Tuesday 27 August 2024

DKT MPANGO ATAKA ZOEZI LA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA ENDELEVU




Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amelitaka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kufanya ukaguzi makini na endelevu wa vyombo vya moto mara mbili kwa mwaka pamoja na kudhibiti magari yanayobeba wanafunzi Mashuleni kwani baadhi ya magari hayo yamekuwa na hali mbaya inayotishia usalama wa Wanafunzi pamoja na madereva wao
Dkt. Mpango ameyasema hayo katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma leo Agosti 26, 2024 wakati akifungua Maadhimisho Wiki ya Nenda kwa Usalama Barababani ambayo Kitaifa yamezinduliwa Dodoma huku akisisitiza kuwa yapo magari yanayobeba wanafunzi kuliko uwezo wake na baadhi ya madereva kuonekana kukosa uweledi na uadilifu jambo linalosababisha madhara mbalimbali ikiwemo ajali.

" Nina mfano halisi ile ajali ya hovyo kabisa iliyotokea Mkoani Arusha na kusababisha Watanzania kuondokewa na watoto wetu Saba.

“Ninawataka Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama Barabarani mkasimamie na muhakikishe kwamba dereva anayepata Leseni ni yule aliyepitia mafunzo stahiki na umahiri wa uendeshaji wa vyombo vya moto, na hii inajumuisha Madereva wote wa magari ya abiria, mizigo, bodaboda na Bajaji.” Amesema

Aidha, Mheshimiwa Dkt. Mpango amepongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi huku akisisitiza kutoa nafasi kwa madereva Wanawake kwani mara kadhaa wanaonekana kuwa makini zaidi ikilinganishwa na baadhi ya wanaume.
Awali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Wizara hiyo itaendelea kusimamia Jeshi la Polisi pamoja na kutoa ushirikiano kwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwa ni pamoja na kufunga kamera barabarani ili kusaidia kupunguza ajali barabarani, kupata upelelezi wa uhakika na wa haraka ikiwemo kubaini mapungufu pale ambapo kuna kosa limefanyika.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhe. Daniel Sillo amesema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kipindi cha miaka 50 ya Usalama Barabarani hali ya Usalama Barabarani imeimarika na kuwa yenye tija ambapo Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limeweza kujenga majengo ya Ofisi Sita za Makatibu wa Mikoa ikiwa ni pamoja na kununua magari ya doria 31 kwa kushirikiana na wadau wa Usalama wa Barabarani

Amesema Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto kwa kutumia Mitambo ya kisasa

"Katika kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Arusha mwaka 2021 kuhusiana na ushirikishwaji wa wadau katika ukaguzi wa vyombo vya moto kwa Teknolojia ya kisasa Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani tuliingia ubia na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kutumia mitambo ya kisasa ya ukaguzi wa vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria ya PPP. Alisema Sillo

Aidha Mhe. Sillo alihitimisha kwa kusema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuepusha ajali barabarani, bado kuna tatizo la baadhi ya madereva wa magari na pikipiki kutokufuata sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali, alitoa Pole kwa watu wote waliopoteza wapendwa wao pamoja na waliopata vilema vya maisha kutokana na ajali za barabarani.


Share:

TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU YA VIWANGO KWENYE MAONESHO YA KITAIFA YA USALAMA BARABARANI DODOMA


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya ubora katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama wa Barabarani yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Dodoma ambapo wameeleza ni jinsi gani wanahakikisha matumizi sahihi ya vipuli vya magari pamoja na uingizaji wa magari used yakiwa salama nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 26, 2024 katika Maonesho hayo, Meneja wa Viwango, Mhandisi Yona Afrika amesema TBS ndio wakaguzi wa magari yaliyotumika nchini kuwa ni salama, pia wanakagua vipuri vya magari kama breki na ukaguzi wa mafuta salama ya magari.

Amesema wamekuwa wakiandaa viwango vya mafuta salama ya magari nchini ili kuhakikisha magari yanayotumika nchini yanatumia mafuta salama ya magari na kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye magari pindi wanapotumia mafuta ambayo si salama.

"TBS tunahakikisha magari yote yanayoingia nchini, yanaingia yakiwa salama na yanachangia kwa kiasi kikubwa usalama barabarani ambapo pia vipuri vya kwenye magari tunahakikisha vinakuwa na ubora unaotakiwa kabla havijatumika kwenye magari". Amesema Mhandisi Afrika.

Share:

HALMASHAURI YA KIGOMA YAPATIWA MAFUNZO JINSI YA KUKABILIANA NA MAAFA



Na Mwandishi Wetu,KIGOMA

Serikali inasimamia na kuratibu shughuli za kuzuia na kukabiliana na majanga kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na 6 ya Mwaka 2022 na kanuni zake za mwaka 2022 kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa inayotekeleza majukumu yake chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo suala la kuzuia na kukabiliana na majanga ni mtambuka na linahitaji nguvu za pamoja katika kulishughulikia.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyofanyika tarehe 26 agosti, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa sehemu ya Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Salum Manyatta amesema, kuongezeka kwa matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii, Maafa haya yamekuwa yakisababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upotevu na uharibifu wa mali, miundombinu na mazingira.

Hivyo Dkt. Manyatta amewataka viongozi wa serikali za vijiji kuhakikisha inafahamu namna ya muundo wa maafa unavyofanya kazi ili kurahisisha uapatikanaji wa taarifa kwa ajili ya kupata namna ya kujiandaa kukabiliana kabla maafa hayajatokea.
“Tunasema serikali Kijiji ni serikali inayotambulika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kwenye ngazi ya Kata tunajulikana kama kamati ya maendeleo ya kata kwa hiyo sisi tunakaa nao kama kuna maeneo yanahusisha Kata ujenzi wa kituo cha Afya, ujenzi wa Zahanati, ujenzi wa Kituo cha Polisi tunafanya kwa kile ambacho tunakiona kinatukwamisha kwenye kazi hivyo tumekuja hapa kwa masaa machache kuna mada mtajifunza kwa ajili ya uelewa wa pamoja maana utekelezaji wa masuala ya maafa yapo kwenye maeneo yetu, maafa hutokea kwa watu na watu wapo kwetu hivyo tukipata uelewa huu tutaweza kukabili jambo hili” alisema Dkt. Manyatta

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Bruno Francis amezitaka Kamati za Maafa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kutumia mafunzo yanayotolewa ya jinsi ya kukabiliana na Maafa ili kupunguza athari na uharibifu wa mazingira katika maeneo yao.

“Sasa leo tumepata fursa ambayo ndio haya mafunzo hivyo kila mtu awe makini tusikilize ili lolote litakalotokea na hatuombei maafa yatokee kwa sababu hakuna mtu anayaleta maafa, yanajitokeza tu bila kutarajia kwa hiyo tutakapojifunza hapa na tukienda kupeana maagizo kuwa kila mmoja atekeleze wajibu wake katika ngazi zote” alisema Bw. Bruno.

Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) imefanya semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii ambapo semina hii itaendeshwa kwa siku mbili kuanzia Agosti 26 hadi Agosti 27, 2024 katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma.






Share:

Monday 26 August 2024

RAIS SAMIA APONGEZA USHIRIKI WA TAWA KIZIMKAZI


Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi cheti cha pongezi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kutokana na ushiriki wake wa kipekee katika Tamasha la Tisa la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar kuazia tarehe 18-25 Agosti, 2024.

Cheti hicho cha pongezi kilipokelewa na Afisa Utalii Mustapha Buyogera katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo, Kizimkazi, Zanzibar.

Katika tamasha hilo, Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wengi na wadau mbalimbali wa utalii ambapo wageni walipata fursa ya kushuhudia wanyamapori hai waliopo katika bustani ya wanyamapori hai.
Share:

Sunday 25 August 2024

TEA NA EATV WAFANYA MATEMBEZI KUHAMASISHA KAMPENI YA NAMTHAMINI


MAMLAKA ya Elimu Tanzania(TEA) kwa kushirikiana na Kituo cha utangazaji EATV leo tarehe 25 Agosti 2024 wameongoza matembezi ya hisani kwa ajili kuhamasisha umma kushiriki katika kampeni ya Namthamini inayolenga kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wa kike mashuleni.

Matembezi hayo yameanzia Makao Makuu ya EATV Dar es Salaam na kupita maeneo ya Bamaga, Sayansi, Makumbusho na Morocco kisha kurejea tena Makao Makuu ya EATV.

Akizungumza katika kampeni hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, Bi. Mwanahamisi Chambega amesema TEA inashiriki kampeni hiyo muhimu kwa vile lengo la kampeni linaendana na majukumu ya Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao TEA inausimamia.

“ Jukumu la Mfuko wa Elimu wa Taifa ni kukusanya raslimali kutoka sehemu mbali mbali kisha kuzitumia raslimali hizo kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, ndio maana TEA leo tunashiriki katika kampeni hii inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia ya wanafunzi wa kike “ amesema Bi. Chambega.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Huduma za Taasisi wa TEA ametumia fursa hiyo kuhamasisha wadau kuchangia kampeni ya Namthamini akiongeza kuwa watapata faida mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupata Hati ya Utambuzi wa Uchangiaji wa Elimu (Certificate of Educational Appreciation- CEA) kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001.

Mdau anaweza kutumia hati ya CEA kuombea nafuu ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato Sura 332 marejeo ya mwaka 2019.

Faida nyingine ni mdau kutangazwa na kutambuliwa kitaifa, ambapo mchangiaji huandikwa katika rejesta ya kudumu ya wachangiaji wa elimu

Awali Balozi wa Kampeni ya Bi. Namthamini Najma Paul alisema kampeni hiyo ambayo imeendeshwa kwa miaka saba na kituo cha utangazaji cha EATV imeweza kufikia Mikoa 20 nchini ambapo wanafunzi elfu 20 wamepatiwa huduma ya Taulo za Kike kwa kipindi cha mwaka mzima.

Katika matembezi hayo wadau muhimu wa TEA wameshiriki ambapo mwakilishi wa Total Energy Bi. Faith Mfugale ameahidi kuwa shirika lake litachangia taulo za kike katika baadhi ya shule wakati mwakilishi wa Shirika la Sayari Safi Bi. Veronica Ussiri ameahidi kuwa shirika lake litaweka miundombinu ya kusafishia maji katika baadhi ya shule zitakazonufaika na kampeni ya Namthamini.
Share:

TANESCO,REA ZASHAURIWA KUNUNUA TRANSFOMA TANALEC, GENERAL TYRE KUFUFULIWA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiangalia Transfoma zinazotengenezwa na Kiwanda cha TANALEC Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024.

 

......

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) ametoa rai kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuongeza kasi ya ununuzi wa transfoma zinazozalishwa na Kiwanda cha Tanelec kwa kuwa Taasisi hizo ni wamiliki wa sehemu ya hisa za kiwanda hicho ili kukiwezesha kiendelee kukua na kuongeza ajira nchini.

Dkt Jafo ameyasema hayo Agosti 24, 2024, Mkoani Arusha, alipotembelea viwanda, kuongea na Wafanyabiara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughjuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto na kuona njia bora ya kuzitatua kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Aidha, Dkt Jafo amelielekeza Shirika la Taifa la Maendeleo NDC kuhakikisha linapata mwekezaji makini kwa ajili ya Kiwanda cha Matairi cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited ili kifufuliwe na kuanza uzalishaji wa matairi lengo la kuongeza ajira na patonla taifa kwa ujumla

Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara, Wamiliki wa Viwanda na Maafisa Biashara wa Mkoa wa Arusha, Waziri Jafo ametoa rai kwa Watanzania kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda na biashara inasonga mbele kwa kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo miundombinu ya maji, barabara, reli, umeme na matlrekebisho mbalinbali ya Sera Sheria na Kanuni.

Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa akiwa Mkoani humo ametembelea Kiwanda cha Maziwa cha Tanzania Dairies Limited (TDL), Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills Limited (Kilitex), Kiwanda cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited, Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited, Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha TANELEC Limited, Kiwanda cha nguo cha Sunflag na Kiwanda Moonlight Tanzania Limited

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ameaidi kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na TAMISEMI ili kuhakikisha changamoto zote za wafanyabiashara zinatatuliwa kwa hatua ili kuhakikisha viwanda vyote mkoani humo vinafanya kazi na Mkoa wa Arusha unakiwa Mkoa wa Mfano katika kuendeleza viwanda na kukiza biashara.

Naye Mkurugenzi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema NDC imepokea maelekezo yote na itayafanyia kazi ilinkuhakikisha kiwa kiwanda cha General tiyre kinafuguka na kufanya kazi kwa ufanisi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Maziwa cha Tanzania Dairies Limited (TDL) kilichopo Unga Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki hakifanyi kazi tangu kilipobinafsishwa 1998.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills Limited (Kilitex), kilichopo Themi Hill wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kilibinafsishwa na hakifanyi kazi.

aziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited kilichopo Njiro wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki hakifanyi kazI.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea na kuongea na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha TANALEC Limited Bw. Zahir Saleh wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kinauwezo wa kutengeneza Transiformer 14,000 kwa mwaka na zinauzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiangalia Transfoma zinazotengenezwa na Kiwanda cha TANALEC Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Sunflag wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kimeajiri takribani wafanyakazi 2800 na kinauza bidhaa zake ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiongea na Wafanyakazi wa Kiwanda Moonlight Tanzania Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kinauza bidhaa zake ndani na nje ya nchi

Share:

Saturday 24 August 2024

WIKI YA AZAKI 2024 KUANZA RASMI SEPTEMBA 9-13 JIJINI ARUSHA


Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

Washiriki zaidi ya 500 kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI), Sekta Binafsi, Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki maadhimisho ya Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 Jijini Arusha. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Agosti 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, amesema kuwa, wiki hiyo imebebwa na kauli mbiu ya Sauti, Dira na Thamani, ikiendana na wakati uliopo na matukio yanayoendelea nchini, ambayo ni pamoja na uchaguzi wa Serikali za mtaa utakaofanyika mwaka huu, uchaguzi mkuu wa mwakani na Dira ya Taifa ya Maendeleo.

 “Tupo kwenye kipindi muhimu sana kwenye demokrasia yetu kama nchi, kwa sababu mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mtaa, wote mnafahamu, pia mwakani tuna uchaguzi mkuu, lakini la jambo la kipekee sana, mwakani tunatarajia kuzindua dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo ni fursa adimu sana inayokuja mara moja kwa muda mrefu. Fursa hii kutokana na umuhimu wake si budi sauti za wananchi zikasika kuchangia maoni yao wenye, kwani dira ya Taifa inapaswa itokane na sauti, mawazo, mitazamo na maoni ya wananchi”, amesema Rutenge. 

Aidha, Rutenge ameongeza kuwa, wiki hiyo pia itakuwa na mijadala mbalimbali inayohusu shughuli za AZAKi nchini, maendeleo ya jamii na ushirikiano baina ya Asasi za Kiraia, Serikali na sekta binafsi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulika kusaidia na kuwezesha watu wenye ulemavu wa macho nchini (CBM), Nesia Mahenge, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKi 2024, amesema kuwa kuelekea katika wiki hiyo maandalizi yamekamilika, ambapo amewashukuru wadau wote waliojitokeza kudhamini na kuwezesha maadhimisho hayo.


Aidha, Mahenge ameeleza kuwa, katika wiki hiyo itayaleta pamoja makundi mbalimbali ikiwemo vijana, jamii, makundi maalum na wadau mbalimbali watakaojadiliana kwa pamoja mada zinazohusiana na kaulimbiu ya maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya wiki ya AZAKI 2024 ni ya sita kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 24,2024

 






Share:

Thursday 22 August 2024

WANANCHI WAANDAMANA POLISI LAMADI WATOTO KUPOTEA




Polisi na wananchi

Shughuli za wananchi wa Kata ya Lamadi wilayani Busega, mkoani Simiyu, zimesimama tangu asubuhi, baada ya wananchi kuandamana katika kituo cha polisi cha Lamadi kwa madai ya kukithiri kwa matukio ya watoto kupotea katika mazingira yasiyojulikana.

Hali hiyo imepelekea wananchi kufunga barabara kuu, inayounganisha mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara, huku wakiyashambulia magari yanayopita barabani kwa mawe wakidai wamechoshwa na matukio hayo.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu, inayoongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga, imefika katika eneo hilo na kuimarisha usalama kwa kuwatawanya wananchi hao kwa kupiga mabomu ya machozi.

Chanzo- EATV
Share:

MABORESHO HUDUMA YA MAJI GOBA

 


Kazi ya kuweka toleo la bomba la inchi 3 kutoka bomba la usambazaji maji la inchi 4 inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Simba Oil

Kazi hiyo inahusisha utolewaji wa maji katika bomba la inchi 4 kuelekea bomba la usambazaji maji la inchi 6 pamoja na ulazaji wa bomba la inchi 3 umbali wa mita 60 ili kuongeza msukumo maji katika eneo ilo.

Kukamilika kwa kazi hiyo itasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Simba Oil, Chasimba, Minji, River View, Goba Zahanati, Shimbi Kati na Mwamuyamu
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger