingia excavators hata 20 kwa wakati mmoja, siyo kwamba ni eneo finyu lisilo na nafasi. 

Pia, na bahati nzuri, eneo la Mwakitolyo na Shinyanga halina mtu yeyote ambaye labda anakosekana "missing person", majirani, ndugu, jamaa, marafiki, wapangaji, wenye nyumba na familia zote za Mwakitolyo na Shinyanga, zinakiri kuwa watu waliokosekana ghafla walikuwa wale 6 waliofariki na wale 11 wanaotibiwa",ameeleza. 

"Kwa hiyo siyo tu kwamba tumekamilisha uokoaji huu kwa uzito wa kipekee, lakini pia tumeongoza kufuatilia ikiwa kuna mtu hapatikani, watu wote wa eneo la ajali wameridhishwa kuwa hakuna mwenzao aliyebakia kwenye kifusi",ameongeza Mkuu huyo wa wilaya.

Mtatiro amesema kuwa majeruhi walioko hospitalini walithibitisha kuwa wakati ajali inatokea, walikuwa watu takribani 17 mgodini na walikuwa wanajuana. 

Aidha, mashine zilifanikiwa kuhamisha kifusi chote, na watu wote walipatikana kutoka humo.

"Kifusi chote kilitolewa eneo la ajali na kuhamishiwa upande mwingine kabisa na ndipo tukapata hao watu 17 kwa mchanganuo huo.  Kama hiyo haitoshi, hata majeruhi walioko hospitalini walitueleza waziwazi siku ya ajali kuwa wakati ajali inatokea mgodini kulikuwa na watu takribani 17 ,wanajuana",amefafanua.

Amesisitiza kuwa taarifa zinazodai kuwepo kwa watu waliobaki chini ya kifusi si sahihi na zinapaswa kupuuzwa.

"Naomba tupuuze taarifa zozote zinazoeleza eti kuna watu, wenzetu, wameachwa chini ya kifusi. Taarifa hizo siyo sahihi, ni potofu, zinalenga kuzua taharuki na zenye malengo yasiyo sahihi - tuzipuuze", amesema Wakili Mtatiro.

Share:

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATAJA MAFANIKIO YAKE KUMI IKIWEMO MAPATO KUONGEZEKA



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetaja mafanikio yake 10 iliyopata katika kipindi cha miaka minne ikiwemo kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii ambapo Serikali imeingiza Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa.

Mafanikio hayo yametajwa leo Mei 19,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo,Dk Pindi Chana wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri Chana amesema Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa.

Aidha, mapato yatokanayo na utalii wa ndani yameongezeka kutoka Shilingi 11 bilioni 46.3 Mwaka 2021 hadi Shilingi bilioni 209.8 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 353.1.

“Hatua hii imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya tisa (9) duniani na kushika nafasi ya tatu (3) Barani Afrika kwa ongezeko la mapato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya UVIKO-19,”amesema Waziri Chana.

Ameyataja mafanikio mengine ni Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali, Tanzania Imeendelea Kutambulika na Kung’ara Kimataifa, Kuimarika kwa Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori, Kuimarika kwa Biashara ya Mazao ya Misitu na Nyuki, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Kurejeshewa Hadhi ya Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (UNESCO Global Geopark).

Mafanikio mengine ni Mafanikio ya 4R za Rais Samia Katika Kukuza Biashara ya Utalii kwa Kuiwezesha Sekta Binafsi, Kuandaa Tuzo za Kwanza za Uhifadhi na Utali, Mafanikio ya Mikakati Mahsusi ya Kutangaza Utalii.
Share:

Sunday, 18 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 19, 2025

Share:

KUTOKA KUFANYA KAZI VIWANDA VYA WAHINDI HADI KUMILIKI BIASHARA KUBWA


Baada ya kufanya vibarua kwa miaka mingi kwenye viwanda vya Wahindi nilichoka na kuamua nianze mpango wa kujiari maana ndipo nasikia kuna faida na watu wengi wameweza kutoka kimaisha.

Ili kufikia lengo langu hilo nilianza kutunza fedha zangu nilizopata kila mwisho wa mwezi ingawa ilikuwa kwa kujinyima sana, sikuwa nakula chakula kizuri wala kuvaa nguo nzuri.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 18,2025



magazeti
Share:

Saturday, 17 May 2025

SIMBA SC YACHAPWA 2-0 NA RS BERKANE FAINALI YA KWANZA SHIRIKISHO


NA EMMANUEL MBATILO,

KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta ugenini dhidi ya wapinzani wao RS Berkane baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika (1st leg).

Katika mchezo huo timu ya RS Berkane ilionekana kuhitaji mabao mengi kwa haraka ambapo walifanikiwa kwa dakika 15 za mwanzo kupata mabao mawili ambayo yaliwekwa kimyani na kiungo machachali raia wa Senagal Mamadou Camara dakika ya 08' ya mchezo pamoja na mshambuliaji wa Morocco Ousama Lamlioui dakika ya 15'.

Mamadou Camara licha ya kufunga bao, aliweza kulikamata dimba la kati na kuwapoteza Fabrice Ngoma pamoja na Yusuf Kagoma.

Simba Sc itahitaji mabao 3-0 au zaidi kwenye mchezo wa pili ambao watakuwa nyumbani ili kuweza kuibuka mabingwa wa Shirikisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger