Wednesday, 6 November 2024

MAKATIBU WAKUU WA BIASHARA WA AFRIKA WATAKIWA KUTEKELEZA AFCFTA KWA VITENDO




KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs),akizungumza na washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Na.Mwandishi Wetu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs) ametoa rai kwa Makatibu Wakuu hao kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) na kuiwezesha Afrika kujitegemea, kuwa na maamuzi na sauti ya pamoja yenye nguvu ili punguza madhara ya misukosuko ya uchumi wa dunia na kuleta maendeleo kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni barani humo.

Dkt. Abdallah ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024.

Akiipongeza Jamhuri ya Liberia kwa kuridhia Mkataba wa AFCFTA, amezihimiza nchi nyingine ambazo bado hazijaridhia Mkataba huo kukamilisha mapema taratibu za ndani za uridhiwaji ili kuwa na utekelezaji wa pamoja wa Mkataba wa AfCFTA unaochochea maendeleo ya sekta mbalimbali kama viwanda, biashara, miundombinu na kukuza uchumi ndani ya Afrika.

Aidha, Dkt. Abdallah amefafanua kuwa Mkutano huo utapokea Taarifa kutoka kwa Kamati za Biashara Mtandao, Uwekezaji, Biashara ya Bidhaa, Wanawake na Vijana katika AfCFTA, Haki Bunifu na Biashara ya Huduma ili kuzijadili na kuziwasilisha katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Biashara Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 - 10/11/2024

Naye Waziri wa Biashara na Mtangamano wa Kikanda wa Ethiopia, Mhe.Yasmin Wohabrebbi, amesema AFCFTA ni nguzo imara inayolenga kuongeza kasi ya biashara baina ya nchi za Afrika, kuimarisha nafasi ya biashara ya Afrika katika soko la dunia, na kuinua mamilioni ya watu kutoka umaskini kwa kuwa unaunganisha watu bilioni 1.3 katika nchi 55 zenye Pato la Taifa la dola trilioni 3.4 za Marekani.

Akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo amesema lengo kubwa ni kuhakikisha Watanzania wanashiriki katika kuzalisha bidhaa bora zitakazopata soko hilo la Afrika ili kukuza biashara, kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa ujumla.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika(STOs) akiongoza Mkutano huo Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/202


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo pamoja na Wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) wakiongozwa na Mshauri Mkuu wa AFCFTA Dkt.Tsotetsi Makong, Novemba 05, 2024 akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha maandalizi kabla ya kushiriki Mkutano wa 19 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STOs) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/2024.


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs),akizungumza na washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.


Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Majadiliano katika Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs)Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/2024


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika(STOs) akiongoza Mkutano huo Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/202
Share:

Tuesday, 5 November 2024

TPDC YACHANGIA MILIONI 50 KUSAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI WA MATIBABU JKCI


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limechangia kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kusaidia watoto wenye uhitaji wa Matibabu ya moyo.

TPDC imechangia fedha hizo kwenye hafla ya uchangishaji fedha kusaidia watoto 1500 wenye matatizo ya moyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Tukio hilo limefanyika jana tarehe 02.11.2024 , Johari Rotana Jijini Dar es salaam.

Share:

ZAIDI YA SH. BILIONI 11 KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 90 SHINYANGA

Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle

📌Kunufaisha Kaya 2,970 kutoka katika Vitongoji 90 ndani ya Wilaya Tatu

📌RC Macha asema Umeme ni kipaumbele cha Rais Samia

Na Mwandishi wetu - Shinyanga

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha Kaya 2,970 Mkoani Shinyanga.

Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle amebainisha hayo Novemba 05, 2024 Mkoani Shinyanga mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anamringi Macha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam.

“Tunamshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kiasi cha shilingi 11,184,759,397.2 kitumike kusambaza umeme katika vitongoji 90 Mkoani hapa, leo hii tumefika hapa kumtambulisha Mkandarasi na tayari maandalizi ya awali ya kutekeleza mradi yameanza,” amesema Mhandisi Dulle.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kufikisha umeme katika vitongoji Mkoani Shinyanga, Mhandisi Dulle amesema kati ya vitongoji 2,703 vilivyopo mkoani humo, vitongoji 930 vimefikishiwa umeme na kwamba vitongoji 90 vitakavyopata umeme awamu hii vitaongeza idadi ya vitongoji vitakavyokuwa na umeme Mkoani Shinyanga.

Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle

Amesema mradi unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24 ambapo utekelezwaji wa mradi ulianza tarehe 3 Septemba, 2024 na utakamilika ifikapo tarehe 19 Agosti 2026 na kwamba vitongoji vitakavyobaki vitaendelea kusambaziwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mhandisi Dulle amebainisha kuwa mradi unatekelezwa katika majimbo sita kutoka katika Wilaya za Shinyanga, Kahama na Kishapu na kwamba kila jimbo vitongoji 15 vitanufaika.

“Mradi huu unalenga kupeleka umeme katika majimbo ya Shinyanga, Solwa, Kishapu,  Msalala, Ushetu na Kahama,” amesema Mhandisi Dulle.

Aidha, Mhadisi Dulle ameainisha hali ya upatikanaji wa umeme maeneo ya vijijini Mkoani Shinyanga sambamba na miradi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa ambapo amesema kati ya vijiji 506 vilivyopo mkoani humo, vijiji 485 vimefikishiwa umeme ambayo ni sawa na asilimia 96 na kwamba vijiji 21 vilivyobaki vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili (REA3R2) chini ya Mkandarasi Tontan Project Technology LTD JV Group Six International.

Amesema vijiji hivyo vipo katika Wilaya ya Kahama na kwamba Mkandarasi anatarajiwa kukamilisha hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameipongeza REA kwa kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kwa utaratibu iliyojiwekea wa kutambulisha wakandarasi kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kote nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha.

“Ujio wenu hapa ni habari njema sana kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya Mkoa wetu; pamoja na huduma zingine za jamii huduma ya umeme imepewa kipaumbele kikubwa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, umeme ni injini ya uchumi hili halina ubishi na sasa matumizi ya umeme yameongezeka, mahitaji kwa ajii ya majumbani na pia kiuchumi,” amesema Mhe. Macha.

Amesema Mkoa wa Shinyanga unaendelea kukua kwa kasi na kwamba kwa sasa shughuli za kiuchumi zimeongezeka ikiwemo uwepo wa viwanda vidogo na vikubwa ambavyo vyote vinahitaji umeme.

“Hapa Shinyanga mbali na Madini pia tunashughulika na kilimo cha mpunga na tungependa kuona mkulima akiongeza thamani ya mazao yake hukohuko unapozalishwa mpunga kwa kukoboa na kupata mchele na hapa faida itaongezeka sambamba na kuandaa ajira na fursa zingine vijijini,” amesema Mhe. Macha.

Aidha, amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anatekeleza mradi kwa ubora na anakamilisha kwa wakati kwani tayari miundombinu ipo hivyo hakuna changamoto yoyote itakayokwamisha utekelezaji wa mradi.

Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Derm Group (T) Limited Mhandisi  Justinus Mutalemwa.

“Tunafuraha kuona zipo kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo hii ya umeme ikiwemo kampuni hii ya Derm, tunatoa wito pia kutumia huduma na watoa huduma kwenye maeneo ya mradi, tutoe kipaumbele kwenye kazi zisizohitaji ujuzi mkubwa kwa wananchi wa maeneo ya mradi,” amesema.

Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Derm Group (T) Limited Mhandisi  Justinus Mutalemwa amesema wamejipanga kikamilifu kutekeleza mradi ambapo kwa sasa wamekamilisha hatua muhimu za awali za mradi, ikiwemo ukaguzi wa eneo na kukagua nguzo kiwandani, na tayari nguzo zimeanza kufika kwenye maeneo ya mradi.

“Tunatarajia kumaliza mradi huu ndani ya muda uliopangwa wa miezi 24. Kazi hii haitakuwa kubwa sana kwa sababu ya umbali wa kilomita 164 tu, tutamaliza kabla ya wakati uliopangwa, kikubwa tunaomba ushirikiano kutoka kwa TANESCO, REA na Serikali ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi unafanikiwa kama ilivyopangwa”,amesema Mhandisi Mutalemwa.Mhandisi Anthony Tarimo 

Naye Mhandisi Mwandamizi kutoka TANESCO Mkoa wa Shinyanga Anthony Tarimo akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga amesema  vitongoji 90 vilivyopendekezwa ni vya umuhimu mkubwa, kwa kuwa vilikuwa na uhitaji mkubwa wa huduma ya umeme, na utekelezaji wa mradi huu utaondoa malalamiko ya wananchi kuhusu ukosefu wa huduma hiyo.

“Jumla ya vijij 485 vimeshafikishiwa Umeme mkoani Shinyanga, vijiji 21 miradi inaendelea kutekelezwa. Tunayo furaha kuona Mkandarasi Derm Group amefika kuanza kutekeleza mradi kwenye vitongoji 90. Hivi vitongoji 90 vilipendekezwa kwa kushirikiana na ofisi za wabunge na kimsingi yalikuwa na uhitaji mkubwa sana wa umeme”,amesema Mhandisi Tarimo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Novemba 5,2024 wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa REA ikimtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited
Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle akizungumza leo Novemba 05, 2024 Mkoani Shinyanga mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle akizungumza leo Novemba 05, 2024 Mkoani Shinyanga mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle akizungumza leo Novemba 05, 2024 Mkoani Shinyanga mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Derm Group (T) Limited Mhandisi  Justinus Mutalemwa

Share:

UZINDUZI WA “AMAZING TANZANIA” WATIA FORA, DKT. ABBASI AELEZA TAMU NA CHUNGU ZA “LOCATION” NA MARAIS WA NCHI


Hatimaye Filamu ya kuitangaza nchi Uchina ya “Amazing Tanzania” iliyomshirikisha Rais Samia Suluhu Hassan, Dr. Hussein Mwinyi na msanii Jin Dong kutoka China, imezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo Waziri wa Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amemwakilisha Rais Samia huku Serikali ya Uchina chini ya Rais Xi Jinping ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utalii, Bw. Lu Yingchuan.

“Tayari tangu filamu hii izinduliwe Beijing Mei mwaka huu idadi ya watalii Wachina wanaokuja nchini imeongeza kutoka 44,000 mwaka jana hadi 54,000 kufika Septemba mwaka huu sawa na ongezeko la watalii 10,000 na bado mwaka wa utalii unaishia Disemba,” anasema Waziri Pindi Chana.


“Moja ya changamoto kubwa ni kuwa ‘location’ na viongozi wakubwa ni pamoja na muda wao kuwa mdogo na hata namna ya kumfanya kiongozi arudierudie kurekodi anapokuwa hajakamilisha vyema inaweza kuwa ngumu.


“Lakini timu zote tuliosimamia nao uzalishaji wa filamu hii na ile ya Royal Tour tunashukuru kuvuka vikwazo vyote hivyo,” ameeleza Dkt. Hassan Abbasi Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii aliyesimamia uzalishaji wa filamu hizo.
Share:

Monday, 4 November 2024

MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAWASILI SHINYANGA, WANANCHI KUPATA FURSA YA MATIBABU BORA


Na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog

Katika juhudi za kuboresha huduma za afya, kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imewasili mkoani Shinyanga leo, Novemba 4, 2024. 

Madaktari 47 kutoka sehemu mbalimbali nchini watatoa matibabu ya kibingwa kwa wananchi kwa muda wa siku sita, wakilenga kusaidia wale wasio na uwezo wa kupata huduma hizo.

Kambi hiyo imepokelewa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo madaktari hao sasa wamesambazwa katika halmashauri zote sita za mkoa. 

Mratibu wa Madaktari Bingwa, Everine Maziku kutoka Wizara ya Afya, ameeleza umuhimu wa kampeni hii akisema“Tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza mpango huu unaosaidia kuboresha afya za wananchi, hasa wale wanaokabiliwa na changamoto za kifedha.”

Mbali na kutoa matibabu, madaktari hao pia watajenga uwezo wa watoa huduma za afya katika hospitali za eneo hilo, na kuanzisha huduma ambazo awali hazikuwepo. 

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Faustine Mlyutu, amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi: “Nawaomba wananchi wa Shinyanga mjitokeze kwa wingi kupata matibabu ya kibingwa kutoka kwa madaktari hawa. Hii ni fursa ya pekee ya kuokoa afya zenu.”

Madaktari, akiwemo Missano Yango kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma, ambaye ni bingwa wa Magonjwa ya nje, ameeleza wamejipanga kutoa huduma bora na kuhamasisha wananchi kujitokeza. 

“Tumejizatiti kutoa huduma stahiki na tunawakaribisha wananchi kwa wingi,” amesema Yango.

Kambi hii ni mwendelezo wa juhudi za serikali kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini na ni nafasi muhimu kwa wananchi wa Shinyanga kuboresha afya zao kwa kupitia matibabu ya kitaalamu na ya kibingwa.

 

Picha ya Pamoja ikipigwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger