Friday, 2 May 2025

WIZARA FEDHA YAPOKEA TUZO MBILI ZA USHINDI SHEREHE ZA MEI MOSI

Katibu wa Hazina Sports Club, Bw.Kelvin Kakoko, akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Na. Peter Haule, Singida.


Wizara ya Fedha imeng'ara kwenye Sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano yaliyoshirikisha Wizara na Taasisi za Serikali.

Tuzo za washindi katika mashindano mbalimbali zimetolewa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.

Akizungumza wakati wa maandamano ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walioshiriki katika sherehe hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Wizara ya Fedha, Bw. Shumbi Mkumbo, alisema kuwa Wizara ya Fedha imenyakua tuzo mbili ikiwemo hiyo ya mshindi wa mpira wa miguu na tuzo ya uendeshaji Baskeli, jambo lililo chochea hamasa kwa watumishi wa Wizara kushiriki zaidi katika michezo.

Alisema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha michezo kwa kuwa inaimarisha afya kwa watumishi na pia inahimiza umoja na mshikamano.

Sherehe hizo kwa Wizara ya Fedha zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu, Bi. Jenifa Christian Omolo na Mkurungenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu, Bi. Fauzia Nombo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa katika Sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, zilizofanyika katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo (kulia), akiwa ameshika moja ya tuzo ambayo Wizara ya fedha imepokea baada ya kushinda mchezo wa mpira wa miguu na kuendesha Baiskeli kwa upande wa Wizara na Taasisi na wakati wa Sherehe za MeiMosi Kitaifa mkoani Singida, kushoto ni Mwandishi Mwendesha Ofisi Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Scholastica Okudo.
Watumishi wa Wizara ya Fedha wakipita mbele ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.
Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa kwenye maandamano wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi), zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo, akiongoza maandamano ya Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi), zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.
Watumishi wanamichezo kutoka Wizara ya Fedha wakifurahia ushindi wa mchezo wa mpira wa miguu na kuendesha Baiskeli kwa upande wa Wizara na Taasisi, wakati wa Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa mkoani Singida.
Mtumishi kutoka Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) Bi. Ridhaeli Zephania, akionesha moja ya tuzo ya ushindi wa mchezo wa mpira wa miguu na kuendesha Baiskeli kwa upande wa Wizara na Taasisi, wakati wa Sherehe za Mei Mosi Kitaifa mkoani Singida.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha kabla ya kuanza kwa maandamano ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, zilizofanyika katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Singida)
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 2,2025




Magazeti 




Share:

MKURUGENZI ZAHARA MICHUZI ATUNUKIWA CHETI CHA MFANYAKAZI HODARI MEI MOSI MASWA


Katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku  ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi,2025 yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Comrade Kenani Kihongosi, amekabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Zahara Muhidin Michuzi, kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi.

Bi. Zahara alihamishiwa wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro, ambako pia  alihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita akifanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotambuliwa na wengi na kuacha alama zisizosahailika.

Tuzo hiyo imetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za viongozi na watendaji wanaoonyesha juhudi, kujituma, uzalendo wa kweli, ufanisi na uongozi thabiti katika utumishi wa umma, hasa katika, kusimamia miradi maendeleo, ukusanyaji wa mapato, kutatua kero za watumishi na wananchi kw ujumla sambamba na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.

Katika hotuba yake, Comrade Kihongosi amewasihi watumishi wa umma kote mkoani Simiyu kuiga mfano wa Bi. Zahara kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama nzuri zisizofutika, uwajibikaji na moyo wa kizalendo.
Share:

Thursday, 1 May 2025

GCLA YAPATA TUZO MAONESHO OSHA

Watumishi wa Mamlaka kutoka kulia ni Judith Lema, Saile Kurata, Emanuel Lewanga na Benny Migire wakiwa wameshika Tuzo na Cheti cha Mshindi wa Pili baada ya kuibuka washindi wa pili kwenye kipengele cha Shughuli za Kitaaluma, za Kisayansi na Kiufundi katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida kuanzia Aprili 24 hadi Aprili 30, 2025.
Tuzo na Cheti cha Mshindi wa Pili ambavyo Mamlaka imekabidhiwa baada ya kuibuka washindi wa pili kwenye kipengele cha Shughuli za Kitaaluma, za Kisayansi na Kiufundi katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida na kuhitimishwa Aprili 30, 2025.
Share:

MJUMBE WA INEC ATEMBELEA VITUO VYA KUANDIKISHIA WAPIGA KURA


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira leo tarehe 01 Mei, 2025 ametembelea na kukagua vituo vya kuandikishia wapiga Kura vilivyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa daftari unaojumuisha mikoa 15 nchini.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa Daftari la awali kwa mikoa 15 nchini ikiwemo na mkoa wa Rukwa kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Mei, 2025 ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger