Saturday, 7 December 2024

KAYA 19,530 KUNUFAIKA NA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU MKOANI ARUSHA


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.

Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Desemba 6, 2024 Mkoani Arusha wakati wa kumtambulisha mtoa huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

"Tumeanza utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unasisitiza miaka 10 kutoka sasa 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na hili linaweza kufikiwa kupitia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo hii ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku," alisema Mhandisi Yesaya.

Alifafanua kuwa REA imeandaa programu mbalimbali ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali ambayo imeasisiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Nishati Safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti ambapo alibainisha kuwa takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka.

"Mradi huu unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya, pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza Mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi," alifafanua Mhandisi Yesaya.

Aidha, alisema kuwa mradi huo vilevile ni nyenzo muhimu ya kupunguza umaskini miongoni mwa jamii za maeneo ya vijijini kwani utatoa fursa kwa akina mama kujikita katika shughuli za uzalishaji mali pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia sababu inaokoa muda ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango huo ambao amesema unakwenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama ya manunuzi ya majiko hayo ya gesi.

"Tunashukuru kwa mawazo haya ya Mhe. Rais na kwa kazi inayofanywa na REA. Ninaamini kwa ruzuku hii iliyowekwa na Serikali, Watanzania walio wengi wataweza kumudu gharama na hii itafanikisha lengo la 80% ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034," alisema.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Lake Gas, Kanda ya Kaskazini, Ismail Juma alithibitisha kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanufaika wa majiko hayo wanafikiwa kikamilifu na alitoa wito kwa wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali kupitia REA.

Alitoa rai kwa wananchi kutumiza masharti ya kupata majiko hayo ya ruzuku ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Taifa cha NIDA ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kila mwananchi.

Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.
Share:

MWANAJESHI MSTAAFU MKE WA MTU WAKUTWA WAMEKUFA WAKICHEPUKA STOO, WAMEGANDANA TABORA

 



Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Tukio la kushtua limetokea mkoani Tabora, ambapo mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Petro Nasari, amekutwa amefariki dunia akiwa na mwanamke mmoja aitwaye Merysiana Edward, ambaye ni mke wa mtu. 

Wawili hao wamekutwa wakiwa uchi wamegandana katika Stoo ya Grocery ya  mzee Nasari, na wote walikuwa wamefariki.

Inaelezwa kuwa mke huyo wa mtu hakuonekana nyumbani kwake usiku ndipo ikabainika amefariki katika chumba kilichokuwa kinatumika kama stoo kwenye Grocery ya mwanaume huyo ambaye ni mmiliki wa grocery hiyo na mwanamke huyo ni mfanyakazi wa grocery hiyo.

Tukio hili limetokea jana katika mtaa wa Majengo, Kata ya Ipuli, ambapo miili ya marehemu hao iligunduliwa katika stoo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali unaendelea.

 Ameongeza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha vifo vyao.

Polisi wanachunguza tukio hili kwa undani zaidi, huku jamii ya Tabora ikishangazwa na hali hiyo

Share:

Friday, 6 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 7,2024



magazeti
Share:

KONGAMANO LA NNE LA WANATAALUMA LAWAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA UTALII


 

Na; Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Chuo cha Taifa Utalii (NCT), Kampasi ya Bustani Jijini Dar es Salaam Dkt. Frolian Mtey, amesema kuwa Chuo hicho kimejipanga katika kuhakikisha kinatoa elimu bora na mafunzo stahiki kwa vijana wa kitanzania na kuimarisha mifumo ya Kidijitali ili wahitimu wake waweze kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira Duniani.

Dkt. Mtey ameyasema hayo katika Kongamano la nne la wanataaluma la kuwakutanisha wadau wa sekta ya Utalii, lililofanyika leo Disemba 5, 2025, Chuoni hapo katika Kampasi ya Bustani Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikiendeleza jitihada zake za kuunga mkono maendeleo katika sekta ya utalii na kuwataka wahitimu hao kuwa waadilifu na kuwajibika kwenye maeneo yao ya kazi, kwani ulimwengu unahitaji uwajibikaji unaoheshimu tamaduni za watu.

“Maarifa ambayo mmepata hapa ni msingi, lakini ubunifu wako, na Kujitolea kwa vitendo endelevu kutafafanua mustakabali wa ukarimu na utalii. Nyinyi ndio waanzilishi wa kidijitali na viongozi wa kesho“ amesema Dkt. Mtey.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi la Kimataifa( ILO,) Bi. Caroline Khamati Mugalla, amesema kuwa sekta ya ukarimu na utalii kutengeneza fursa za kazi zenye staha na kwamba Sekta hiyo hutoa mamilioni ya ajira, haswa kwa vijana na wanawake.

“Ni mahali ambapo ujuzi unaweza kukua, na kazi zinaweza kuongezeka. Ndio maana ILO ipo mstari wa mbele katika masuala ya kukuza programu za mafunzo.

“Tumeunga mkono mipango hii kwa miaka mingi kwa sababu tunaamini katika kuwekeza katika ukuzaji ujuzi, kusaidia kuunda kazi nzuri na kukuza ujumuishaji wa kijamii“ ameeleza Bi. Mugalla.

Aidha amewakumbusha wahitimu hao kazi watakazofanya zina uwezo mkubwa wa kuunganisha watu, kuweka kumbukumbu, na kujenga na kujenga msingi utakaotumika kuwakaribisha wageni katika kupata huduma bora kwenye maeneo mbalimbali.

Naye mhitmu aliyeshika nafasi yajumla kwa kupata alama za juu kwenye masomo yake Ernest Julius ameupongeza uongozi wa Chuo hicho na wakufunzi waliofanikisha kufaulu masoo yake na kuahidi kwenda kufanyiakazi yale yote aliyoyapata na kujifunza katika Chuo hicho.

PICHA NA; HUGHES DUGILO



Share:

ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YA BARRICK,TAIFA GAS NA WADAU WAKE YAWAFIKIA WANANCHI TARIME


Baada ya kupatiwa mafunzo wanufaika wakijaribu jinsi ya kutumia majiko hayo
Mnufaika wa msaada wa majiko ya gesi kutoka Taifa Gas,Barrick kupitia kampeni ya kupinga ukatili inayoshirikisha wadau mbalimbali akiwa na uso wa furaha na matumaini mapya baada ya kukabidhiwa majiko ya gesi na kupatiwa elimu ya matumizi yake. Nishati inayotokana na mtungi wa kilo 6 ni sawa na kuni kilo 68 ambazo wangelazimika kuzitafuta porini au kuzinunua.
Mkufunzi wa nishati kutoka Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko akifurahi kwa kubeba jiko kichwani baada ya kuona wanufaika wameelewa somo la matumizi ya nishati ya gesi kwa ajili ya kuwapunguzia adha ya kuhangaika kutafuta kuni na mkaa sambamba na kufanikisha utunzaji wa Mazingira
Wananchi wakipatiwa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na matumizi ya majiko ya gesi
Wananchi wakipatiwa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na matumizi ya majiko ya gesi
Mnufaika wa msaada wa majiko ya gesi kutoka Taifa Gas,Barrick kupitia kampeni ya kupinga ukatili inayoshirikisha wadau mbalimbali akiwa na uso wa furaha na matumaini mapya baada ya kukabidhiwa majiko ya gesi na kupatiwa elimu ya matumizi yake. Nishati inayotokana na mtungi wa kilo 6 ni sawa na kuni kilo 68 ambazo wangelazimika kuzitafuta porini au kuzinunua.
Mnufaika wa msaada wa majiko ya gesi kutoka Taifa Gas,Barrick kupitia kampeni ya kupinga ukatili inayoshirikisha wadau mbalimbali akiwa na uso wa furaha na matumaini mapya baada ya kukabidhiwa majiko ya gesi na kupatiwa elimu ya matumizi yake. Nishati inayotokana na mtungi wa kilo 6 ni sawa na kuni kilo 68 ambazo wangelazimika kuzitafuta porini au kuzinunua.
Mnufaika wa msaada wa majiko ya gesi kutoka Taifa Gas,Barrick kupitia kampeni ya kupinga ukatili inayoshirikisha wadau mbalimbali akiwa na uso wa furaha na matumaini mapya baada ya kukabidhiwa majiko ya gesi na kupatiwa elimu ya matumizi yake. Nishati inayotokana na mtungi wa kilo 6 ni sawa na kuni kilo 68 ambazo wangelazimika kuzitafuta porini au kuzinunua.
Baadhi ya wanufaika katika picha ya pamoja na wadau wanaoendesha kampeni hii ya kupinga ukatili wa kijinsia
***

Kampuni ya Barrick Nchini Kupitia Mgodi wake wa North Mara kwa Kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas wameendelea kutoa elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia Wilayani Tarime Mkoani Mara kwa wananchi wanaoishi vijiji vinavyozunguka Mgodi wa North Mara.

Elimu hiyo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia imeambatana na kampuni ya Taifa Gas Kugawa Majiko ya Gesi ya kupikia kwa kaya zaidi ya 222 zinazozunguka Mgodi huo.

Licha ya Kupatiwa Elimu juu ya kupinga Ukatili wa kijinsia Washirika wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya nishati salama kutoka kwa mkufunzi wa nishati kutoka Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko ambaye amesema kuwa kampuni hiyo iko mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhimiza jamii kutumia nishati safi ya kupikia kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira.

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mafunzo hayo wamewashukuru wadau hao kwa kupatiwa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia sambamba na kurahisishiwa maisha kwa kupatiwa majiko ya gesi sambamba na kupatiwa elimu ya matumizi ya nishati hiyo.
Share:

Thursday, 5 December 2024

MALECELA APONGEZA UIMARA WA CCM NA SERIKALI ZAKE KUTUMIKIA WATANZANIA


-Ataka uzalendo zaidi sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Akizungumza leo tarehe 5 Desemba 2024, baada ya kutembelewa nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Malecela alipongeza chama hicho kwa kuendelea kuonesha uongozi imara chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Malecela ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), alisema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM unaendelea kwa kasi na umedhihirisha dhamira ya kweli ya chama hicho kuwatumikia Watanzania.

Alibainisha kuwa mafanikio ya Rais Dkt. Samia, hususan katika sekta za maendeleo ya miundombinu, afya, na elimu, yanapaswa kuwa chachu ya wanachama kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama, ambacho kimejengwa juu ya misingi imara ya kutumikia watu.

“Wanachama wa CCM wanapaswa kuwa mfano bora wa uzalendo kwa wengine. Hili ni jukumu letu la kihistoria, ambalo tunapaswa kuliheshimu kwa vitendo,” alisema Malecela.

Kwa upande wake, Balozi Nchimbi alimshukuru Malecela kwa mchango wake wa mawazo na uzoefu unaoendelea kuwa hazina kubwa kwa Chama na Serikali.

Alisema viongozi wastaafu kama Malecela wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri unaosaidia kuimarisha utendaji wa chama katika nyanja mbalimbali.

“Uzoefu wenu ni mwanga kwetu. Tunaendelea kuthamini mawazo yenu ambayo yamekuwa nguzo muhimu kwa chama na taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.

Katika mazungumzo hayo, Malecela pia alitoa wito kwa wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano na maadili ya chama, akisisitiza kuwa hiyo ni mojawapo ya misingi ya mafanikio ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Aliwaasa viongozi wa sasa wa CCM kuendeleza kazi nzuri wanayoifanya huku wakizingatia misingi ya haki, uwazi, na uwajibikaji.

Alisema maadili ya uongozi bora yamekuwa kichocheo kikubwa cha imani ya wananchi kwa CCM.

“Huu ni wakati wa kuchapa kazi zaidi, kuhakikisha tunazidi kuimarisha maendeleo ya nchi yetu huku tukiheshimu dhamira kuu ya chama ya kuwatumikia wananchi,” alihitimisha Malecela.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger