Thursday, 6 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 6,2025

 




               


             
Share:

Wednesday, 5 February 2025

CAG KICHERE AIPA HEKO TANROADS UJENZI UWANJA WA NDEGE MSALATO




Na Mwandishi Wetu,Dodoma

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Charles Kichere amepongeza kasi ya ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato wenye ukubwa wa hekta 4,500 ( hekari 11000).

CAG Kichere ametoa pkngezi hizo leo tarehe 4 Februari 2025 wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja cha ndege wa Msalato Jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na maafisa kutoka ofisi ya CAG amempongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania-TANROADS Mhandisi Mohamed Besta pamoja na Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa uwanja huo wa Msalato ambapo amesema kuwa muda mwingi hutumika akiwa ofisini kusoma ripoti za miradi pasipo kujionea mambo makubwa yayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Katika ripoti zetu za ukaguzi tunasoma lakini ni vyema kuja kama hivi kujionea ni kitu gani kinachoendelea eneo la mradi, kwahiyo tumeona nini kimetokea" Amekaririwa CAG Kichere
Kichere amehimiza wakandarasi wa mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukanilisha mradi huo kwa wakati unaotakiwa ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kutovamia maeneo hayo ya uwanja kwani ni alama ya mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla wake.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania-TANROADS Mhandisi Mohamed Besta amesema kuwa uwanja huu utakamilika rasmi mwezi Novemba 2025 na kuanza kutumika ifikapo Julai 2025.

Mhandisi Besta amesisitiza kuwa wananchi wanautazama uwanja huo kama sehemu ya uwekezaji nchini hivyo kasi ya ujenzi itaendelea ili ukamilike kwa wakati.

Naye Msimamizi wa mradi Mhandisi Kendrick Chawe amesema kuwa uwezo wa uwanja huo kiteknolojia na ufanisi wa maegesho ya ndege una uwezo wa kuchukua ndege 17 kwa wakati mmoja " Parking space zipo za kutosha, hivyo unaweza kupokea ndege 17 kwa wakati moja" Amekaririwa

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato unatakuwa kiungo muhimu cha usafiri wa anga nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Ulimwengu kwa ujumla wake ambao utachochea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa.





Share:

TGNP, AGA KHAN WATOA MAFUNZO KWA WARAGHBISHI NGAZI YA JAMII UTEKELEZAJI WA MRADI WA TUINUKE PAMOJA


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akifungua mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii katika wilaya za Chemba, Kondoa TC, Kondoa DC, Mkoani Dodoma
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Aga Khan Foundation kupitia Mradi wa Tuinuke Pamoja unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania wametoa mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka wilaya za Chemba, Kondoa TC na Kondoa DC, mkoani Dodoma. 

Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia tarehe 04 hadi 07 Februari, 2025, Jijini Dar es Salaam na lengo kuu ni kuimarisha uwezo na ujuzi wa Waraghbishi katika kuongoza na kuwezesha ujenzi wa usawa wa kijinsia na ukombozi wa wanawake kwa kutumia mbinu za Shirikishi katika ngazi ya jamii.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, amesema malengo ya mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa dhana za jinsia na itikadi ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi. 

"Lengo ni kukuza uelewa wa falsafa ya Uraghbishi kwa kutumia mbinu ya “U” tatu (Upimaji, Uchambuzi, na Utekelezaji) kwa vitendo, pamoja na kuibua na kuchambua masuala ya kijinsia kwa kutumia mbinu na nyenzo mbalimbali za kiraghbishi. Vilevile, mafunzo haya yatasaidi kuimarisha ujuzi wa uchambuzi na shirikishi (PAR) pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na uwezo wa kuutumia katika utekelezaji wa miradi ngazi ya jamii",ameeleza Liundi.

Lilian Liundi amesema kwa mara ya kwanza, mradi huu umeonyesha utofauti mkubwa kwa kuzingatia kwamba ruzuku itatolewa moja kwa moja kwa vikundi vya jamii, jambo ambalo linarahisisha utekelezaji wa miradi na kujenga uwezo wa haraka kwa vikundi vya wanawake.

 Amesisitiza kuwa, ingawa mashirika makubwa ya kitaifa mara nyingi hupokea ruzuku kutoka kwa wafadhili, mradi huu umeleta mabadiliko kwa kuwatengenezea fursa wanawake, ambao ndiyo wanaoathirika zaidi na masuala ya umaskini na ukatili wa kijinsia.

Ameeleza kuwa, Mradi huu wa Tuinuke Pamoja unalenga kuwawezesha wanawake wengi, ambao mara nyingi wamekuwa wakiathirika zaidi na changamoto za kijinsia, ukatili, na umaskini. 

"Lengo kuu ni kuboresha nafasi ya wanawake katika nyanja za uongozi na kumiliki uchumi, kwani hadi sasa, idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi na kumiliki mali bado ni ndogo",amesema.

Lilian ameelezea kuwa mradi huu ni muhimu kwa sababu unatoa fursa kwa wanawake wengi katika jamii ya vijijini, ambapo masuala ya kijinsia yanaonekana kutokuwa na usawa, na mara nyingi wanawake hawa wanakutana na changamoto kubwa.

Mradi huu ni chachu ya mabadiliko katika kuboresha maisha ya wanawake, kuimarisha uongozi wao na kuongeza usawa wa kijinsia katika jamii.

Mafunzo haya ya Uraghbishi yana nafasi muhimu katika kuhamasisha na kuimarisha juhudi za kijinsia, na pia kutoa ujuzi wa kuchambua masuala ya kijinsia na kutatua changamoto zinazowakumba wanawake na utaendelea kutoa matokeo chanya na kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii.
Meneja Mradi Tuinuke Pamoja Nestory Mhando akizungumza namna mradi utakavyofanya kazi katika wilaya za Chemba, Kondoa TC, Kondoa DC mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii yanayofanyika katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa Waraghbishi na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi alipokuwa anafungua mafunzo ya siku nne ya Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii katika wilaya za Mkoa wa Dodoma
Picha ya pamoja.
Share:

Tuesday, 4 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 5, 2025

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger