Tuesday, 4 February 2025

FWITC MAFINGA NI FURSA YA VIJANA KUPATA UJUZI WA KUONGEZA THAMANI MAZAO YA MISITU




Na. Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma

Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Viwanda vya Misitu (FWITC) kilichopo Wilayani Mafinga mkoani Iringa ambacho kiko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ni fursa muhimu kwa vijana kupata maarifa ya kuongeza thamani mazao ya misitu hususan mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa anatoa majibu Bungeni baada ya swali lililoulizwa na Mhe. Deodatus Philip Mwanyika ambaye alitaka kujua Serikali itachukua hatua gani za kuhakikisha uvunaji wa rasilimali za misitu unazingatia uongezaji thamani.

Mhe. Kitandula alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya vijana 27 wa kozi ndefu na vijana 103 wa kozi fupi wamehitimu ambao hutumika kutoa mafunzo kwa wakulima wa miti katika mikoa hiyo.

“Serikali imeandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Mazao ya Mbao yaliyohandisiwa wa mwaka 2021 pamoja na Mpango Kazi wake wa mwaka (2021–2031). 

Mpango Mkakati huu umesaidia katika kuimarisha uzalishaji na biashara ya mazao ya misitu yaliyohandisiwa, ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 48 vinavyozalisha bidhaa ya venia katika Mikoa ya Iringa na Njombe na kati ya viwanda hivyo, viwanda 27 vipo katika jimbo la Njombe Mjini” aliongeza Mhe. Kitandula
Vilevile, Wizara imeandaa kanuni kupitia Tangazo la Serikali Na. 266 la tarehe 31 Machi ,2023 linalolenga kusimamia usafirishaji wa bidhaa na mazao ya misitu yanayoingia na yanayoenda nje ya nchi.

Aidha hadi kufikia Desemba, 2024 kiasi cha mita za ujazo 38,056 za bidhaa za misitu zilizoongezewa thamani (EWPs) zenye thamani ya USD 9,079,813 zilisafirishwa kwenda nje ya nchi.
Share:

BAADA YA MTWARA NI ZAMU YA KILIMANJARO, WIZARA YA KATIKA NA SHERIA HAIPOI








Na Dotto Kwilasa, KILIMANJARO

Wizara ya Katiba na Sheria imeanzisha kambi mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutoa mafunzo ya uraia na utawala bora, huku ikielekeza juhudi zake katika kutoa elimu ya masuala ya sheria kwa wananchi.

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa Wizara wa kufikisha huduma za kisheria kwa wananchi ili kukuza utawala bora na haki za binadamu katika jamii.

Hatua hii ya kuendesha mafunzo mkoani Kilimanjaro inafuatia mara baada ya mafunzo ya yaliyotolewa mkoani Mtwara kwa viongozi wa ngazi mbalimbali, kuanzia mkoa, wilaya, kata, hadi vijiji.

Pia, mkoa wa Mtwara ulikuwa na kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, ambapo wananchi walipatiwa huduma za kisheria bure katika halmashauri zote tisa za mkoa huo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa Haki, Jane Lyimo, ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yanawaleta pamoja viongozi na wadau wa haki kwa ajili ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kiutendaji.

Amesisitiza kuwa mpango huu utaziba ombwe lililopo kwenye jamii kwa kuwaachia wananchi wa chini nafasi ya kujua na kuelewa haki zao, hivyo kuwapa fursa ya kufaidika na huduma za kisheria.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mafunzo haya yatasaidia katika kuboresha utawala bora na kupunguza matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu, na kwamba baada ya mkoa wa Kilimanjaro kupokea mafunzo haya, watendaji na viongozi wataweza kuboresha huduma kwa wananchi na kuhakikisha sheria zinafuatwa ipasavyo.

"Tupo hapa kusikiliza kero za wananchi na kuenenda kwa misingi ya haki na maendeleo kwa nchi yetu," amesema Jane Lyimo.


Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Yusuf, alieleza kuwa mafunzo haya ni ya muhimu sana kwa viongozi na watendaji wa mkoa, kwani yatawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa haki na kuleta manufaa kwa jamii.

Amesema kuwa viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro wana jukumu la kutumia mafunzo hayo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa misingi ya utawala bora.

"Ni matumaini yetu sisi kama viongozi wa Mkoa mtayafanyia kazi mafunzo haya katika kufanikisha na kuleta tija kwenye majukumu yenu," amesema Kiseo Yusuf.

Mratibu wa Mafunzo hayo, Prosper Kisinini, amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kuwaongoza watendaji kutoa huduma bila ubaguzi, kwa kuhakikisha kuwa sheria na haki zinatimizwa kwa usawa na ufanisi.


Amesema mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuboresha usimamizi wa haki za binadamu na kuhimiza utawala bora katika mikoa mbalimbali, na hivyo kutengeneza mazingira bora ya kisheria kwa wananchi wa Tanzania.







Share:

Monday, 3 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 4, 2025

Share:

CCM KUWATAMBULISHA RASMI WAGOMBEA URAIS, MAKAMU KWA WANACHAMA WAKE JANUARY 5 MWAKA HUU DODOMA




Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA.Amos Makalla
amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM)kikiwa kinatarajia kuadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake kinatarajia kuwatambulisha Rasmi wagombea wake kwa wanachama katika nafasi ya ngazi ya Urais na Makamo kwa wanachama wake Januari 5,2025 jijini Dodoma.

Makalla amezungumza hayo leo January 3,2025 Jijini hapa wakati amezungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi .

"Tunatarajia kuwa na jambo kubwa,tutawatambulisha wagombea wa Urais na Makamu wa Rais Tanzania bara na Tanzania Visiwani,CCM inafanya sherehe yake ya kutimiza miaka 48 tangu kuzaliwa kwake na katika tukio hilo jambo kubwa ni kuwatangaza wagombea ambao walipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais na makamu ya Rais kwa Tanzania bara pamoja na mgombea Urais kwa Tanzania visiwani, "amesema
Mbali na hayo Makala amefafanua," Ijulikane kuwa kwa sasa CCM inawatangaza wagombea wao kwa wana CCM na muda ukifika watambulishwa kwa wananchi ili kufanikisha suala la kutimiza masuala ya uchaguzi kikatiba lakini sasa hivi ni muda wa wanachama wa CCM kutambilishwa wagombea wao,”amesema

Kutokana na hayo amewataka wana CCM wote kutoka Mikoa jirani na walioko katika Dodoma kuhakikisha wanafika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo .

“Niwakaribishe watanzania wote walioko Dodoma na nje ya Dodoma wana CCM na wasiokuwa wana CCM kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajiri hii siyo ya kupewa kadi kila mtu anakuja,”amesema.




Share:

AZMA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA UMEME WA UHAKIKA WAKATI WOTE- MHE. KAPINGA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akijadiliana jambo na Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Februari 03, 2025.

📌 Serikali yafuatilia kwa karibu upatikanaji umeme Lushoto

📌 Vijiji vyote Nkasi vyafikiwa na huduma ya umeme

**

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema ni azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika na unaotabirika kwa ajili ya shughuli za kijamii na  kimaendeleo. 

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Januari 03, 2025 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la la Mbunge wa Lushoto Mhe. Shabani Shekilindi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaondoa changamoto ya kukatika umeme katika Wilaya ya Lushoto kwa kuweka suluhisho la kudumu.

"Tutafuatilia kwa hii wiki moja kufahamu ni nini changamoto ya kukatika kwa umeme Wilaya ya Lushoto, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge iwapo kuna matengenezo tutahakikisha yanakamilika kwa haraka", amesisitiza Mhe. Kapinga.

Akijibu swali Mbunge wa Nkasi Kusini, Mhe. Vicent Mbogo aliyetaka kufahamu uwepo wa nishati ya umeme katika Kijiji cha Msamba-Masokolo, Lyapinda, Izinga na Lyele na katika Vitongoji vya Kisenga na Lupata, Mhe. Kapinga amesema Wilaya ya Nkasi ina jumla ya vijiji 90  ambapo vyote  vimepatiwa huduma ya umeme vikiwemo vijiji vya  Lyele na Lyapinda. 

Aidha, amesema Kitongoji cha Lupata kilichopo katika Kijiji cha Lyapinda kitapata umeme  kupitia mradi wa Vitongoji  15 vya Mbunge utakaotekelezwa na Mkandarasi aitwae M/s  STEG International Services Ltd ambaye ameshakamilisha  hatua za upimaji na usanifu. 

Ameongeza kuwa, uhakiki wa Kitongoji cha Kisenga umekamilika na Kitongoji hicho  kitapatiwa  umeme kupitia mradi wa vitongoji (HEP IIB).



Share:

WANANCHI WA WILAYA YA URAMBO WASHAURIWA KUFUGA NYUKI KATIKA HIFADHI YA MSITU



Na Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma

Wananchi wa Wilaya ya urambo wameshauriwa kutumia maeneo ya hifadhi za Msitu za Mpanda Line wenye ukubwa wa Hekta 427,363.2, Msitu wa Hifadhi Ulyankulu wenye ukubwa wa Hekta 239,841.4 na Msitu wa Hifadhi wa vijiji vya Kangeme, Itebulanda na Utenge (KIU) wenye ukubwa wa ekari 860 kufanya shughuli za ufugaji wa Nyuki

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Margareth Simwanza Sitta aliyetaka kujua Serikali itatenga lini eneo la sehemu ya Hifadhi ya Mto Ugalla ili Wananchi waweke mizinga ya asali.

Aidha Mhe. Kitandula alisema kuwa shughuli za ufugaji nyuki kwa wakazi wa Urambo na maeneo jirani kwa sasa zinafanyika katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Uyumbu yenye ukubwa wa kilomita za mraba 839 iliyopo Tarafa ya Usoke, Wilaya ya Urambo ambapo Wananchi kupitia vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki wameendelea kutumia eneo hilo mara baada ya Hifadhi ya Msitu Ugalla Kaskazini kupandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Taifa Mto Ugalla.

Vilevile Naibu Waziri aliongeza kuwa Sheria ya Hifadhi za Taifa Sura ya 282 hairuhusu matumizi ya rasilimali zilizoko ndani ya maeneo ya hifadhi za Taifa badala yake Sheria hiyo inaruhusu uhifadhi wa wanyampori, utalii wa picha (non-consumptive utilization of resources) na tafiti za kisayansi.

Pia kwa mujibu wa Sheria ya Hifadhi za Taifa [kifungu cha 6(1)], mara eneo linapotangazwa kuwa hifadhi ya Taifa, haki, madai, upendeleo wowote uliokuwepo awali kuhusiana na chochote ndani ya eneo lililotangazwa kuwa hifadhi ya Taifa hukoma mara moja dhidi ya mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Kitandula alisema serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo yaliyohifadhiwa ili kuendelea kujenga uelewa wa masuala ya uhifadhi wa maliasili hasa pale inapotokea eneo hilo linapandishwa hadhi.
Share:

WAZIRI JAFO AUNDA KAMATI YA WATU 15 KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO



WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam wakati akitangaza timu ya watu 15 kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Soko la Kariakoo ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

..........

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo ameunda Timu ya watu 15 kwa ajili ya kufuatilia changamoto inayowakumba wafanyabiashara wa Kariakoo ya wawekezaji wageni wanaokuja nchini na ajenda ya uwekezaji kinyume chake wanajishughulisha na biashara za rejereja (Wamachinga) na kuathiri uchumi wa wafanyabiashara wazawa.

Dkt. Jafo alitangaza Timu hiyo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo ambapo kuhusu utatuzi wa Changamoto mbalimbali zilizopo katika Soko hili ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Dkt Jafo alifafanua kuwa Timu hiyo inayojumuisha wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi itafanya kazi kwa siku 30 na itaanza kazi hivi karibuni ikiongozwa na Mwenyekiti wao Edda Tandi Luoga Mkuu wa Chuo cha Elimu ya biashara (CBE)

Aidha, Dkt. Jafo akieleza majukumu ya timu hiyo amesema Timu hiyo inatakiwa kufanya utafiti kwa kina kwa soko la kariakoo, kubaini ukubwa wa tazizo la wageni kupewa vibali na leseni za kufanya biashara nchini zinazoweza kufanywa na watanzania, kuchambua uhalali wa vibali na leseni zilizotolewa kwa wafanyabiashara wageni.

Aidha Dkt Jafo amesema Timu hiyo itafanya kazi ya kubaini sekta na aina ya biashara na maeneo yenye changamoto kwa wageni hapa nchini, kuchunguza utaratibu na upatikanaji wa nyumba za kufanyia biashara kwa wageni, kuchunguza udhaifu wa mfumo na uwezekano wa wageni kutumia njia zisizo rasmi kufanya biashara hapa nchini,

Aidha, Timu hiyo inatakiwa kutoa mapendekezo ya hatua za haraka zitakazoweza kuchukuliwa na taasisi katika kudhibiti wageni wanaoingia kufanya biashara na ajira zinazostahili kufanywa na Watanzania.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger