Sunday 7 July 2024

LIGI YA BUTONDO KISHAPU SHAGY CUP YAHITIMISHWA KWA KISHINDO! BODABODA FC YALAMBA MIL. 1.5


Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo na mdhamini wa ligi ButondoKishapu Shagi Cup

Na Sumai Salum - Kishapu

Timu ya Bodaboda Fc ya Kishapu mkoani Shinyanga imeibuka na  ubingwa wa mshindi wa kwanza kwa bao la goli 1 kwa "Nunge" (0) dhidi ya Fama FC ya Igaga katika Ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup na kuondoka na kitita cha Tsh. 1,500,000/=.
 
Akizungumza Julai 6,2024 katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga palipochezwa ligi hiyo wakati akifunga mashindano hayo Mbunge wa jimbo la Kishapu na mfadhili wa ligi iliyoanza Mei,15,2024 huku timu 16 zikishiriki  Mhe. Boniphace Butondo amesema kuwa mchezo umekuwa mzuri hakukuwa na taarifa zozote za matukio ya kutisha hivyo na hatoishia hapo bali michezo itaendelea.

"Pongezi kwenu mshindi wa kwanza (Bodaboda fc Kishapu),mshindi wa pili Fama FC pamoja na mshindi wa tatu Ngundangali FC kiukweli mmekuwa waungwana kwa kipindi hiki chote cha mashindano haya na hata leo ninapoyafunga nikiwa mgeni rasmi napenda kutamka kuwa hatutaishia hapa bali tujiandae hivi karibuni tena tutaanza kule Masanga ligi nyingine na nitafadhili kama kawaida jezi kwa timu zote kumi na sita (16) na mipira na timu zote zilizoshiriki ligi hii zitashiriki na Masanga pia tuwe tayari ndugu zangu", amesema Mhe. Butondo.

Aidha amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Lubaga pamoja na serikali kwa kuwa na utayari wa kuipokea ligi hiyo na kuwa wavumilivu katika kipindi chote huku akitoa wito kwa viongozi wa timu zote kuhakikisha usajili wa wachezaji unaibua vipaji vya vijana wa ndani ya Kishapu kwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Joseph Mkude amezipongeza timu zote zilizoshiriki na kusema kuwa umewaweka pamoja vijana licha ya kuwa wanatoka maendmwo tofautitofauti ya Kishapu na nje.

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Kishapu na mwenyeji wa mashindano hayo Mhe. Joel Ndettoson amemshukuru Mbunge Butondo kwa mchango mkubwa wa kuwaleta vijana pamoja na kuwapongeza timu zote huku akiongeza kuwa si rahisi kombe kuvuka Daraja (kutoka nje ya watoto wa mjini kata ya Kishapu)

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga  Cde. Benard Werema ameendelea kuwashukuru vijana wote waliomwamini na kumuombea kuchaguliwa nafasi hiyo adhimu ya kuwatumikia wananchi na amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Aidha zawadi mbalimbali za fedha taslimu zimetolewa kwa Golikipa Bora,Kocha bora,Msemaji Bora wa mashabiki,Timu yenye nidhamu pamoja na Mashabiki bora.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo na mdhamini wa ligi ButondoKishapu Shagi Cup akizungumza katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga ligi hiyo ilipokuwa ikichezwa na timu kuni na sita (16)  akidhamini  kwa kutoa jezi na mipira kwa timu zote - Picha zote na Sumai Salum
Diwani wa kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akizungumza kwenye kilele cha ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup iliyofungwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe Boniphace Butondo ambae pia ni mdhamini wa ligi hiyo huku ushindi ukibakia kata ya Kishapu kwa Bodaboda FC.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akiwasalimia wananchi na kutoa pongezi kwa timu zote zilizoshiriki katika ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga Wilayani humo huku Bodaboda Fc ikiondoka na kitita cha 1,500,000 na kombe kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fama FC ya Igaga.
Mbunge wa jimbo la Kishapu  Mhe. Boniphace Butondo (kulia) na Mhe.Mkuu wa  Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakiteta jambo katika ufungaji ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup huku bodaboda FC kuibuka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Fama FC  katika Viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani humo
Kiungo Madia Madoshi aliyeiletea ushindi  Bodaboda Fc wa goli 1-0 dhidi ya Fama FC Ligi ya Butondo Shagi cup iliyomalizika  Julai 6,2024 katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga na kufungwa na mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo na kuondoka na kitita la 1,500,000 na kombe.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM mkoa wa Shinyanga Bw. Benard Werema akizungumza kwenye ufungaji ligi ya Butondo Kishapu Shagy Cup  katika uwanja wa mpira wa shule ta Msingi Lubaga huku bodaboda FC Kishapu ikiibuka mshindi wa kwanza katika  ligi hiyo.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 7, 2024










Share:

Saturday 6 July 2024

TAWA YANADI FURSA ZA UWEKEZAJI MAONESHO YA 48 YA KIMATAIFA ALMAARUFU SABASABA 2024


Na Beatus Maganja, Dar es Salaam.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kuhamasisha Umma wa watanzania wawekezaji na wageni kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza katika maeneo inayoyasimamia huku ikijinasibu kuwa na fursa lukuki za uwekezaji.

Akiongea na wageni waliotembelea banda la TAWA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Afisa utalii Daud Tesha amesema TAWA ina uwanda mpana wa fursa za uwekezaji unaotoa mwanya kwa wawekezaji wa aina mbalimbali kuwekeza katika Taasisi hiyo.

Akizitaja fursa hizo Tesha amesema yapo maeneo mengi yanayohitaji wawekezaji na uwekezaji katika Taasisi hiyo kama vile maeneo ya utalii wa picha kwenye maeneo ya hifadhi za Wanyamapori, maeneo ya kihistoria yenye Utalii wa kiutamaduni, eneo la uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA), Uwindaji wa Kitalii na Ufugaji wa Wanyamapori.

"TAWA imetenga maeneo kadhaa Kwa ajili ya kufanyika shughuli za utalii wa picha kutokana na ikolojia na aina ya vivutio vilivyopo katika maeneo hayo ikiwemo Pori la Akiba Mpanga/Kipengere eneo ambalo lina maporomoko ya maji zaidi ya 10 ambayo hutoa burudani safi kwa watalii" amesema Daud Tesha.

"Maeneo mengine ni Pori la Akiba Wamimbiki, Tabora ZOO, Ruhila ZOO , Makuyuni Wildlife Park ambapo wananchi wanakaribishwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Utalii ikiwemo kujenga Kambi za Kulala wageni (Campsites), Hosteli, Loji na maeneo ya mapumziko mafupi kwa watalii (Picnic Sites) ameongeza

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi Wote kutembelea banda la TAWA Ili kupata maelezo ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi hiyo.

"Kama kauli mbiu ya Maonesho haya inavyosema kuwa Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji, nitumie fursa hii kuwaambia watanzania wote kuwa TAWA ni Taasisi sahihi kwa biashara na uwekezaji kwani inatoa fursa za uwekezaji wa aina mbalimbali kama vile ujenzi wa loji, kumbi za mikutano katika maeneo yetu, kambi za watalii, michezo ya watoto lakini kama haitoshi mwekezaji anaweza akatumia fursa ya kuwekeza katika mashamba ya wanyamapori, bustani za wanyamapori n k" amesema Maganja.

"Kwahiyo hii ni fursa adhimu Kwa wawekezaji wote kutembelea banda letu ili waweze kupata ufafanuzi wa fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi yetu" ameongeza

Maonesho haya yenye Kauli Mbiu "Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji" yameanza 28 Juni, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati 14 Julai, 2024
Share:

TBS KANDA YA MASHARIKI YATEKETEZA TANI 4.5 ZA BIDHAA HAFIFU


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), Kanda ya Mashariki limeteketeza bidhaa hafifu tani 4.5 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 90 mara baada ya kufanya ukaguzi na kufanikiwa kukamata bidhaa hizo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo ambalo limefanyika leo Julai 5,2024 Pugu Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Kanda ya Mashariki, Francis Mapunda amesema kuwa walifanya oparesheni ya Ukaguzi Kanda ya Mashariki na kubaini kuwepo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara kuuza bidhaa zilizo chini ya kiwango.

Amesema kuwa bidhaa hizo wamezikamata katika Mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro na Pwani ambapo bidhaa hizo zilikuwa hazijasajiliwa, zilizoisha muda wa matumizi pamoja na bidhaa zisizosalama kwa walaji.

Aidha amewaonya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zilizoisha muda wake ambapo amesema wanapaswa kuwa na utamaduni wa kukagua bidhaa zao na kama zimeisha muda wake ni vyema wakaziondoa mara moja ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.

Pamoja na hayo amewaasa wananchi kuwa makini na ununuaji wa bidhaa sokoni ikiwemo chakula kuangalia tarehe ya za kutengenezwa na tarehe za kuisha muda wake lakini vilevile na kuangalia kwenye mitandao ya kijamii bidhaa ambazo zimepigwa marufuku kwamba si salama kwa matumizi ya binadamu.
Share:

Friday 5 July 2024

Video : KALUNDE - BHALOMOLOMO

 

Share:

SEKTA YA MADINI IMEWAFUNGULIA FURSA WATANZANIA, CHANGAMKENI

Na Wizara ya Madini

Kama umekuwa ukifuatilia kwa karibu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kuwezesha ushiriki wa Watanzania katika uchumi wa Madini ni vizuri kuona matokeo chanya yanayopatikana kupitia hatua mbalimbali kuanzia Marekebisho ya Sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017 ambayo yalijumuisha hitaji la matumizi ya huduma na bidhaa zinazopatikana nchini Tanzania.

Marekebisho haya yalipelekea kutungwa kwa Kanuni za ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini za Mwaka 2018.

Matokeo ya utekelezwaji wa Kanuni hizo hadi sasa yameonesha dalili nzuri za maendeleo katika eneo hili muhimu la uchumi kwani idadi ya watanzania wanaotoa huduma na kuuza bidhaa kuanzia migodi ya uchimbaji mdogo, Kati hadi uchimbaji mkubwa unazidi kuongezeka.

Dalili hizi zinadhihirishwa na namna ushiriki wa watanzania ulivyoongezeka kupitia takwimu mbalimbali ikiwemo za mwaka 2023 zinazoonesha namna kampuni za kitanzania zilivyouza bidhaa na huduma migodini zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.48 ambayo ni sawa na asilimia 90 ya mauzo yote yaliyofanyika migodini yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.65. 

Aidha, mauzo hayo yaliyofanywa na kampuni za kitanzania kwa mwaka 2023 yalikuwa ni zaidi ya mauzo yaliyofanywa Mwaka 2022 ambayo yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.08 sawa na asilimia 86 ya mauzo yote ya Dola za Marekani bilioni 1.26.

Katika kuendelea kuimarisha huduma hizi kutokana na mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji katika Sekta ya Madini, tayari kampuni tatu (3) za kitanzania zimejenga viwanda vya kutengeneza vifaa vinavyotumika migodini katika eneo la Buzwagi Special Economic Zone. 


Kampuni hizo ni East African Conveyors Supplies Limited imejenga kiwanda cha kuzalisha conveyor belts zinazotumika kusafirisha miamba wakati wa uchakataji wa madini kilichopo Manispaa ya Kahama ambapo ujenzi wake umekamilika na tayari  kimeanza usambazaji wa bidhaa hizo katika migodi ya ndani na nje ya nchi. 

Pia, Kampuni ya Max Steel Limited iliyopo jijini Dar es Salaam inatarajia kuzalisha vifaa vinavyotumika kushikilia miamba (wire-mesh na rock-bolts) kwenye uchimbaji wa chini ya ardhi ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90.


Vilevile, Kampuni ya Rock Solutions Limited inajenga kiwanda jijini Mwanza cha kuzalisha core-trays zinazotumika kutunzia sampuli za miamba iliyochorongwa ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90. Aidha, tayari kuna kampuni 8 zimeonesha nia ya kujenga viwanda vya uzalishaji bidhaa hizi.

Kwa Serikali haya ni mafanikio makubwa na ndiyo sababu Wizara inaendelea kuhamasisha watanzania na wadau wengine kuchangamkia fursa hizo za uwekezaji kupitia eneo la utoaji huduma migodini.  Kwa upande wa Wizara imeendelea kukutana na kujadili kwa pamoja na wadau kupitia majukwaa maalum kwa lengo la kuendelea kuboresha zaidi eneo hilo kwani kupitia uwekezaji huo, taifa litaendelea kupiga hatua kubwa za kiuchumi kupitia Sekta ya Madini.

Hivyo, kupitia makala hii, watanzania na wadau wengine wanahamasishwa kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha vifaa pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotumika migodini ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Dhamira ya Serikali ni kuona Tanzania inakua kinara duniani kwa kuzalisha bidhaa za migodini zinazokidhi mahitaji na hivyo kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za migodini.

Vilevile, bado  kuna fursa tele katika eneo la utoaji huduma migodini kutokana na migodi mikubwa na ya kati ambayo iko mbioni kuanzishwa katika miaka ya karibuni katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania.

Serikali   kwa upande wake inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini na ndiyo sababu inaendelea kuvutia wawekezaji zaidi hivyo, jukumu la kuona fursa hizi na kuzitumia ni la watanzania. Aidha, matokeo haya hayajatokea tu bali kupitia juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya kuifanya Tanzania kitovu cha madini duniani.


#VISION 2030: MadininiMaisha&Utajiri

 #InvestInTanzaniaMiningSector


Share:

TANZANIA KUWA NCHI YA KWANZA AFRIKA KUFANYA FILAMU NA NCHI YA KOREA KUSINI


Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Filamu Korea Kusini Yang Jongkon amesema Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza Africa kufanya movie na nchi hiyo huku akiahidi kuja nchini akiwa kuonana na waigizaj wa filamu.

Akizungumza na baada ya waigizaji katika mji unaoongoza kwa filamu duniani ujulikanao kama Busan amesema Rais huyo wa filamu Korea kusini YANG Jongkon amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea.

"Hivyo basi nami sina budi kueleza kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza tutakayoshirikiana nayo tutakapoingia Afrika. Kwa sasa tunamalizia kuimarisha bara la Asia kwenye tasnia hii ya filamu,"amesema.

Waigizaji hao ambao wapo katika ziara ya kujifunza makubwa zaidi katika soko la filamu nchini Korea kusini wameahidiwa na wameahidiwa makubwa na Rais Jongkon.

Rais Yang Jongkon ameahidi kuja Tanzania kuonana na wasanii wa Tanzania akiongozana na baadhi ya watengeneza filamu wa Korea.

Wasanii kutoka Tanzania wamefanikiwa kutembelea Studio kubwa za Busan na kuona jinsi filamu za kikorea ambazo zimetokea kupendwa sana na watanzania zinavyotengenezwa.

Filamu hizo maarufu zinazotambulika kama Kdrama(Korean drama) zimetokea kuiteka dunia na kuiweka Korea juu kabisa katika masoko ya filamu kimataifa.

Wakati Rais YANG Jongkon akizungumza hayo mjini Busan aliendelea kwa kukazia kuwa atahakikisha anaendelea kuudumisha na kuimarisha uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini.

Ameshukuru sana kwa zawadi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ilikabidhiwa na kiongozi wa msafara huo wa wasanii Steve Nyerere.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger