Wednesday, 31 July 2024
TCB BENKI YATOA VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 50 SUMBAWANGA
BIL 3 ZIMETOLEWA MATENGENEZO BARABARA ZILIZOATHIRIWA NA EL-NINO MKOANI NJOMBE-ENG RUTH
Tuesday, 30 July 2024
MBUNGE MTATURU AITAKA RUWASA KUKAMILISHA MRADI MAPEMA
WAGOMBEA URAIS WAELEZA WATAKAVYOIFANYA TLS KUWA NA NGUVU
Wagombea wa nafasi ya Urais katika Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) wakiwa kwenye mdahalo.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ukitarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu jijini Dodoma, wagombea nafasi ya Urais wamejinadi namna ya kujenga chama hicho kwenye misingi yenye nguvu ikiwamo kuondokana na vishoka katika taaluma hiyo.
Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni Wakili Sweetbert Nkuba, Paul Kaunda, Revocatus Kuuli, Emmanuel Muga, Ibrahim Bendera na Boniface Mwabukusi.
Akizungumza juzi kwenye mdahalo wa wagombea hao jijini Dar es salaam, Mgombea wa Urais TLS, Wakili Revocatus Kuuli, alisema “Wako Mawakili vishoka ambao ni matapeli tu na kwanza huwezi kuwaita Mawakili. Matapeli wa kisheria hawatakuwepo nikiwa Rais wa TLS.”
Alisema kuwa Wakili kishoka ni kosa la jinai na vyombo vinavyoshughulika na jinai kama polisi vina wajibu wa kushughulika na watu hao.
“Kuna baadhi ya watu wanakiona chama hicho kupoteza ubora, lakini wagombea ambao tunagombea sasa tumeweka mikakati ya kukirudisha chama kuwa na nguvu na kutekeleza misingi iliyowekwa ya chama,”alisema.
Mgombea Wakili Boniface Mwabukusi alisema atarudisha taaluma ya uwakili katika misingi kwa kuwa TLS ni taasisi kongwe.
“Mimi ni simba nitakayeongoza kundi la simba na watanzania wataanza kuona uwepo wa chama hiki kwa kuwa TLS ina wajibu kwa wananchi, serikali, wanachama na utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka katika mhimili ya dola,”alisema.
Alisema TLS ndio kiungo wa kuifanya nchi ishamiri kiuchumi, kisiasa na kidemokrasia.
“Nataka kuleta umoja kwenye uwakili kwasasa umegawanyika, tunapokuwa na TLS yenye kuwajibika nchi zinavamiwa kiuchumi ni wajibu wa TLS kuongoza watanzania kujua ukweli wa kisheria wa mikataba ya kimataifa na sera tunazoingia, nikipewa nafasi anakwenda kubadili mfumo wa watu kufikiri TLS ni jukwaa la kutafuta mambo fulani.”
“Hatutaruhusu mawakili kunyanyasika katika taifa hili, kanuni zinazoongoza malipo kwa mawakili zinakatisha tamaa, tusipokuwa na ulinzi katika taaluma yetu hakuna aliye salama,”alisema.
Mgombea Wakili Emmanuel Muga, alisema akichaguliwa ataimarisha utawala kwa kutengeneza kamati zenye uwezo wa kufanya kazi na kuifanya TLS kufuata taratibu za kisheria na sio kuendesha mambo yake kiholela.
“Nitasimamia wajibu wa TLS kwa wanachama, serikali na kwa wananchi, na mimi sitakuwa Rais wa TLS wa kufoka foka kwa kuwa sina mamlaka yangu peke yangu ya kutoa tamko ambalo halijatokana na kamati ya uongozi wa TLS,”anasema.
Naye, Mgombea Wakili Sweetbert Nkuba alisema kama atachaguliwa kuwa Rais wa TLS atahakikisha taasisi hiyo inalinda heshima yake na kuwasambaratisha vishoka walioko kwenye kada hiyo ambao hawajasomea sheria.
Alisema atahakikisha mawakili wote wanasajiliwa na ofisi zao zitambulike kisheria ili kuwabaini mawakili wababaishaji.
“Nitaimarisha TLS tunatakiwa kuwa na nguvu na sauti moja ambayo itasaidia uimara wa chama, hivyo ni muhimu kupata viongozi makini wenye dhamira thabiti ya kusimamia chama na si ujanja ujanja,”alisema.
MAWAKILI VIJANA
Wakili Nkuba alisema akipata nafasi hiyo atahakikisha mawakili vijana chipukizi hawatozwi ada nyingi kuwa mawakili, kuwajengea weledi kwa kuwa wengi wao wanashindwa kufanya kazi zao kwa kukosa mitaji na maeneo ya kufanyia kazi.
Aidha, Mgombea Wakili Paul Kaunda alisema anataka kuwalinda na kuwatetea mawakili wachanga kwa kuwaongezea thamani na heshima ikiwamo kuanzisha Wakili APP ambayo watajisajili na itarahisisha wao kupata wateja.
Kadhalika, Mgombea Wakili Ibrahim Bendera alisema amedhamiria kuwaunganisha mawakili vijana na wale wenye uzoefu ili kuwasaidia kujijenga kitaaluma kutokana na wengi wao kushindwa kuanzisha ofisi zao kwa kukosa mitaji huku Wakili Muga akisema ataanzisha utaratibu wa kuwasaidia mawakili wachanga kwa kusimamiwa na mawakili wazoefu.
Monday, 29 July 2024
NCHIMBI AWAPONGEZA MTWARA VIJIJINI UTEKELEZAJI ILANI YA CCM
SERIKALI KUFADHILI MASOMO YA TEKNOLOJIA YA NYUKILIA
Sunday, 28 July 2024
WANAFUNZI NAMNA PEKEE YA KUMLIPA RAIS SAMIA NI KUSOMA KWA BIDII-KATIMBA
Saturday, 27 July 2024
SIKU YA BAHARI AFRIKA; WANAWAKE SEKTA YA BAHARI WAASWA KULINDA MAZINGIRA
Na Grace Semfuko, Maelezo.
Wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya bahari nchini, wameungana na wanawake wenzao Duniani kuadhimisha siku ya bahari Afrika ambapo katika maadhimisho hayo wamesema ni muhimu kulinda mazingira ili kuwe na uchumi endelevu wa mazao katika sekta hiyo.
Wanawake hao leo Julai 27, 2024 wameadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi katika fukwe za Coco Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya bahari (WOMESA) Bi. Fortunata Kakwaya amesema wanaunga mkono juhudu za serikali za kulinda na kuendeleza gukwe za bahari ili kuweza kuwa na uchumi wa buluu imara na endelevu.
“Kama mjuavyo, kama bahari itachafuliwa hatutakuwa na mazingira safi ya bahari, kwa maana hiyo hatutakuwa na uchumi wa buluu endelevu, na ndio maana tumekuja kusafisha hii fukwe na kutoa elimu ili jamii ione umuhimu wa kulinda mazingira ya bahari, zoezi hili pia linalenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuhifadhi mazingira” amesema Bi Kakwaya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali amesema Tanzania kama taifa la lililozungukwa na neema ya maji linafanikisha kufanya biashara ya usafirishaji na nchi zingine, hivyo kuongeza pato la taifa.
“Tunapoadhimisha tulio hili tunafanya kumbukumbu ya utajiri tuliopewa na Mwenyezi Mungu kama Bara la Afrika, kwa hapa Tanzania tumejaaliwa kuwa na maji na fukwe ndefu, yenye kilomita Zaidi ya 1,400, kupitia maji tunapata chakula na kufanikisha shughuli zetu za kiuchumi, sasa Tanzania kama taifa la maji tunafanikisha biashara sio tu ya nchi yetu lakini pia ya nchi zingine, katika Afrika nchi kama 32 zina ukanda wa pwani, zinapakana na bahari na theluthi ya nchi hizo hazihusiani na bahari, hasara wanazopata ni pamoja na kutumia mapato yao mengi ya nchi zaidi ya asilimia 40 kwa ajili ya kufanya biashara za kimataifa kupitia njia ya maji, kwa hiyo sisi kama nchi tumejaaliwa kuziepuka gharama hizo na badala yake pesa hiyo inatumika katika mambo mengine ya kijamii” amesema Bw. Mlali.
Nae Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Tanzania (TASU), Bw.Josiah Mwakibuja, amewataka mabaharia nchini kutoa taarifa pindi wanapokutana na viashiria vya uhalifu wawapo kwenye majukumu yao.
“Baharia ni mtu ambaye ana nidhamu na welezi, ni mtu ambaye amesoma, kuna baadhi ya masomo ambayo tunafundishwa mtu aweje katika meli au kwenye jamii, hao wanaoshiriki kufanya uhalifu ni wahalifu kama wahalifu wengine, na hao hawana weledi wa kibaharia, baharia ni mtu wa heshima, natoa wito tuwe na ushirikiano na vyombo vinavyohusika na usalama wa nchi , tuwe wepesi wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pale tunapoona matukio ya uhalifu” amesema Bw. Mwakibuja.