Sunday, 6 October 2024

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. MWINYI AONGOZA HAFLA MAALUM YA SHUKRANI YA "UZAZI NI MAISHA" KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

 04 Oktoba 2024, Zanzibar: Katika jitihada za kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameongoza hafla maalum ya Shukrani ya "Uzazi Ni Maisha"Oktoba, 04  2024 Ikulu Mjini Zanzibar. 

Tukio hilo, ambalo limefanyika likiwakilisha awamu ya tatu ya program ya Uzazi Ni Maisha chini ya kauli mbiu “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama”, liliandaliwa na Shirika la Amref Health Africa -Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Absa Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mashuhuri zaidi ya 300 kutoka sekta tofauti wakiwemo viongozi wa makampuni mbalimbali, mashirika, wanadiplomasia, taasisi za serikali, washirika wa maendeleo, jumuiya za wanadiaspora na wawakilishi wa vyombo vya habari. Hafla hiyo mbali na kusherehekea mafanikio na mchango wa wadau wote tangu kuzinduliwa kwa program ya Uzazi ni Maisha mwaka 2021, pia ililenga kukusanya fedha za ziada kusaidia azma ya serikali ya kumarisha uzazi salama.

Akizungumza katika hafla hiyo Rais Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi aliipongeza Amref Health Africa -Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Absa Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar katika kuendesha program hiyo, huku akitoa shukrani za dhati kwa wafadhili na wadau wote kwa kujitolea kwao. 

Alisisitiza umuhimu wa mchango huo katika kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga, na kutoa wito wa kuendelea kuungwa mkono na makampuni mbalimbali na mashirika ili kufanikisha azma hiyo.
“Leo tunasherehekea hatua muhimu katika juhudi zetu za kupunguza vifo vya mama na mtoto,” Rais Mwinyi alisema. 

“Tunafanya kazi kuelekea malengo makubwa: kupunguza vifo vya mama hadi chini ya 70 kwa kila vifo 100,000 vya uzazi hai, vifo vya watoto wachanga hadi 12 kwa kila vifo 1,000 vya uzazi hai, na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hadi 25 kwa kila vifo 1,000 vya uzazi hai ifikapo mwaka 2030. Licha ya maendeleo, bado tunakutana na changamoto, hasa katika kupata rasilimali zakutosha kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba. Nahimiza wadau na washirika zaidi kujiunga nasi ili kufikia malengo haya.”
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa-Tanzania Dkt. Florence Temu, alitoa shukrani kwa washirika wote ambao wamechangia kufanikisha program ya Uzazi ni Maisha. Alisisitiza dhamira ya Amref kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar katika kuboresha uzazi salama na afya ya mama na mtoto, sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto katika vituo vya afya vya Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Amref Health Africa – Tanzania, Anthony Chamungwana, alisema  Amref Tanzania itaendelea kuwa mshirika thabiti katika ajenda ya huduma za afya kwa wote (Universal Health Coverage). “Kama ilivyobainishwa katika mpango mkakati wa Amref Tanzania wa  mwaka 2023 hadi 2030. Mkakati elekezi unazingatia huduma za afya kwa wote, mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika sekta ya afya, usalama wa afya na matumizi ya taarifa na teknolojia katika utekelezaji wa afua zetu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi S.Laiser, alisisitiza juu ya  dhamira ya benki hiyo katika kuboresha huduma za jamii. "Benki ya Absa Tanzania inajivunia kuunga mkono program ya Uzazi Ni Maisha kwa kuwa tunaamini itasaidia kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto hapa Zanzibar. Mchango wetu wa TZS 70,000,000 unaakisi kujitolea kwetu katika kuimarisha mustakabali wa Tanzania na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini."

Hadi sasa program hii ya Uzazi Ni Maisha imeweza kukusanya ahadi za jumla ya kiasi cha TZS 989,831,145 kati ya ahadi hizi imekwishapokea kiasi cha shilingi TZS 740,457,422 ambazo zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya 28. kuhakikisha usalama na ustawi wa akina mama na watoto wachanga. Program hii imejiwekea lengo la kukusanya angalau shilingi bilioni moja, michango na ahadi mbalimbali za kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba.

Program hii itaendelea kuwa wazi kwa mwaka mmoja (mpaka 2025) ikishirikisha wadau na watu mbalimbali hadi lengo litakapofikiwa. Michango inaweza kutolewa kupitia namba ya Vodacom Lipa 5529421, Tigo 6633523 au kupitia tovuti ya wogging.amref.org.

Shukrani maalumu kutoka kwa mdhamini mkuu, Benki ya Absa Tanzania; M & D Chemical & Surgical Ltd, Tanzania Ports Authority, NBC Bank, NMB Bank, ITV/ Radio One, EATV/Radio, Swahili Sweatshop, Dalberg Tanzania, Siemens Healthcare LLC, na kila mmoja aliyewezesha Programu ya Uzazi ni Maisha) kuanzia (2022-2024) kufanikiwa.   

Share:

KITUO CHA AFYA SEGESE KIANZE KAZI IFIKAPO MWEZI OKTOBA - WAZIRI NDEJEMBI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Deogratius Ndejembi akitembelea  kituo cha afya Segese Halmashauri ya Msalala 

NA NEEMA ISRAEL - MSALALA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Deogratius Ndejembi amemtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhakikisha kituo cha afya Segese kinaanza kufanya kazi mara moja kwani jengo la OPD tayari limekamilika na vitendea kazi vya kuanzia vipo.

Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo leo Oktoba 6, 2024 alipotembelea kituo cha Segese na kubaini baadhi ya mapungufu ambapo amesema watumishi wanatumia mianya kutokukamilika kwa majengo kupiga fedha za mapato ya ndani.

Aidha Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha amewataka Wahandisi wakabidhi majengo yanayolingana na thamani ya fedha zinazotolewa.

Akisoma taarifa za ujenzi wa kituo hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha amesema Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2022 kupitia mapato ya ndani shilingi 470,000,000/= baada ya wananchi wa Kata Segese kukosa huduma za afya ambapo walianza na ujenzi wa majengo manne, jengo la wagonjwa wa nje OPD, Maabara, Upasuaji na jengo la mama na mtoto.

Ujenzi wa jengo la OPD limegharimu kiasi cha 208,839, 549.9 ambapo umekamilika kwa asilimia 96 na asilimia zilizobaki ni kuingiza umeme, maji na thamani.

Kituo hicho kikikamilika kinatarajiwa kuhudumia wakazi 36,247 wa Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala.

Jengo la mama na mtoto lililokamilika kwa asilimia 70 na kugharimu shilingi 77,501,992.32
Majengo ya maabara na OPD ambayo yamekamilika kwa asilimia 96 ambapo jengo la maabara limegharimu 96,957,632.58 na jengo la wagonjwa wa nje OPD limegharimu 208,839,549.9
Waziri Ndejembi akizungumzia suala la kituo cha afya kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi waanze kupata huduma za afya ifikapo mwezi wa 11

Mkuu wa mkoa Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha afya Segese ambapo amewataka wahandisi kukabidhi majengo kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa

HODI SIMIYU, NCHIMBI AKIANZA ZIARA YA SIKU 3

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba 2024, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameanza ziara mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kukagua uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina na pia kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

Share:

Saturday, 5 October 2024

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. MWINYI AONGOZA HAFLA MAALUM YA SHUKRANI YA "UZAZI NI MAISHA" KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

04 Oktoba 2024, Zanzibar: Katika jitihada za kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameongoza hafla maalum ya Shukrani ya "Uzazi Ni Maisha"Oktoba, 04  2024 Ikulu Mjini Zanzibar. 

Tukio hilo, ambalo limefanyika likiwakilisha awamu ya tatu ya program ya Uzazi Ni Maisha chini ya kauli mbiu “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama”, liliandaliwa na Shirika la Amref Health Africa -Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Absa Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mashuhuri zaidi ya 300 kutoka sekta tofauti wakiwemo viongozi wa makampuni mbalimbali, mashirika, wanadiplomasia, taasisi za serikali, washirika wa maendeleo, jumuiya za wanadiaspora na wawakilishi wa vyombo vya habari. Hafla hiyo mbali na kusherehekea mafanikio na mchango wa wadau wote tangu kuzinduliwa kwa program ya Uzazi ni Maisha mwaka 2021, pia ililenga kukusanya fedha za ziada kusaidia azma ya serikali ya kumarisha uzazi salama.

Akizungumza katika hafla hiyo Rais Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi aliipongeza Amref Health Africa -Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Absa Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar katika kuendesha program hiyo, huku akitoa shukrani za dhati kwa wafadhili na wadau wote kwa kujitolea kwao. 

Alisisitiza umuhimu wa mchango huo katika kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga, na kutoa wito wa kuendelea kuungwa mkono na makampuni mbalimbali na mashirika ili kufanikisha azma hiyo.
“Leo tunasherehekea hatua muhimu katika juhudi zetu za kupunguza vifo vya mama na mtoto,” Rais Mwinyi alisema. 

“Tunafanya kazi kuelekea malengo makubwa: kupunguza vifo vya mama hadi chini ya 70 kwa kila vifo 100,000 vya uzazi hai, vifo vya watoto wachanga hadi 12 kwa kila vifo 1,000 vya uzazi hai, na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hadi 25 kwa kila vifo 1,000 vya uzazi hai ifikapo mwaka 2030. Licha ya maendeleo, bado tunakutana na changamoto, hasa katika kupata rasilimali zakutosha kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba. Nahimiza wadau na washirika zaidi kujiunga nasi ili kufikia malengo haya.”

Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa-Tanzania Dkt. Florence Temu, alitoa shukrani kwa washirika wote ambao wamechangia kufanikisha program ya Uzazi ni Maisha. Alisisitiza dhamira ya Amref kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar katika kuboresha uzazi salama na afya ya mama na mtoto, sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto katika vituo vya afya vya Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Amref Health Africa – Tanzania, Anthony Chamungwana, alisema  Amref Tanzania itaendelea kuwa mshirika thabiti katika ajenda ya huduma za afya kwa wote (Universal Health Coverage). “Kama ilivyobainishwa katika mpango mkakati wa Amref Tanzania wa  mwaka 2023 hadi 2030. Mkakati elekezi unazingatia huduma za afya kwa wote, mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika sekta ya afya, usalama wa afya na matumizi ya taarifa na teknolojia katika utekelezaji wa afua zetu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi S.Laiser, alisisitiza juu ya  dhamira ya benki hiyo katika kuboresha huduma za jamii. "Benki ya Absa Tanzania inajivunia kuunga mkono program ya Uzazi Ni Maisha kwa kuwa tunaamini itasaidia kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto hapa Zanzibar. Mchango wetu wa TZS 70,000,000 unaakisi kujitolea kwetu katika kuimarisha mustakabali wa Tanzania na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini."

Hadi sasa program hii ya Uzazi Ni Maisha imeweza kukusanya ahadi za jumla ya kiasi cha TZS 989,831,145 kati ya ahadi hizi imekwishapokea kiasi cha shilingi TZS 740,457,422 ambazo zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya 28. kuhakikisha usalama na ustawi wa akina mama na watoto wachanga. Program hii imejiwekea lengo la kukusanya angalau shilingi bilioni moja, michango na ahadi mbalimbali za kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba.

Program hii itaendelea kuwa wazi kwa mwaka mmoja (mpaka 2025) ikishirikisha wadau na watu mbalimbali hadi lengo litakapofikiwa. Michango inaweza kutolewa kupitia namba ya Vodacom Lipa 5529421, Tigo 6633523 au kupitia tovuti ya wogging.amref.org.

Shukrani maalumu kutoka kwa mdhamini mkuu, Benki ya Absa Tanzania; M & D Chemical & Surgical Ltd, Tanzania Ports Authority, NBC Bank, NMB Bank, ITV/ Radio One, EATV/Radio, Swahili Sweatshop, Dalberg Tanzania, Siemens Healthcare LLC, na kila mmoja aliyewezesha Programu ya Uzazi ni Maisha) kuanzia (2022-2024) kufanikiwa.   

Share:

DAWA ILIYONISAIDIA KUBEBA UJAUZITO BAADA YA KUSUMBUKA SANA

Naweza kusema hakuna furaha anayokuwa nayo mwanamke kama kuitwa Mama, daima siwezi kuisahau siku ambayo nilimshika kwa mikono yangu mtoto wangu wa kwanza kwa mara ya kwanza.

Chozi la furaha lilinitoka bila mwenyewe kujua, nilijikuta nalia tu kwa furaha niliyokuwa nayo, moyo wangu ulihemewa kwa furaha ambayo ni vigumu kuelezeka na kueleweka.

Nasema hivyo kwa sababu kuu mbili; kwanza kujifungua salama mtoto wangu wa kwanza akiwa na afya tele, pili ni kwamba niliangaika sana kutafuta mtoto hadi ukafikia wakati wa kuanza kukataa.

Jina langu kwa sasa naitwa Mama Anna, ni mkazi wa Katavi, katika ndoa yangu nilikaa miaka zaidi ya mwili bila kujaliwa mtoto ingawa nilikuwa na kiu sana kumzalia mume wangu. 

Mume wangu alikuwa ananipa moyo na kunishauri niwe na subra kwani kila jambo lina wakati wake, nilimkubalia ila moyoni nafsi yangu ilikuwa haijatulia kabisa. Kiu yangu ni kujaliwa mtoto tu.

Wakati mmoja nikiwa nasoma gazeti fulani, niliweza kuona tangazo la Dr Bokko kuwa wanatoa tiba kwa wanawake wanaosumbuka kupata mtoto, nilishawishika kuwasiliana nao licha ya kuwa tayari nilikuwa nimeshazunguka kwa wataalamu wengi.

Baada ya kuongea nao waliambia dawa zao zimewasaidia wanawake wengi kupata watoto, hivyo nisiwe na wasiwasi hata kidogo, basi walinitumia dawa zao na kunipati maelezo jinsi ambavyo naweza kuzitumia na kupata matokeo yaliyokusudiwa.

Nashukuru dawa zili ziliweza kunisaidia na sasa naitwa Mama Anna na Anna mwenyewe tayari ana mtoto wake, watoto wangu ndio furaha ya maisha yangu, kwa hakika kila siku siwezi kuacha kuwakumbuka Dr Bokko kwa msaada walionifanyia.

Ninatoa wito kwa wenye shida au magonjwa, kusumbuliwa na mapenzi, ndoa, biashara, kukosa ujauzito n.k, basi wasisite kuwatembelea Dr Bokko, sio lazima usafiri hadi ofisini kwao, unaweza kuongea nao kwa njia ya simu na utasaidiwa kwa haraka. Piga simu +255618536050.
Mwisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger