Tuesday, 15 October 2024

MAFIA BOXING PROMOTION WAUNGA MKONO KAMPENI YA RAIS DKT SAMIA SULUHU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 




Na Oscar Assenga,TANGA

KAMPUNI ya Mafia Promotion Boxing imetoa msaada wa majiko ya Gesi kwa wanawake wanaojishughuli na uuzaji wa vyakula katika masoko ya Mgandini, Makorora na Mlango wa Chuma yaliyoko jijini Tanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.

Licha ya kugawa mitungi hiyo ya gesi lakini wametoa msaada mwengine wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto yatimacha Green Cresent Ophanege Foundation cha Jijini humo .

Hatua ya kampuni hiyo kuunga mkono juhudi hizo inatokana na ushindi walioupata mabondia mbalimbali wanaodhaminiwa na kampuni hiyo ambao walipata ushindi katika mapambano yao walipopanda hivi mwanzoni mwa mwezi 0ctoba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Mkurugenzi wa Matangazo na Uzalishaji kutoka Kampuni ya Mafia Promotion Omari Clayton alisema pambano hilo lilichagizwa na Technical Knock Out ‘KO’ ya Rais Dkt. Samia Suluhu.

Alisema baada ya ushindi huo wapewa fedha taslimu kama zawadi kwa mabondia hao ambayo imewatia hamasa kuhakikisha wanazidi kuijengea heshima Tanzania kupitia mchezo wa ngumi.

Alisema kwamba jambo ambalo wameifanya kwa kugawa majiko hayo ya gesi ni kama sehemu ya kurudisha kwa jamii ikiwa ni utaraibu wao na wanaungana na watanzania kupitia Kampeni ya Rais Dkt. Samia ya kuhamasisha juu ya matumizi ya nishati safi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni katika kupikia na shughuli nyingine hali ambayo inasababisha mabadiliko ya tabianchi na uzalishaji wa hewa ukaa.
Alisema kwamba kampuni hiyo ya Mafia wanaunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kupambana na kuhamasisha watanzania kuhama kutoka kwenye matumizi ya mkaa na kuni kupikia na kwenda kwenye matumizi ya nishati safi.

“ Ndio maana leo tumegawa majiko ya gesi kwa mama zetu wanapika vyakula katika masoko yaliyopo katika jiji la Tanga” Alisema Clayton.
“Tumehamasika na tunampongeza sana Rais wetu Dkt. Samia kuja na ‘KO ya Mama’ na kuwazawadia mabodia wetu ambao walipambana kuhakikisha wanabakisha mikanda hapa Tanzania na walifanikiwa na tunamuahidi kwamba mama kupitia Mafia Boxing tutazidi kuiheshimisha Tanzania”Alisema .

Akizungumza kwa niaba ya mabondi wenzanke Ibrahim Mafia alisema kwamba haikuwa rahisi kupamba ulingoni kutokana na mpinzani wake kuwa imara lakini kupitia maombi ya watanzania alipambana kuhakikisha anawapa furaha kwa kupata ushindi .

“Ule ushindi ni ushindi ni ushindi wetu lakini pia ni ushindi wa watanzania walikuwa wakituombea tumepokea zawadi kutoka kwa Rais wetu mama Samia tukaona hatuwezi kuitumia peke yetu bali tushirikiane kile ambacho tumepata kwa kuwapa majiko ya gesi na kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima tunaomba mzidi kutuombea dua ili wakati mwingine tuweze kutoa kikubwa zaidi. Alisema Mafia”

Bondia Ibrahim Mafia alipanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Enoch Tettey raia wa Ghana kuwania mkanda wa dunia ‘World Boxing Council Bantamweight’ wenye uzito wa Kg 53 katika ukumbi wa City Center Hall Magomeni Sokoni na hatimaye kufanikiwa kubwaga chini mpinzani wake kwa KO.
Hata hivyo wakina mama mntilie ambao walipata majiko hayo waliwapongeza mabondia wote kwa ushindi walioupata pamoja na kuishukuru Kampuni ya Mafia Boxing Promotion kwa kuwapatia mitungi ya gesi ambayo itawasaidia katika shughuli zao.
Tunawashukuru kwa zawadi zenu na sisi tunaendelea kuwaombea kwa Mungu hakika atawalipa tulikuwa na changamoto ya kupata mkaa kwa ajili ya kupikia lakini sasa kupitia majiko haya yatatusaidia kurahisisha shughuli zetu za kupika kila siku .
Share:

Monday, 14 October 2024

DAWA YA KUMZUIA MUME ASIENDE KULALA NJE YA NDOA

Ukweli ni kwamba katika ndoa wanawake wengi hupitia changamoto mbalimbali kutokana na tabia za wanaume wao kuwa na mapango wa kando, hilo kufanya kushindwa kuhudumia familia vizuri.

Nasema hivyo kwa sababu hilo lilishawahi kunipata maishani mwangu, mume wangu hakuijali familia yake kwa lolote lile licha ya kuwa alikuwa na kazi na anapokea mshahara kila mwezi.

Sikujua tatizo lilikuwa ni nini hasa, kila ambapo ningemuuliza ni wapi fedha zake zinakwenda, basi angekuwa mkali kiasi cha kuibuka mgomvi mkubwa ndani ya nyuma yetu.

Hali hiyo ilikuwa inaniumiza sana mimi kama mwanamke, maana mimi nimeolewa tena kwa ndoa halali kabisa, ni lazima yeye kama mume anihudumie mimi mkwe, lakini hakufanya hivyo.

Baada ya kuchunguza simu yake kwa muda mrefu, nikaja kugundua kuwa alikuwa na mahusiano na wanawake wengi, hao ndio hasa walikuwa wanachukua fedha zake na yeye kuisahau familia yake.

Niliumia sana baada ya kubaini hilo, nilijiona sina thamani tena kwake, niliona ni bora nirudi kwa wazazi wangu, lakini kila ambapo nilipokuwa nawafikiria watoto wangu wataishije, nilikuwa naishiwa nguvu ya kufanya.

Wazo lilinijia kuwa nitafute watu wa mitishamba wanaweza kunisaidia kumtuliza huyo mwanaume, ndipo nikakutana na Dr Bokko ambao ndio waliokuja kuiponya ndoa yangu.

Baada ya kuwaeleza tabia ya mume wangu jinsi ilivyokuwa, waliniambia wanaweza kumfunga, hivyo hatoweza tena kuwa na mpango wa kando maisha yake yote.

Niliwaambia basi wamfunge tu, na kweli tangu wakati huo naona ametulia nyumbani na kuzidisha mapenzi kwangu, na sasa anahudumia familia yake vizuri na fedha zinaonekana ndani ya nyumba tofauti na hapo awali.

Ninatoa wito kwa wenye shida au magonjwa, kusumbuliwa na mapenzi, ndoa, biashara, kukosa ujauzito n.k, basi wasisite kuwatembelea Dr Bokko, sio lazima usafiri hadi ofisini kwao, unaweza kuongea nao kwa njia ya simu na utasaidiwa kwa haraka. Piga kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

RAIS SAMIA ATETA NA ZUHURA YUNUS


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Zuhura Yunus, jijini Mwanza leo Oktoba 14,2024 kwenye maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru. Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu) Kazi,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi.
Share:

RAIS SAMIA AELEKEZA MAKAMPUNI YA MADINI KUCHANGIA NA KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA VETA GEITA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyaelekeza makampuni ya madini kuchangia na kushirikiana na chuo cha VETA Geita katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi.

Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo hayo alipotembelea wakati akifunga Maonyesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini, jana, tarehe 13 Oktoba, 2024.

Mhe. Rais amesema ushirikiano huo pia uwawezeshe vijana kujifunza na baada ya kuhitimu wafanye kazi kwenye makampuni ya madini yaliyopo ndani ya mkoa wa Geita.

Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Martin Shigella kuratibu suala hilo na kuhakikisha linatekelezwa.

Chuo cha VETA Geita ni chuo cha hadhi ya mkoa ambacho kimeanza mafunzo mwaka 2024 na kina uwezo wa kudahili wanafunzi 720 kwa kozi ndefu na kozi fupi 1500 kwa mwaka na kwa sasa chuo kinatoa mafunzo katika fani za Umeme na Bomba, na chuo kinatarajia kutoa zaidi ya fani 13 katika maeneo mbalimbali.
Share:

WAZIRI DKT. SELEMANI JAFO APOKEA TUZO YA TANTRADE URATIBU BORA WA MAONESHO YA MADINI GEITA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo tuzo kwa niaba ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) kwa kutambua usimamizi bora na uratibu wa Maonesho ya biashara ndani na nje ya nchi na kutoa huduma ya kliniki ya biashara kipindi cha Maonesho ya 7 ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika Viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita, maonesho hayo yamefungwa Leo Oktoba 13, 2024 ,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo tuzo kwa niaba ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) kwa kutambua usimamizi bora na uratibu wa Maonesho ya biashara ndani na nje ya nchi na kutoa huduma ya kliniki ya biashara kipindi cha Maonesho ya 7 ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika Viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita, maonesho hayo yamefingwa Leo Oktoba 13, 2024 , Kushoto ni Waziri wa Madini Anthony Mavunde.

Share:

Sunday, 13 October 2024

DKT. SHEKALAGHE AHIMIZA SHIUMA KUWA KITU KIMOJA KWA MAENDELEO YA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO


Na WMJJWM, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe amewataka viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) ngazi ya Taifa na mikoa kuwa kitu kimoja na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zinazosimamiwa na Serikali kwa maendelea ya wafanyabiashara ndogondogo nchini.

Hayo ameyasema Oktoba 11, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu miongozo ya uratibu wa utoaji mikopo kwa viongozi wa SHIUMA, ili waweze kushirikiana na Serikali katika kutoa hamasa na elimu kwa ŵafanyabiashara ndogondogo kuendelea kujitokeza kujisajili kwenye Mfumo wa Kidigitali wa Kusajili Wafanyabiashara Ndogondogo (WFB).

"Baada ya mafunzo haya, ni matarajio yangu kuwa, juhudi zenu za kutoa hamasa kwa wafanyabiashara ndogondogo litazaa matunda tunapoelekea kwenye uzinduzi wa Vitambulisho na Mikopo yenye mashart nafuu itakayoanza kutolewa na Serikali kupitia Benki ya NMB na kitambulisho cha kidigitali kitakuwa moja ya dhamana yako", amesema Dkt. Shekalaghe.

Ameongeza kuwa, Wafanyabiashara ndogondogo wana mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, akisisitiza kwamba, Dhamira ya Serikali ya kutoa vitambulisho hivyo imeambatana na faida nyingi zikiwemo kutambulika na taasisi mbalimbali, kuunganishwa na mifumo ya NIDA, NAPA na Huduma nyingine za kijamii.

Aidha, Dkt. Shekilaghe amewaasa viongozi wa SHIUMA kuendelea kuwa wazalendo na kuwa mfano mzuri na watakaporejea watoe mrejesho kwa wafanyabiashara ndogondogo, pamoja na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Kwa upande wa mwenyekiti wa SHIUMA mkoa wa Pwani Filemon Maliga , amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuwatambuwa, kuboresha mazingira ya wao kufanya kazi kwa umoja pamoja na kuwapambania kuwaunganisha na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mikopo yenye masharti nafuu.

Uzinduzi wa utambuzi na usajili wa vitambulisho vya kidijitali unatarajiwa kufanyika Otoba 17, 2024 jijini Arusha.
Share:

Friday, 11 October 2024

ALIIBA NG'OMBE WANGU ILI AKALIPE MAHARI

Jina langu ni Simon kutoka kaunti ya Vihiga, nilikuwa mfanyabishara haswa wa kilimo, nilikuwa na ng’ombe wawili wa maziwa ambao walikuwa wananipa faida kubwa sana kutokana na uuzaji wa maziwa.

Nilifanya pia ukulima wa nyanya lakini uuzaji maziwa ulikuwa na faida sana kulinganisha na kilimo cha nyanya, kazi hii iliniwezesha kulipia wanangu karo ya shuleni, kuwezesha wanangu kupata lishe bora na hata kufanya maendelea mengi pale nyumbani.

Ng’ombe wangu walikuwa wenye afya kutokana na mimi kujua ni kipi haswa walihitaji ili kuleta faida, ila siku moja niliamka na kukuta zizi la ng’ombe langu lilikuwa wazi.

Kufumba na kufungua macho hapakuwa na mifugo wangu niliowategemea, nilikumbwa na mshutuko wa moyo na hata nilidhani kwamba walikuwa tu karibu, kumbe walikuwa tayari wameshaibiwa.

Niliripoti kituo cha Polisi mjini Luanda, niliamini kwamba Polisi wangenisaidia kupata haki lakini kila mara walisema kwamba walikuwa wakifanya uchunguzi kubaini ni wapi walikuwa mifugo wangu.

Ama kwa hakika sikuridhishwa na majibu yale ya polisi kwani nilikuwa nikitaka mifugo wangu, mara Eunice akanielekeza kwa Dr Bokko, aliniambia ni mtaalamu wa mitishamba ambaye anaweza kunisaidia kupata suhisho.

Nilifika kwa Dr Bokko na akanishugulika na kunipa ukakika kwamba baada ya siku mbile wezi wa mifugo yangu yatapatika wala nisiwe na wasiwasi.

Siku tatu baada ya kurejea nyumbani, niliitwa kwenye familia moja kwa uharaka, nilipofika nilipata umati mkubwa wa watu nje ya nyumba ya mtumishi mmoja.

La kushangaza ni kwamba alikuwa ni Pasta wa dhehebu letu, yeye ndiye alikuwa ameiba mifugo yangu, alisema kwamba alifanya vile kwa kuwa alitaka kuwatumia kulipa mahari yake.

Niliwarejesha mifugo wangu nyumbani, tangu siku ile hakuna yeyote anayethubutu kushika mali yangu.

Pia Dr Bokko hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa, husuluhisha shida za kifamilia kama kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba na mwenza wako wa maisha nk. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Dr Bokko kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

WADAU WA SEKTA YA MADINI WATEMBELEA BANDA LA TBS MAONESHO YA SABA YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA


Na Mwandishi Wetu, Geita

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekutana na wadau wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla na kuwapata elimu kuhusu masuala ya madini.

Shirika hilo limekutana na wadau pamoja na wananchi hao kuwapatia elimu hiyo kwenye Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita kuanzia Oktoba 02 ambapo yatafungwa Oktoba 13.

Maonesho hayo yalifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo jana, Afisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, alisema shirika hilo linaandaa viwango vya sekta ya madini, hivyo alisema kupitia maonesho hayo wanakutana na wadau wa sekta hiyo na kuwapa elimu.

Aidha, Mtemvu alisema mbali na kukutana na wadau wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla, kupitia maonesho hao wanakutana na wajasiriamali na kusikiliza na kutatua changamoto zao na kuwaelimisha na kuwahamasisha kuhusishana na umuhimu wa kuzalisha bidhaa zilizothibitishwa ubora na shirika hilo.

Mtemvu alisema shirika hilo litaendelea kutimiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wajasiriamali wanashiriki katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.

Alisema Serikali inatumia sh. milioni 250 kwa mwaka kugharamia gharama zote za wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha, hivyo wanapofika TBS wanapata huduma hiyo bure.

"Ndiyo maana tumetumia fursa hii na Maonesho ya Madini kuelimisha taratibu za kufuata ili kuwezakuthibitisha bidhaa zao bure," alisema Mtemvu.

Akifungua maonesho hayo ,Dkt. Biteko alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha, kuvutia na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya madini ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.
Share:

Thursday, 10 October 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 11, 2024

Share:

NJIA TULIYOTUMIA KUSHINDA KESI BAADA YA KUDHULUMIWA SHAMBA LETU

Jina langu ni Juma, siku moja mtu mmoja tajari alivamia shamba letu na kukatakata kila kitu kilichokuwa humo kama mazao na hata kubomoa nyumba yetu na kudai kuwa shamba hilo lilikuwa lake na hakutaka kuona mtu yeyote shambani humo.

Alimuonya mama yangu hasiaribu kumshtaki kortini kwani atakuwa anapoteza muda wake kama yeye ana fadha nyingi na kuweza kuwapa Majaji wa Mahakama rushwa hivyo ni lazima kuwa atashinda.

Hivyo kwa uwoga mama yangu alinyamaza kama maji mtungini, aliweza kunipigia simu na kuniarifu yote hayo na kuniomba niende nyumbani kumsaidia jambo hilo.

Niliweza kurudi nyumbani kwetu kutoka Nairobi na kuenda kwa tajiri yule na kumuuliza mbona alifanya kitu kama hicho, cha kushangaza mwanaume huyo aliwaita Polisi na kuwaarifu kuwa nimemtishia kumtoa uhai.

Nilifikishwa kwenye kituo cha Polisi na kutozwa faini, siku iliyofuatia maafisa wa Polisi walikuja tulikokuwa tumehamia na kutupa onyo kali kama tutaendelea kumsumbua tajiri yule aliyepokonya shamba letu.

Baada ya wiki moja hivi mke wangu aliniomba nifike kortini kutafuta haki, aliniambia kuwa atanionyesha njia rahisi ya kuweza kuishinda kesi hiyo, basi nilifanya hima na kufika mahakamani na kumshtaki tajiri yule. 

Niliporejea nyumbani mke wangu alinipeleka kwa Dr Bokko, niliweza kuwaeleza kila kitu, walifanya ganga ganga zao na kunipa ahadi za kuishinda kesi ile.

Siku iliyofuatia tuliweza kufika kortini na Jaji aliagiza tajiri yule kuturejeshea shamba alilotupokonya, pia alitozwa faini ya Ksh100,000, Mama yangu alirejeshewa shamba lake na kwa sasa anaishi maisha yake mazuri.

Pia Dr Bokko wanatibu magonjwa kama saratani ya mapafu, kifua kikuu na mengine mengi, pia wanatatua mizozo ya ndoa, mashamba na mapenzi. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

Wednesday, 9 October 2024

NJIA TULIYOTUMIA KUSHINDA KESI BAADA YA KUDHULUMIWA SHAMBA LETU

Jina langu ni Juma, siku moja mtu mmoja tajari alivamia shamba letu na kukatakata kila kitu kilichokuwa humo kama mazao na hata kubomoa nyumba yetu na kudai kuwa shamba hilo lilikuwa lake na hakutaka kuona mtu yeyote shambani humo.

Alimuonya mama yangu hasiaribu kumshtaki kortini kwani atakuwa anapoteza muda wake kama yeye ana fadha nyingi na kuweza kuwapa Majaji wa Mahakama rushwa hivyo ni lazima kuwa atashinda.

Hivyo kwa uwoga mama yangu alinyamaza kama maji mtungini, aliweza kunipigia simu na kuniarifu yote hayo na kuniomba niende nyumbani kumsaidia jambo hilo.

Niliweza kurudi nyumbani kwetu kutoka Nairobi na kuenda kwa tajiri yule na kumuuliza mbona alifanya kitu kama hicho, cha kushangaza mwanaume huyo aliwaita Polisi na kuwaarifu kuwa nimemtishia kumtoa uhai.

Nilifikishwa kwenye kituo cha Polisi na kutozwa faini, siku iliyofuatia maafisa wa Polisi walikuja tulikokuwa tumehamia na kutupa onyo kali kama tutaendelea kumsumbua tajiri yule aliyepokonya shamba letu.

Baada ya wiki moja hivi mke wangu aliniomba nifike kortini kutafuta haki, aliniambia kuwa atanionyesha njia rahisi ya kuweza kuishinda kesi hiyo, basi nilifanya hima na kufika mahakamani na kumshtaki tajiri yule. 

Niliporejea nyumbani mke wangu alinipeleka kwa Dr Bokko, niliweza kuwaeleza kila kitu, walifanya ganga ganga zao na kunipa ahadi za kuishinda kesi ile.

Siku iliyofuatia tuliweza kufika kortini na Jaji aliagiza tajiri yule kuturejeshea shamba alilotupokonya, pia alitozwa faini ya Ksh100,000, Mama yangu alirejeshewa shamba lake na kwa sasa anaishi maisha yake mazuri.

Pia Dr Bokko wanatibu magonjwa kama saratani ya mapafu, kifua kikuu na mengine mengi, pia wanatatua mizozo ya ndoa, mashamba na mapenzi. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

LSF NA NORTH – SOUTH COOPERATION ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO LONGIDO.



Longido, Arusha 08 Oktoba 2024.

LSF, kwa kushirikiana na wadau wake NORTH-SOUTH COOPERATION kutoka Luxembourg, imekamilisha mradi wa miaka miwili unaojulikana kama ‘Wanawake Tunaweza,’ ambao umeleta mafanikio makubwa katika kuwawezesha wanawake na watoto wa kike kutoka jamii ya Kimasai wilayani Longido.

Mradi huu, ulioanza kutekelezwa mwaka 2022, umelenga kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi kwa kuwajengea uwezo kupitia vikundi vya wanawake 11 na kuwaanzishia miradi mbalimbali ya ujasiriamali kama vile ufugaji wa mifugo, uuzaji wa nafaka, utengenezaji wa urembo wa Kimasai, kilimo cha bustani, pamoja na shughuli za VICOBA.

Kupitia mradi huu, akinamama wameweza kuanzisha kikundi cha pamoja kijulikanacho kama ‘Osiligi’ na wamepatiwa vyerehani 11 kwa ajili ya kushona taulo za kike zinazotumika tena (Reusable Sanitary Pads). Taulo hizi zimesaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa kike katika shule za Lekule na Namanga, ambao ni miongoni mwa wanufaika wakuu.

Mbali na hayo, mradi umeweza kuwasaidia watoto wa kike kupata mazingira bora ya kusomea kwa kujenga mabweni mapya, huku zaidi ya wasichana 1,214 wakiwa wamefaidika kupitia shughuli mbalimbali za elimu, usawa wa kijinsia, na haki zao za msingi.

Aidha, zaidi ya wanawake 209 wamenufaika moja kwa moja katika eneo la ujasiriamali, huku jumla ya watu 2,500 wakiwemo wanaume na wanawake wa Longido wakielimishwa juu ya masuala ya kijinsia na haki ya mwanamke kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huu.

Mradi pia umeweza kuwajengea uwezo viongozi wa kimila takribani 20, huku wakishirikiana na wanaume shupavu (Male Champions) 7 waliopatiwa mafunzo maalum kupitia shirika la WASHEWILO, ambalo pia linapata ufadhili kutoka LSF, ili kuleta mabadiliko chanya katika mtazamo wa jamii kuhusu haki za wanawake.

Mafanikio mengine makubwa ni kuboresha chumba cha Tehama (ICT room) katika shule ya Namanga, kwa kuweka kompyuta, viti, na vifaa vya kisasa vinavyowezesha wanafunzi 40 kupata elimu ya Tehama kwa wakati mmoja.

Pamoja na maboresho haya, kampeni ya upandaji miti katika mashule na jamii imewezesha miche 1,420 kupandwa na kuhudumiwa licha ya changamoto ya ukame kwenye eneo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huu, Meneja Mawasiliano wa LSF alitoa wito kwa serikali ya wilaya na wadau wengine kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanadumishwa na kuendelezwa.

Alisisitiza kuwa, licha ya hatua kubwa iliyofikiwa, bado kuna maeneo ya kuboresha hasa katika kupanua masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa vikundi hivyo na kuhakikisha kuwa mipango ya kuwasaidia kinamama hao inafuatiliwa na kutekelezwa kikamilifu.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Lekule iliyopo Longido Mkoani Arusha, akiwafundisha wanafunzi wa Shule hiyo somo la Kompyuta katika Chumba kilichokarabitiwa kwa Ufadhili wa LSF kwa Kushirikiana na North - South Cooperation ya nchini Luxembourg.
Share:

Tuesday, 8 October 2024

RC MWASSA : WAGOMBEA FANYENI KAMPENI ZA KISTAARABU NA ZENYE STAHA



Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa mkoa wa Kagera hajat Fatma Mwassa amewataka wagombea wote na vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na zenye staha katika uchaguzi wa serikali za mtaa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 8,2024 amesema kuwa novemba mosi hadi saba wagombea watachukua fomu na kurudisha huku Novemba 20 hadi 26 itakuwa zoezi la kampeni kwa wagombea.

Aidha amesema kuwa mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na watu wenye umri wa miaka18 na kuendelea wapatao 1,566,530 ambapo amewataka watu wote hao kujitokeza katika zoezi la kupiga kura ili kutumia haki yao ya kimsingi na kikatiba ya kupiga kura na kusema kuwa mkoa wa kagera una vituo vya uandikishaji wa wapiga kura vipatavyo 3,833.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewakaribisha wananchi wote, makampuni ya uzalishaji wa vyakula, wakulima, wafugaji na wavuvi kushiriki kwa pamoja katika maadhimisho ya chakula duniani.


Amesema kuwa maadhimisho ya siku ya chakula duniani mwaka huu yanaadhimishwa kitaifa katika Mkoa wa Kagera.


Aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya ccm manispaa ya Bukoba kuanzia tarehe 10 -16 octoba 2024 na kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 13, na kufungwa na waziri wa kilimo Mh. Hussein Bashe tarehe 16 Oktoba mwaka huu.


Maadhimisho hayo yatakuwa na shughuli mbalimbali ambazo ni mashindano ya mitumbwi ya uvuvi wa samaki, mashindano ya upishi wa asili, ushirikishwaji wa watoto katika unywaji wa maziwa, maonesho ya chakula, burudani,elimu ya uhifadhi wa chakula salama,na udhibiti wa sumu kuvu, Huku yakiambatana na kauli mbiu ya mwaka huu "haki ya chakula kwa wote kwa maisha bora ya sasa na yajao".







Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger