Sunday 4 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 4,2024



Share:

Saturday 3 August 2024

MWAMBUKUSI ASHINDA URAIS TLS



Na, Mwandishi wetu kutoka - Dodoma.

Agosti 2, 2024 umefanyika uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia na hatimae matokeo ya kura yameamua Boniface Mwabukusi kushikilia kiti hicho.

Mwabukusi ambaye alionekana kuwa imara na jasiri wakati kampeni zake ameibua sura mpya baada ya kuibuka na kura 1,274 sawa na asilimia 57.4 dhidi ya wapinzani wake watano ambao ni Ibrahim Bendera, Emmanuel Muga, Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli na Paul Kaunda.

Uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma huku matokeo yakitangazwa majira ya saa tano usiku katika hali isiyo ya kawaida sababu ikitajwa kuwa ni msiba wa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho ikapelekea muda kusogezwa mbele.


Share:

MAHAFALI YA 12 CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO YAFANA.."TUMIENI ELIMU MLIYOPATA KWA MANUFAA YA JAMII"

Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Shinyanga, Mwl. Paschal Shiluka akizungumza kwenye mahafali ya 12.

Na Elisha Shambiti - Misalaba Media

Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Shinyanga, Mwl. Paschal Shiluka, amewataka wahitimu wa kozi za afya katika chuo hicho wasiifanye elimu waliyoipata kuwa mali yao bali kuwa mali ya jamii ili kuweza kuisaidia jamii zao kuondokana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na afya.

Katika hotuba yake kwenye mahafali ya kumi na mbili (12) ya chuo hicho yaliyofanyika Ijumaa, Mwl. Shiluka alisema kuwa wahitimu wanapaswa kutumia elimu waliyoipata kuzigeuza changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii zao kuwa fursa ambazo zitawaletea maendeleo binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho, Dk. Luzila John, amewataka wahitimu hao kwenda kuwa mabalozi wema wa chuo hicho katika jamii zao kwa kuzingatia maadili mema, kwani elimu na taaluma bila maadili si kitu chochote.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT), Mch. Mwl. Josephales Mtebe, amesema kuwa wahitimu wanapoenda kufanyia kazi taaluma zao wanapaswa kuonyesha upendo na ukarimu kwa wagonjwa, jambo litakalosaidia wagonjwa kupata nafuu kabla ya kupatiwa matibabu mengine.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mzava, ambaye alimuwakilisha mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Paschal Patrobas Katambi, katika mahafali hayo, amesema kuwa wahitimu wanapaswa kujua kuwa serikali haiwezi kuwaajiri vijana wote wanaohitimu masomo yao na badala yake wajifunze kujitegemea wenyewe kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii zao kama vile kutumia fursa za mikopo kwa makundi ya vijana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali.

Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kilianzishwa mwaka 1957 kikianza na udahili wa wanafunzi kumi na mbili ambapo Agosti 2,2024 jumla ya wanachuo 316 wamehitimu mafunzo yao kutoka kozi za maabara ya viwanda, uuguzi na ukunga, maabara ya binadamu, utabibu na famasia.
Mgeni rasmi, Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mzava akizungumza kwenye mahafali ya 12 katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Agosti 2,2024.
Katibu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT), Mch. Mwl. Josephales Mtebe, akizungumza kwenye mahafali ya 12 katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Agosti 2,2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho, Dk. Luzila John, akizungumza kwenye mahafali ya 12 katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Agosti 2,2024.
Watumishi wa chuo.



Share:

Friday 2 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 3, 2024












Share:

Video Mpya : NYANDA SHETO - KAYA

 

Share:

Thursday 1 August 2024

SIJAWAHI KUSHINDWA KESI YOYOTE MAHAKAMANI

Ingawa sijawahi kusomea mambo ya sheria mahali popote pale lakini katika miaka zaidi ya 15 katika viunga vya Mahakama sijawahi kushindwa kesi, mara zote huwa naibuka mshindi tu.

Jina langu ni Pascal, nimeshawahi kushtakiwa Mahakamani zaidi ya mara 10 kwa mashauri mbalimbali ambayo naweza kusema mengi yalikuwa ya uongo ambayo yalikuwa yanatengenezwa na watu wenye nia mbaya na mimi.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 niliwahi kufungwa jela miaka mitano kwa kesi ya uongo kabisa, naweza kusema kama ningekuwa na uwezo wa kifedha wakati ule wa kuweka Wanasheria, basi ningeshinda.

Nilikaaa jela miaka mitano ya mateso, lakini kwangu ilikuwa ni kama kunipa funzo la jinsi gani napaswa kuishi na watu na kikubwa zaidi ni namna ya kutazama mambo kwa jicho la tatu.

Unajua watu wengi tumekuwa na kasumba kuwa mambo yenye gharama kubwa ndio ambayo yana uhakika zaidi katika uhitaji wetu wowote ule.

Lakini hilo halina ukweli wowote ule, kwani kuna mambo mengi mazuri na kuna huduma nyingi nzuri zenye matokeo makubwa ambazo unaweza kuzipata kwa bei nafuhu zaidi na kwa urahisi zaidi.

Ndivyo ilikuwa kwangu pale nilipokuja kukutana na Kiwanga Doctors ambaye alinipatia dawa ya kuweza kushinda kila kesi ambayo inafunguliwa Mahakamani dhidi yangu.

Mtu huyu ambaye amesaidia watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki niliamua kumtafuta mara moja kutokana sikuwa na uwezo wa kuwalipa Wanasheria kusimamia kesi zangu.

Ila kupitia Kiwanga Doctors nimekuwa nashinda kila shauri hadi baadhi ya watu wamekuwa wakinifuta na kuniuliza nawezaje.

Jibu langu kwao siku zote limekuwa ni moja tu; kuwa Kiwanga Doctors ndiye siri ya ushindi na wale wote ambao walinisikiliza na kuamua kumtafuta wamekuja kwangu na kunipongeza na kunishukuru.

Ukiachana na hayo, kumbuka Kiwanga Doctors anaweza kukuwezesha kushinda bahati nasibu, kukuondolea migogoro ya mashamba, migogoro ya mapenzi, kuikinga biashara yako na kukupa mvuto wa kimapenzi.

Anatibu magonjwa kama presha, kifafa, kisonono, kaswendwe, upungufu wa nguvu za kiume na mengineo, watembelee leo upate suluhu kwa matatizo yanayo kutatiza.

Kwa maelezo  zaidi tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com pia waweza kumpigia simu kwa namba +255763926750 au +254769404965 au tuma barua pepe kupitia kiwangadoctors@gmail.com

Mwisho.


Share:

RAIS SAMIA AWEKA HISTORIA KUBWA UZINDUZI WA SGR

 *Rais Samia aweka historia kubwa uzinduzi wa SGR

* Samia anajenga kilomita 1,800 za reli ya SGR, huku Awamu ya 5 ikianzisha ujenzi wa kilomita 721

* Tanzania sasa inaelekea kuwa na reli ndefu kuliko zote kwenye bara zima la Afrika

* Rais Samia ametimiza ndoto za marais wote waliopita tangu Tanzania ipate uhuru

* Asilimia 86 ya reli yote ya SGR ya Tanzania inajengwa chini ya utawala wa Rais Samia 


Agosti 1, 2024

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka historia leo kwa kuzindua rasmi huduma za usafiri wa treni ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na makao makuu ya nchi Dodoma na hivyo kutimiza ndoto za marais wote waliomtangulia tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Ndoto ya kuiunganisha Dar es Salaam na Dodoma kwa reli ya kisasa ya SGR ilianza tangu enzi za utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Kwanza.

Naye Rais wa Awamu ya 2, Ali Hassan Mwinyi, aliendeleza ndoto hiyo na kupokewa kijiti na Rais Benjamin Mkapa wa Awamu ya 3.

Chini ya uongozi wa Rais Mkapa, nchi tatu za wakati huo za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Tanzania, Kenya na Uganda, ziliweka makubaliano ya kujenga reli ya SGR kuunganisha mataifa hayo.

Rais wa Awamu ya 4, Jakaya Kikwete, naye aliendeleza ndoto hiyo kwa serikali yake kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) ya ujenzi wa reli ya SGR.

Rais wa Awamu ya 5, John Magufuli, alionesha uthubutu kwa kuanza ujenzi wa kilomita 721 za reli ya SGR.

Alipoingia madarakani Machi 2021, Rais wa Awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan, aliendeleza ujenzi wa reli ya SGR kwa kasi ya ajabu na kuongeza kilomita nyingine 1,800

Jumla ya kilomita 2,102 za reli ya SGR zinazoendelea kujengwa nchi nzima, huku kilomita 1,800 zikiwa zinajengwa na Rais Samia.

Hii inamaanisha kuwa asilimia 86 ya reli yote ya SGR ya Tanzania inajengwa chini ya uongozi wa Awamu ya 6 ya Rais Samia.

Ujenzi huu mkubwa unaifanya Tanzania kuwa nchi ya Afrika yenye SGR ya urefu mkubwa zaidi barani humo.

Ujenzi unaoendelea wa reli ya SGR kwa kasi kubwa unatarajiwa kufika hadi kwenye mikoa ya mipakani na kuiunganisha Tanzania na nchi jirani, hivyo kukuza fursa za kilimo, biashara na uchumi.

Inatarajiwa kwamba ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi mkoa wa Mwanza utakamilika mwaka 2026, wakati reli ya Dar es Salaam hadi Kigoma itakamilika mwaka 2027, kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Reli la Tanzania (TRC).

Kukamilika kwa reli ya SGR kutafungua biashara ya mizigo na abiria kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi nchi jirani.

Huduma ya usafiri wa abiria kupitia treni ya kasi ya umeme ya SGR pia itaongeza biashara kati ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma na nchi jirani.

Thamani ya viwanja vya Dodoma na Morogoro inatarajiwa kuongezeka kwa kasi kutokana na usafiri wa SGR kwani sasa hivi mtu anaweza kutoka Dar es Salaam asubuhi akafika Morogoro au Dodoma akafanya shughuli zake na kurudi Dar es Salaam siku hiyo hiyo.

Inachukua chini ya masaa manne kusafiri kwa treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma, wakati usabiri wa basi hutumia muda mrefu mara mbili ya huo.

Tanzania inatarajiwa kupata mapinduzi makubwa kwenye maendeleo yake kutokana na ujenzi wa reli ya SGR unaofanywa na Serikali ya Rais Samia.

Share:

HUDUMA ZA AFYA KUTOLEWA MAONESHO YA NANENANE DODOMA




Na Mwandishi wetu, Dodoma

Wizara ya Afya pamoja na ldara na Taasisi zake inashiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika Viwanja vya nanenane Nzunguni Dodoma.

Huduma mbalimbali za Afya zinatarajiwa kutolewa katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na Elimu ya Afya kuhusu Mtindo bora wa Maisha ,umuhimu wa mazoezi, lishe,vipimo vya uwiano uzito na urefu, afya ya akili, vipimo vya Virusi vya UKIMWI,uchunguzi wa awali Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti,Dawati la Elimu ya Afya na Uhamasishaji jamii, Elimu ya Afya ya Mazingira,Elimu ya Afya kuhusu Tiba Asili na Elimu ya Afya kuhusu Malaria na magonjwa mengine mbalimbali.

Viongozi wa Wizara ya Afya akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Utawala Wizara ya Afya Bi.Fatma Kalovya,Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Simon Nzilibili, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Englibert Kayombo, Bi. Grace Msemwa , Mratibu wa Mabadiliko ya Tabia katika Jamii Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Evance Simkoko Afisa Afya Wizara ya Afya wamewasili katika banda la Wizara ya Afya kujionea Maandalizi yanavyoendelea.

Maonesho ya Nanenane kitaifa yamefunguliwa rasmi leo tarehe 1,Agosti, 2024 Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa hadi Agosti 8,2024 ambapo Huduma mbalimbali za Afya zitatolewa bila malipo hadi tarehe 10, Agosti, 2024.

Share:

Wednesday 31 July 2024

MELI KUTOKA CHINA ZITAENDELEA KUTIA NANGA BANDARI YA TANGA

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Kampuni ya Uwakala wa Meli Seafront  Shipping Service (SSS), kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuleta meli yenye shehena ya mizigo mchanganyiko 
inayokadiriwa kuwa takribani tani (14,000) kutoka nchini Chiina wamoja hadi bandari yaTanga.

Hii inaweka alama ya kipekee kuwahi kutokea kwa meli ya mizigo mchanganyiko kuweza kushusha kiwango kikubwa cha mizigo mchanganyiko,zaidi ya magari 500 na aina nyingine ya mizigo mchanganyiko kuweza kushushwa katika bandari hiyo.

Meneja mkuu wa kampuni hiyo Neelakandan CJ amesema baadhi ya mizigo itaelekea katikanchi Jirani kama Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya watu wa Kongo (D.R.C), Malawi, Rwanda nakadhalika na mizigo mingine itabaki hapa nchini kwa maana ya (localgoods),

"Kimsingi haya ni mafanikio makubwa na muhimu kwa maendeleo ya Bandari ya 
Tanga, bandari hii inatarajia pia kupokea aina nyingi ya mizigo kuelekea nchi za jirani, na hii itafanya wafanyabiashara, watoa huduma za usafiri, mawakala wa 
forodha,jamii za wafanyabiashara wa ndani" amesema.

"Kwa pamoja tunanufaika kwa kiwango cha juu kutokana na meli zitakazokuwa zinatia nanga bandari ya Tanga moja kwa moja kutoka bandari za Kimataifa
zaidi, kutakuwa nameli za mizigo 
mchanganyiko kuanzaia 3 mpaka 4 kipindi cha hivi karibuni, ambazo tayari zimepangwa kuingia bandari ya Tanga" ameeleza.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga Masoud Mrisha amesema ujio wa meli hiyo ni matokeo makubwa ya maboresho ya Bandari hiyo na Kwa mara ya kwanza meli kubwa imetia nanga.

Mrisha amesema mbali na meli hiyo, kampuni hiyo itaendelea kuleta meli nyingine ndanya mwezi Agosti lakini pia itaendelea kuwa mteja wa kupitisha mizigo yake katika bandari ya Tanga.

Amebainisha kwamba kupitia maboresho hayo wamefanikiwa kuingiza meli kubwa zipatazo 35 zilizobeba tani 330,173 ndani ya mwezi wa saba mwaka huu, na kwa mwaka wa fedha 2024/25 tayari wamekwisha pokea meli 31 wakati lengo ni kuingiza meli 19 hali iliyopelekea kuvuka malengo 

"Tumeanza mwanzo mzuri, mwaka jana mwezi kama huu wa saba tulihudumia meli zenye tani 46 na mwaka huu kabla mwezi haujaisha tumesha hudumia meli zenye tani 96, kwahiyo dalili njema, na mwaka huu tumewekewa lengo la tani milioni 1.4" amefafanua Mrisha.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger