Sunday, 4 May 2025

SHY WOMEN’S DAY OUT YATIKISA TENA SHINYANGA! WANAWAKE WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI, UONGOZI UCHAGUZI MKUU 2025

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SHEREHE ya Wanawake Shy Women’s day Out imefana, huku wanawake wakitakiwa kupendana,kushikamana pamoja na kuchangamkia fursa za kiuchumi na uongozi.

Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Women For Change,imefanyika jana katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga,ambapo mgeni rasmi ni Naibu Spika Baraza la Wawakilishu Zanzibar Mgeni Hassan Juma, huku mshereheshaji akiwa ni Dk. Kumbuka.

Awali akisoma taarifa ya Kikundi cha Women For Change Mwenyekiti wa Kikundi hicho Sara Sawe, amesema kuwa sherehe hiyo ya Women’s Day Out imefikisha miaka Sita sasa,ikiwa na lengo la kuwakutanisha wanawake sehemu moja,kufurahi,kutengeneza mtandao,pamoja na kupeana fursa za kiuchumi.

Amesema kwenye sherehe hiyo huwa zinatolewa mada mbalimbali ambazo zinawajengea wanawake maarifa yakiwamo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa kutoka kwa watalaamu mbalimbali ambao wamebobea kwenye masuala hayo.

“Kikundi chetu cha Women For Change tulikianzisha mwaka 2013, kwa lengo la kusaidiana,kuinuana kiuchumi,kushirikiana huduma za kijamii pamoja kusaidia watu wenye uhitaji,”amesema Sara.

“Baadaye ndipo tukaja na wazo la kuwa tunafanya sherehe ya kuwatoa “out” wanawake wa Shinyanga “Shy Women’s Day Out”ili kuwakutanisha pamoja,kufurahi,kubadishana mawazo,kutengeneza “Connection” na kupeana fursa za kiuchumi na sasa sherehe hii imefikisha miaka 6,”ameongeza Sara.

Aidha,amesema kikundi hicho ni mdau mkubwa wa Serikali katika kuchagiza maendeleo, na kwamba wamekuwa wakitoa Madawati shuleni,kusomesha wanafunzi hadi vyuo vikuu,wameshakarabati bweni katika Kituo cha kulea watoto wenye Ualbino.
Ametaja misaada mingine ni kuwapatia mitaji Wajasiriamali wadogo na kwamba mipango yao ya mwaka huu 2025 ni kufanya pia ukarabati wa Jengo la Magereza ya Shinyanga kwa ajili ya wafungwa kulitumia kwa chakula na kazi hiyo walishaianza na imefikia asilimia 85.

Amesema mipango mingine ni kuwa na Taasisi kubwa ya kifedha kwa ajili ya kusaidia wanawake,pia kujenga ukumbi mkubwa na hata kutumika kwa mikutano ya kitaifa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi,akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwenye sherehe hiyo, amekipongeza kikundi hicho cha Women For Change kwa kuwakutanisha wanawake wenzao na kupeana maarifa mbalimbali.

Mgeni rasmi Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma, amewashukuru Women For Change kwa kumheshimisha, huku akiwasihi wanawake waishi kwa kupendana,kushikamana ili wapate kunyanyuka kwa pamoja.
Amesema matatizo ya wanawake karibia yote yanafanana hivyo kupitia sherehe hiyo,kila mmoja abadilike sasa na kuishi kama ndugu,kushikana mikono na kuinuana kiuchumi.

Amewataka pia wanawake watumie fursa zilizopo za kiuchumi na kwamba sheria inawapatia wanawake kipaumbele katika kupata Zabuni,pamoja na kuchangamkia mikopo ya halmashauri asilimia 10.
Katika hatua nyingine amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu 2025 kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge, sababu nafasi ya Rais yupo Dk. Samia kwa upande wa Tanzania na Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi.

Pia,amewataka wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi huo waendelee kudumisha amani na utulivu, pamoja na kuendelea kuuenzi Muungano.


TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change Sara Sawe akizungumza.
Mwenyekiti wa Sherehe ya Women's Day Out 2025 Faustina Kivambe akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
MC Dk.Kumbuka akisherehesha.
Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma (kulia)akiwa na Mwenyekiti wa Women For Change Sara Sawe.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi (kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa Sherehe ya Women's Day Out Faustina Kivambe.
Mr Black akitoa somo la uchumi.
Sherehe ya Women's Day Out ikiendelea.








Utoaji wa vyeti vya shukrani kwa wadhamini wa sherehe hiyo ukiendelea.
Picha za pamoja zikipigwa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 4,2025



Magazeti ya leo
Share:

Saturday, 3 May 2025

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI, SINGIDA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Kwenye maadhimisho hayo, Benki ya CRDB ambayo ni Mwajiri Bora zaidi nchini, iliungana na Watanzania pamoja na dunia nzima kusherehekea mchango wa wafanyakazi katika kukuza uchumi.

Benki hiyo iliwakilishwa na viongozi kutoka Makao Makuu pamoja na wafanyakazi kutoka makao makuu, kanda ya kati na matawi ya Singida wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo aliyesindikizwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa.
Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (watano kushoto) akiwa na wageni wengine kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipita mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzinia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.
Magari ya Benki ya CRDB yakiwemo Matawi yanayo temebea yakishiriki katka maadamano ya Mei Mosi yaliyofanyika katika viwannja vya Bombadia Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wafanyakazi waliokuwa wakipita kwa maandamano mbele yake wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (katikati) akiwa na wageni wengine kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger