Sunday, 2 February 2025

DC MTATIRO AONGOZA UTOAJI TUZO USIKU WA WADAU SHUPAVU SHINYANGA 2025, AIPONGEZA HOLYSMILE!

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Taasisi ya HolySmile imetoa tuzo kwa  wadau mbalimbali wanaofanya vizuri katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi yenye manufaa kwa jamii ya Shinyanga katika kutoa hamasa kwa taasisi na kuchagiza uwajibikaji.

Hafla hiyo imefanyika Februari 1, 2025 katika ukumbi wa Makindo uliopo manispaa ya Shinyanga ikihudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika na taasisi, na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya utoaji tuzo, mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro ameipongeza Taasisi ya HolySmile kwa juhudi zake za kutambua na kuthamini mchango wa taasisi na mashirika binafsi katika maendeleo ya jamii na utoaji huduma na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kutatua changamoto za kijamii.

"Nitoe shukurani za dhati kwa HolySmile kwa kuandaa tuzo hizi, kwa taasisi na na mashirika yanayofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali ndani ya wilaya yetu, Mashirika na taasisi  zinayopata tuzo leo yameonyesha mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma bora kwa jamii, ni matumaini yangu kuwa haya siyo mafanikio ya mwisho, bali ni chachu ya kufanya zaidi kwa ustawi wa wananchi wa Shinyanga," amesema DC Wakili Mtatiro.

Aidha Wakili Mtatiro ametoa rai kwa wadau na wawekezaji kuendelea kuwekeza ndani ya wilaya ya Shinyanga ili kuongeza fursa kwa wananchi huku akibainisha jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo ujenzi wa treni ya umeme pamoja na uwanja wa ndege wa Ibadakuli uliopo manispaa ya Shinyanga.

"Nchi yetu inaendelea kupata maendeleo kwa kasi sana ikiwemo mkoa wa Shinyanga ambapo ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege, treni ya umeme maendeleo haya yanayoendelea kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita niwaombe wadau tuendelee kuwekeza Shinyanga ili kuongeza fursa kwa wananchi wa Wilaya hii na Mkoa wa ujumla", ameongeza DC Wakili Mtatiro.

Tuzo zilitolewa kwa mashirika na taasisi zilizojipambanua katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, mazingira, na maendeleo ya vijana.

Mkurugenzi wa Taasisi ya HolySmile, Arnold Bweichum amesema kuwa tuzo hizo ni sehemu ya mkakati wa kutambua mchango unaotolewa na  taasisi mbalimbali na kuhamasisha ubora na uwajibikaji kwa mashirika na taasisi zinazojituma kwa dhati kuleta maendeleo.



               
Share:

Wimbo Mpya : NG'WANA MARIA - NATHUTOLELA MCHALO

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 2,2025

 




       
Share:

Saturday, 1 February 2025

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UENDESHAJI WA KIWANDA CHA KMTCL




Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,akizungumza wakati wa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,wakisikiliza uwasilishwaji wa Taarifa ya Utendaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

.....

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati na Kielelezo ya Liganga Mchuchuma, Magadi soda na ufufuaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited yenye maslahi makubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) wakati wa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwasilisha Taarifa ya UTENDAJI WA Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa KMTC ili kiweze kujiendesha wenyewe, kuongeza wigo wa utoaji huduma zake kuanzia kwenye viwanda hadi kwenye migodi ili kusaidia viwanda vingi vinavyohitaji vipuri na kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza vipuri nje ya Nchi.

Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara Bw. Needpeace ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara yake itayafanyia kazi maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kushirikiana na Kamati hiyo katika kuhakikisha Kiwanda hicho cha msingi kinachotengeneza vipuri kwa ajili ya viwanda vingine kinafanya kazi kwa tija na ufanisi katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania hususani wamiliki wa Viwanda kupenda kununua na kitumia vipuri mbalimbali vya zinazotengenezwa na KMTC ili kukilinda na kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, kuongeza ajira, Pato la Taifa na kuendeleza Viwanda na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe akitoa elimu kwa wajumbe hao ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiwezesha NDC kutekeleza Miradi ya kielelezo (Flagship projects) ambapo imefanikiwa kulipia fidia wananchi kupisha Mradi unganishi wa Mchuchuma na Liganga na kusaini Mkataba wa Uchimbaji Madini ya Chuma Maganga Matitu, Magadi Soda Engaruka, Kufufua Kiwanda cha KMTCL pamoja na kuendeleza miradi mingine mikubwa ya kimkakati na kielelezo kwa ajili ya maslahi mapana ya Nchi hii.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,akizungumza wakati wa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.
Share:

MADIWANI MBINGA WASIMAMISHA KAZI WATENDAJI WA VIJIJI KWA UBADHIRIFU WA MILIONI 28


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Desderius Haule akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wakiwa kwenye kikao

Na Regina Ndumbaro - Mbinga. 

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, limewasimamisha kazi Watendaji saba wa vijiji kwa tuhuma za ubadhirifu wa Shilingi 28,236,400/=. 


Fedha hizo zilipatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato vya Halmashauri kupitia mashine za POS lakini hazikupelekwa benki kama inavyotakiwa.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Desderius Haule, ametoa maamuzi hayo Januari 31,2025 baada ya Baraza kugeuka kuwa kamati maalum ya kujadili suala hilo. 

Amesema uchunguzi uliofanywa na tume maalum ulibaini kuwa Watendaji hao walitumia fedha hizo bila kufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kushindwa kuomba idhini ya kubadili matumizi au kuhamisha fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine.


Haule ameeleza kuwa Watendaji hao walifikishwa kwenye Kamati ya Maadili, ambapo Madiwani waliunga mkono mapendekezo ya tume ya uchunguzi na timu iliyoundwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya kuwachukulia hatuanapia kupewa agizo la kurejesha fedha walizochukua.

Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa Halmashauri hiyo, Festo Mwangalika, amewataja Watendaji waliohusika pamoja na kiasi cha fedha walizoshindwa kupeleka benki. 

Watendaji hao ni Festho Komba (Sh. 7,527,100), Mwajuma Matily (Sh. 580,000), Shaban Mkongo (Sh. 582,000), Fotnatus Ngongi (Sh. 2,626,000), Keneth Moyo (Sh. 10,448,000), Sotely Kawhili (Sh. 2,734,300) na Gaston Mbunda (Sh. 3,739,000).

Katika hatua nyingine, Baraza la Madiwani limemsimamisha Diwani wa Kata ya Mapera, Betram Komba, kutohudhuria vikao vitatu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kikanuni, kutoa lugha isiyo staha, na kufanya vurugu kwenye kikao cha Baraza.


Haule amewapongeza Madiwani na Watumishi wa Halmashauri kwa kazi nzuri ya kusimamia ukusanyaji wa mapato, hali iliyoiwezesha Halmashauri hiyo kuwa kinara wa makusanyo kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma.


 Amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa fedha za umma.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger