Wednesday, 12 March 2025

PIC YAIPONGEZA TBA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI NZUGUNI DODOMA



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),Mhe.Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12,2025 mara baada ya kamati yake kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),kwa ujenzi wa nyumba bora huku ikiwasisitiza kuendelea kusimamia matunzo ya nyumba hizo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 12,2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Augustine Vuma wakati kamati hiyo ilipotembelea awamu ya pili ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi 3500 unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Mhe.Vuma , amesema mradi huo umebuniwa kwa ubunifu wa hali ya juu na unatekelezwa kwa viwango vinavyoridhisha. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha nyumba hizo zinatunzwa vizuri ili zidumu kwa muda mrefu.


“Napongeza Wizara, TBA kwa ubunifu huu mzuri, hakikisheni zinasimamiwa vizuri ili kuwepo makazi ya kutosha kwa watumishi wa serikali na wateja hao waendelee kufurahia huduma za nyumba nzuri.

Aidha ameishauri TBA kushirikiana na taasisi kama TARURA ili kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya mradi huu kwa kiwango cha lami.


Kwa upande wake Kaimu katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme,Mhandisi Mwanahamis Kitogo amesema kuwa wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na kamati ya PIC pamoja na ushauri waliowapatia ili kuboresha huduma wanazozitoa kwa jamii hasa katika utendaji na usimamizi wa nyumba wanazojenga.

“Maelekezo yametoka wakati kuna sera na miongozo ambayo tayari Wizara imeshaitoa kwa ajili ya kuboresha TBA katika utendaji wake wa kazi zaidi kwa hiyo maelekezo hayo tuliyoyapokea ni kama nyongeza ya jitihada ambazo tayari Wizara imeshazifanya kwa hiyo tutakwenda kutasimamia na tutafanya vizuri zaidi ya hapa tunavyofanya,” amesema Mhandisi Mwanahamisi


Naye Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro, amesema TBA itaingia ubia na sekta binafsi ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa haraka na kwa ufanisi. Amebainisha kuwa TBA tayari imesaini makubaliano na wawekezaji kutoka nje ambao watashiriki katika awamu ya pili ya mradi.

“Mbali na kushirikiana na sekta binafsi, tunapunguza gharama za ujenzi kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata zege hapa Nzuguni,” amesema Arch. Kondoro.

Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Meneja Mradi kutoka TBA, Emmanuel Julius almesema kuwa awamu ya pili ya uendelezaji inahusisha ujenzi wa nyumba 60 za chini na nyumba 90 zitakazokuwa kwnehe majengo matatu yenye sakafu 5 kila moja ili kuwa na matumizi sahihi ya ardhi na kufikia lengo kwa urahisi na ubora.

“Katika mpango wa utekelezaji wa awamu ya pili umeanza na ujenzi wa nyumba 50 za chini na maghorofa mawili ambayo kila moja lina uwezo wa kuchukua familia 30, unatekelezwa ba TBA kwa utaratibu wa Buni jenga kwa gharama ya sh. Bilioni 28.2.”

Katika nyumba 50 zilizoanza kujengwa katika awmau hii ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo nyumba 23 kazi ya kupaua inaendelea na nyumba 24 zipo hatua ya msingi, tatu zimekamilika ambapo moja itatumiwa kwa huduma za afya na moja kituo cha polisi.”

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakikagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),Mhe.Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12,2025 mara baada ya kamati yake kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.


Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme(DTES), Mhandisi Mwanahamisi Kitogo,akiipongeza Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro,akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Share:

DKT. BITEKO AWASILI BARBADOS KUNADI NISHATI SAFI KIMATAIFA








Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati




Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi ya Nishati endelevu utakaofanyika katika jiji la Bridgetown kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi, 2025.




Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini humo, Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Mhe. Lisa Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole




Aidha, Dkt. Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali kuhusu matumizi ya Nishati endelevu kimataifa ikiwemo Nishati safi ya kupikia ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya nishati isiyokuwa safi.




Dkt. Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake, Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba.




Share:

RAIS SAMIA AONYA MA DC , WAKURUGENZI WANAONYATIA UBUNGE... "MTAKOSA VYOTE"

Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapa onyo kali Wakurugenzi,Wakuu wa Wilaya na Viongozi wote waliochini ya Mwamvuli wa Serikali za mitaa kwa kuwataka kutoa taarifa mapema kwa wanaotaka kurudi kwa wananchi na kuomba ridhaa ya kuwaongoza ili viongozi walio chini yao wapandishwe hadhi na kushikilia nafasi zao badala ya kuacha Serikali za mitaa bila viongozi na kuongeza kuwa kwa atakaye fanya hivyo bila kutoa taarifa basi ajiandae kukosa yote kwa kupoteza cheo na kuiacha nafasi aliyokuwa akiitumikia.
Share:

Tuesday, 11 March 2025

SERIKALI IMEFANYA JITIHADA KUBWA KUWEZESHA WANAWAKE KUPIGA HATUA KIMAENDELEO

 


Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwa katika kazi ya vikundi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akielezea malengo ya Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Timu (Shule Bora) Bi. Virginie Briand (kushoto) na Bi. Zainab Dhanani (katikati) kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera,Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam


Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Bi. Mwanaamani Mtoo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya jitihada kubwa katika kuwawezesha wanawake kupiga hatua kimaendeleo.

Bi. Mtoo ameyasema hayo leo kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.

Amesema uwezeshwaji wa wanawake umefanyika kwa ushirikiano wa Viongozi wa Serikali pamoja na wanawake na wanaume kwani hakuna maendeleo ya wanawake pasipokuwa na wanaume kama ambavyo Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 2008 ilivyotanabaisha katika Sura ya 5 ambayo inazungumzia Anuai za Jamii katika Utumishi wa Umma ambao umeleta msukumo mpya wa ufanisi na tija kwenye utendaji kazi kwa kutumia ujuzi na vipaji walivyonavyo.

Aidha, Bi. Mtoo amesema kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 298 pamoja na Kanuni za Mwaka 2022 zimeelekeza uzingatiaji wa masuala ya kijinsia ambapo Ofisi hiyo imetoa Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia unaopaswa kutumika wakati wa usimamizi wa rasilimaliwatu ikiwemo kwenye masuala ya usaili na michakato ya ajira ili kuhakikisha watumishi wanawake au kundi la jinsi yenye uwakilishi mdogo linapewa fursa katika nafasi za ajira kwa kuzingatia sifa na vigezo.

“Mwongozo huu ni kielelezo tosha cha dhamira ya Serikali ya kuimarisha ujumuishwaji wa jinsia katika Utumishi wa Umma jambo ambalo ni muhimu katika kuboresha utendaji kazi serikalini unaoiwezesha Serikali kuimarisha uchumi wa nchi na utoaji wa huduma kwa wananchi wote. Amesisitiza Bi. Mtoo.

Ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Elimu ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kuibua viongozi mbalimbali wakiwemo wanawake kujumuishwa na kuleta uwiano sawa wa jinsia.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kutambua thamani ya mwanamke, inampongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo katika taifa hili.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid Maulid amesema kongamano hilo limelenga kujadili mustakabali wa Mwanamke na Uongozi katika Elimu ambapo itawawezesha kupata maoni, ushauri na mapendekezo yatakayoleta matokeo na mikakati itakayowezesha kupiga hatua kubwa kwa maendeleo ya ustawi wa taifa.
Share:

MWENYEKITI UVCCM KAGERA AMPAMBANIA RAIS SAMIA








Na Lydia Lugakila

Karagwe 

Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Uvccm)Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewahimiza Vijana Mkoani Kagera Kutafuta kura za Mgombea Urais mwaka 2025 Dkt. Samia Suluhu Hassan Ili Mkoa wa Kagera Uweze Kuongoza katika kura za jumla.  


Akizungumza na baadhi ya Vijana Katika Ukumbi wa CCM Uliopo Mjini Kayanga Wilayani Karagwe ikiwa ni Ufunguzi Wa ziara ya Siku kumi na sita ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (Uvccm)Mkoa wa Kagera siku ambayo itakuwa maalum kwa Kukutana na Vijana Wa Chama cha Mapinduzi Ccm Faris amesema kuwa Vijana wa chama cha Mapinduzi Wanatakiwa kutafuta kura nyingi za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Mgombea Urais kwa mwaka huu wa 2025 kwani tayari amepitishwa na Wajumbe wa Halmashauri mkuu Kuwa Mgombea Urais . 


"Tunatamani sana Mkoa Wetu upate heshima ya kuongoza kwenye kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini kura nyinyi kama Wanakaragwe wekeni malengo ya kusema kura za Nchi Nzima  au za Majimbo Karagwe iwe ya kwanza katika Kupiga Kura za Rais Samia”Amesema Faris 


Aidha Faris amewapongeza Wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa Kuendelea Kumuamini Mbunge Wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi kwa Kuwa Mbunge wao ambaye pia amewapatia fursa ya kuwatafutia miradi mikubwa ya Maendeleo Ikiwemo miradi ya maji,Afya na Barabara.


Hata hivyo ziara hiyo itaendeshwa na kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera, chini ya Mwenyekiti wake Faris Buruhani kwa siku 16 ndani ya Mkoa wa Kagera na Kampeni hii itapita kwenye wilaya zote 8 za Chama kwa  kuyafikia makundi ya Vijana wa Vyuo na Vyuo vikuu kwenye wilaya zote,Vijana wa Shule za Sekondari,Vijana waliopo vijiweni na mitaani,Vijana walioko kwenye kambi ya mafunzo,Vijana waliyojiajiri kwenye sekta zisizo rasmi,Viongozi wa dini na viongozi wa Kimila.

Share:

Monday, 10 March 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 11,2025




Magazeti

Share:

RC ROSEMARY SENYAMULE MGENI RASMI MISA - WADAU SUMMIT 2025


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Misa Tanzania na wadau (MISA-TAN - Wadau Summit 2025)  itakayofanyika Machi 14, 2025, jijini Dodoma. Kongamano hili linaloandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika  Tawi la Tanzania (MISA - TAN), litawakutanisha waandishi wa habari na wadau wa habari na mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Share:

JAMII YAASWA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO




Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Jamii imeaswa kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na Magonjwa ya mlipuko ikiwemo Marburg.

Hayo yamebainishwa na Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera Bi.Domina Jeremiah wakati akitoa elimu ya Afya katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ng'ambo.

Amesema miongoni mwa tahadhari muhimu za kuchukua katika kujikinga ni pamoja na kuwa na desturi ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono.

"Tunasema Kinga ni bora kuliko Tiba hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari, tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni, tusisalimiane kwa kushikana mikono,pia toa taarifa kwa uongozi wa Kijiji, mtaa, Kituo cha Huduma za Afya kilichokaribu nawe au piga 199 bure"amesema.

Aidha, ametaja baadhi ya dalili za ugonjwa wa Marburg ni kutoka damu mwilini, Homa , kuhara au kuharisha damu na unaweza kuenezwa kwa kugusa majimaji ya mgonjwa ikiwemo jasho, damu, nguo, matandiko ya mtu mwenye maambukizi na kuchangia vitu vyenye ncha kali,maambukizi kutoka kwa wanyamapori ikiwemo sokwe, tumbili.

Mchungaji Samwel Mbilanga ni Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ng'ambo Wilayani Biharamulo ameishukuru Serikali kwa kuweka jitihada kubwa za Utoaji wa Elimu ya Afya huku akisema Kanisa hilo limejizatiti katika masuala ya Afya .

"Tunashukuru Serikali kwa kuweka Kipaumbele cha elimu ya Afya ambapo na sisi kama Kanisa moja ya jambo kubwa tunalozingatia ni masomo ya Afya kanisani na tumehakikisha kuwa na ndoo za maji tiririka kila lango la Kanisa na chooni, na suala la ulaji huwa tunazingatia sana Afya"amesisitiza.

Aidha, Mchungaji Mbilanga amesema katika kipindi suala la maombi kwa kushikana wamesitisha ili kuzua maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.

Nao baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo akiwemo Marther Nyanjara pamoja Zabron Mfungo wamesema kupitia elimu hiyo watakuwa mabalozi wa kueneza ujumbe kwa waumini wengine hasa kwa kusambaza namba 199 na kuepuka kugusana .

Katika utoaji wa elimu ya Afya kanisani hapo,baadhi ya wadau walioshiriki ni pamoja na Uwakili kutoka UNICEF, Africa CDC na Muunganiko ya Redio za Kijamii Tanzania(TADIO).








Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger