Sunday, 16 March 2025

ASKOFU MTEULE WA KKKT DAYOSISI YA MWANGA DKT. MONO APOKELEWA KWA SHANGWE KUBWA SHINYANGA


Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry

Na Isaac Masengwa
*******************
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Daktari Daniel Henry Mono amepewa mapokezi makubwa na waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayofanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Mapokezi hayo makubwa yakiongozwa na Askofu wa dayosisi hiyo Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu, yamekuwa mapokezi ya kwanza tangu ateuliwe kuwa askofu wa dayosisi ya Mwanga na yamefanyika leo Machi 15, 2025.

Akizungumza katika sala fupi ya mapokezi hayo iliyofanyika katika usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga, Askofu mteule Daktari Daniel Henry Mono amesema kuwa hakutegemea kukutana na mapokezi makubwa kama haya.


"Kwa kweli leo nimetekewa kwa sababu ukweli kabisa sikujua kama kuna jambo la namna hii. Nimekutana na jambo ambalo sikulitegemea kabisa, nimeona magari, watu na tarumbeta ambapo nilijikuta nikitekewa"

"Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa yote aliyotenda, ninamshukuru kwa jinsi alivyonipitisha katika utumishi wake na mpaka sasa ameniita tena kutumika katika nafasi hii kubwa."

"Pia nikushukuru sana baba Askofu Yohana Ernest Nzelu, umekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu, nimeishi na wewe kama rafiki na kama ndugu. Hata ulipofika wakati wa kufanya kazi na wewe nimefurahi sana kufanya kazi na mimi. Pia nikushukuru hata kwa jinsi umenishauri katika kuliendea jambo hili."

"Lakini pia nikushukuru sana baba Askofu mstaafu Makala, umekuwa mwalimu wetu mwema katika utumishi huu. Umenipa malezi mazuri ya kiutumishi, umetuntengeneza hadi kuwa hivi nilivyo. Kupata nafasi kama hii wewe umekuwa sehemu ya kufikia hatua hii."

Naye Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Yohana Ernest Nzelu, amemshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii ya utumishi aliyoipata askofu mteule Daktari Mono.

"Ni haki yetu kama dayosisi kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii aliyoipata

"Nimshukuru sana Baba Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala kwa kuwa yeye ndio amekuwa lango la wengine kupata nafasi kama hizi. Katika utumishi wako umekuwa chanzo cha sisi wengine kupata nafasi hizi."

"Nimepokea barua kutoka dayosisi ya Mwanga wakiniomba Daktari Mono uende ukatumike katika dayosisi ya Mwanga".

"Nami nimewajibu majibu ya awali kuwa Daktari Mono atakuja kutumika katika dayosisi ya Mwanga tukiwa tunasubiri maamuzi ya mwajiri wake"

Naye kwa upande wake askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo Askofu Makala amempongeza Askofu mteule Daniel Mono na kumtaka kuwa kiongozi atakayeandaa viongozi wajao.

"Ukipewa nafasi ya kuongoza andaa wengine ili kanisa liweze kusonga mbele. Baba askofu mteule hongera sana, wewe nenda kafanye kazi ya Mungu kwa kadri Mungu atakavyokutumia."

Daktari Daniel Henry Mono ni msaidizi wa Askofu wa dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria. Na alichaguliwa na mkutano mkuu wa dayosisi ya Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro kuwa askofu wa pili wa dayosisi hiyo yeye akiwa katika majukumu yake Nchini Burundi.

Hii inakuja baada ya aliyekuwa Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo Chediel Sendoro kufariki dunia mwaka jana Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akitoa neno la shukrani kwa waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakati wa mapokezi

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akitoa maelekezo wakati wa mapokezi yaAskofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono


Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akiwasili usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakati wa mapokezi hayo
Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel Mono akifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo

Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono.
Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala (katikati), Mama Askofu mstaafu Mdiakonia Lilian Makala (kushoto) na Chaplain wa Kanisa Kuu Mchungaji Zinyangwa Silas Mkiramweni wakifuatili kwa makini tukio la kumpokea Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Henry Mono

Akofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (kulia) na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi (kushoto) wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu wakati wa mapokezi hayo


Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono




Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akifauatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi yake mkoani Shinyanga
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akifuatilia kwa umakini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono (kulia), Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (katikati) Mama Askofu Lilian Yohana Ernest Nzelu (katikati) na Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel Mono (kulia) wakiwa wanafuatilia kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo

Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Kwaya ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga
Waumini na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga wakati wa mapokezi
Waumini na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga wakati wa mapokezi
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono

Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 16,2025










Share:

Saturday, 15 March 2025

JUMBE ATOA TIKETI 100 MASHABIKI WA STAND UNITED FC KUSHUHUDIA MECHI DHIDI YA MTIBWA SUGAR, MILIONI 2 WAKISHINDA, LAKI 2 KILA GOLI IKO PALE PALE

 

Mhandisi James Jumbe Wiswa, mdau mkubwa wa michezo na mpenzi wa timu ya Stand United FC, ameahidi kutoa motisha ya kipekee kwa timu hiyo endapo itaifunga Mtibwa Sugar FC katika mchezo wa Ligi ya Championship utakaochezwa Machi 17, 2025, katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga. Ahadi hiyo ya milioni mbili ni sehemu ya juhudi za kuboresha michezo na kuhamasisha wachezaji wa Stand United FC kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Machi 14, 2025, mjini Shinyanga, mdau wa michezo Jackline Isaro, amesema Mhandisi Jumbe ametoa ahadi hiyo ya shilingi milioni mbili kama sehemu ya kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kuhakikisha timu ya Stand United inafanikiwa kuingia Ligi Kuu ya Tanzania.

 Isaro amesisitiza kuwa motisha hiyo ni muhimu kwa timu hiyo, kwani inatoka katika mdau ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kuona timu hiyo inaendelea kufanya vizuri.

Mhandisi James Jumbe, ambaye pia ni mkazi wa Shinyanga, ameeleza kuwa amehamasika kutoa motisha hii ili kusaidia timu ya Stand United FC, ambayo ni timu muhimu kwa jamii ya Shinyanga. Jumbe aliweka wazi kuwa ikiwa timu itashinda na kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar FC, atatoa zawadi ya shilingi milioni mbili kama ishara ya kutambua na kuenzi juhudi za wachezaji. 

Aidha, amesema kwamba atatoa shilingi 200,000 kwa kila goli litakalofungwa na Stand United katika mchezo huo, ikiwa ni motisha ya ziada kwa wachezaji kuongeza juhudi.



Motisha ya Tiketi Bure kwa Mashabiki

Mbali na motisha kwa wachezaji, Mhandisi Jumbe pia ameahidi kununua tiketi 100 kwa ajili ya mashabiki wa Stand United FC, ili waweze kuingia bure uwanjani. Huu ni msaada mkubwa kwa mashabiki, ambao mara nyingi wanakutana na changamoto za kiuchumi kuweza kumudu gharama za tiketi za uwanja. Jackline Isaro alieleza kuwa hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kwamba mashabiki wanapata nafasi ya kuwa sehemu ya mchezo huo muhimu, huku pia wakionyesha ushirikiano mkubwa kwa timu yao ya Stand United.

“Motisha hii ni sehemu ya kuongeza nguvu na hamasa kwa timu ya Stand United na mashabiki wake. Tunataka kuhakikisha kuwa timu inapata sapoti kubwa kutoka kwa jamii na mashabiki ili iweze kufikia malengo yake ya kurejea kwenye Ligi Kuu,” amesema Isaro.

Wito kwa Wananchi wa Shinyanga

Isaro pia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao ya Stand United FC katika mchezo huo wa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar. Alisema kuwa ni muhimu kwa timu hiyo kupata pointi tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumbani ili kuhakikisha wanarejea kwenye Ligi Kuu ya Tanzania na kurejesha heshima ya mkoa wa Shinyanga katika ulingo wa michezo.

“Tunataka kurudisha heshima ya mkoa wetu wa Shinyanga kwa kuiinua timu ya Stand United FC, ambayo inadhaminiwa na Jambo Group. Mchezo huu ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio ya timu yetu, na tunawaomba wananchi wa Shinyanga wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao,” amesema Jackline.

Stand United FC Yajivunia Motisha

Kwa upande wake, Afisa Habari wa Stand United FC, Ramadhani Zoro, alitoa shukrani kwa Mhandisi James Jumbe na Jambo Group kwa motisha hii ya kipekee. Zoro ameeleza kuwa ahadi ya shilingi milioni mbili na motisha ya tiketi 100 kwa mashabiki, pamoja na shilingi 200,000 kwa kila goli, ni mambo yatakayosaidia kuongeza ari ya wachezaji na kuhakikisha wanashinda mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

“Tunamshukuru Mhandisi Jumbe kwa motisha hii. Kuahidi milioni mbili iwapo tutashinda na tiketi 100 kwa mashabiki ni jambo kubwa na muhimu kwa timu yetu. Timu yetu iko tayari na mazoezi yanaendelea vizuri. Tunaahidi kuleta ushindi katika mchezo huu muhimu,” amesema Zoro.

Stand United FC inatarajia kushuka uwanjani dhidi ya Mtibwa Sugar FC katika mechi ya muhimu ya Ligi ya Championship, huku wakilenga kushinda ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu na kurejesha heshima ya mkoa wa Shinyanga katika michuano ya kitaifa.

Share:

JAMES JUMBE PLEDGES 2 MILLION SHILLINGS AND FREE TICKETS FOR STAND UNITED FC FANS AHEAD OF UPCOMING MATCH

 

Engineer James Jumbe Wiswa, a prominent sports enthusiast, has pledged to reward Stand United FC with a sum of 2 million Tanzanian Shillings if they defeat Mtibwa Sugar FC in their upcoming match scheduled for March 17, 2025, at the CCM Kambarage Stadium in Shinyanga.

Additionally, Engineer James Jumbe has announced that he will purchase 100 tickets for Stand United FC fans, allowing them to enter the stadium for free.

 Furthermore, he will continue motivating the players by offering 200,000 Tanzanian Shillings for each goal scored by Stand United during the match.

This initiative is a great effort to inspire both the players and fans, boosting the team’s morale and enhancing the competitive spirit in the league.

Share:

TAKUKURU YAPONGEZWA KWA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI

 

Mjumbe wa kamati tendaji ya Mwanza Press Club Tonny Alphonce
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imepongezwa kwa kutoa elimu ya uchaguzi kwa makundi mbalimbali nchini.

Akichangia mada ya kanuni za uchaguzi na nafasi ya vyombo vya habari katika uchaguzi ujao kwenye mkutano wa MISA - TAN na Wadau, Mjumbe wa kamati tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (Mwanza Press Club) Tonny Alphonce amesema kuna umuhimu wa taasisi zingine kutoa elimu ya uchaguzi mkuu kama walivyofanya TAKUKURU mkoa wa Mwanza.

Alphonce amesema kipindi cha uchaguzi kinagusa jamii nzima hivyo taasisi zote zinazofanya kazi na wananchi zina wajibu wa kutoa elimu ya uraia ili makundi yote yaweze kushiriki kwa manufaa ya taifa.

"Watoa mada wamesema hapa uchaguzi ni mchakato,Mimi niwapongeze TAKUKURU mkoa wa Mwanza ninapotoka kwa kuwa wao walitoa elimu na kusisitiza kuwa kuna umuhimu wa kuripoti habari kabla,wakati na baada ya uchaguzi", amesema Alphonce.

Hayo yamejadiwa katika Mkutano ulioandaliwa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania(Misa Tan) Kwa kuwakutanisha Wadau mbalimbali kuangalia ushirikiano wa pamoja.

Share:

JESHI LA POLISI DODOMA KUMUENZI SHUJAA WA USALAMA BARABARANI IHUMWA



Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limempatia vitendea kazi na elimu Elias Makasi ambaye kwa mwaka wa 18 sasa amekuwa akijitolea kuwavusha barabara wanafunzi wa shule ya msingi ya Jenerali Musuguri iliyopo Kata ya Ihumwa jijini Dodoma. 

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo vyenye michoro ya alama za usalama barabarani pamoja na viakisi mwanga Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SACP) George katabazi amepongeza uongozi wa Shule hiyo kwa kumuamini mzee huyo na kuwasaidia kuwavusha wanafunzi pindi wanapoenda shuleni na kutoka na kuepuka ajali.

"Mzee Eliasi amekuwa mzalendo wa kweli kwa kuwasaidia wanafunzi hawa kuepukana na ajali zisizo za lazima sisi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma tunamuunga mkono na tutampatia pia elimu ya usalama barabarani ili aendelee kuwanusuru watoto hawa na ajali za barabarani kutokana eneo hili kuzungukwa na makazi ya watu na vyombo usafiri kupita Karibu na shule,"amesema Rpc Katabazi.

Aidha katabazi amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kupitia kitengo cha usalama barabarani limeweka mikakati ya kuzifikia shule zote za mijini na vijijini hususani shule za msingi zilizopo kwenye makazi watu na kuziwazesha vifaa vya vyenye michoro ya usalama barabarani pamoja na elimu itakayo saidia kulinda kizazi hicho cha wanafunzi na ajali za barabarani.

Vilevile Katabazi ametoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuheshimu sheria za usalama barabarazi na kutoa kipao mbele kwa wanafunzi pindi wanapo kuvuka barabara huku akisisitiza wananchi wanao ishi karibu na maeneo ya shule kuwa wazalendo kwa kuwasaidia wanafunzi kuwavusha barabara.

Kwa upande wake Elias makasi pamoja uongozi wa shule hiyo wamelishukuru Jeshi la Polisi Kwa kutambua mchango wao na kutoa elimu pamoja askari wa Usalama barabarani watakao shirikiana kuwasaidia watoto kuwavusha katika eneo hilo la Ihumwa kutokana njia hiyo kuu kuwa na wingi wa vyombo vya Usafiri.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na mkakati huo wa kuzifikia shule zote zilipo Jijini Dodoma makundi mbalimbali ya watu ili kudhibiti ajali za Barabarani.






Share:

Thursday, 13 March 2025

UVCCM KAGERA KUWAKATAA WASALITI KATIKA CHAMA


Na Lydia Lugakila  -Kyerwa  

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka wananchi katika Kata ya Kibingo, Wilayani Kyerwa, Mkoani Kagera, kuacha tabia ya kuwachagua viongozi wa vyama vingine, na badala yake wachague Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimeleta mageuzi makubwa.

Akizungumza kuhusu mageuzi hayo, Faris ametaja hasa katika zao kubwa la Mkoa wa Kagera, ambalo ni zao la kahawa. Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameliboresha kwa kulipa heshima kubwa na kulipandisha bei.

Akizungumza na baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kijiji cha Rwenkende, Kata ya Kibingo, Wilayani Kyerwa, Mkoani Kagera, wakati wa ziara ya siku 16 ndani ya mkoa huo, ambapo lengo lilikuwa ni kutafuta kura mpya kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Faris amesema wananchi na wanachama wa CCM wanatakiwa kuacha mazoea ya kuwachagua viongozi wa vyama vingine, na badala yake wachague viongozi wanaotokana na CCM.

Faris ameongeza kuwa Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mageuzi ndani na nje ya Mkoa wa Kagera. 

Ametolea mfano bei ya zao la kahawa, ambapo bei imepandishwa kutoka shilingi 1,200 hadi shilingi 5,000, na kusema kuwa wananchi wa Kata ya Kibingo wanatakiwa kumlipa Rais Samia kwa kumpigia kura za kutosha wakati wa uchaguzi.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama wa CCM katika Kata ya Kibingo kutokuweka usaliti wa aina yoyote wakati uchaguzi mkuu unapokaribia, bali wawe na mapenzi mema kwa wagombea wa CCM, kwani CCM ndicho chama kitakachowaletea maendeleo.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wamesema kuwa wakati wa uchaguzi mkuu, watajitokeza kwa wingi kumpigia kura Rais Samia, kwa sababu amewapambania hadi kupandisha bei ya zao la kahawa na kuleta miradi mikubwa ya maendeleo.


Share:

SEforALL KUIMARISHA USHIRIKIANO UPATIKANAJI NISHATI ENDELEVU



Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Viongozi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi ya nishati endelevu kwa watu wote unaofanyika nchini Barbados wameshauri kuimarishwa kwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu kwa gharama nafuu.

Akizungumza katika mkutano huo unaofanyika jijini Bridgetown, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania kwa upande wake chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepanga kuwawezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Amesema, kupitia mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) unaozalisha megawati 2,115 utawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika na endelevu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi katika ngazi mbalimbali.

Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, utekelezaji wa lengo namba 7 katika mpango wa maendeleo ya milenia unahitaji ushirikiano miongoni mwa Serikali na sekta binafsi katika kuboresha upatikanaji wa nishati safi ikiwa ni moja ya utatuzi wa changamoto zilizopo.

Amesema ni muhimu kwa mataifa kuwekeza katika miundombinu kwa ajili ya upatikanaji wa nishati safi sambamba na kuweka mifumo ya ubunifu na utashi katika kuwezesha upatikanaji wa nishati kwa usawa bila kuacha makundi mengine.

Naye, Waziri Mkuu wa Barbados, Mhe. Mia Mottley amesema ni wakati sasa wa kuweka mkakati wa kimataifa na kukubaliana kushirikiana kumaliza changamoto ya upatikanaji wa nishati kwa wote.

Akizungumzia mkutano wa misheni 300 (M300) uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mia amesema inatia simanzi kuwa na watu zaidi ya milioni 600 barani Afrika wanaishi bila huduma ya umeme suala ambalo limesababisha changamoto katika nchi nyingi duniani.

“Tunahitaji kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo, uwe ufumbuzi wa ndani au kutoka katika nchi yoyote duniani,” amesema Mhe. Mottley.

Kwa upande wake, Rais wa Sierra Leone, Mhe. Julius Maada Bio amesema katika kipindi hiki ambapo nishati ni nyenzo muhimu katika upatikanaji wa maendeleo, ni muhimu kuwezesha watu na makundi yote kupata nishati hususani katika maeneo ya vijijini yanayokabiliwa na umasikini uliokithiri.

“Wanawake na watoto ambao wanatumia muda mwingi kutafuta nishati ambayo sio safi kwa ajili ya kupikia, wanatakiwa kuwezeshwa kupata nishati safi na hivyo kutumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo,” ameongeza.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mtendaji Mkuu SEforALL, Damilola Ogumbiyi, amesema zinahitajika ajenda madhubuti za kuwezesha kukabiliana na vitendo vinavyotokana na matumizi ya nishati isiyo safi

“ Tumeshuhudia matokeo yanayosababishwa na ukosefu wa nishati safi kama vile uharibifu wa mazingira unaosababisha ukame na mafuriko ambayo kwa kupata nishati safi tunaweza kuondokana nayo,” amesema.

Mkutano huo wa kimataifa ni mwendelezo wa mikutano ya kikanda na kimataifa inayokusudia kupata suluhisho la changamoto zinazotokana na matumizi ya nishati chafu.

Mwezi Januari, 2025, viongozi na wakuu wa nchi mbalimbali barani Afrika na taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika walikutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kuwawezesha watu takribani milioni 300 barani Afrika kupata huduma ya nishati ya umeme.







Share:

AZANIA BANK ROCKCITY- MWANZA YAZIKARIBISHA AMCOS KAGERA KUJIINUA KIUCHUMI

 

Na Lydia Lugakila - Kyerwa 

Meneja wa Benki ya Azania tawi la Rockcity Mall, Mkoani Mwanza Bi Bernadeta Makigo amezikaribisha AMCOS zote zilizopo Mkoa wa Kagera na maeneo mengine kuijaribu benki hiyo ki huduma kwani ni benki inayotoa kinahitajiwa na mteja kwa wakati lengo likiwa ni kuwawezesha kununua zao la Kahawa kwa Wananchama wake na kujiinua ki uchumi.

Makigo ametoa kauli hiyo katika mkutano Mkuu wa kawaida wa Wanachama uliofanyika Machi 12,2025 katika eneo la kiwanda cha kukoboa Kahawa kilichopo Rubwera wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.

Makigo amesema kwa mwaka huu wamejikita sana kwa Wilaya za Karagwe na Kyerwa kwa ajili ya kuwafikia wakulima na AMCOS zinazoendesha zao la Kahawa.

Aidha ameongeza kuwa benki hiyo ina wateja wao ambao walishafunguliwa akaunti zaidi ya 2000 kwa mwaka 2024 na walikopesha AMCOS moja kwa ajili ya kununua Kahawa na kiasi walichoambiwa hawakuwapunguzia wala kuwaongezea.

Amesema kuwa kwa Mkoa wa Kagera wao walianza kuingia na kujitangaza katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa tangu mwaka 2019 ambapo walitoa huduma mbalimbali za kufungua akaunti na huduma nyinginezo.

"Kuna AMCOS kama za tumbaku zilizoko Tabora walipata changamoto ambapo tumbaku iliungua lakini bima walifidiwa kutokana na kuwa na bima", amesema Makigo.

Akiielezea benki ya Azania amesema ni Benki ya wananchi wote kwa sababu inamilikiwa na mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii ikiwemo PSSSF, NSSF, NHIF, WCF, EADB na wananchi hivyo mtu unapoenda kutibiwa hospitali au unapochangia wafanyakazi wako au kulipia ada yoyote ujue unaiwezesha benki hiyo kuendelea.

"Tuna mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara mbalimbali, mikopo  ya kilimo, mikopo ya wastaafu, mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na mikopo kwa Watumishi wa umma" ,amesema Meneja huyo.

Hata hivyo amezikaribisha AMCOS zote kuijaribu benki hiyo ili kuona watakavyowahudumia kwa wakati ili waweze kununua zao la Kahawa kwa Wananchama na kuwa kwa mwezi Juni mwaka 2024 walitoa huduma kwa AMCOS 3 katika Wilaya ya Kyerwa na Rockcity walitoa 1 na  walifurahi kununua Kahawa kutoka kwa Wanachama wao huku akiomba kuwa wakitumia taasisi nyinginezo za kifedha kuomba mkopo wasisite kuitumia benki hiyo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger