Saturday, 8 June 2024

DC NYAMAHANGA : LIMENI MAZAO YA BIASHARA



Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga ( aliyekaa katikati)akiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika

Na Mariam Kagenda _Kagera

Serikali Wilayani Muleba Mkoani Kagera imewataka wakulima kulima mazao ya kibiashara ambayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kasumba ya  kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikisababisha hali ya utegemezi kwenye jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema hayo wakati akifunga mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika vya matunda na mbogamboga yaliyoandaliwa na tume ya maendeleo ya ushirika (TCDC).

Dkt. Nyamahanga amesema kuwa bado kuna changamoto ya jamii kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kwao hivyo kuna haja ya viongozi hao wa ushirika kuhamasisha wakulima kujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake mrajisi msaidizi sehemu ya uhamasishaji na uratibu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika TCDC Bw. Ibrahimu Kadudu amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wakulima wa mboga mboga  kuwa ushirika mmoja ambao utawasaidia kupata mbegu na masoko ya uhakika kwa wakati mmoja.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika

Share:

WAKAZI WA KIGOMA WAASWA KUJIHADHARI NA MIKOPO KAUSHA DAMU




Na Chedaiwe Msuya, WF, Kigoma

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, Kanal Anthony Mwakisu amewataka Wananchi kukopa kwenye taasisi za fedha zilizosajiliwa na Serikali na kutambulika kwa kuwa itasaidia kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwa mkopaji kwa kuwa taasisi hizo zinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria.

Kanalı Mwakisu alitoa rai hiyo baada ya kukutana na wataalam wa Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Benki Kuu na wataalam wengine kutoka Taasisi za Serikali waliofika Wilayani mwake kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kwenda kukopa Fedha kwenye benki na Taasisi nyingine za fedha zilizosajiliwa na zinazotambulika kisheria na siyo kwenda kukopa Fedha kwenye vikundi ambavyo havijasajiliwa na serikali.

"Matumizi ya Fedha ni muhimu sana, hivyo wananchi wasikope tu kwenye vikundi ambavyo havijasajiliwa". Amesisitiza Kanali Mwakisu

Aidha, Kanali Mwakisu alisema kuwa Serikali imekusudia kuhakikisha wananchi wengi wanapata uelewa wa masuala ya fedha ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika huduma rasmi za fedha.

"wakulima msifanye matumizi mabaya ya Fedha zenu mnapo vuna mazao yenu bali fedha hizo zitumieni Kwenye matumizi sahihi ikiwemo kupeleka watoto shule". Aliongeza Kanali Mwakisu

Kwa upande wake Bw. Stanley Kibakaya ambaye ni Afisa Usimamizi wa Fedha, Wizara ya Fedha, aliwataka wananchi wanapokopa waangalie viwango vya riba ndipo wakope na wanapokopa wahakikishe wanabaki na nakala ya mkataba ili panapotokea changamoto mkataba huo uwalimde.

Kwa upande wake, Bw. Abonaventula Frederick, mkaazi wa Kasulu aliishukuru Wizara ya Fedha kwa Kutoa Elimu hiyo ambapo aliiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu katika maeneo mengine kwani asilimia kubwa ya wananchi hawajui wapi wanatakiwa kuhifadhi fedha zao na wapi wanatakiwa wakope.

"Wananchi wengi hawajui wapi pakuhifadhi fedha zao na wengi wamekopa sehemu ambazo siyo sahihi hali ambayo imesababisha wauze mali zao ikiwemo mashamba ili walipe mikopo wanayodaiwa, hivyo wengi wakipata elimu hii wataelimika'. Alisema Bw. Frederick.

Naye Bi. Stephanie Fulmasi alisema kuwa wamepata elimu kupitia filamu ambayo imeandaliwa na Wizara hiyo na kupitia filamu hiyo wamejifunza namna gani wakina mama wanatakiwa kwenda kukopa sehemu sahihi na siyo kukopa sehemu yenye riba kubwa". Amesema Bi. Stephanie.

Mafunzo ya elimu ya fedha yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Fedha yanalengo la kufikisha elimu na uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha.Kata zilizofikiwa mpaka sasa ni Buhingwe, Mnanila, Kinazi, Kasulu, Makere – VETA na Mvugwe.


Matukio ya picha yakionesha wataalamu kutoka Wizara ya Fedha wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi wa Kigoma kupitia semina, mikutano, na warsha wakilenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya fedha na njia za kuboresha hali zao za kiuchumi. Matukio hayo yalifanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kigoma, yakijumuisha wananchi kutoka kata na vijiji vya Mnanila, Kinazi, Kasulu, Makere na Mvugwe. Lengo lilikuwa ni kutoa maarifa na mbinu za kifedha zinazoweza kusaidia wananchi kuimarisha ustawi wao wa kiuchumi na kibiashara, hivyo kuongeza maendeleo katika jamii na kukuza uchumi wa eneo hilo.
Share:

DC NYAMAHANGA : LIMENI MAZAO YA BIASHARA



Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga ( aliyekaa katikati)akiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika

Na Mariam Kagenda _Kagera

Serikali Wilayani Muleba Mkoani Kagera imewataka wakulima kulima mazao ya kibiashara ambayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kasumba ya  kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikisababisha hali ya utegemezi kwenye jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema hayo wakati akifunga mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika vya matunda na mbogamboga yaliyoandaliwa na tume ya maendeleo ya ushirika (TCDC).

Dkt. Nyamahanga amesema kuwa bado kuna changamoto ya jamii kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kwao hivyo kuna haja ya viongozi hao wa ushirika kuhamasisha wakulima kujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake mrajisi msaidizi sehemu ya uhamasishaji na uratibu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika TCDC Bw. Ibrahimu Kadudu amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wakulima wa mboga mboga  kuwa ushirika mmoja ambao utawasaidia kupata mbegu na masoko ya uhakika kwa wakati mmoja.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika

Share:

Friday, 7 June 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 08, 2024








Share:

WAPIGAKURA 11,936 KUPIGA KURA KWAHANI




Na Mwandishi wetu

Wapiga kura 11,936 wanatarajiwa kupiga kura kesho tarehe 09 Juni, 2024 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo tarehe 07 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akisoma risala kwa ajili ya uchaguzi huo na kuongeza kwamba uchaguzi utahusisha vituo 29 vya kupigia kura.

“Jumla ya wapiga kura 11,936 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) watashiriki katika uchaguzi huu mdogo na jumla ya vituo 29 vya kupigia kura vitatumika,” amesema Jaji Mwambegele.

Wagombea wanaowania Kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani majina yao na vyama katika Mabano ni Bw. Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makaini), Bi. Nuru Abdulla Shamte (DP), Bi. Mwanakombo Hamad Hassan (NLD), Bi. Zainab Maulid Abdallah (CCK), Bi. Tatu Omary Mungi (UPDP), Bw. Khamis Yussuuf Mussa (CCM) na Bi. Jarade Ased Khamis (AAFP).

Wengine ni Bw. Kombo Ali Juma (NRA), Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad (UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi. Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).

Mwenyekiti wa Tume amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea, mawakala wa vyama, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba hawapigi kampeni siku ya kupiga kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

“Alama za vyama vya siasa zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi haviruhusiwi kutumika kesho tarehe 08 Juni, 2024 ambayo ni siku ya uchaguzi,” amesema.

Jaji Mwambegele ameongeza kwamba zoezi la kupiga kura katika maeneo yote ya uchaguzi litafanyika katika vituo vilevile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ameongeza kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.

“Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi kamili (10:00) jioni katika mstari na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura. Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni,” amesema.

Jaji Mwambengele amebainisha kwamba watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Amesema, Tume imeandaa majalada ya nukta nundu katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu wa kuona kupiga kura bila usaidizi. Aidha, Kwa wapiga Kura wenye ulemavu wa kuona ambao hawawezi kutumia majalada hayo, wataruhusiwa kwenda vituoni na watu watakaowachagua wenyewe kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

“Katika kituo cha kupigia kura, kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto kituoni,” amesema.

Kuhusu wapiga kura kurudi nyumbani baada ya kupiga kura, Jaji Mwambegele amesema hilo ni sharti la kisheria na kwamba maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa, Serikali na Tume yanaelekeza hivyo.

Alisisitiza kwa kusema “wapiga kura watatakiwa kuondoka kituoni mara wanapomaliza kupiga kura ili kuepusha msongamano na vitendo vinavyoweza kuchochea uvunjifu wa amani. Hivyo, Tume inawashauri wananchi kujiepusha na mikusanyiko katika maeneo ya vituo vya kupigia kura”.

Ametoa rai kwa wapiga kura katika Jimbo la Kwahani, kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura, ili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Share:

TBS YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani kwa kuendelea kusisitiza ulaji wa chakula salama kwa wananchi ili kuondokana na madhara ya kiafya na kiuchumi ikiwemo kushindwa kumudu katika biashra ya ushindani.

Hayo yamebainishwa leo Juni 7, 2024 Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi wakati akifungua mdahalo wa wadau katika kuadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani.

Amesema ulaji wa chakula kisicho salama umehusishwa na magonjwa mbalimbali, pamoja kusababisha changamoto nyingine za kiafya kama vile ukuaji duni kwa watoto, hali duni ya lishe kwa wakubwa na watoto, pamoja na kuongezeka kwa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), inakadiriwa kuwa kila mwaka mtu mmoja katika kila watu kumi huugua kutokana na ulaji wa chakula kisicho salama duniani, na kuwa, watu 420,000 kati ya wanaougua hufariki.

"Wadau tunahimizwa kujenga uwezo katika kuzuia, kung’amua na kukabiliana na dharura zitokanazo na chakula kisicho salama. Kila mmoja katika nafasi yake analo jukumu la kufanya tathmini juu ya vihatarishi vinavyoweza kusababisha uchafuzi wa chakula na madhara yake, pamoja na kuweka miundombinu ya kukabiliana na hali hiyo, endapo ikitokea". Amesema Dkt. Katunzi.

Amesema Serikali kupitia taasisi zake imekuwa na mipango ya kukabiliana na vihatarishi vya usalama wa chakula na kuimarisha mfumo wa udhibiti wa usalama wa chakula, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufuatiliaji na uratibu wa masuala mtambuka na kuimarisha mawasiliano kati ya serikali, wafanyabiashara wa chakula na jamii kwa ujumla.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa ni wajibu wa wafanyabiashara wa chakula kuimarisha mifumo ya uzalishaji ili kuhakikisha uzalishaji wa chakula salama, kushirikishana uzoefu na kuimarisha mawasiliano kati yao na walaji.

Vilevile amesema walaji wanalo jukumu la kuelewa vihatarishi vya usalama wa chakula na mazingira yanayosababisha uchafuzi wa chakula, madhara yatokanayo na kula chakula kisicho salama, kutoa taarifa juu ya chakula kisicho salama, pamoja na kufahamu namna ya kukabiliana na matukio yatokanayo na ulaji wa chakula kisicho salama.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama kwa mwaka huu (Chakula Salama: Jiandae kwa usiyoyatarajia) inatahadharisha juu ya umuhimu wa kujiweka tayari wakati wote kukukabiliana na vihatarishi inayoweza kuathiri usalama wa chakula na pia utayari wa kukabiliana na madhara yatokanayo na chakula kisicho salama.
Share:

CCM MKWAKWANI KUWA KAMA BENJAMINI MKAPA





Na Oscar Assenga, TANGA.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Wallace Karia amesema kwamba ukarabati unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani utakapokamilika utawezesha uwanja huo kuwa kama wa Benjamini Mkapa wa Jijini Dar es Salaam.

Karia aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman kuangalia maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo ambao msimu huu utatumika kwa ajili ya michuano ya Kimataifa.

Alisema kwamba shughuli za ukaraibati kwenye uwanja huo tayari umeanza na majani yanayotakiwa kuwekwa hapa ni ya aina ya Babuda na tayari shirikisho la soka nchini watapeleka majani hayo na yapo njiani yanakuja.

Alisema kwa sasa maandalizi kwa ajili ya pichi kwa ajili ya kuondoa majani yaliyokuwepo na udongo yanaendelea na wataalamu wa TFF wataingia leo (Jumamosi) kueleza ni aina gani ya udongo utakaowekwa na jinsi gani ya kuweza kuotosha hayo majani ili yaweze kuota na kuwa na kiwango kinachostahili.

“Majani hayo yatakapokuwa yameota utakuwa ni uwanja huo na wa Benjamini Mkapa ambazo zina majani hayo hivyo kuiwezesha Pichi ya CCM Mkwakwani kuwa kama ya Uwanja wa Mkapa”Alisema Rais Karia

Aidha alisema kwamba suala la vyumba na majukwaa Mwenyekiti nimeshafanya utaratibu wa kumleta mchoraji ambaye amechora na amesema Jumamosi tutapata michoro ya kuweza kurekebisha na tutahakikisha angalau kama Munga atawawezesha uwanja huo tutaweka siti kama wanavyotaka uwanja mzima “Alisema

Hata hivyo alisema kwamba hata kama timu hiyo ikiingia kwenye hatua ya makundi bado timu hizo zitakuja kucheza Tanga Mkwakwani.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani alisema kwamba timu ya Coastal Union inatokea mkoani humo na hawana uwanja wenye kukudhi vigezo vya CAF maanake itapelekea timu ya Coastal wanapocheza nchini ikacheze kwenye maeneo mengine nchini nje ya mkoa huo.

“Niwahakikishia wana Tanga kama kiongozi wa kuisimamia Serikali kwenye mkoa wa Tanga na CCM ambayo wanadhamana kubwa ya kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu ambaye anahimiza michezo wa mpira wa miguu na michezo mengine ambaye amejitoa mhanga kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu unakua hapa nchini na kuzisaidia timu mbalimbali lazima tuhakikishe katika mashindano hayo Coastal Union watacheza kwenye mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani”Alisema Mwenyekiti Rajab

Naye kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,Hassan Muhsin alisema vita wamepambana kutokushuka daraja zaidi ya mara tatu na sasa wanashukuru Mungu mwaka huu wamepata nafasi ya 4.

“ Lakini tunamhsukuru Mungu msimu uliopita tumepambana kufika nafasi ya 4 na mashindano hayo tulionayo mbeleni yanahitajika maandalizi makubwa sana ule ushirikiano ulikuwepo awali unatakiwa kuzindishwa mara dufu”Alisema

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger