Friday, 2 May 2025

MKURUGENZI ZAHARA MICHUZI ATUNUKIWA CHETI CHA MFANYAKAZI HODARI MEI MOSI MASWA

Katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku  ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi,2025 yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Comrade Kenani Kihongosi, amekabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Zahara Muhidin Michuzi, kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi.

Bi. Zahara alihamishiwa wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro, ambako pia  alihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita akifanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotambuliwa na wengi na kuacha alama zisizosahailika.

Tuzo hiyo imetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za viongozi na watendaji wanaoonyesha juhudi, kujituma, uzalendo wa kweli, ufanisi na uongozi thabiti katika utumishi wa umma, hasa katika, kusimamia miradi maendeleo, ukusanyaji wa mapato, kutatua kero za watumishi na wananchi kw ujumla sambamba na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.

Katika hotuba yake, Comrade Kihongosi amewasihi watumishi wa umma kote mkoani Simiyu kuiga mfano wa Bi. Zahara kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama nzuri zisizofutika, uwajibikaji na moyo wa kizalendo.
Share:

Thursday, 1 May 2025

GCLA YAPATA TUZO MAONESHO OSHA

Watumishi wa Mamlaka kutoka kulia ni Judith Lema, Saile Kurata, Emanuel Lewanga na Benny Migire wakiwa wameshika Tuzo na Cheti cha Mshindi wa Pili baada ya kuibuka washindi wa pili kwenye kipengele cha Shughuli za Kitaaluma, za Kisayansi na Kiufundi katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida kuanzia Aprili 24 hadi Aprili 30, 2025.
Tuzo na Cheti cha Mshindi wa Pili ambavyo Mamlaka imekabidhiwa baada ya kuibuka washindi wa pili kwenye kipengele cha Shughuli za Kitaaluma, za Kisayansi na Kiufundi katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida na kuhitimishwa Aprili 30, 2025.
Share:

MJUMBE WA INEC ATEMBELEA VITUO VYA KUANDIKISHIA WAPIGA KURA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira leo tarehe 01 Mei, 2025 ametembelea na kukagua vituo vya kuandikishia wapiga Kura vilivyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa daftari unaojumuisha mikoa 15 nchini.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa Daftari la awali kwa mikoa 15 nchini ikiwemo na mkoa wa Rukwa kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Mei, 2025 ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.
Share:

EFG YATOA MAFUNZO YA USAWA WA KIJINSIA, UONGOZI NA HAKI ZA KIRAIA KWA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI MANISPAA YA SHINYANGA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) limeendesha mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo ya siku mbili (Mei 1-2, 2025) yanafanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga, yakiwaleta pamoja wanawake wafanyabiashara kutoka masoko sita ya Manispaa ya Shinyanga ( Soko Kuu, Ibinzamata, Ngokolo, Kambarage, Nguzo Nane na Majengo Mapya).

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Ford Foundation, Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta, amesema lengo kuu ni kuwajengea uwezo wanawake wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi, kufanya maamuzi na kusimamia shughuli za kibiashara katika mazingira ya soko.
 Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta

“Tunataka kuona wanawake wakiongoza, wakielewa haki zao na wakihusika moja kwa moja katika kupanga na kusimamia ajenda zinazowagusa. Mafunzo haya ni sehemu ya mchakato wa kuwawezesha,” amesema Bi. Suzan.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Sauti ya Mwanamke Sokoni, iliyoanzishwa Oktoba 2011, na ambayo hadi sasa imetekelezwa katika zaidi ya masoko 47 katika mikoa 10 nchini Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Lindi, Mtwara, Mbeya, Iringa, Tanga (Lushoto), Musoma na Dodoma.
Kwa upande wake, Afisa Utawala wa EfG, Bi. Evah Buhembo, amewatia moyo wanawake hao kuendeleza ushirikiano wao kwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na fursa za mikopo kutoka halmashauri, na hivyo kuimarisha biashara zao na kujenga uongozi thabiti ndani ya jamii ya wafanyabiashara.

“Kupitia ushirikiano na vikundi, wanawake wanaweza kupata mikopo, kushirikishana maarifa na kusimama imara kama viongozi katika maeneo yao ya biashara,” amesema Bi. Evah.

EfG ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa rasmi tarehe 6 Agosti 2008, likiwa na dhamira ya kuinua sekta isiyo rasmi, hasa kwa wanawake, kwa kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, msaada wa kisheria, kuwezesha usawa wa kijinsia katika fursa za kibiashara, na kushawishi sera zinazolenga maendeleo jumuishi.
 
Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta akizungumza wakati wa
mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
 Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta akizungumza wakati wa
mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Utawala wa EfG, Bi. Evah Buhembo akitoa mada kuhusu Uongozi na Haki za Kiraia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

 Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mshiriki wa mafunzo akichangia hoja wakati Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia kwenye mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Wanawake wafanyabiashara sokoni wakifuatilia mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger