Wednesday, 25 December 2024

TUME YATOA NENO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BVR MBEYA


Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akikagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Desemba 24, 2024. Mkoa wa Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akikagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Desemba 24, 2024. Mkoa wa Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akikagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Desemba 24, 2024. Mkoa wa Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.



Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akikagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Desemba 24, 2024. Mkoa wa Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati ametembelea mafunzo hayo na kuwataka Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya kutambua umuhimu wa zoezi hilo kitaifa hivyo wanapaswa kwenda kulitekeleza kwa umakini mkubwa.


Mkoa wa Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.

Share:

Tuesday, 24 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 25, 2024

Share:

NI LAZIMA TULINDE RASILIMALI ZETU ZA UVUVI KWA WIVU MKUBWA- DKT. KIJAJI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akiangalia kifungashio cha samaki wanaochakatwa kwenye kiwanda cha "Pride of Nile PVT" kilichopo Wilaya ya Muleba mkoani Kagera mara baada ya kufika hapo Disemba 23, 2024. Wengine pichani ni viongozi alioambatana nao kwenye ziara hiyo na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akiangalia moja ya minofu ya Sangara inayopatikana kwenye kiwanda cha Kuchakata Samaki cha "Pride of Nile PVT" kilichopo Wilaya ya Muleba mkoani Kagera mara baada ya kufika hapo Disemba 23, 2024. Wengine pichani ni wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchakata samaki cha "The pride of Nile PVT" kilichopo Wilayani Muleba mkoa wa Kagera Bw. Manoj Manoharan (kushoto) akieleza yanayofanywa na kiwanda chake kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na timu yake ya Viongozi na Watendaji wa Wizara hiyo (kulia) walipotembelea hapo Disemba 23, 2024.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchakata samaki cha "The pride of Nile PVT" kilichopo Wilayani Muleba mkoa wa Kagera Bw. Manoj Manoharan (kulia) akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na timu yake ya Viongozi na Watendaji wa Wizara hiyo (kushoto) ramani ya kiwanda hicho wakati wa ziara yake hapo Disemba 23, 2024.

****
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ametoa wito kwa Watanzania, hususan wale wanaojihusisha na shughuli za uvuvi kulinda rasilimali hizo za asili ili kuwahakikishia wananchi kukuza uchumi wao kwa misingi endelevu na kuwahakikishia upatikanaji wa malighafi (samaki) wawekezaji wa sekta binfasi waliowekeza kwenye viwanda vya kuchakata samaki na mnyororo wake wa thamani ili kukidhi uwezo wa viwanda hivyo.

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema hayo Disemba 23, 2024 alipotembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Pride of Nile PVT Ltd kilichopo katika Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera ambapo amebainisha kuwa uwekezaji huo ni matunda yanayotokana juhudi za Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, za kuimarisha mazingira bora na wezeshi sambamba na kuhamasisha sekta binafsi kupanua wigo wa kuongeza thamani ya mazao ghafi ya sekta za uzalishaji, ikiwemo uvuvi.

"Jukumu letu kama Watanzania kwa sasa ni kuzilinda rasilimali hizi za asili kwa wivu mkubwa sana kwa sababu mbali na kutupatia ajira na kipato kwa mtu mmoja mmoja, pia rasilimali hizi zinanufaisha uchumi wa nchi kwa ujumla"

Aidha, Mhe. Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wananchi kuongeza nguvu kwenye ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ili kupumzisha shughuli za uvuvi wa asili na kuwapatia nafasi samaki wa asili (wild fish) wazaliane vya kutosha, sambamba na kumuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuongeza kasi ya uhamaishaji wa ufugaji wa samaki kwa vizimba.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhe. Dkt. Abel Nyamahanga, amesema kuwa asilimia 70 ya eneo la Wilaya hiyo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria na hivyo kufanya sehemu kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Muleba kuwa wavuvi jambo linalowafanya kuwa na kila sababu ya kulinda rasilimali za Ziwa hilo kwa nguvu kubwa.

Akisoma taarifa ya mchango wa kiwanda chao kwenye soko la ajira, Meneja Ubora wa kiwanda hicho, Bw. Hamza Mustapha amesema kuwa kiwanda hicho kimefanikiwa kuajiri Watanzania 125 ambapo pia wanachangia uchumi wa Taifa kwa kulipa mrabaha na kodi mbalimbali za Serikali. Vile vile, Bw. Hamza alibainisha kuwa upatikanaji mdogo wa malighafi (samaki aina ya sangara) unapelekea kiwanda hicho kutumia chini ya asilimia 50 ya uwezo wake uliosimikwa na hivyo kuiomba Wizara kuja na mkakati shirikishi wa kuhakikisha kunapatikana sangara wa kutosha kwa ajili ya kulisha viwanda ili kukuza mauzo nje na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

Awamu ya kwanza ya ziara ya Mhe. Dkt. Kijaji kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mara, Mwanza, na Kagera) ambayo ililenga kufuatilia ufanisi wa sekta, kusikiliza na kupokea changamoto na mapendekezo ya wadau, kuzindua viwanda vya samaki, kuzindua uvunaji wa samaki wafugwao kwa njia ya vizimba kupitia program ya jenga kesho iliyo bora (BBT Life), na kufungua fursa mbalimba zilizopo kwenye sekta ya uvuvi kupitia viwanda vya kuchakata samaki  na ukuzaji viumbe maji  (hususani samaki aina ya sato) imehitimishwa leo tarehe Desemba 23, 2024 ambapo anatarajia kufanya awamu ya pili ya ziara hiyo mapema mwezi Januari 2025.
Share:

TRA TANGA YAJIVUNIA KUKUSANYA BILIONI 153.6 JULAI - NOVEMBA 2024

Na Hadija Bagasha - Tanga

Mamlaka ya ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA Mkoa Tanga imejivunia kukusanya kiasi cha bilioni 153.6 mwaka huu kwa mwezi Julai  hadi mwezi Novemba tofauti na kiwango cha bilioni 78 walichokusanya mwaka jana ndani ya kipindi hicho.


Makusanyo ya kiasi cha shilingi bilioni 153, ni kati ya mambo ambayo Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato TRA Mkoa wa Tanga inajivunia ikiwa na wateja wao mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ziara yao kutembelea wafanyabiashara mbalimbali Jijini Tanga Meneja wa TRA Mkoa Tanga Thomas Masese amesema mwaka 2024 umeanza kwa mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo kuanzia mwezi julai hadi Novemba wamevuka matarajio ya ukusanyaji ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

 “Kwa mikezi mitano hii ya mwanzo kuanzia mwezi julai 2024 mpaka mwezi Novemba tulikuwa na lengo la kukusanya bilioni 131.6 lakini tumekusanya bilioni 153.6 sawa na ufanisi wa asilimia 117,

“Tukitaka kujilinganisha na mwaka jana katika kipindi kama hiki tulikuwa na lengo la kukusanya bilioni 88 tukakusanya bilioni 78 sawa na ufanisi wa asilimia 85 hivyo toka mwaka jana tulipokusanya bilioni 78, mwaka huu tumekusanya bilioni 153 ni ongezeko la takribani asilimia 196.”alisisitiza Meneja Masese.

Wateja waliotembelewa na Mamlaka hiyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano ,na kuongeza kasi ya ulipaji wa kodi kwa maendeo ya nchi yao huku wakilaani baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kupila kodi.

“Tunawashukuru TRA kwa kututembelea na kutuona ni walipaji wazuri wa kodi lakini sio tu walipaji wazuri wa kodi lakini tumekuwa mabalozi wazuri mwanzo ilikuwa tukiona TRA tunakimbia lakini sasa wamekuwa ni marafiki zetu nah ii ni kutokana na mahusiano mazuri waliyo nayo kwetu chini ya Meneja Masese aliyepo sasa,”alisisitiza mmoja wa wafanyabiashara hao.

Mamlaka hiyo imeitaka jamii kujenga utamaduni wa kudai risiti mara wanapofanya biashara,ikiamini kama jamii itaimarisha utamaduni wa aina hiyo ,ongezeko la makusanyo mwaka huu yanaweza kuongezeka mara dufu hapo mwakani .

Share:

Monday, 23 December 2024

RC KAGERA ATOA TAHADHARI KUELEKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA


Na Lydia Lugakila -Bukoba.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amewatahadhalisha Wananchi Mkoani Kagera kujiepusha na na matumizi ya vilevi haswa madreva wawapo barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinapoteza uhai wa Watanzania.


Mwassa ametoa Kauli hiyo Desemba 22, 2024 katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika Ofisi za Mkoa huo.


Amesema kuwa ulevi kwa asilimia kubwa unasababusha ajali hivyo watumiaji wa vyombo vya moto wahakikishe waendeshe kwa umakini ili waepuke ajali zinazoweza kujitokeza.


"Tunaposherehekea siku kuu hizi za Christmas na Mwaka mpya tujiepushe na yote yanayoweza kutugharimu pia wazazi tuwaangalie watoto wasitembee wenyewe barabarani kwani ajali ni nyingi lakini msiwaruhusu kwenda fukwe za bahari bila uangalifu" alisema Mwassa.


Alisema kuwa Mkoa ulimpoteza mtoto hivi karibuni baada ya kuzama ziwani hivyo sehemu zote za hatari wasipelekwe watoto kucheza.


Aidha aliongeza kuwa katika siku kuu hizo ni vyema watoto wakapelekwa katika maeneo yanayotambuliwa kwa michezo yao.


Mwassa pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kutowapeleka watoto katika maeneo ya baa ili kulinda ustawi na makuzi.


Hata hivyo alieleza kusikitishwa na ajali iliyotokea Wilayani Biharamulo Mkoani humo iliyosababisha watu 11 kufariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa ikiwa siku za hivi karibuni pia kumetokea ajali mbaya katika Wilaya ya Karagwe na kusababisha vifo na majeruhi ambapo pia aliwapa pole Watanzania na wanakagera kutokana na majonzi hayo.

Share:

JESHI LA POLISI LATAKA WANANCHI KUONGEZA TAHADHARI MSIMU HUU WA SIKUKUU


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 23,2024
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 23,2024.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linahamasisha wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ili kuimarisha usalama katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 23,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi na vyombo vya usalama ni muhimu katika kupambana na uhalifu na kuhakikisha kuwa mazingira ya sherehe yanakuwa salama kwa kila mmoja. 

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha sikukuu, kuna hatari ya wahalifu kutumia fursa ya msimu huu kufanya uhalifu, hivyo ni muhimu kila mtu kuwa macho na kutoa taarifa kwa wakati.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, na pia amekumbusha wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ili kuhakikisha kuwa usalama unadumishwa na kila mmoja anapata fursa ya kufurahi na kusherehekea kwa amani.

Katika hatua nyingine, Kamanda Magomi ameeleza mafanikio ya misako na operesheni mbalimbali zilizofanyika kuanzia Novemba 27, 2024 hadi Disemba 22, 2024, ambapo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata wahalifu na vielelezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na silaha aina ya Gobore, madini bandia, pombe ya moshi, na pikipiki.

 Katika operesheni hiyo, watuhumiwa 81 walikamatwa na vifaa mbalimbali vilivyohusiana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na madini bandia gramu 250 yadhaniwayo kuwa ni Dhahabu, Bhangi gramu elfu 9, Mirungi bunda 09, Pombe ya moshi lita 113, Sola panel 07, Betri 04 za Sola, Pikipiki 11, Kadi 03 za Pikipiki, Antena 04 za ving'amuzi, Simu 03, Redio 02, Baiskeli 02, Mashine ya Bonanza 01, Kamera 01, na Mitambo 04 ya kutengeneza pombe ya moshi.

Kamanda Magomi pia ametangaza mafanikio ya kesi mahakamani, ambapo jumla ya kesi 18 zimepata mafanikio, na washitakiwa wameshapatikana na adhabu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha jela kwa washitakiwa wanne wa unyang'anyi wa kutumia silaha.

 Aidha, kesi nyingine zimehusisha makosa ya kubaka, kumlawiti, kumiliki nyara za serikali kinyume na sheria, dawa za kulevya, wizi, na uvunjaji wa nyumba, ambapo washitakiwa wamehukumiwa kifungo cha kati ya miezi mitatu hadi miaka 30 jela.

Kwa upande wa operesheni za usalama barabarani, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 5,376, ambapo makosa ya magari yalikuwa 3,767 na makosa ya bajaji na pikipiki yalikuwa 1,609. 

Wahusika walilipa faini za papo kwa hapo. 

Jeshi la Polisi pia limeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia, ulinzi shirikishi, na usalama barabarani, na limezindua kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 23,2024
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger