Sunday, 4 May 2025
Saturday, 3 May 2025
BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI, SINGIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Kwenye maadhimisho hayo, Benki ya CRDB ambayo ni Mwajiri Bora zaidi nchini, iliungana na Watanzania pamoja na dunia nzima kusherehekea mchango wa wafanyakazi katika kukuza uchumi.
Benki hiyo iliwakilishwa na viongozi kutoka Makao Makuu pamoja na wafanyakazi kutoka makao makuu, kanda ya kati na matawi ya Singida wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo aliyesindikizwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa.

Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (watano kushoto) akiwa na wageni wengine kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipita mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzinia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.
Magari ya Benki ya CRDB yakiwemo Matawi yanayo temebea yakishiriki katka maadamano ya Mei Mosi yaliyofanyika katika viwannja vya Bombadia Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wafanyakazi waliokuwa wakipita kwa maandamano mbele yake wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (katikati) akiwa na wageni wengine kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.
UVUTAJI SIGARA KWA MIAKA 20 ULIVYOIWEKA MATATANI NDOA YAKE
Kwa miaka mingi nilikuwa napambana kuhakikisha kuwa naacha kuvuta Sigara lakini hilo lilinishinda kabisa, kuna wakati niliweza kukaa hata wiki moja bila kuvuta lakini nikipita mahali nikasikia mtu anavuta ghafla kiu inakuja.
Tayari mwili wangu ulikuwa umeanza kupata madhara kutokana na uvutaji Sigara, kila mara nilikuwa nakohoa hasa nyakati za usiku, jambo hilo lilikuwa linamkwaza sana mke wangu kiasi kwamba aliamua kuhama chumba tulichokuwa tunaishi pamoja.
Nilianza kutumia dawa za mitishamba na kufuata aina flani ya kanuni za kisaikolojia ili kuweza kuondoka katika kifungo hicho lakini sikweza kufanikiwa.








Magazetini