Thursday, 9 January 2025

Picha : RC MACHA AONGOZA KIKAO KAZI NA VIONGOZI WA SERIKALI MKOA WA SHINYANGA KUBORESHA UTENDAJI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Alhamisi Januari 9, 2025, wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri. 

Lengo la kikao hicho ni kutoa salamu za Serikali na kukumbushana wajibu na majukumu ya kila mmoja katika utekelezaji wa kazi za kila siku.

Mhe. Macha amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu, akisema kuwa kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa manufaa ya wananchi na kuhakikisha maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga yanaendelea kwa kasi.

PICHA NA KADAMA MALUNDE - MALUNDE 1 BLOG

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Alhamisi Januari 9, 2025, wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Alhamisi Januari 9, 2025, wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Alhamisi Januari 9, 2025, wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Alhamisi Januari 9, 2025, wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali, na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri. 
Share:

TTB NA SHIRIKA LA NDEGE LA UTURUKI KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA





Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeingia makubaliano na Shirika la Ndege la Uturuki kutangaza utalii wa Tanzania duniani kupitia safari za ndege za shirika hilo.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumatano Januari 8, 2025 jijini Dar es Salaam, huku ikielezwa kuwa lengo ni kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji katika sekta hiyo nchini.

Katika hafla ya makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru amesema wamechagua shirika hilo la ndege kwa sababu lina idadi ya ndege zaidi ya 490 na linafanya safari zake katika miji zaidi ya 350.

“Kwa Afrika tu, linafanya safari zaidi ya 61, hivyo Tanzania itaweza kutangazwa vizuri katika hiyo miji yote duniani,” amesema Mafuru.

Ameongeza kuwa matangazo ya vivutio vya utalii vya Tanzania yatakuwa katika ndege za shirika hilo, tovuti, na ofisi zao zote duniani.

Pia, yatawalenga abiria wenye safari zenye lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki nchini Tanzania, Kadir Karaman amesema makubaliano hayo yataimarisha lengo la pamoja la kuifungua Tanzania kwenye masoko ya utalii ya kimataifa, pia yatakuwa na manufaa kwa pande zote.
Share:

Wednesday, 8 January 2025

KAYOMBO AGAWA MADAWATI 135 SHULE YA MSINGI MISUFINI

Na Regina Ndumbaro - Ruvuma 

Diwani wa Kata ya Misufini B, Manispaa ya Songea Mjini, mkoani Ruvuma, Christopher Fabian Kayombo leo tarehe 8 Januari, 2025 amekabidhi madawati 135 kwa Shule ya Msingi Misufini ili kuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi. 

Tukio hilo limefanyika kwa ushirikiano wa karibu na Mratibu wa Kata, Ndugu Adolf Challe, ambapo madawati hayo yamekabidhiwa rasmi kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ndugu Credo Komba, pamoja na Mtendaji wa Mtaa, Bi Agnes Ndunguru.

Diwani Kayombo amesema kuwa wanaishukuru serikali ya mama samia kwa na mkurugenz wa Manispaa Ya songea kwa kuwapa kiasi cha fedha shilingi milioni 25 kwa ajili ya madawati na pia ametoa kiasi cha shilingi milioni 13 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa katika shule hiyo.

Katika ukabidhi  huo wa madawati viongozi waliohudhuria   ni pamoja na Katibu  mwenezi wa Kata wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Misufini B, pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Misufini, Bi Bahati Ally Mbano.

 Wakati wa makabidhiano hayo, Diwani huyo amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na jamii ili kuimarisha sekta ya elimu, huku amewataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono jitihada za maendeleo ya shule.

 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ndugu Credo Komba, amewashukuru viongozi wa serikali na wadau wote waliosaidia kufanikisha upatikanaji wa madawati hayo. 

Amesema kuwa madawati hayo yamekuja wakati muafaka, kwani shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati, hali iliyokuwa ikihatarisha ubora wa elimu.

Naye Mtendaji wa Mtaa, bi. Agnes Ndunguru, ametoa pongezi kwa Diwani na viongozi wote waliounga mkono juhudi hizo huku amesema kuwa hatua hiyo ni mfano wa uongozi bora na wenye kujali maendeleo ya wananchi pia amesisitiza  umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika kuboresha miundombinu ya shule ili kuinua viwango vya elimu katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mratibu Kata  kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Adolf Challe, amewahimiza wananchi wa Misufini B kuendeleza mshikamano na kushirikiana na viongozi wao katika kutekeleza miradi ya maendeleo. 

Amesema kwamba wamejipanga vyema na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maendeleo ya wanafunzi katika sekta ya elimu.


Share:

PAKA MWEUSI ATUMWA KUHARIBU BIASHARA

Kutana na mwanadada aitwaye Janeth alikuwa mmiliki wa duka dogo (genge) huko Mbeya ambapo aliuza mboga na bidhaa nyingine za nyumbani kwa wateja wake waaminifu ambao walimpenda sana.  

Alikuwa akisimamia duka hilo kwa zaidi ya miaka mitano na alikuwa amepata sifa nzuri lukuki katika jamii inayomzunguka, alijulikana kwa uaminifu wake, fadhili na hata ukarimu.

Lakini siku moja kila kitu kilibadilika, Janeth alifika dukani kwake asubuhi na kumkuta paka mweusi akiwa amekaa kwenye kaunta yake akimtazama kwa macho yake ya njano. 

Alishtuka na kuogopa kwani hakuwahi kumuona paka wa aina hiyo hapo awali, na aliamini kwamba paka weusi ni ishara ya bahati mbaya, roho mbaya au mikosi katika biashara. 

Alijaribu kumfukuza paka yule lakini ilikataa kuondoka na badala yake alimrukia na kumparua hadi kutokwa na damu. Alipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna mtu aliyejitokeza kumsaidia. 

Janeth alijihisi mnyonge na kukosa tumaini, huku akijiuliza paka huyo anataka nini kutoka kwake na anakusudio gani katika biashara yake ambayo imekuwa ikiipa mapato tele ya kuendesha maisha yake kwa miaka mingi. 

Aliamua kuwaita Dr Bokko, kundi la waganga wa kienyeji ambalo lina uwezo wa kutatua tatizo lolote, Janeth alikuwa ameona matangazo yao kwenye runinga na mtandaoni, hivyo alijua watamsaidia kumuondolea paka huyo na kumrudishia amani ya akili.

Aliwapiga kupitia namba zao na kueleza hali yake, walimwambia asiwe na wasiwasi na kwamba watakuja dukani kwake haraka iwezekanavyo. Pia walimwambia awalipe ada kidogo jambo ambalo alikubali kufanya.

Aliwangoja kwa hamu wafike, akitumaini kwamba wangeweza kumfukuza paka huyo na pia kuhakikisha biashara yake inaendelea kukua na kupata faida mana tayari wateja walianza kumkimbia kwa kumuogopa paka huyo.   

Hatimaye walipofika, walikuwa wamevalia mavazi ya rangi na shanga, huku wakiwa wamekubeba mfuko wenye mimea na zana nyingine, walisalimiana na Win na kumhakikishia kuwa watamtatulia tatizo lake. 

Walimwomba atoke nje ili wamshike paka, waliingia dukani na kufunga mlango, Win akawasikia wakiimba na kugonga kuta. Alisikia harufu ya moshi na uvumba. 

Baada ya lisaa limoja walitoka dukani huku wakitabasamu na kumshika paka yule mikononi, walimwambia Janeth kwamba wamefanikiwa kuondoa laana kutoka kwa paka huyo. Pia walimwambia kwamba wamebariki duka lake, na kwamba litavutia wateja wengi na kupata faida zaidi. 

Walimkabidhi paka na kumwambia amtunze kama rafiki yake, Janeth alifarijika na kushukuru, aliwashukuru sana, na kuwalipa ada yao kisha kuondoka zao. 

Alifungua duka lake na kuwakaribisha wateja wake, alishangaa na kufurahi kuona kwamba wateja wanakuja kwa wingi kuliko hata ilivyokuwa mwanzo na sasa biashara yake imechangamka sana. Mpigie Dr Boko kwa namba  +255618536050 au tembelea tovuti yake. 

Mwisho. 

Share:

MISA TAN YAFANYA ZIARA PSSSF NA KUJIONEA UFANISI WA MFUKO HUO

Na Mwandishi wetu - Dodoma

Uongozi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA Tan ) imefanya ziara ya kujenga mahusiano kwenye Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSSSF Jijini Dodoma na kujionea ufanisi wa mfuko huo kwenye kuwahudumia watanzania.

Mwenyekiti wa MISA Tan. Bwana Edwin Soko alisema lengo kuu la ziara hiyo ni uongozi mpya wa MISA Tan kujitambulisha kwa PSSSF ili kuongeza mahusiano na mfuko huo pamoja na kuona utendaji wa mfuko huo Kwa kuwa waandishi wa habari Tanzania ni wanafaika wa mfuko huo na ni mabalozi wazuri wa shughuli za PSSSF. wakiwemo wanachama wa MISA Tan.

"Nimejifunza mengi Kwa kutembelea Idara mbalimbali ndani ya PSSSF kama vile idara ya kupokea simu Kwa wateja(Call Centre), Idara ya huduma Kwa wateja, Idara ya mafao Kwa wateja na Idara ya utunzaji wa taarifa za wanachama, huko kote nimeona  umahiri wa wafanyakazi wa PSSSF kwenye kutoa huduma Kwa watanzania", alisema Soko.

Pia Bwana Soko alimpongeza  Mkurugenzi wa PSSSF Bwana Abdul-Razak Badru Idara  nzima ya  Mahusiano na Elimu Kwa umma kwa kufanya kazi vizuri hususani kwenye kuwa kiungo muhimu katika kutoa  taarifa za huduma mbalimbali za  PSSSF kwa vyombo vya habari Nchini ili kuwapa nafasi watanzania kupima ufanisi wa Mfuko huo.

Naye Bibi Regina Kumba  Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF alieleza kuwa majukumu makubwa ya PSSSF ni kusajiri wanachama, kukusanya michango , kuwekeza na kutoa mafao Kwa wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF  kupitia mafao ya ya muda mrefu kama vile mafao ya uzeeni, mafao ya ulemavu, mafao ya kifo na  mafao ya wategemezi.

Pia Bibi Kumba alieleza pia mafao ya muda mfupi yakiwemo , mafao ya kukosa ajira, na mafao ya uzazi.

Bibi Kumba alieleza kuwa, PSSF inafanya kazi kwa katika Kanda mbalimbali Kwa kutumia mifumo ya kisasa ya utunzaji wa kumbukumbu za wanachama Kwa lengo la kuboresha mahusiano na wateja wote wa PSSSF.

Kwa pamoja uongozi wa MISA Tan na idara ya Mahusiano na Elimu kwa Umma zimekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye kufanya kazi kwa pamoja ikiwemo kuhamasisha waandishi wa habari kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya PSSSF pamoja na kuwa mabalozi wa wazuri wa PSSSF ili kujenga Leo yetu na kesho yetu Kwa pamoja.
Share:

MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI RUVUMA KUTOA ELIMU YA UTUMIAJI VIPIMO MWAKA 2025

 

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ruvuma Edward Mkanjabi

Na Regina Ndumbaro Ruvuma 

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ruvuma Edward Mkanjabi, ameeleza kuwa katika mwaka 2025, Wakala umejipanga kuhakikisha matumizi sahihi ya vipimo katika biashara na sekta nyingine muhimu. 

Aina za vipimo vinavyosimamiwa na Wakala ni pamoja na mizani ya mazao, mita za maji, na pampu za mafuta. 

Hata hivyo amesema changamoto zimeendelea kujitokeza, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vipimo batili na upungufu wa uelewa miongoni mwa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi. 

Mkanjabi amebainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara bado hawajahamasika kutumia vipimo sahihi, jambo linaloathiri haki ya mlaji na ushindani wa haki katika soko. 

Ili kukabiliana na changamoto hizi, Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ruvuma umeandaa mikakati kabambe kwa mwaka 2025. Mikakati hiyo inajumuisha kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu madhara ya kutumia vipimo batili, kufanya kaguzi za kushtukiza katika maeneo ya biashara, na kuhakikisha vipimo vyote vinavyotumika vinakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa. 

Aidha, Wakala umejipanga  kuhakikisha utekelezaji wa sheria na kanuni za vipimo unafuatwa ipasavyo. 

Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ruvuma utaendelea kuboresha huduma zake kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuwajengea uwezo watumishi wake .

Meneja Mkanjabi ametoa wito kwa wafanyabiashara wote mkoani Ruvuma kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa. 

Ameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaobainika kutumia vipimo batili au kukiuka taratibu za vipimo,  ili kulinda haki za walaji na kuhakikisha biashara inafanyika kwa uwazi na uaminifu.

Share:

Tuesday, 7 January 2025

MENEJA TARURA ATOA TAKWIMU ZA BAJETI YA UKARABATI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

 

Na Regina Ndumbaro-  Ruvuma

Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mkoani Ruvuma, Silvester Chinengo, ametangaza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 38.394 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo. Akizungumza katika ofisi za TARURA wilayani Songea Mjini tarehe 7 Januari, Chinengo alieleza kuwa bajeti hiyo inalenga kuboresha hali ya barabara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema mkoa wa Ruvuma una mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 7,146 ambapo asilimia 1.8 ya barabara hizo zina lami, asilimia 20 zina changarawe, na asilimia zilizobaki zikiwa za udongo. Hata hivyo, amefafanua kuwa asilimia 65 ya barabara hizo zimeboreshwa kwa kiwango cha lami, hatua inayolenga kupunguza changamoto za usafiri na usafirishaji.

Chinengo alitaja changamoto kadhaa zinazokabili miundombinu ya barabara, ikiwa ni pamoja na upungufu wa fedha, uharibifu unaotokana na matumizi mabaya ya barabara hasa magari makubwa, pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile mvua kubwa na mafuriko. Alibainisha kuwa hali hiyo mara nyingi huathiri ubora wa barabara na kuongeza gharama za matengenezo.

Kwa mujibu wa meneja huyo, TARURA imejipanga kushirikiana na jamii na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hizo. Alihimiza ushirikiano wa karibu na wananchi kwa kutoa elimu ya utunzaji wa barabara na kuhamasisha matumizi sahihi ya miundombinu hiyo ili kuongeza uimara wake na kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara.

Aidha, alisisitiza kuwa TARURA itaendelea kufuatilia miradi ya ukarabati na ujenzi wa barabara kwa ukaribu ili kuhakikisha viwango bora vinazingatiwa. Alisema lengo ni kuhakikisha barabara zinakuwa katika hali nzuri na zinachangia maendeleo ya uchumi na kijamii kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma.

Kwa kumalizia, Chinengo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na TARURA katika kulinda miundombinu hiyo muhimu. Alisema jitihada hizo zitasaidia kuongeza ufanisi wa usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kuboresha maisha ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger