Wednesday, 12 March 2025
PIC YAIPONGEZA TBA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI NZUGUNI DODOMA
DKT. BITEKO AWASILI BARBADOS KUNADI NISHATI SAFI KIMATAIFA
RAIS SAMIA AONYA MA DC , WAKURUGENZI WANAONYATIA UBUNGE... "MTAKOSA VYOTE"
Tuesday, 11 March 2025
SERIKALI IMEFANYA JITIHADA KUBWA KUWEZESHA WANAWAKE KUPIGA HATUA KIMAENDELEO

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwa katika kazi ya vikundi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akielezea malengo ya Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Timu (Shule Bora) Bi. Virginie Briand (kushoto) na Bi. Zainab Dhanani (katikati) kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera,Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo.
Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Bi. Mwanaamani Mtoo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya jitihada kubwa katika kuwawezesha wanawake kupiga hatua kimaendeleo.
Bi. Mtoo ameyasema hayo leo kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Amesema uwezeshwaji wa wanawake umefanyika kwa ushirikiano wa Viongozi wa Serikali pamoja na wanawake na wanaume kwani hakuna maendeleo ya wanawake pasipokuwa na wanaume kama ambavyo Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 2008 ilivyotanabaisha katika Sura ya 5 ambayo inazungumzia Anuai za Jamii katika Utumishi wa Umma ambao umeleta msukumo mpya wa ufanisi na tija kwenye utendaji kazi kwa kutumia ujuzi na vipaji walivyonavyo.
Aidha, Bi. Mtoo amesema kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 298 pamoja na Kanuni za Mwaka 2022 zimeelekeza uzingatiaji wa masuala ya kijinsia ambapo Ofisi hiyo imetoa Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia unaopaswa kutumika wakati wa usimamizi wa rasilimaliwatu ikiwemo kwenye masuala ya usaili na michakato ya ajira ili kuhakikisha watumishi wanawake au kundi la jinsi yenye uwakilishi mdogo linapewa fursa katika nafasi za ajira kwa kuzingatia sifa na vigezo.
“Mwongozo huu ni kielelezo tosha cha dhamira ya Serikali ya kuimarisha ujumuishwaji wa jinsia katika Utumishi wa Umma jambo ambalo ni muhimu katika kuboresha utendaji kazi serikalini unaoiwezesha Serikali kuimarisha uchumi wa nchi na utoaji wa huduma kwa wananchi wote. Amesisitiza Bi. Mtoo.
Ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Elimu ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kuibua viongozi mbalimbali wakiwemo wanawake kujumuishwa na kuleta uwiano sawa wa jinsia.
Ameongeza kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kutambua thamani ya mwanamke, inampongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo katika taifa hili.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid Maulid amesema kongamano hilo limelenga kujadili mustakabali wa Mwanamke na Uongozi katika Elimu ambapo itawawezesha kupata maoni, ushauri na mapendekezo yatakayoleta matokeo na mikakati itakayowezesha kupiga hatua kubwa kwa maendeleo ya ustawi wa taifa.
MWENYEKITI UVCCM KAGERA AMPAMBANIA RAIS SAMIA
Na Lydia Lugakila
Karagwe
Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Uvccm)Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewahimiza Vijana Mkoani Kagera Kutafuta kura za Mgombea Urais mwaka 2025 Dkt. Samia Suluhu Hassan Ili Mkoa wa Kagera Uweze Kuongoza katika kura za jumla.
Akizungumza na baadhi ya Vijana Katika Ukumbi wa CCM Uliopo Mjini Kayanga Wilayani Karagwe ikiwa ni Ufunguzi Wa ziara ya Siku kumi na sita ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (Uvccm)Mkoa wa Kagera siku ambayo itakuwa maalum kwa Kukutana na Vijana Wa Chama cha Mapinduzi Ccm Faris amesema kuwa Vijana wa chama cha Mapinduzi Wanatakiwa kutafuta kura nyingi za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Mgombea Urais kwa mwaka huu wa 2025 kwani tayari amepitishwa na Wajumbe wa Halmashauri mkuu Kuwa Mgombea Urais .
"Tunatamani sana Mkoa Wetu upate heshima ya kuongoza kwenye kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini kura nyinyi kama Wanakaragwe wekeni malengo ya kusema kura za Nchi Nzima au za Majimbo Karagwe iwe ya kwanza katika Kupiga Kura za Rais Samia”Amesema Faris
Aidha Faris amewapongeza Wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa Kuendelea Kumuamini Mbunge Wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi kwa Kuwa Mbunge wao ambaye pia amewapatia fursa ya kuwatafutia miradi mikubwa ya Maendeleo Ikiwemo miradi ya maji,Afya na Barabara.
Hata hivyo ziara hiyo itaendeshwa na kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera, chini ya Mwenyekiti wake Faris Buruhani kwa siku 16 ndani ya Mkoa wa Kagera na Kampeni hii itapita kwenye wilaya zote 8 za Chama kwa kuyafikia makundi ya Vijana wa Vyuo na Vyuo vikuu kwenye wilaya zote,Vijana wa Shule za Sekondari,Vijana waliopo vijiweni na mitaani,Vijana walioko kwenye kambi ya mafunzo,Vijana waliyojiajiri kwenye sekta zisizo rasmi,Viongozi wa dini na viongozi wa Kimila.
Monday, 10 March 2025
RC ROSEMARY SENYAMULE MGENI RASMI MISA - WADAU SUMMIT 2025





















































