Saturday, 1 March 2025

WAJUMBE WA BODI YA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA WASILISHENI MAPENDEKEZO YATAKAYOLETA TIJA KWA TAIFA - SIMBACHAWENE



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizindua bodi hiyo kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma wakiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa bodi hiyo uliozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya Waziri huyo kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikabidhi vitendea kazi kwa wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu, Bi. Mariam Mwanilwa mara baada ya Waziri huyo kuwasili kwa lengo la kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.


Na. Veronica Mwafisi-Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara kuwasilisha mapendekezo ya Kima cha chini cha mshahara yanayochozingatia hali halisi ya maisha na maslahi ya wafanyakazi ili kuepuka migogoro na kushuka kwa morali ya wafanyakazi, tija na uzalishaji.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Simbachawene amesema Kima cha Chini cha Mshahara ni suala muhimu sana na lisiposhughulikiwa vizuri linaweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima na hivyo kuzorotesha uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, Kima cha chini cha mshahara kisichozingatia hali halisi ya uchumi ni hatari katika maendeleo ya nchi hasa kutokana na ukweli kwamba kunaweza kusababisha kutokea kwa mfumuko wa bei, na kuongeza gharama za uendeshaji.

Waziri Simbachawene amesema Bodi ya Mshahara katika Sekta ya Umma ina jukumu la kufanya uchunguzi na kupendekeza kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Utumishi wa Umma kuhusu Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma, hivyo katika kutekeleza majukumu haya, Bodi ina wajibu wa kuzingatia maslahi ya nchi na mustakabali wa uchumi wa nchi wakati wa kutoa mapendekezo stahiki.


Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda amesema pamoja na uzinduzi wa bodi hiyo, Wajumbe watapatiwa mafunzo kwa ajili ya kujengewa uwezo zaidi na kupata uelewa kuhusu majukumu ya upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika Utumishi wa Umma.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma, Bw. Mathias Kabunduguru amemuahidi Waziri Simbachawene kuwa watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na malengo yaliyokusudiwa katika kupendekeza na kutoa ushauri kwa ustawi wa nchi.


Uteuzi wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara umefanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 35(1) cha Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho kupitia kifungu cha 14(b) cha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ajira na Kazi (The Employment and Labor Laws (Miscellaneous Amendment Act) Na. 24 ya mwaka 2015.

Kupitia Marekebisho hayo yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 08/07/2015, Serikali ilianzisha Bodi mbili, moja kwa ajili ya Sekta binafsi na nyingine kwa ajili ya Sekta ya Umma. Marekebisho hayo yalilenga kuboresha ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.
Share:

TEAM FEBRUARY WASHEREHEKEA MWEZI WA KUZALIWA KWA KUTOA MSAADA KWA WAZEE USANDA

Kikundi cha watu maarufu kama Team February, kinachojivunia watu waliozaliwa mwezi wa pili, kimeonyesha moyo wa huruma kwa kufanya matendo ya kijamii kwa kutoa msaada kwa Wazee wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Wazee cha Busanda, kilichopo katika Kata ya Usanda, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Team February wametembelea kituo cha kulelea Wazee cha Busanda Februari 28,2025















Share:

DKT. KAZUNGU AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI YA AEE INTEC YA AUSTRIA


📌 Yaeleza nia ya kuwekeza katika teknolojia mpya ya Joto la Jua (Solar thermal)

📌 Solar thermal kutumika hospitali, viwanda, masoko ili kupunguza matumizi ya umeme

📌 Dkt.Kazungu aikaribisha nchini

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia Endelevu ya Nishati (AEE INTEC) ya nchini Austria, Bw. Christopher Brunner ambaye ameeleza nia ya  kampuni hiyo kuwekeza katika teknolojia mpya ya Joto la Jua (Solar thermal) inayotumika katka kuchemsha maji yanayoweza kutumika katika Shule, Hospitali, Vyuo, Viwanda na Masoko ambayo inawezesha  kupunguza matumizi ya umeme.

Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Gaborone nchini Botswana ambapo Dkt Kazungu anaongoza  Ujumbe wa Tanzania kushiriki Wiki ya Nishati Endelevu kwa Nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC).

“Tanzania tuna rasilimali ya kutosha ya Jua ambayo inaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. tunahitaji teknolojia rahisi  za kisasa na za gharama nafuu katika kuendeleza nishati ya Jua.” Amesema Kazungu

Katika kuhakikisha Tanzania inanufaika na programu hiyo kupitia Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Kazungu ameialika Taasisi ya AEE kuja nchini ili kufanya mazungumzo na Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi zinazohusika na uendelezaji wa nishati ya jua.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya AEE, Bw. Christopher Brunner alimueleza  Dkt. Kazungu kuwa, taasisi hiyo inahusika kutoa mafunzo na kutekeleza miradi ya mifano (Solar Thermal Training & Demostration Initiative - SOLTRAIN) katika maeneo ya Nishati, Viwanda, Afya, Elimu na Kilimo kwa Afrika na duniani kwa ujumla.

Alieleza kuwa kwa Afrika Taasisi hiyo inafanya kazi katika nchi mbalimbali ikiwemo Botswana, Lesotho, Afrika ya Kusini na Zimbabwe na inashirikiana na Serikali za nchi hizo katika utekelezaji wa miradi ya umeme jua kwa njia mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo kwa wazawa kuhusu utengenezaji wa vifaa vya umeme jua.

Aliongeza kuwa, kampuni hiyo pia  inawajengea uwezo makundi ya vijana na wanawake katika maeneo mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa nishati ya Jua ambapo Taasisi hiyo inatarajia kuongeza wigo wa Programu katika nchi za Malawi na Zambia.

 Mazungumzo kati ya Dkt. Kazungu na Bw. Brunner yalihudhuriwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na Mtaalam wa Nishati Jadidifu, Mhandisi Justine Malaba.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 1,2025

 




             


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger